BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
Zitto awasha moto
Halima Mlacha
HabariLeo; Tuesday,December 25, 2007 @00:01
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameliomba Bunge kuipitia upya adhabu ya kumsimamisha, akidai kwamba imesababisha adhalilike na kushushiwa hadhi ndani na nje ya nchi. Zitto pia anataka Spika na mawaziri wengine kadhaa wachukuliwe hatua, kwa madai kwamba walinukuliwa na vyombo vya habari wakisema yeye ni mwongo bila madai hayo kuthibitishwa.
Kwa mujibu wa barua aliyomwandikia Spika wa Bunge jana (nakala yake gazeti hili inayo), mbunge huyo ametoa ombi hilo kwa kuwa anaamini adhabu hiyo haikuwa halali kwake kutokana na kutofuata kanuni za Bunge na pia kutopewa nafasi ya kujitetea. Mbunge huyo alisimamishwa kazi za Bunge kwa mikutano miwili Agosti 14, mwaka huu, kwa madai ya kusema uwongo dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kuhusiana na mkataba wa madini uliosainiwa nje ya nchi.
Adhabu hiyo imekwisha na anatarajiwa kuanza kuhudhuria vikao vya Bunge baadaye mwezi ujao. Zitto alifika katika ofisi ndogo za Bunge binafsi jana majira ya mchana kuwasilisha barua hiyo kwa Spika ambaye yuko safarini. Adhabu niliyopewa iliniweka katika wakati mgumu sana na hata kunishushia heshima si tu katika jamii ya Tanzania, bali katika jamii ya kimataifa. Nimekuwa nikionekana ni Mbunge mwongo
Mheshimiwa Spika licha ya kwamba nina nafasi na haki ya kuomba chombo kingine cha dola kama Mahakama kupitia adhabu hii, nimesita kufanya hivyo ili kulipa Bunge nafasi ya kujikosoa, ilisema sehemu ya barua hiyo ya Zitto. Katika barua hiyo, ambayo Zitto alikiri kuiandika, pia aliomba Bunge hilo kupitia vifungu vyote vya Kanuni za Bunge, ikiwamo kumsikiliza katika kikao cha kamati, kauli za viongozi wa Bunge na wa Tawi la Utendaji kuhusu adhabu aliyopewa ili kuona kama kanuni za Bunge na Sheria namba 3 ya mwaka 1988 hazikuvunjwa.
Alisema kama chombo hicho kikiridhika kuwa viongozi waliotajwa pamoja na hatua ya mbunge huyo kupewa adhabu ilikuwa ni kinyume na kanuni na sheria zilizopo za Bunge basi, chombo hicho kiombe radhi. Alisema Bunge lina taratibu za kuleta hoja bungeni ambazo zimeshafafanuliwa katika kanuni za chombo hicho na kuainishwa wazi kwamba hoja haiwezi kutolewa juu ya hoja nyingine.
Kanuni zetu zimesema wazi kabisa katika kifungu cha 59-3 kuwa iwapo mbunge anashutumiwa uongo bungeni au kutoa lugha ya kuudhi, atapewa muda ili kuthibitisha analoshutumiwa mheshimiwa Spika .sijawahi kupewa muda wa kuthibitisha chochote, alisema Zitto katika barua hiyo.
Alisema muda wa kuwasilisha hoja yake, viongozi wa Bunge waliueleza kama ndio muda aliopewa kuthibitisha maneno yake, muda ambao aliouomba kikanuni kuleta hoja yake binafsi na haukuwa wa kuthibitisha jambo lolote.
Alisema maamuzi ya kumsimamisha kwa kusema uongo bungeni yalimdhalilisha binafsi na mbele ya jamii na kudunisha utu wake. Adhabu niliyopewa iliniweka katika wakati mgumu sana na hata kunishushia heshima si tu katika jamii ya Tanzania hata kimataifa.
Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved