Zitto Vs Spika

Sio dhamira yangu kusema hili lakini napenda kusema kama suala hili litashughulikiwa kisias kama mwanzoni

Amini, Amini nawaambieni: hakika mtu sasa ata katwa mguu.
 
Huyu Sitta anavyonichefua sitaki hata kuongelea issues maana ni nyingi na pana sana, nitaongelea kidogo tu jinsi gani arrogance yake inavyo-expose kufilisika kisiasa.

Kama Spika kweli ame-dismiss hoja za Zitto kama ni za "mtoto" inabid kabla ya kuiingilia issue aombe msamaha kwa Zitto na watoto wa Tanzania.

1.Ninaamini kisheria "mtoto" hawezi kuchaguliwa kuwa mbunge Tanzania.Furthermore Spika, hata kama anamuongelea Zitto kama "mtoto" in the sense ya mtu wa generation ambayo anaweza kuwa sawa na mtoto wake hii apart from being "age discrimination" haimuondolei "mtoto" haki ya kusema.Kuna nyakati "watoto" wanakuwa sawa na "wakubwa" wanakosea.Kauli ya Spika inamu-expose yeye mwenyewe kama mbabe asiyetumia hoja na anaye abuse utamaduni wa kuheshimu wakubwa kiumri to brutally force his misguided views.Kama Zitto angesema something along the lines of "Wazee wanazuia maendeleo" mara moja angeitwa mtovu wa nidhamu, kwa nini Sitta aweze ku-discriminate based on age lakini vijana wasiweze kufanya the same thing.This should be about the issues and not about age.

Spika waombe radhi watoto wa Tanzania maana ulichosema kinaamanisha kuwa watotot hawawezi kusema cha maana.


Sasa kama spika amesema yafuatayo barua ya Zitto

Kwa kuzingatia, maneno yaliyojaa ufedhuli na ubabe dhidi ya Bunge kama Taasisi na dhidi ya Viongozi wa Bunge, Spika wa Bunge, kwa wakati mwafaka ataifikisha barua hiyo ya Mhe. Zitto kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kupata ushauri wake. "

Huyu Spika anajua maana ya neno fedhuli? Kama Zitto angekuwa fedhuli asingekubali hata kutumikia adhabu yao.Nani mbabe kati ya Zitto anayepeleka issues zisikilizwe bungeni na Spika anayetumia lugha ya kihuni, iliyojaa arrogance ya entitlement ya old boy network na dharau kwa watoto wa Tanzania?
 
Spika kitanzini

na Charles Mullinda
Tanzania Daima

NGUVU za Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa zinaelekea kuporomoka baada ya kambi yake kuu kuanza kumgeuka.


Sitta, ambaye mara kadhaa tangu aliposhika wadhifa wa Uspika amekuwa akijikuta katika migongano ya hapa na pale na wabunge na wananchi, amekuwa akiitegemea zaidi kambi ya wabunge vijana kumkingia kifua, wakiwemo wale wa kambi ya upinzani.



Kambi hiyo ya wabunge vijana, sasa imemgeuka Spika baada ya matukio ya hivi karibuni kuhusu uamuazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, ‘kukata rufaa’ akilitaka Bunge lipitie upya adhabu ya kusimamishwa aliyopewa mwezi Agosti.

Baada ya kupokea barua ya mbunge huyo kuhusu suala hilo, Spika alikaririwa akimbeza Zitto na kusema kuwa anamuonea huruma kutokana na kuonyesha kwake (Zitto) kutokomaa kisiasa.

Zitto ni mmoja wa wabunge mahiri katika kambi ya wabunge vijana, ambao mara kadhaa wamelitikisa Bunge kutokana na hoja zao na pia, ingawa ni mbunge wa upinzani, amekuwa moja ya nguzo muhimu za Spika hasa kwa mahasimu wake wa kisiasa wa ndani ya chama chake.

Habari zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili, zilieleza kuwa Zitto, amemuweka Spika Sitta katika wakati mgumu baada ya kuendelea na msimamo wake wa kutaka adhabu yake ipitiwe, licha ya kauli ya Sitta.

Ingawa jana katika mahojiano yake na gazeti hili alisema hataki kulumbana na Spika Sitta katika suala hilo kwa sababu anamuheshimu sana, Zitto aliendelea kusisitiza kwamba anachotaka ni haki itendeke kwa sababu anaamini adhabu iliyotolewa na Bunge dhidi yake haikuwa sahihi.

“Ninamuheshimu sana Spika, sipendi kabisa kubishana naye, ninachokiomba ni haki itendeke kwa sababu ninaamini sikutendewa haki kwa kupewa adhabu ile, sijaridhika. Lakini kamati ikiketi na kupitia adhabu hiyo nitaridhika na maamuzi yake,” alisema Zitto.

Aidha, akizungumzia madai kwamba alisambaza barua yake hiyo kwa vyombo vya habari na katika mtandao wa ‘internet’, jambo ambalo Spika amekaririwa akieleza kuwa ni kinyume cha taratibu za Bunge, Zitto alisema hilo si kweli kwa sababu alitoa nakala kwa kiongozi wa upinzani bungeni na kwa katibu wa Bunge tu.

Huku akiongea kwa kuchagua maneno, Zitto alisema kamwe hana nia ya kutumia nafasi hiyo kutafuta umaarufu. “Sikutumia nafasi kujitafutia umaarufu kama inavyoelezwa, ningetaka hivyo ningezungumzia jukwaani, kwa sababu wakati naadhibiwa watu wengi walikuwa hawampendi Spika, hapo ndipo ningemchafua.

“Ninasema kweli, ningetaka umaarufu ningekwenda mahakamani, nina orodha ndefu ya wanasheria wazuri wanaotaka suala hili nilipeleke mahakamani na wao watalisimamia ili haki ipatikane, lakini mimi nasema hapana, na tangu nilipoadhibiwa nilikuwa kimya, nimetumikia kifungo kimya, hiyo yote ni kwa sababu ya kumuheshimu tu Spika, ni unyenyekevu wa hali juu,” alisema Zitto.

Inadaiwa kuwa msimamo huu wa Zitto na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na Spika dhidi ya barua iliyoandikiwa na mbunge huyo, unaashiria kuwa Spika ana wasiwasi kuwa iwapo Kamati ya Kanuni za Bunge itaipitia upya adhabu hiyo, Bunge linaweza kujikuta matatani kwa kukiuka kanuni au desturi zake.

Wataalamu wa wafuatiliaji wa masuala ya Bunge waliozungumza na gazeti hili walieleza kuwa, Bunge linaendeshwa kwa kanuni na desturi ambazo huliongoza kufikia maamuzi yake, lakini katika kesi ya Zitto, vyote hivyo havikufuatwa.

Ukweli huu unathibitishwa na adhabu kadhaa zilizokwishatolewa na Bunge kwa wabunge ikiwemo aliyopewa aliyewahi kuwa Mbunge wa Temeke, Augustino Mrema baada ya kutamka bungeni kuwa serikali imepanga kumuua yeye (Mrema) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharrif Hamad.

Mrema aliliambia Bunge kuwa habari hizo alipewa na aliyewahi kuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa Imran Kombe. Bunge lilimpa Mrema siku tano za kuthibitisha maelezo yake, lakini alishindwa kufanya hivyo na kujikuta akiadhibiwa kusimama kufanya shughuli za Bunge kwa muda wa siku 40.

Baadhi ya wabunge walioadhibiwa kwa utaratibu wa kupewa siku za kuthibitisha kauli zao ni pamoja na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa aliyetiwa hatiani kwa kuchezea taarifa za Bunge kuhusu sakata la fedha za matibabu zilizotumiwa na Hassy Kitine.

Mwingine ni Philemon Ndesamburo ambaye aliadhibiwa na Bunge baada ya kushindwa kuthibitisha kauli yake kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, aliwaambia wafanyabiashara wakitaka mambo yao yawanyookee, wajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa kuzingatia mlolongo huu wa matukio ya adhabu zilizokwishawahi kutolewa bungeni, kambi ya wabunge vijana imepanga kumshinikiza Spika kuiamuru Kamati ya Kanuni za Bunge kuipitia upya adhabu hiyo na kwamba matokeo yake yatachambuliwa ili kuona kama kamati hiyo inafanya kazi kwa kufuata haki.

Mmoja wa wabunge vijana kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, alilieleza gazeti hili kuwa kambi ya wabunge vijana haikubaliani na msimamo wa Spika na inataka adhabu ya Zitto ipitiwe mpya kwa sababu hata Rais Jakaya Kikwete ameonyesha kwa vitendo kutokubaliana na adhabu hiyo.

“Adhabu aliyopewa Zitto ilitokana na hoja yake ya kutaka mkataba wa Buzwagi uchunguzwe, wabunge wa CCM waliungana kumpinga kwa sababu wanazozijua na ambazo sasa Watanzania wengi wanazijua, wakamsimamisha.

“Lakini ninaamini walimsimamisha kwa sababu za kiitikadi, ingawa mimi sikuwepo, hawa wamemsimamisha, rais kaunda kamati ya kupitia upya mikataba ya migodi ya madini ukiwemo huo wa Buzwagi, haijalishi hata kama kaunda kisiasa au kwa dhamira ya dhati, kinachoonekana hapo ni kwamba rais amekubaliana na hoja ya Zitto.

“Na kama rais amekubaliana na hoja ya Zitto, maana yake ni kwamba adhabu aliyopewa na Bunge haikuwa sahihi, sasa Bunge linapaswa lijitizame upya, vinginevyo kulishitaki ni sawa tu.

“Kwa Spika, kumuita mbunge mtoto ni jambo la ajabu sana kwa mtu tunayemuheshimu kama yeye, utoto wa mtu haupimwi kwa umri bali hoja zake, wanaomsikiliza Zitto akitoa hoja wanajua kama ni mtoto au la… katika hili atauona utoto wetu,” alisema Halima kwa kujiamini.

Pamoja na hayo yoye, kivuli cha Rais Kikwete nacho, ambacho kimekuwa kikiyaandama maamuzi ya Spika, kinaonyesha kumuweka katika hali ngumu zaidi kwa vile kimekuwa kikipingana naye kila mara.

Kwa uchache, Rais Kikwete alionekana kutofautiana na Spika pamoja na wabunge mapema mwaka jana, pale walipokosoa madai yao ya nyongeza ya mishahara na marupurupu wakati taifa likiwa katika hali ngumu ya chakula na ukosefu wa umeme.

Kikwete pia ameonekana kutofautiana na Spika na wabunge wa CCM baada ya kuunda kamati ya kupitia upya mikataba ya madini, jambo ambalo lilikuwa likidaiwa na Zitto kabla ya kusimamishwa na wabunge wa CCM.

Wafuatiliaji wa masuala ya Bunge wanaeleza kuwa iwapo Spika Sitta hatatumia busara zaidi katika kutatua mgogoro huu na kambi ya wabunge vijana, na hivyo kusababisha kufarakana nao, atakuwa amebakia peke yake jambo ambalo ni hatari zaidi kwa siasa za hapa nyumbani.

Wengi wamemtaka akumbuke kazi kubwa iliyofanywa na wabunge hao, wakati wa sakata lake na Mbunge Malima, ambapo baadhi ya vigogo ndani ya chama chake waliamua kumshughulikia huku wakiwa na dhamira ya dhati ya kumuengua katika Uspika.

Sitta aliokolewa na kambi ya wabunge vijana, baada ya Mdee kuwasilisha hoja bungeni, akilitaka Bunge kumuadhibu Malima kwa kumdhalilisha mbunge na kiti cha Uspika, hoja ambayo iliua nguvu za wapinzani wa Spika na kumpa mwanya wa kukwepa mashambulizi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.

Hizi News tu...!It is full of subjective insuniation, Nit picking!
 
Aidha, akizungumzia madai kwamba alisambaza barua yake hiyo kwa vyombo vya habari na katika mtandao wa ‘internet', jambo ambalo Spika amekaririwa akieleza kuwa ni kinyume cha taratibu za Bunge, Zitto alisema hilo si kweli kwa sababu alitoa nakala kwa kiongozi wa upinzani bungeni na kwa katibu wa Bunge tu.


Haya ndio mambo yanayo washushia hadhi wanasiasa tunao amini kuwa ni "machachari" sasa hapa ana kana kitu gani?

Zitto kwanini unakosa gutts za kusema ni kweli umesambaza barua hii kwenye mitandao?

Kuna hatari ya kuruka maji na kukanyaga kinyesi halafu tukayatafuta maji kunawa!
 
.....na tangu nilipoadhibiwa nilikuwa kimya, nimetumikia kifungo kimya, hiyo yote ni kwa sababu ya kumuheshimu tu Spika, ni unyenyekevu wa hali juu," alisema Zitto.
Zitto this is so dissapointing, its obvious huyo Spika hakuheshimu, heshima ninavyojua inatakiwa isiwe one way traffic.Una potential ya kuwa mkuu wa nchi lakini kama unashindwa kutuonyesha kuwa una uwezo wa kupigania haki yako binafsi pale ambapo unaamini umeonewa kwa kigezo tu cha kumuheshimu mtu, what message are you sending out?tutaamini vipi kuwa utakuwa na uwezo wa kupigania haki za majority wanyonge?hutaendelea kukaa kimya kwa kigezo hicho hicho cha kuwaheshimu wanaotuonea? Au ndio umeanza kuingiwa na woga? Au ndio posho za za Kamati zimeanza kuku soften? Pse give us another reason.
 
.....na tangu nilipoadhibiwa nilikuwa kimya, nimetumikia kifungo kimya, hiyo yote ni kwa sababu ya kumuheshimu tu Spika, ni unyenyekevu wa hali juu,” alisema Zitto.
Zitto this is so dissapointing, its obvious huyo Spika hakuheshimu, heshima ninavyojua inatakiwa isiwe one way traffic.Una potential ya kuwa mkuu wa nchi lakini kama unashindwa kutuonyesha kuwa una uwezo wa kupigania haki yako binafsi pale ambapo unaamini umeonewa kwa kigezo tu cha kumuheshimu mtu, what message are sending out?tutaamini vipi kuwa utakuwa na uwezo wa kupigania haki za majority wanyonge?hutaendelea kukaa kimya kwa kigezo hicho hicho cha kuwaheshimu wanaotuonea? Au ndio umeanza kuingiwa na woga? Au ndio posho za za Kamati zimeanza kuku soften? Pse give us another reason.

Kana,

Mi nafikiri Zitto alifanya vyema kuonyesha maturity kuliko hata hao "wazee" wanaotakiwa kuwa nayo zaidi kwa mujibu za utamaduni wetu.Zitto alichofanya ni kumpa Spika the benefit of doubt, sasa Spika mwenyewe kwa lugha yake iliyojaa kejeli na arrogance anajinyonga kwa kujionyesha kuwa hastahili kupewa heshima.

Nafikiri kulikuwa na haja ya kuonyesha unyenyekevu, if only kutowapa msemo wa kuwa "Zitto fedhuli" au he is immodestly cocky.Kwa ku-extend gesture ya heshima with the highest discipline, even when wronged Zitto has my highest respect regardless of other details.In a civilized system,you just cannot fail him for that in my humble opinion.

Now the Speaker failed the test of civilization, do not join him.
 
Kana,

Mi nafikiri Zitto alifanya vyema kuonyesha maturity kuliko hata hao "wazee" wanaotakiwa kuwa nayo zaidi kwa mujibu za utamaduni wetu.Zitto alichofanya ni kumpa Spika the benefit of doubt, sasa Spika mwenyewe kwa lugha yake iliyojaa kejeli na arrogance anajinyonga kwa kujionyesha kuwa hastahili kupewa heshima.

Nafikiri kulikuwa na haja ya kuonyesha unyenyekevu, if only kutowapa msemo wa kuwa "Zitto fedhuli" au he is immodestly cocky.Kwa ku-extend gesture ya heshima with the highest discipline, even when wronged Zitto has my highest respect regardless of other details.In a civilized system,you just cannot fail him for that in my humble opinion.

Now the Speaker failed the test of civilization, do not join him.
Pundit,
This wasnt just a matter of civilisation, I dont see it that way. Haka ka utamaduni ka "hewala bwana" ndio kametufikisha hapa tulipo leo hii, kama unaamini hujatendewa haki yako,you should put up a good fight bila kujali muhusika on the other end.Sometimes you have to get nasty and show them that you cant be messed about, ukikaa kimya- im sure they will do it again and again, hata kama sio kwako wewe watamfanyia huu ushenzi mbunge mwingine.
 
Sasa hapo ndiyo angewapa msemo ya kuwa "Zitto amevimba kichwa".Mimi ninavyoliona hili swala sasa hivi ni swala kubwa kuliko Zitto.It is about reason vs arrogance.You cannot defeat arrogance by arrogance because you will not establish the moral higher ground to distinguish the two.You defeat arrogance by reason, which is exactly what Zitto did.Mambo ya bunge yana kawaida ya kuwa na some messy bureaucracy, muheshimiwa alihitaji time ku-regroup and make a come back.

Hii ni classic "Rocky" move au "rope a dope" unampa adui ushindi wa battle au raundi yeye anafikiri ameshinda vita au game nzima.Halafu una-unleash a ferocious attack.Kwa sababu Sitta amejionyesha hafai kuheshimiwa, sasa ni wakati wa kum-expose yeye na his weak suppositions (such cheap shots kama "watoto",c'mon man, did this guy really say that shyt? if so where is the outrage?)
 
Masatu una uhakika gani kuwa wabunge tuliowachaguwa ndio walioshinda kura? Au unataka kutuambia kuwa hujui kama kuna wabunge walioingiwa kwa nguvu za system? na sina maana wale wa upendeleo, bali ni wale walio ingizwa kwa kura za wizi na mizengwe.
 
Wajameni natanguliza heshima,

Kuna analysis alifanya Mzee Shivji kuhusu hizi taratibu za bunge. Kwa mtu anayejua ilipo tunaomba link ili kwa wale waliosahau tujikumbushe.
Mimi ninamsapoti Kabwe 100% especially kwa ajili ya kuweka precedent. Na wale waliofananisha hii move ya Kabwe na Chess na Draught, perfect analogy.

Kuhusu Kabwe kupeleka issue kwenye mahakama ya wananchi pale Jangwani, nadhani hakuna sababu kwa sasa. Kwa kuisukuma issue taratibu, na kufanya discussion iwe ndefu, ndivyo ambavyo mapungufu ya wabunge, spika, na viongozi wengine yanaendelea kuwa FRESH katika vichwa vyetu. 2010 ni mbali kidogo, mengi yanaweza kutokea. Sijui uchaguzi mkuu ungefanyika leo matokeo yangekuwa vipi...
Niliposoma barua ya Kabwe, ilinikumbusha msemo wa Kipare kwamba huwezi kusema "Baba ni mwongo", unatakiwa kusema "Baba anachekesha.."

Keep it up Kabwe, tusaidie vilaza kuzifahamu kanuni na taratibu za Bunge, maana hii inakuwa kama elimu mpya kwetu pamoja na wabunge wetu. Miaka yote nilipokuwa nasoma UD sikuwahi kusoma "By Laws" {help pls with spelling}, nafikiri wengi wa wabunge wetu hawasomi "by laws" za Bunge na hoja kama hizi zinasaidia kupeleka watu shule.
 
I was watching this movie "Amazing Grace", it is about the abolition of slavery and how William Wilberfoce had to go through insurmountable odds to advance that noble cause at a time when Brittannia was funded by the bloody labor od slaves in the sugar plantations of West Indies and the people had less than apathy towards slavery, it was thought to be good business.

For some reasons I saw parallels between Wilberfoce in the House of Commons and Zitto in our supposedly "august" Bunge, the astronomical odds against progress,the discouraging lack of mass involvement, the zeitgeist, they all conspired against Wilberfoce and are now seemingly conspiring against Zitto.But in the end, with determination, hard work and persisten resolution through time and a little help from a few good friends the nobler cause always triumphs.

We shall establish a better nation based on principled and progressive ideas, and do away with the oppressive "entitled" oligarchy through a reasoned attack based on the education and mobilization at the grassroot level.

Do your part, the first step is speaking up as MP Zitto did.
 
Utoto wa Zitto uko wapi?

Padri Privatus Karugendo Januari 9, 2008
Raia Mwema

KABLA ya kwenda mbali, niweke sawa jambo hili; kwamba kuna watoto wenye akili ya watu wazima na kuna watu wazima wenye akili ya kitoto.

Hii inatokea pote duniani si Tanzania tu. Unakuta watoto, vijana wana hekima na busara kuliko watu wazima, na watu wazima bado wananyonya vidole na kufungwa nepi!

Mfano mtu mzima anayehongwa milioni moja na kuachia mabilioni yakaondoka, au mtu anayeteketeza maslahi ya Taifa na kufumba macho wakati rasilimali za nchi hii zinaporwa kwa vile amehongwa vijisenti, huyo bado ananyonya kidole na kufungwa nepi! Ni mtu mzima, hata kama ana miaka 50-60, bado anakuwa na akili za kitoto!

Kama Zitto Kabwe ni mtoto basi ni kati ya watoto wenye hekima na busara kuliko watu wazima; atakuwa ni mtoto mwenye akili ya watu wazima!

Nilikuwa sijaisoma barua ambayo Zitto, amemwamndikia Spika Sitta. Niliposikia kwenye vyombo vya habari kwamba Zitto, alikuwa amechukua hatua za kitoto, nilijawa na wasiwasi. Zitto, ninayemfahamu amevuka hatua ya kunyonya kidole, si mtu wa kufungwa nepi; umri wake ni mdogo sawa, lakini ni ule wa wanamapinduzi wote duniani, umri wa bwana Yesu Kristu.

Hata Mwalimu Nyerere, wakati anapigania uhuru wa Tanganyika, alikuwa kijana mdogo. Joseph Kabila, ni kijana mdogo, lakini anaweza kuiongoza DRC pamoja na matatizo makubwa ya nchi hiyo. Ipo mifano mingi wa vijana wanaopambana kiutuuzima.

Nimepata bahati ya kusoma barua hiyo kwenye gazeti hili toleo lililopita. Nimeisoma zaidi ya mara tano, nikitafuta Utoto wa Zitto. Nimejitahidi sana kuona ni wapi kijana huyu kakosea. Maneno yake yote yamepimwa vizuri, kanuni za Bunge, amezizingatia. Kosa lake liko wapi? Kumwandikia Spika au barua ya Spika kuonekana kwenye mtandao? Vyombo vya habari vilimnukuu Spika Sitta, akiilalamikia barua ya Zitto, kwamba kwa barua hiyo Zitto hakuonyesha ukomavu wa kisiasa na ni dalili za ‘Utoto’.

Vyombo vya habari vyenye uchokozi viliiweka hivi ‘Spika Sitta amsikitikia Zitto’. Baada ya kuisoma barua ya Zitto, nimejiuliza maswali: je ni utoto wa Zitto au ni kuchoka kwa Sitta?, je ni utoto wa Zitto au ni dalili za Sitta kushindwa kusoma alama za nyakati?

Inaonekana Spika Sitta, anaelekea kuchoka na kushindwa kusoma alama za nyakati. Juzi juzi alikuwa mtu wa kwanza kupinga ripoti ya utafiti wa REDET kwamba hadhi ya Bunge imeshuka. Vyombo vya habari vilimnukuu akisema: “ Sikubaliani na matokeo ya utafiti huo. Mimi nina uzoefu wa siku nyingi katika masuala ya Bunge. Inashangaza sana wakati huu Bunge lina kanuni mpya zinazoimarisha utendaji wake, lakini utafiti unaonyesha wananchi hawana imani.

Bunge limekwisha kukamilisha kufanya mabadiliko katika kanuni zake ambazo ni tofauti na za awali. Kanuni za sasa zinalipa nguvu zaidi Bunge katika utendaji. Inashangaza sana haya matokeo. Kanuni zetu ni mpya na ni nzuri.

Inawezekana hii taasisi (REDET) iliyofanya utafiti ni chombo tu kinachojitafutia umaarufu”.

Kama si kuchoka ni nini? Spika Sitta, anasema Bunge lina kanuni mpya, na wakati huo huo anasema Barua ya Zitto ni ya kitoto na ni ya mtu ambaye hakukomaa kisiasa. Labda tatizo ni kwa vile Zitto, anasema kwamba ikibainika Bunge, lilikosea, limwombe radhi. Bunge, lenye kanuni nzuri ni lazima lifanye hivyo! Inawezekana Bunge, halikosei? Bunge linaundwa na malaika watupu? Tunajua kabisa kwamba Bunge ni chombo kitukufu, lakini linaundwa na watu, linaundwa na vyama vya kisiasa. Bunge, letu karibia ni la chama kimoja, chama ambacho kinashutumiwa kuiba kura wakati wa uchaguzi, kinashutumiwa kwa rushwa na ufisadi; wingi wa wabunge wa chama hiki ndani ya Bunge unaweza kulisukuma Bunge, kufanya makosa. Mfano mzuri ni kesi ya Zitto.

Kama Spika Sitta, asingekuwa mwanachama wa CCM, kesi ya Zitto, isingekuwa kama ilivyokwenda. Ilionekana wazi, hata kwa mtu mwenye akili ndogo kabisa, kwamba Wabunge wa CCM na wakiwa na Spika wao, walikuwa wakitetea maslahi ya chama chao, si maslahi ya Taifa.

Zitto, alikuwa akitetea maslahi ya taifa kwa kuhoji mkataba wa Buzwagi. Lakini mjadala uliofuata, ulitoa picha ya CCM kupambana na wapinzani. Hata wabunge wa CCM, tuliowazoea kuwasikia wakitetea maslahi ya Taifa, walifunga midomo yao wakati wa mjadala wa Buzwagi. Waliweka chama mbele na Taifa nyumba. Aibu!

Nafikiri hapa kuna somo. Kuna haja ya Katiba mpya. Na kuangalia namna mpya ya kumpata Spika wa Bunge. Kuna haja Spika wa Bunge, kutoka nje ya vyama vya Siasa. Tukio kama la Zitto na sasa matukio ya Kenya, yanatufundisha. Spika wa Bunge na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ni wawe ni watu wasiokuwa na upande wowote.

Wawe ni watu wanaoheshimika katika jamii, watu wasiokuwa na uchu wa mali na madaraka, watu wenye uzalendo unaozidi mipaka. Tumejifunza kwamba kumbe Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kama ameteuliwa na Rais aliye madarakani au kama ni mwanachama wa chama tawala, basi atatenda kwa maelekezo ya Rais au maelekezo ya chama chake.

Ijionyesha wazi katika Katiba, kwamba Spika wa Bunge na Mweneyekiti wa Tume ya Uchaguzi ni watu wasiofungamana na upande wowote.

Yaliyotokea Kenya, yanaweza kutokea hapa. Ubabe wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya Samuel Kivuitu wa kutangaza aliyeshindwa, kwa vile yuko madarakani, hauna tofauti na kile anachokiita Zitto ‘abuse of majority’. Adhabu yake ilitolewa ‘kiubabe’ na Bunge, kwa vile ‘majority’ ni wabunge wa CCM.

Je, kesho na keshokutwa ikijitokeza CCM kushindwa, watakubali hawa? Si watakuwa kama Mwai Kibaki? Hivyo tusimpuuze Zitto. Tumsikilize na kuhakikisha mbegu mbaya za kutuiingiza kwenye machafuko zinachambuliwa na kutupwa motoni!

Kwenye barua yake, Zitto anamwabia Spika Sitta:

“Mheshimiwa Spika, kwa misingi ya kanuni zetu nilizonukuu hapo juu ninaleta kwako maombi ili Kamati ya Kanuni za Bunge ipitie upya adhabu niliyopewa na Bunge ambayo mimi ninaamini haikuwa halali, haikufuata Kanuni za Bunge, haikuzingatia tamaduni za Bunge (maamuzi ya Bunge yaliyopita) na kubwa zaidi haikunipa nafasi ya kujitetea”.

Utoto uko wapi kwenye hoja hiyo hapo juu? Kama kanuni zilifuatwa, Spika Sitta, amjibu Zitto. Kama ni kweli Zitto, alipata nafasi ya kujitetea, Spika Sitta, aonyeshe wazi. Kama ni kweli kanuni hazikufuatwa, ieleweke. Hadhi ya Bunge, itapanda, endapo wananchi watashuhudia jinsi kila kitu bungeni, kinavyofanywa kwa ukweli na uwazi. Ujana wa mbunge, jinsia ya mbunge au chama cha mbunge kisiwe kigezo cha kumnyanyasa na kumdhalilisha.

Zitto, anaendelea kujieleza:”Mheshmiwa Spika, mimi kama Mbunge katika Bunge lako ninaamini ya kwamba adhabu niliyopewa ilifikiwa kwa shinikizo la kiitikadi na hata kufikia kundi moja la wabunge kutumia vibaya wingi wao bungeni (abuse of majority) na kuniadhibu bila kufuata kanuni za Bunge”.

Utoto uko wapi kwenye hoja ya hapo juu. Bahati nzuri Shughuli za Bunge hutangazwa moja kwa moja. Sote tuliona ushabiki na shinikizo la kiitikadi. Haiwezekani kwamba hakuna hata mbunge mmoja wa CCM, ambaye hakuguswa na mkataba wa Buzwagi.

Haiwezekani kwamba wabunge wote wa CCM, walifurahishwa na mkataba wa Buzwagi. Inawezekana kwamba walikuwa hawajafuatilia, lakini baada ya maelezo ya Zitto, kwa nini hawakuchukua hatua ya kufuatilia?

Zitto, bado anaonekana ni mtu mwenye busara kubwa, maana kwenye barua yake anaonyesha heshima aliyonayo kwa Bunge: “ Mheshimiwa Spika, licha ya kwamba nina nafasi na haki ya kuomba chombo kingine cha dola kama Mahakama kupitia adhabu hii, nimesita kufanya hivyo ili kulipa Bunge nafasi ya kujikosoa”.

Kuna utoto kwenye maneno hayo hapo juu? Ni kweli Zitto, ni mdogo wa umri, lakini mawazo yake na matendo yake ni ya mtu mzima, tena mtu mzima mwenye hekima na busara. Hoja zake zinaonyesha uzalendo wa hali ya juu. Kumpuuza ni kujiabisha, na kwa mambo kama hayo hadhi ya Bunge itaendelea kudidimia.

Kinachojionyesha wazi kwenye barua ya Zitto, ni kwamba Spika Sitta, alishindwa kulisimamia vizuri swala lake:

“Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, wewe Mheshimiwa Spika ndiye unapaswa kuhakikisha kuwa utaratibu Bora unafuatwa bungeni..Kanuni 58(1)”.

Malalamiko ya Zitto, yanaonyesha wazi kwamba kama Spika Sitta, asingekumbwa na kirusi cha ushabiki na itikadi, adhabu iliyotolewa dhidi yake isingetolewa.

Ukweli ulio wazi, ambao inashangaza sana Spika Sitta, hauoni, ni kwamba hadhi ya Bunge, imepungua kwa kiasi kikubwa baada ya adhabu ya Zitto. Wengi waliofuatilia matangazo hayo walikatishwa tamaa na uamuzi wa Bunge wa kumsimamisha Zitto.

Madini ni sekta nyeti ambayo imekuwa ikilalamikiwa. Zitto alikuwa akihoji sekta ya madini juu ya usiri wa Mkataba wa Buzwagi. Kwa vyoyote vile angekuwa na mvuto kwa Watanzania wengi wanaotilia shaka zoezi zima la uchimbaji wa madini. Hoja zake zilikuwa na ushawishi mkubwa na hadi leo hii hazijajibiwa ipasavyo.

Ingawa watu hawakufahamu Kanuni za Bunge, kwamba hoja haiwezi kutolewa juu ya hoja, kwa akili tu za kuzaliwa, waliweza kuuona uonevu aliotendewa Zitto.

Yeye analifafanua vizuri: “Mheshimiwa Spika, Bunge lina taratibu za kuleta hoja bungeni. Taratibu hizi zimefafanuliwa kinagaubaga katika Kanuni za Bunge na zimeanisha wazi kabisa ya kwamba hoja haiwezi kutolewa juu ya hoja nyingine na kwamba muda wa kutoa taarifa za hoja umewekewa taratibu ndani ya Kanuni za Bunge”.

Kwa kesi ya Zitto, hoja ya kumsimamisha ilitolewa juu ya hoja yake mwenyewe na kuamuliwa hapo hapo!

Ni bora Mheshimiwa Spika Sitta, aanze kusoma alama za nyakati. Enzi za Bunge la chama kimoja, zimepita. Enzi za mtu kuonewa, kudhalilishwa akakaa kimya zimepitwa na wakati. Enzi za kuwasikiliza wazee na kuogopa kuwakosoa zimepitwa na wakati. Enzi za chama kimoja zimepitwa na wakati. Kwa vile Taifa letu liliamua kufuata siasa ya vyama vyingi, hakuna njia nyingine zaidi ya kuwa na Bunge, linaloendana na mfumo huu mpya.

Spika Sitta, ana nafasi ya pekee kulibadilisha Bunge likawa na sura mpya. Kama anataka Tanzania, imkumbuke, basi afanye mabadiliko makubwa ndani ya Bunge letu. Juhudi zake za kutunga kanuni mpya za Bunge, ziendane na juhudi za ushawishi wa Katiba mpya ili siku zijazo Spika wa Bunge awe ni mtu asiyefungamana na chama chochote cha kisiasa.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa S. L. P. 114 Magu, Mwanza. Simu: 0754 633122
 
Vitu vingine mnarudishsa mijadala nyuma. Ebu liachceni hili suala lijadiliwe huko bungeni tusikie mwisho wake. Zitto wote tunampenda lakini hatuwezi kuwa "yes" people kwa kila atakachofanya. Hii ni kumpa big head huyu kijana. Kuna mazuri mengi anayafanya lakini yasitupe kiburi sana, ebu tusikie kamati ya maadili ya bunge itafanya kazi gani na barua hiyo ya Zitto.
 
Vitu vingine mnarudishsa mijadala nyuma. Ebu liachceni hili suala lijadiliwe huko bungeni tusikie mwisho wake. Zitto wote tunampenda lakini hatuwezi kuwa "yes" people kwa kila atakachofanya. Hii ni kumpa big head huyu kijana. Kuna mazuri mengi anayafanya lakini yasitupe kiburi sana, ebu tusikie kamati ya maadili ya bunge itafanya kazi gani na barua hiyo ya Zitto.

Kamati ya maadili ya bunge itafanya kazi yake, na sisi kama Watanzania tuna haki ya kulijadili hili swala bila kusubiri maamuzi ya bunge. Hili bunge uchwara unafikiri litajadili swala hili bila kupatwa na kirusi cha CCM na kuweka mbele maslahi ya chama chao badala ya kanuni za Bunge na maslahi ya Tanzania!? :confused:

Mpaka hii leo wameshindwa kuipitia mikataba siri ya madini kwa manufaa Watanzania wote, leo hili la Mtanzania mmoja wataweza kulitendea haki wakati walishindwa kutenda haki kwa Watanzania 39milioni na rasilimali zao!? :confused:

Fumbua macho uone hali halisi.
 
Ndugu Bubu~
Nafikiri una data nyingi lakini naomba ziambatane na topic zinazozungumzwa. Mra nyingi ninakuwa na imani na infor zako, maana nyingi zina fact. Lakini hii ya kumtetea Zitto kila kukicha nafikiri tupunguzer speed. Zitto naye ni mtu kama wewe hivyo kuna mahali atateleza na kuna mahali atafanikiwa. Kwa hili la barua kwa spika bado ninaona kwamba amekurupuka lakini sitaki kuongea sana maana lipo mikononimwa kamati. Likitoka huko sasa mjadala utafunguliwa rasmi either kuilaumu kamati kwa maamuzi au kuipongeza. Au kumsupport Zitto (which I know you will) au Kumsupport Spika (Mzee wa kanuni) lakini yote haya tusubiri. Huwa sipendi kujump on conclusion.
 
Kwa hiyo haturuhusiwi kujadili suala hili mpaka kamati ya maadili imalize kulipitia!? :confused:

Tangu lini kujadili swala fulani kukawa ni kujump to the conclusion!?
 
The record must show how the people feel.What is a forum without discussion?

It is like life without breathing.
 
kujadili mijadala ya kitaifa ni dalili mojawapo ya taifa lililo hai. Ni dalili ya kukua kwa demokrasia.

Toka Mwanzo mimi niliweka wazi suala hili kwamba siyo ZITO versus BUNGE katika sarakasi za nani zaidi, Zitto mwenyewe nadhani anafahamu kwamba kufanya hivyo ni political suicidal, bali hili suala ni Zitto versus kanuni na taratibu, kwamba lazima tuweke rekodi sawa kwa manufaa ya kizazi hiki na kizazi kijacho.lazima tuweke reference juu ya maamuzi mbalimbali ambayo vizazi vijavyo wata refer,tutakuwa hatujajifunza somo iwapo tatizo kama litajitokeza baadae halafu watu washindwe kuchukua maamuzi mazuri.

Wanaofikiri kwamba motive ya kujadili suala hilo ni Zitto as Zitto wanakosea vibaya sana,hata yeye Zitto mwenyewe ninaimani anafanya haya kwa ajili ya manufaa ya yeye(politically) na Taifa ambayo ni mambo mema.

Hili jambo haliwezi kukaliwa kimya mpaka suluhisho lipatikane, otherwise tukilikalia kimya tutatoa picha mbaya sana kwa baadhi ya Watawala kwamba watanzania wakisema leo basi kesho wanasahau, kitu ambacho ni kibaya mno kwa mustakbali wa taifa.

Kanuni za Bunge ni lazima zifuatwe na zirekebishwe ikibidi ili Bunge lifanye kazi ya kuisimamia Serikali vizuri
 
Back
Top Bottom