Zitto Kabwe: Tukemee wabakaji kusamehewa kiholela

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameonekana kutofurahishwa na uamuzi wa Rais Magufuli kusamehe wafungwa ambao ni wanamuziki mashuhuri, Nguza Viking (Babu Seya) na mwanaye 'Papii Kocha'.

Tangu utangazwe msamaha huo, Zitto amekuwa akiandika na kutoa kauli zinazoonesha kupingana na jambo hilo licha ya Rais kuwa na mamlaka kikatiba kumsamehe mfungwa yeyote akiona inafaa..

Miongoni mwa kauli zake huko Twitter;

"I have read judgement that convicted Babu Seya and son. And judgements at the high court appeal, appeal at court of appeal and petition at African Court. I am appalled by decision to pardon convicted rapists. Devastated by statements to congratulate such a decision" ZZk.

"Waliozomea na kuzodoa ahadi ile walikuwa sahihi. Wanaomzomea Rais kwa kutoa msamaha wapo sahihi pia. Hakuna sababu kuzodoana. Tukemee wabakaji kusamehewa kiholela" ZZK.
Kwa hili kwa mara ya kwanza namuunga mkono Zitto,hii ni tabia mbaya ambayo viongozi wakiendeleza kwa kuangalia umaarufu wa mfungwa basi italeta matabaka kwenye maamuzi ya haki ambayo ndio msingi wa haki,je ni wangapi wenye makosa kama ya Babu Seya wamesamehewa?na je wale wahanga wa babu Seya wanajisikiaje .Kumsamehe mbakaji wa watoto kunaleta picha isiyo nzuri kwa ustawi wa jamii.Nashangaa wanaoshangilia uamuzi huu wa raisi wa kumwachia babu Seya wao wanaangalia umaarufu na muziki badala ya kuwahurumia watoto ambao tayari maisha yao yameharibiwa milele,tumesahau kwamba sote tu wazazi,sijui ungekuwa ndio mzazi wa wale watoto waliofanyiwa ubaya na babu Seya ungejisikiaje na haya maamuzi.Kwa hili namuunga mkono Zitto na nimehuzunishwa sana na maamuzi ya Mh raisi.
 
Halafu hili swala la kubakwa na kulawitiwa tena watoto wengine class 1. Najaribu kuwaza kwamba ikiwa MTU mzima hawezi kuhimili the first time, hivi mtoto si anakufa kabisa? Kweli maumbile Yale yaweze kuhimli MTU mzima halafu azoee kabisa? Najaribu tu kuwaza huko kubakwa na kulawitiwa. Ingekuwa kunajisiwa hapo ningeweza sema inawezekana. Sijui lakini ILA omba sana wewe mwanaume yasikukute haya maana ni mazito mno. Mimi nshawahi kusingiziwa na vibinti kuwa nilivitaka kimapenzi kisa vilinikosea. Vilinidhalilisha sana na kidogo yanipate yakunipata maana watu walishalishikikila kidedea lakini Mungu alisimama upande wangu.


Pole sana mkuu. Nimekusoma vizuri sana.
 
Ni huzuni kubwa sana pale unapoona wabakaji na walawiti wa watoto wadogo wanapopokelewa Kama mashujaa.
Watanzania wengi hawajitambui.
 
Naungana na ZZk,nimefadhaika sana,Nyie mnao shangilia kama mna watoto,imagine leo mtoto wako atoke shule akuambie amebakwa na mwalimu utafanyaje?je akiwa amelawitiwa?afu mwalimu asifanywe kitu?

Imagine wewe ni Mwalimu halafu watoto baada ya kutoka shule wakakusingizie kwa wazazi wao kuwa umewabaka au umewalawiti kisha ukafungwa jela kifungu cha maisha na familia yako kumbe kuna kitu nyuma ya pazia haki yako ha familia yako utakuwa wapi? Hili jambo bwana anayejua ukweli ni babu seya mwenyewe na wale wahanga waliodai kubakwa na Mungu aliyejuu, wale watoto ni watu wazima kwasasa wanajua ukweli kuhusu suala la babu seya na familia yake kama kweli babu seya aliwabaka pamoja na watoto wake basi mungu aisamehe familia ya babu seya na kama hawakuwabaka basi mungu awasamehe wale na siwezi sema nafsi zao ziwahukumu kwakuwa walikuwa watoto kipindi kile na mtoto ni kana benders hufwata upepo unakoelekea
 
Imagine wewe ni Mwalimu halafu watoto baada ya kutoka shule wakakusingizie kwa wazazi wao kuwa umewabaka au umewalawiti kisha ukafungwa jela kifungu cha maisha na familia yako kumbe kuna kitu nyuma ya pazia haki yako ha familia yako utakuwa wapi? Hili jambo bwana anayejua ukweli ni babu seya mwenyewe na wale wahanga waliodai kubakwa na Mungu aliyejuu, wale watoto ni watu wazima kwasasa wanajua ukweli kuhusu suala la babu seya na familia yake kama kweli babu seya aliwabaka pamoja na watoto wake basi mungu aisamehe familia ya babu seya na kama hawakuwabaka basi mungu awasamehe wale na siwezi sema nafsi zao ziwahukumu kwakuwa walikuwa watoto kipindi kile na mtoto ni kana benders hufwata upepo unakoelekea
Mkuu mahakama zote zinisingizie mimi tu?unajua hii kesi imepitia mahakama ngapi?Au ushabiki wa dansi unakusumbua?Kwa hiyo hawa wazazi wameambiwa na huyo mnayemdhani wafanya hii conspiracy?
 
Miaka 14 waliyokaa jela kama kuna watoto waliobakwa sasa watakuwa wamezidi miaka 18. Kama ni hivyo je haitakuwa jambo jema sasa wajitokeze watuambie kama kweli au magumashi? Maana sijawahi kumwona hata mmoja ambaye amejitokeza kusema Babu Seya na wanawe walimbaka. Maana huu ni wakati muafaka tuwaone ili tuwe na cha kuzungumza, vinginevyo kesi ilikuwa fake.


Nakama hawakubakwa ni busara wakamuombe babu seya msamaha tena kupitia vyombo vya habari
 
vipi yule jamaa wa songea aliyemeoa mama yake, nae huamini ?
Watu kama nyie mpo wengi,wale ni wabakaji na walawiti wa vibinti vidogo. ndio maana wao hawaongelei kesi ilikuwaje. HataYuda Iskariote angeomba msamaha mi naamini angesamehewa.
 
Swala hapa watanzania tuliowengi hatukuuamini hatia ya familia ya Babu Seya. Tuliamini kesi yao ilikuwa ya kubambikiza. Wapo wengi wamekuwa convicted kwa Kesi za kubambikiza, kwahiyo issue siyo kusamehe wabakaji, ni kuwaweka huru watu ambao hawakuwa na hatia ya kosa hilo walilohukumiwa nalo.
 
Kitendo cha kukimbiwa na viungo muhimu kwenda kuchezea chama kubwa, kimemchanganya kocha mkuu. Sasa hata chama kile kikishinda husema wamebebwa. Tumshauri asajili wengine au akiona inafaa na yeye ahamie tu hukohuko, maana chama si yeye pekee, wapo wengine watakao kiendeleza.
 
Mie kwa upande wangu nimefurah kutoka babu seya haiwezekan familia nzima ikawa wabakaji
Ila inawezekana watoto wadogo kuwalaghai madaktari, polisi na Mahakama na wao kukubali pasi na shaka kwamba walilawitiwa. Kama ndivyo basi system yetu Ina matatizo kuliko tunavyodhani kama watoto wanaweza wadanganya watu wazima na taaluma zao
 
Pia ikumbukwe Mawakili wa Chadema walishiriki kwa kiwango kikubwa kwenye utetezi wa Kesi hii kwahiyo wanajua kiini cha ndani cha Kesi ndio maana hata Mgombea wetu akawa na ujasiri wa kusema akiwa Rais atafuata taratibu husika kuwayoa gerezani. Siyo kwasababu walikuwa watu maarufu ila ni kwasababu tuliamini katika kutokuwa na hatia kwao.
 
Mpk sasa najiuliza umuhimu wa babu seya,kiasi kwamba alikua ajenda/ahadi ya mgombea Fulani,kwamba akishinda atamuachia huru (alibezwa sana hawa zaidi na upande wa Pili) lkn upande ule ule uliobeza ahadi ile ya mgombea yule Leo wanajivunia babu seya kuachiwa huru na mh Rais
 
Hiyo tabia yenu ya kufwata nyumanya kama fisi ndio inawaponza?! Hivi hamuwezagi jianzishia jambo lenu? Mpaka msubiri jambo aanzishe Mag ndio muanze kulijadili? Ina maana gani hiii kwenu?


Mkuu hah hah hah hah hah MH.JPM modo wa wengi.

Ameshavijua vichwa vinavyojiita wapinzani jinsi ya kwenda navyo.
 
Back
Top Bottom