Huyu anahitaji ushauri nasaha tu...
Nadhani mahakama ya maana kwa mwanasiasa ni wananchi. Katika hili jambo kila mwananchi mwenye akili timamu alisha-make opinion na kutoa hukumu kwamba bunge lilikosea na Zitto alikuwa right. Sasa mimi sioni verdict kubwa na ya maana zaidi ya ile inayotolewa na wananchi.
115256 said:Spika amshangaa Zitto
hii
hii itasadia kuleta challenge katika maamuzi mazima ya bunge, iwapo hili litaingia katika rekodi za bunge kwamba bunge limewahi kujirudi kwa kupitia maamuzi yake hamuoni kuwa itakuwa ni tofali jingine katika ukuta wa demokrasia?
Pundit,
Ikiwa Zitto kisha tumikia kifungo chake, leo analitaka bunge letu liweke kikao kwa ajiri yake kwa fedha za walalahoi, hivi kweli huoni kama hapa kuna utata kidogo maanake ingekuwa busara sana kama angeyafanya haya ktk kukata rufaa ya hukumu ile.
Tumekwisha toka huko na wananchi tunafahamu kuwa Zitto was right na tumeweza kumuunga mkono kila mahala.
Binafsi barua kama hii angeipeleka kwa JK, copy Bunge kutoa ufafanuzi kwa rais na wananchi maanake kama mbunge alikuwa na haki zote kuendelea kuwawakilisha wananchi wa Kigoma. na muhimu akisema hatua ambazo anataka zichukuliwe dhidi ya viongozi waliojaribu kulipotosha bunge na wananchi. Wabunge wanaweza pendekeza mbunge fulani kujiuzuru kwa kulipotosha bunge na kumbuka pia President ana uwezo na nguvu ya kuvunja hata bunge zima maadam pawe na sababu ya kufanya hivyo.
Ok tuseme Bunge wakubali kulitokea makosa ya taarifa kuwakilishwa na kila mmoja wao ajenge hoja ya kusema nilipiga kura yangu kutokana na ushahidi uliokuwepo wakati huo. Sitta apitishe kuwa hapakuwa na kosa -Then nani wa kumlaumu?... sii ndio yale ya wabunge wa marekani walipopiga kura kuunga mkono vita ya Iraq? leo hii wanashindwa hata kuchomoa na hata yule aliyekubali makosa anashindwa kusema wazi kuwa tuondoke Iraq no more support ya majeshi yetu Iraq isipokuwa wanazunguka tu....Tunachotaka ni hitimisho la swala la Buzwagi hayo ya bunge sisi tayari tumekwisha jua nani mgonvi wetu mpango wa kutubu hauwezi badilisha ukweli.
Spika amshangaa Zitto
na Tamali Vullu
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, ameeleza kushangazwa kwake na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kumuandikia barua akimtaka aiagize Kamati ya Kanuni ya Bunge kupitia upya adhabu aliyopewa.
Zitto alisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge Agosti 14, mwaka huu, kwa madai ya kusema uongo wakati akiwasilisha hoja binafsi akitaka Bunge liunde kamati kuchunguza, pamoja na mambo mengine, kusainiwa kwa mkataba wa mradi wa mgodi wa Buzwagi nje ya nchi.
Mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi mapema mwaka huu katika hoteli moja jijini London, Uingereza.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Sitta, alisema ingawa bado hajapata barua hiyo, lakini amezisoma habari kuhusu hatua ya Zitto katika vyombo vya habari.
Alisema kuwa baada ya kusoma, hakutegemea barua ya aina hiyo inaweza kuandikwa na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bado sijapata barua, ndiyo kwanza narejea kutoka India, lakini sikutegemea mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuandika barua ya aina hiyo, ingawa kila mtu ana uhuru wa kuzungumza.
Barua hiyo nimeisikia kwenye vyombo ya habari, ina maneno ya ajabu, nasubiri nipate barua hiyo ndiyo nitajua la kufanya, alisema Spika.
Source: Tanzania Daima
I hear you Mkandara, basically niliainisha argument yako versus haja ya ku set precedent ya rule of law katika post yangu huko nyuma katika thread hii (relentless resolute vs political tact).
Hufikiri kwamba ni muhimu kuweka precedent as a matter of record, na kufuata rule of law ili kesho wanetu wakitaka kufuatilia mambo hata miaka 10-20/ 100 au zaidi baadaye kuwe na historia kwamba bunge lilishawahi kuchemsha na vichwa vikaona na bunge likajirudi? Au hata kama halijajirudi kwa kiburi motion ya bunge kujirudi ilikuwa tabled?
Hii ndiyo sababu nilisema hili swala linachukua umuhimu mkubwa zaidi ya issue ya Zitto kwa sababu linagusa utaratibu mzima wa jinsi bunge linavyofanya kazi.The CCM dominance in parliament can be unhealthy, this has the potential of checking the unhealthy elements.Vitu vyote viwekwe mezani, tujue nani hasomi miswada, nani anapiga kura kwa utii wa chama, nani CCM lakini mwanamapinduzi wa kweli anayeunga mkono hoja za msingi za wapinzani na kadhalika.
Nafikiri hili ni muhimu.Europe na North America hawajapata maendeleo kwa kuwa content au non-confrontational watu wamepigana ma civil war na ma-revolution kuchinjana katika ma guillotine huko France and so on.Tukiogopa kukwaruzana kwa maneno tena kwenye bunge kidemokrasia tutafika kweli?
Viongozi wa Tanzania wananichekesha sana.Sasa wewe mtu barua hujaipokea ushaanza kudakia mambo kutoka press, ukikuta barua iliyochapishwa gazetini ni feki si aibu tupu kwa Spika mzima kujiropiokea mineno tu.
Sitta alivyom-succeed Msekwa nilikuwa nin sigh of relief kwa maana ya kufikiri kwamba we could not possibly get anything worse than Msekwa.Yaani sasa naona ingawa Msekwa alikuwa na michemko yake lakini ukimlinganisha Msekwa na Sitta katika ratio ni sawa na kumlinganisha Nyerere na Kikwete!
Tuliza ball babu, ngojea upokee barua halafu utaongea.HAraka ya nini au ndiyo usongo wa kumtoa nishai Zitto pamoja na ushabiki wa CCM?