Featured content

Kumbukizi | Siku moja kabla ya Uhuru wa Tanganyika, nini kilitokea Desemba 8, 1961?
Leo tunajua kwamba tarehe 9 December 1961 Tanganyika ilipata Uhuru. Tunajua Nyerere alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza. Tunajua bendera ilishushwa na ya Tanganyika ikapandishwa. Lakini kuna swali moja ambalo historia ya vitabu mara nyingi hailisimulii kwa undani: Tanganyika ilikuwaje siku moja tu kabla ya Uhuru? Kiufupi, tarehe 8 December 1961, mtu wa kawaida aliishi katika nchi ambayo bado ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza, lakini kesho yake ingekuwa taifa huru. Dar es Salaam ilikuwa...
Petroli yapanda, EWURA yasema sababu ni mgogoro wa Kisiasa Mashariki ya Kati
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa nchini, ambazo zinaanza kutumika leo Oktoba 7, 2026. Bei ya Petroli kwa Dar imefikia Tsh. 4,057 kutoka Tsh. 3,796, bei kubwa ya Septemba ilikuwa Tsh. 4,099 (Katoro – Kagera) kwa Oktoba ni Tsh. 4,370 (Kyerwa – Kagera).
Prof. Mkenda: Bodi ya Walimu kuanza kutoa Leseni kwa Walimu wote Nchini
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali kupitia Bodi ya Taaluma ya Ualimu nchini (TTPC) imeanza maandalizi ya kuratibu na kutoa leseni rasmi za ufundishaji kwa walimu nchini. Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza thamani, heshima na nidhamu katika taaluma ya ualimu, huku ikihakikisha kuwa kila anayefundisha anatimiza vigezo vinavyotambulika kisheria. Profesa Mkenda ameyasema hayo Bagamoyo mkoani Pwani, wakati akizungumza na watendaji wa Wakala wa...
Mwabukusi: Msajili sajilini vyama vya Gen Z, wapeni vinavyoendana na lugha yao
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, ameiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuongeza usajili wa vyama vipya ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya kushiriki katika siasa. Mwabukusi amesema vijana wanapaswa kupewa fursa ya kuwa na vyama vinavyoendana na mitazamo na lugha yao, akisema hatua hiyo inaweza kuwapa nafasi ya kujihusisha na siasa kupitia njia rasmi. “Mheshimiwa Msajili, ambalo ninaloliomba kwa dhati, sajilini vyama,” amesema Mwabukusi.
Prof. Kabudi: Kiongozi akichaguliwa huwezi kumwita Haramu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kuheshimiana katika kueleza tofauti zao za kisiasa, akisema matumizi ya lugha kama kumuita kiongozi mwenzake ambaye amechaguliwa “haramu” sio sahihi. Prof. Kabudi amesema hayo leo Oktoba 7, 2026 katika Uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika hoteli ya Hyatt-Regency jijini Dar es Salaam ambapo yeye alikuwa...
Kenya yaripoti mgonjwa wa kwanza wa Ebola
Kenya imethibitisha kesi yake ya kwanza ya Ebola baada ya raia wake aliyekuwa akiishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuugua na kufariki baada ya kusafiri hadi Nairobi. Mamlaka za afya tayari zimewatambua watu 28 waliokutana naye, wakiwemo wanafamilia na wahudumu wa afya, huku wakifuatilia pia abiria 23 na wahudumu wanne wa ndege aliyosafiria.
Bodi ya Ligi: Tutatumia ‘Gas Detector’ kukagua hewa vyumbani katika Dabi ya Kariakoo
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Cornel Barnabas, amesema vifaa maalum vya gas detector vitatumika kukagua hali ya hewa katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mchezo wa dabi ya Kariakoo. Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha timu zinapata mazingira salama na sahihi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo. Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya TFF jijini Dar es Salaam, Barnabas amesema kifaa hicho kitaweza kupima kiwango cha oksijeni na kubaini uwepo...
Ghana yapiga marufuku kuhubiri kwenye Mabasi, Jela Miezi 8, faini Dola 52
Ghana ni nchi yenye Wakristo wengi, ambapo kuhubiri injili kwenye vyombo vya usafiri wa umma ni jambo lililozoeleka. Katika mabasi ya masafa marefu, mara nyingi wachungaji huonekana na kusikika wakihubiri injili. Wakati mwingine husimama kwenye ngazi karibu na dereva, huku wengine wakitembea ndani ya basi wakisoma Biblia na kuwataka wenye dhambi watubu kwa sauti kubwa. Wanaendelea kuhubiri hata safari inapochukua saa kadhaa. Baadhi ya abiria wanaoamini dini hiyo huwapa wahubiri fedha kama...
Zimbabwe: Chivayo, mke wake wafariki kwa ajali ya Helikopta
Serikali ya Zimbabwe (kupitia msemaji mkuu Nick Mangwana) imethibitisha kuwa leo jioni, Septemba 30, 2026, helikopta iliyokuwa na watu 6 (mfanyabiashara mashuhuri, abiria wengine, na marubani wawili) imeanguka katika eneo la Marondera na hakuna aliyepona. Mamlaka na vyombo vya habari nchini Zimbabwe na kimataifa vimethibitisha kuwa mfanyabiashara huyo ni Wicknell Chivayo, na alikuwa ameambatana na mke wake (Lucy "Lulu" Muteke) pamoja na watu wengine waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo...
Huna BANDO na unataka kutumia AI? Muulize AVA chochote, upate jibu papo hapo tena bure!
Teknolojia mpya ya akili unde ya sauti, “Ask VIAMO Anything – AVA,” imezinduliwa kuwawezesha wananchi kupata majibu ya maswali mbalimbali bila intaneti. Kwa sasa, huduma hii ni bure kwa watumiaji wa Vodacom, wanaoweza kuuliza maswali kwa sauti kupitia simu zao na kupata majibu. Teknolojia hiyo inalenga pia kuwafikia wananchi wasio na simu janja au uwezo wa kutumia huduma zinazohitaji intaneti.
DRC | Mwanasiasa wa chama tawala auawa baada ya kuhamasisha uelewa kuhusu Ebola
Mwanasiasa wa chama tawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Marie-Celestin Karondwa, amepigwa hadi kufariki dunia baada ya kushiriki kipindi cha redio kilicholenga kutoa elimu kuhusu Ebola. Tukio hilo lilitokea Jumapili, Septemba 27, 2026, Mjini Butembo, Mkoa wa Kivu Kaskazini. Karondwa, aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya UDPS mjini Butembo na msemaji wa chama hicho, alishambuliwa baada ya kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ebola. Kwa mujibu wa...
James Mbatia: Kisheria mimi ni Mwenyekiti halali wa NCCR-Mageuzi
Mwanasiasa mkongwe, James Mbatia, amesisitiza kuwa kisheria yeye ndiye Mwenyekiti wa halali wa chama cha NCCR-Mageuzi kufuatia hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
Lissu: Waambieni Viongozi wa Dini waseme, wasinyamaze, Nchimbi yuko wapi?
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, akiwa Kizimbani baada ya kuahirishwa kwa Kesi yake amehoji alipo aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, huku akiwataka viongozi wa dini kutonyamazia suala hilo. "Nchimbi hajapatikana? Waulizeni Maaskofu waseme kwenye Makanisa yao, viongozi wa dini waseme! Viongozi wa dini wasinyamazie haya mambo ya hovyo... Makamu wa Rais yuko wapi? Kwa nini mnanyamaza?" Soma >> Tundu Lissu: Mimi niko gerezani, nasikia Dkt...
Wanu: Uwezekano mvua za El Nino umesababisha tubadili ratiba za Mitihani ya Taifa
Kutokana na tahadhari ya mvua za El Nino Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefanya marekebisho ratiba ya mitihani ya kitaifa na upimaji iliyotakiwa kufanyika Oktoba na Novemba mwaka huu. Akizungumza leo Ijumaa Septemba 25, 2026 Naibu Waziri wa Elimu, Wanu Hafidh Ameir amesema uamuzi huo umefanyika ili kuhakikisha usalama wa mitihani hiyo, wanafunzi na wasimamizi.
Ludovick Utouh: Utekelezaji wa mapendekezo ya CAG hauridhishi, uko chini ya 40%
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh, amesema utekelezaji wa mapendekezo yanayotokana na ukaguzi wa CAG bado hauridhishi, huku kiwango cha utekelezaji kikiwa chini ya asilimia 40.
Makonda: Wenzetu wakiendelea na mapambano, tutaingia mtaani kuuza juzi zetu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, ametishia kuwa iwapo kampuni ya Sandaland ikiendelea na msimamo wao bila kuongeza ubora wa jezi za timu ya taifa, Serikali itatangaza fursa kwa wabunifu na vijana Watanzania kubuni jezi mbadala na kila mtu kuingia mtaani kuuza zake. " Mungu akipenda, wiki ijayo kama wenzetu wakiendelea kuwa na mapambano, basi tutatangaza design kwa wazawa ambao ni Watanzania, kudesign jezi. Alafu sisi tutaingia mtaani kuuza. Sasa kila mtu si...
Makonda: Tukisema jezi ni mbaya mnatupeleka Mahakamani? Hatuna haki ya kutoa maoni?
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, amekemea vikali vitendo vya baadhi ya viongozi na wadau wa michezo kutumia vitisho vya kisheria dhidi ya wananchi na wanahabari wanaokosoa muundo na ubora wa jezi za timu ya taifa. Makonda amesisitiza kuwa Katiba ya Nchi inampa kila mwananchi uhuru wa kutoa maoni na kujieleza, hivyo si jambo la busara kuwatisha au kuwapeleka mahakamani Watanzania wanaosema ukweli pale jezi ya nchi yao inapokuwa mbaya au isiyokidhi viwango.
BASATA yamfungia Harmonize kufanya Muziki, Nandy atozwa Faini
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia msanii Rajab Abdulkahali (Harmonize) kujishughulisha na kazi za sanaa kwa namna yoyote ile hadi atakapotekeleza maagizo aliyopewa, ikiwemo kulipa faini ya shilingi milioni tano (Tsh 5,000,000/=) na kushusha video ya wimbo wake wa "Kudos" kwenye mitandao ya kijamii. Hatua hii imechukuliwa baada ya msanii huyo kubainika kusambaza video ya wimbo huo inayokiuka maadili ya Mtanzania na kuvunja heshima ya msikilizaji au mtazamaji, bila kutoa utetezi.
Lissu: Kwa Sheria za Tanzania na ushahidi uliotolewa, haiwezekani nihukumiwe kifo
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, inaendelea leo Jumatano, Septemba 23, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. Mahakama kinatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi, mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru. Hatua ya leo ni uwasilishaji wa maelezo ya mwisho (final submissions) kutoka pande zote mbili, baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wake kwa mashahidi 17 na upande wa utetezi kufunga ushahidi...
Polisi: Dereva wa TARURA alitishia kwa ‘bastola’ bandia, tumemkamata
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Sath John Masawa (31), dereva wa TARURA kwa tuhuma za kumtishia kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola halisi bali 'toyi', dereva wa basi la SATCO, Said Fadhili (54), baada ya kudaiwa kukwangua gari la TARURA. Polisi imebaini gari hilo pia lilikuwa namba za usajili zisizo sahihi.
Back
Top Bottom