BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
- Thread starter
- #41
Siyo kila kosa linalofanywa na viongozi jeuri wa CCM linahitaji kusuburi mpaka wakati wa uchaguzi ili wananchi wawashikishe adabu. Kwanza tunajua jinsi CCM walivyokuwa na mtandao wa kuiba kura. Hivyo inawezekana kabisa kwamba hiyo 2010 wasiadhibiwe kwa makosa yao chungu nzima.
Nchi ina sheria na kama zinakiukwa basi kuna mahakama ambazo zinaweza kusaidia kujua ni nani aliye mkosaji na adhabu ipi ambayo mkosaji huyo anastahili. Zitto ameonyesha uungwana wa hali ya juu kusubiri mpaka alipomaliza adhabu yake ili kuomba haki itendeke dhidi ya adhabu hiyo. Kuna ushahidi wa kutosha tu kuhusiana na nani alikuwa mkweli katika swala la Buzwagi.