Featured content

Fahamu mambo mbalimbali kuhusu gari aina ya Subaru Forester
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU GARI HII Wakuu rafiki yangu mmoja yupo interested na hizi gari aina ya Subaru Forester lakini kabla hajaingiza maamuzi mzima mzima alitaka kujua yote ya husuyo hizi aina za haya magari. Stability zake, upatikanaji wa spare na mengine yote ambayo mtu yeyote angependa kuyajua.Huyu jamaa yupo mkoani na amejaribu kuangalia aina hizo hazipo na yeye yupo interested nayo kwa kuwa ni 4DW kulingana na maeneo anayoishi anahitaji mkoko wa namna hiyo. Kwa...
Meli ya mafuta yenye bendera ya Tanzania yatekwa nyara na maharamia wa Somalia
Meli ya mafuta yenye bendera ya Tanzania, MT ASANA, imetekwa na maharamia wanaoshukiwa kutoka Somalia katika pwani ya Yemen, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo. Tukio hilo lilitokea baada ya meli hiyo kuondoka Mukalla, Yemen siku ya Ijumaa. Baada ya kutekwa, meli hiyo ilipelekwa katika pwani ya Caluula, eneo la Bari kaskazini mashariki mwa Somalia, ambako inaendelea kushikiliwa na watekaji, kwa mujibu wa maafisa wa eneo la Puntland.
Bobi Wine appoints Nambeshe acting NUP President
National Unity Platform (NUP) President Robert Kyagulanyi Ssentamu, popularly known as Bobi Wine, has appointed Hon. John Baptist Nambeshe as the party’s Acting President, replacing Dr. Lina Zedriga Waru, whose four-month tenure has ended.
Mapfumo defends US$1 million Chivayo deal, says his principles remain intact
Chimurenga music legend Thomas “Mukanya” Mapfumo has defended his decision to accept a US$1 million performance offer from businessman Wicknell Chivayo, saying the deal does not mean he has abandoned his values, activism or support for ordinary Zimbabweans. The 81-year-old music icon has faced criticism from some fans and social commentators who accused him of compromising his long-standing reputation as a voice for social justice and human rights.
AZAKI: Serikali ya Tanzania imeilipa kampuni ya BGR Group Tsh. Bilioni 7.886 kuisafisha taswira ya nchi
Wawakilishi wa Asasi za Kiraia (AZAKI) Tanzania, Julai 16, 2026, wamesema kumekuwa na jitihada za kutumia njia za mkato kushughulikia changamoto za kisiasa na kiutawala nchini badala ya kuzingatia misingi ya katiba na utawala wa sheria. Wamedai kuwa kumekuwa na matukio ya utekaji, mateso, kuwekwa mahabusu kwa baadhi ya watu na vifo vinavyodaiwa kuhusishwa na mazingira ya kisiasa, huku wakisema hatua hizo zinalenga kunyamazisha sauti zinazotetea amani na uwajibikaji. Soma: AZAKI: Hali ya...
Dkt. Bana: Hamuwezi kuridhiana wakati Kiongozi mmoja wa kisiasa yuko Gerezani
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana, amesema mchakato wa maridhiano hauwezi kuanza au kufanikiwa ikiwa bado kuna kiongozi wa kisiasa anayekabiliwa na kesi mahakamani, huku akisisitiza kuwa pande zote lazima zijiridhishe kwanza kabla ya kukaa meza moja. Dkt. Bana amesema ni vyema kusubiri hukumu ya mahakama kwa kuwa ndiyo chombo chenye mamlaka ya kutoa haki.
Sierra Leone: Serikali yafuta Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Rais wa zamani, Ernest Bai Koroma
Serikali ya Sierra Leone imefuta mashtaka yote, yakiwemo ya uhaini, yaliyokuwa yakimkabili Rais wa zamani wa nchi hiyo, Ernest Bai Koroma, aliyekuwa akihusishwa na jaribio la mapinduzi ya serikali lililotokea mwaka 2023. Koroma, mwenye umri wa miaka 72, amekuwa akikanusha kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi la Novemba 2023. Katika tukio hilo, watu wenye silaha walivamia ghala la silaha la jeshi na magereza kadhaa, ambapo wafungwa wapatao 2,000 walitoroshwa.
TLS, LHRC, Dk. Slaa wamburuza Mahakamani Waziri Katambi kwa kuzuia mikutano ya Kisiasa
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Dk. Willibrod Slaa, wamefungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Tabora, wakipinga kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, kuhusu zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Mbali na Katambi, wadaiwa wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Morogoro: Wananchi wapinga mauaji yanayofanywa na Askari wa Hifadhi
Ndugu na jamaa wa kijiji cha Kisaki mkoani Morogoro wameandamana na kutoa malalamiko mazito dhidi ya askari wa wanyamapori (maliasili) kwa tuhuma za kuwauwa kikatili wananchi wanaoingia msituni kutafuta riziki zao, kama vile kukata mbao. Mmoja wa wananchi, ameeleza kuwa vitendo hivyo vya ukatili vimekithiri na kuacha majonzi makubwa kwa jamii, huku akiongeza kuwa msituni kuna mafuvu na miili mingi ya binadamu wenzao waliopoteza maisha kwa kupigwa risasi na askari hao
Biashara ya genge inalipa sana, kinachokwamisha watu ni kuwekeza mtaji mdogo sana
Mdau amesema biashara ya kuuza genge ni mojawapo ya biashara nzuri na yenye faida, lakini changamoto inayowafanya wengi wasifanikiwe ni kuanza na mtaji mdogo sana. Ameeleza kuwa kuwekeza mtaji wa mfano wa shilingi 80,000 pekee kunafanya iwe vigumu biashara kukua, huku akisisitiza kuwa mafanikio yanahitaji uwekezaji wa kutosha na kuondoa hofu ya kupata hasara.
Morocco kujenga uwanja mkubwa zaidi duniani kwa ajili ya Kombe la Dunia 2030
Morocco kujenga uwanja mkubwa zaidi duniani kwa ajili ya Kombe la Dunia 2030 Uwanja huo utajengwa katika eneo la El Mansouria, kilomita 38 kaskazini mwa jiji la Casablanca, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Morocco kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2030, ambalo litaandaliwa pamoja na Hispania na Ureno. Kampuni za usanifu za Populous na Oualalou + Choi ndizo zimebuni mradi huo, unaotarajiwa kuifanya Grand Stade Hassan II kuwa uwanja mkubwa zaidi wa soka duniani.
Msigwa: Kinachomponza Lissu ni Akili, mmeamua kufungia Akili yake ndani ya Gereza
Kada wa CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, amesema Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, hapaswi kulazimishwa kuomba msamaha ili aachiwe huru, akisisitiza kuwa hana kosa linalohitaji msamaha.
Prof. Tibaijuka: Rais naendelea kushauri Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki
Waziri wa zamani, Profesa Anna Tibaijuka, amemshauri Rais Samia kumwachilia huru Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye amekuwa rumande katika Gereza Kuu la Ukonga kwa zaidi ya mwaka mmoja akisikiliza kesi ya uhaini inayomkabili. Kupitia ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa X, Tibaijuka amesema kesi hiyo imechukua muda mrefu bila kukamilika na kumtaka Rais kuongozwa na hekima na busara alizoonyesha alipotoa sera ya maridhiano ya 4Rs.
Oburu Oginga: Chama cha ODM kumuunga mkono Ruto Uchaguzi Mkuu wa 2027
Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kimetangaza kuwa hakitasimamisha mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa Kenya wa mwaka 2027, badala yake kitamuunga mkono Rais William Ruto kuwania muhula wa pili madarakani. Kauli hiyo ilitolewa, Julai 12, 2026, na kiongozi mwandamizi wa ODM, Oburu Oginga, ambaye amesema uamuzi huo umetokana na mazungumzo ya kisiasa yanayoendelea kati ya chama hicho na viongozi wa serikali.
IMF yaipatia Tanzania mkopo Nafuu wa takriban Tsh. Trilioni 1.16
Wizara ya Fedha imeeleza kuwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeidhinisha kutolewa kwa Dola za Marekani Milioni 443.9 (takriban Tsh. Trilioni 1.16) kwa Tanzania baada ya kukamilisha tathmini za mwisho chini ya programu za ECF inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii na RSF ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
FIFA yafikiria uwezekano wa Kombe la Dunia kushirikisha timu 64 ifikapo 2030
Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amesema shirikisho hilo litajadili uwezekano wa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia la mwaka 2030 kutoka timu 48 hadi 64. Amesema pendekezo hilo litajadiliwa na kamati husika baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia la 2026, akisisitiza kuwa mashindano hayo yanapaswa kutoa fursa kwa mataifa mengi zaidi kushiriki.
Kombe la Dunia 2026: Timu nne bora duniani zatinga nusu fainali kwa mara ya kwanza
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia la FIFA, timu nne zinazoongoza katika viwango vya ubora vya FIFA (FIFA World Rankings) zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali. Hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026 imekamilika kwa kuzikutanisha timu nne bora duniani kwa mujibu wa viwango vya FIFA: Ufaransa, Argentina, Hispania na England.
Senegal yamtimua kocha Pape Thiaw na benchi lake la ufundi
Shirikisho la Soka la Senegal limemfuta kazi kocha mkuu Pape Thiaw na benchi lake lote la ufundi baada ya kutolewa katika hatua ya 32 bora, wiki chache tu baada ya kusaini mkataba mpya kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia la FIFA. Senegal ilikuwa ikitarajiwa kuwa miongoni mwa timu zitakazowania ubingwa wa Kombe la Dunia, baada ya kuifunga Morocco katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Januari 2026.
Jumuiya ya Madola yaipa Tanzania siku 30 Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu
Wakuu, Nimeona niwaletee mrejesho na uchambuzi wa waraka muhimu sana ambao umetoka leo tarehe 10 Julai 2026 kutoka kwa Kundi la Mawaziri wa Jumuiya ya Madola linaloshughulikia Demokrasia na Haki za Binadamu (CMAG - Commonwealth Ministerial Action Group). Kikao chao cha 73 kimefanyika leo kwa dharura (extraordinary session) na kutoa Tamko la Kuhitimisha (Concluding Statement) ambalo sehemu kubwa limejadili hali ya kisiasa na haki za binadamu hapa nchini kwetu Tanzania. Kwa ufupi, Tanzania...
ACT: Tunataka uchunguzi huru na wa haraka kuhusu Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania
Chama cha ACT Wazalendo kimetaka kufanyika kwa uchunguzi huru na wa haraka kuhusu uchaguzi wa viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), baada ya kuzuka kwa sintofahamu kuhusu matokeo ya Uchaguzi wa Urais, ambapo Leonard Thadeo aliyepata kura moja alitangazwa mshindi.
Back
Top Bottom