Ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, umefungwa rasmi leo Agosti 17, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, ameiambia mahakama kuwa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa, Jamhuri imeona mashahidi 17 waliotoa ushahidi wanatosha kuthibitisha hoja zao.
Lissu ameeleza kuwa hana pingamizi na uamuzi huo, huku Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan...