Featured content

Sadio Mané atangaza kustaafu kuichezea Senegal, baada ya miaka 14
Baada ya Senegal kuondolewa kwa maumivu katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 kufuatia kufungwa mabao 3-2 na Ubelgiji, nyota wa timu hiyo, Sadio Mané, ametangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa. Mané (34), alitangaza uamuzi huo kupitia taarifa iliyochapishwa na gazeti la Senegal la Le Quotidien, akihitimisha safari ya miaka 14 akiwa na timu ya taifa ya Senegal. "Fahamuni kwamba nilijitoa kwa kila kitu kwa ajili ya bendera hii. Nilitoa uwezo wangu wote na siku zote nilipigania...
Mnyika: Fedha za 'ToneTone' ziko salama, kwa sasa anayehusika kusaini ni Katibu Mkuu
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amethibitisha kuwa fedha zote zinazochangwa na wananchi pamoja na wanachama, ikiwemo mifumo ya kielektroniki na zile za "tonetone" zinazokusanywa mikutanoni, ziko salama kabla na baada ya matumizi. Mnyika aliongeza kuwa, kwa mujibu wa taratibu za kifedha za kitaasisi, yeye kama Katibu Mkuu ndiye Afisa Masuhuli wa chama ambaye anasimamia uidhinishaji huo.
Taharuki za Kisiasa nchini zinaweza kuathiri fursa ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2027?
Tanzania inatarajiwa kuandika historia kwa kuwa kati ya wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Michuano hiyo inatazamiwa kufungua fursa kubwa na nyingi kutokana na kukusanya mataifa mbalimbali, hivyo kuwa kivutio kwa mashabiki Duniani. Wakati maandalizi yakishika kasi, Mdau anasema hali ya Kisiasa tangu na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 imekuwa na vipindi vya taharuki, inachangiwa na wito wa maandamano unaosambazwa mitandaoni na Wanaharakati au vikundi visivyojulikana.
Rais Samia: Maridhiano si udhaifu, bali ni ukomavu wa kisiasa unaojenga umoja wa nchi
Rais Samia Suluhu amesema maridhiano ni ishara ya ukomavu wa kisiasa unaojenga umoja na kuheshimiana, akisisitiza kuwa siasa zinapaswa kuongozwa na hekima, utu na maslahi ya taifa badala ya mivutano isiyoisha. Amesema wananchi wanahitaji amani, usalama na utulivu, akizungumza Julai 9, 2026, wakati wa kushuhudia Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa kati ya CCM na ACT-Wazalendo katika Viwanja vya Ikulu, Zanzibar.
NECTA yafuta matokeo ya Kidato cha 6 na Ualimu waliotumia ChatGPT kujibu mtihani
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 58 baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Waliofutiwa matokeo ni watahiniwa 44 wa Mtihani wa Kidato cha Sita na 14 wa Mtihani wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi (DPEE), baadhi wakitajwa kutumia AI (Chatgpt).
Neymar Jr atangaza kustaafu kuichezea Timu ya Taifa ya Brazil
Neymar Jr ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya taifa baada ya Brazil kutolewa kwenye Kombe la Dunia na Norway katika hatua ya 16 Bora, ikiwa ni mara ya kwanza Brazil kushindwa kufika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia tangu mwaka 1990.
JWTZ: Wasioitakia mema nchi yetu, wanahamasisha kufanya vurugu, hatutasita kuchukua hatua
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wananchi kupuuza wito wowote unaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaohusika na vitendo hivyo. Katika taarifa yake kwa umma, JWTZ imesema kuwa ina jukumu la kulinda usalama wa nchi na wananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Taifa Sura ya 192. Jeshi hilo limeeleza kuwa litaendelea kushirikiana...
Yanga yatozwa Tsh. Milioni 100 kwa kutumia 'Jumba la Maajabu'
Klabu ya Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni 100 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kukiuka kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara katika mchezo namba 233 dhidi ya JKT Tanzania, uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-0. Adhabu hiyo imetolewa baada ya wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi wa Yanga kushindwa kutumia chumba rasmi cha kuvalia katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, na badala yake kutumia nyumba iliyopo nje ya Uwanja.
Lissu: DPP anilipe fidia kwa taabu aliyonisababishia kwa siku 139
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu ameiomba Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Mashtaka DPP na amlipe fidia kwa ucheleweshaji wa shauri lake. Lissu amesema hayo mbele ya Majaji watatu wa rufani Shimiwa Mwarija, Muruke na Khamis ambapo amedai kuwa kesi yake imwcheleweshwa kwa makusudi kwa siku 139 huku akikaa gerezani kwa mwaka mmoja na miezi mitafu sasa.
Katambi: Ambaye anaona sina Mamlaka tutakutana kwenye sheria
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi wakati akifanya mahojiano na UTV Julai 1, 2026, amesema maandamano yoyote yanapaswa kufuata taratibu za kisheria ili yarasimishwe na kuwekwa katika mazingira salama. Akijibu swali kuhusiana na kifungu cha sheria katika Katiba inayompa Waziri wa Mambo ya Ndani Mamlaka ya kutoa kauli ya kusimamsisha Mikutano ya vyama vya siasa, amesema "Sasa, mamlaka ukimuuliza ya waziri, ni ya kikatiba na ya sheria ya Police Force and Auxiliary Services."...
Ronaldo kustaafu soka la Kimataifa baada ya Kombe la Dunia 2026
Dada yake Cristiano Ronaldo, Katia Aveiro, amesema kuwa nahodha huyo wa Ureno anakaribia kuaga rasmi timu ya taifa baada ya Kombe la Dunia 2026.
RC Sirro: Kwa uzoefu wa askari wetu kifo cha dereva wa Heche kilikuwa cha kawaida
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Simon Sirro, amesema kuwa kwa mujibu wa uzoefu wa askari na wataalamu wa serikali, kifo cha dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), John Heche, kinaonekana kuwa cha kawaida.
Mwanachama wa CCM, David Nkindikwa aripotiwa kutoweka tangu Juni 24
Pichani ni David Nkindikwa ni Mwanachama wa CCM lakin mitandaoni huwa anajiita Mwanaharakati Mzalendo. Soma Pia: Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi Nkindikwa alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Samia. Kupitia ukurasa wake wa Instagram alikuwa anakosoa sana Serikali na alikuwa haogopi Juni 24 majira ya saa moja jioni alimuaga mkewe kwamba anaenda kumnunulia Ice Cream maana mkewe ni mgonjwa, tangu muda huo mpaka sasa hajarudi na simu zake...
Jaji Mkuu: Viongozi wa Kisiasa wasiingilie shughuli za Kisheria
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Madalali Juni 30, 2026 amesema hatarajii kuona viongozi wa kisiasa wakiingilia utendaji wa shughuli za Mahakama kwa kigezo cha nyadhifa walizonazo katika kamati za ulinzi na usalama za mikoa au wilaya.
Rungwe: Salm aliingilia majukumu ya Mwenyekiti, amemtenguliwa
Mwenyekiti wa Chama CHAUMMA, Hashimu Rungwe, ametangaza maamuzi ya Halmashauri Kuu ya chama hicho iliyoketi Juni 30, 2026, jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu imemtengua rasmi Katibu Mkuu wa chama, Salum Mwalimu Juma, kuanzia tarehe hiyo ya kikao. Maamuzi hayo yamekuja baada ya kutathmini mwenendo mzima wa uongozi ndani ya chama huku Halmashauri Kuu ya CHAUMMA ikimemteua Benson Kigaila kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho.
Kigaila: Sheria haisemi chama kiombe kibali kufanya Mikutano au Maandamano
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Benson Kigaila amesema tabia ya serikali kushiriki kuvunja sheria inatakiwa kupingwa na kila Mtanzania anayetaka utawala wa sheria, hadharani na sirini. Haya mambo lazima yapingwe kwa nguvu zote kwani yanahatarisha misingi ya demokrasia nchini. Kigaila amefafanua kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 haitaki vyama kuomba kibali, bali kutoa taarifa ya saa 48 kwa Jeshi la Polisi ili liandae ulinzi na sio kuzuia mikutano.
Pendekezo: Iundwe 'Yanga Law', wanaokaidi vyumba vya kubadilishia nguo wapokwe alama 3
Mdau wa soka amependekeza kuundwa kwa sheria maalumu aliyoipa jina la 'Yanga Law' kuelekea msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya NBC ili kuimarisha nidhamu, ushindani na hadhi ya ligi. Amesema kutokana na matukio yanayojirudia ya baadhi ya klabu, hususan Yanga SC, kudaiwa kukaidi taratibu za matumizi ya vyumba rasmi vya kubadilishia nguo, kuna haja ya kuweka adhabu kali zaidi ili kukomesha tabia hiyo na kuondoa vitendo vinavyoonekana kushusha hadhi ya ligi.
Kocha wa Uholanzi Koeman ajiuzulu baada ya kutupwa nje Kombe la Dunia
Ronald Koeman amejiuzulu rasmi kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi baada ya timu hiyo kutolewa kwenye Kombe la Dunia 2026 katika hatua ya 32 bora kufuatia kufungwa na Morocco kwa mikwaju ya penalti. Koeman ametangaza uamuzi huo siku baada ya kipigo hicho kilichokatisha safari ya Uholanzi kwenye mashindano hayo.
Salum Mwalimu ajiuzulu kwa muda CHAUMMA kupisha uchunguzi
Katibu Mkuu wa Chama cha CHAUMMA, Salum Mwalimu, ametangaza kujiondoa kwa muda katika nafasi yake ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizowasilishwa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho. Katika barua aliyomwandikia Mwenyekiti wa Taifa wa CHAUMMA, Hashim Rungwe, Juni 30, 2026, Mwalimu amesema uamuzi huo unalenga kutoa nafasi kwa uchunguzi huru kufuatia tuhuma zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Juni 29, 2026, katika makao makuu ya chama hicho, Kinondoni Biafra, Dar.
Mpina: ACT Wazalendo tunaenda mahakamani kupinga Sheria ya Fedha 2026
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema chama hicho kimepanga kufungua kesi mahakamani kupinga baadhi ya vipengele vya Sheria ya Fedha wa mwaka 2026, kikidai kuwa vinaongeza mzigo wa kodi kwa wananchi wa kipato cha chini huku vikitoa misamaha kwa wawekezaji wakubwa.
Back
Top Bottom