Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,970
- 10,462
Nimpongeze class mate wangu mheshimiwa Zitto kwa barua hiyo, lazima ahakikishe kuwa haki inatendeka. Binafsi sitarajii sisiemu kama chama ama wabunge wake, ama spika kuomba radhi na kuonesha kuwa walikosea katika suala zima la adhabu kwa mbunge huyu, hata kama kosa lao limeoneshwa wazi na Kikwete, kwamba wapi walichemka na inabidi warekebishe. Kamati waliyoipinga bungeni ndio hiyo Kikwete kaiunda kwa mlango wa nyuma. Sio hulka ya sisiemu kujikosoa, kwa mtazamo wao, wao wako sahihi kila wakati.
Pamoja na hayo, na uwingi wao katika bunge hii haumfanyi Zitto kutokupeleka barua yake kwao kwa kuhofia kuwa itatupwa kapuni, hata kama wataikalia ama hawataifanyia chochote, cha muhimu ifike kwa wahusika. Hatuwezi kufika popote kama tutakuwa na mawazo mgando na ya kukata tamaa kama ya mheshimiwa Masatu katika pointi yake hapo juu, kwamba Zitto anapoteza muda. Hakuna muda unaopotea hapo, lazima haki itendeke.
Long live Zitto!