Membe, Japo Umeonewa, Usifanye Kosa la Lowassa!, Ila CCM ya Ajabu!, Uamuzi based on Illegal Evidence ni Void Ab Initial!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,

Naomba kulianza bandiko hili kwa kutoa pongezi kwa Kamati Kuu ya CCM kufanya maamuzi magumu. Hata kama mimi binafsi sikubaliani na maamuzi hayo, lakini kitendo tuu cha CCM kufanya maamuzi magumu, hii ni plus traits kwa chama cha Mapinduzi, just being decisive, kwasababu CCM ndio imetawala nchi yetu tangu tupate uhuru, na tumefika hapa tulipofika kutokana na viongozi wa CCM ambao pia ndio viongozi wa nchi, kushindwa kufanya maamuzi magumu kwa kuogopa watu, Mwenyekiti wa sasa wa CCM, rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ameonyesha anaweza, japo sii lazima uamuzi uwe wa haki, lakini ile uwezo wa kuamua tuu na kufanya maamuzi magumu bila kuogopa, ni plus traits kwake na kwa CCM mpya, rais Magufuli angekuwa rais toka enzi za EPA, Meremeta, Deep Green, TanGold, Radar, Richmond, etc, saa hizi, tungekuwa tunazungumza mengine, Big Up CCM, big up CC ya CCM na Big up Mwenyekiti wa CCM, kitu muhimu katika kufanya maamuzi magumu ni kutenda haki, maamuzi magumu bila kutenda haki kutasababisha karma reprises against CCM na viongozi wake waliosimamia dhulma hii, karma huwaga haina mswalie Mtume na haijali nani ni nani!.

Huu ni ushauri wa bure kwa Benard Membe, kwanza ameonewa, pili japo umeonewa, usifanye kosa kama la Edward Lowassa la kuhama CCM kwa hasira na kujiunga na upinzani ili kuikomoa CCM, Ila CCM nayo ni chama cha ya ajabu!, kinawezaje kutoa uamuzi wa kuwaadhibu wanachama wake waliokipigania chama hicho kwa machozi jasho na damu, based on ushahidi ulipatika illegally hivyo uamuzi huo kisheria ni Void Ab Initial!.

Lakini kwasababu ni uamuzi wa kichama na sio wa kiserikali, na CCM pia kina ule udikiteta kama wa Chadema, mwanachama yoyote akikishitaki chama mahakamani, anakuwa amejifukuzisha, hivyo Membe atulie tuu na kujistaafia tuu kwa amani.

Tangu baada ya kuenea kwa taarifa ya kutimuliwa kwa Membe kutoka CCM, kinachozungumzwa kila kona ni matokeo tuu, sijasikia popote chanzo kilichosababisha yote haya kikizungumzwa, the motive behind kilichotokea, the undelying facts, and the causative factors, sana sana kwa sasa watu wanasubiri kwa hamu kumsikia Benard Membe akitoa kauli yake and what next.

Hivyo haya ni maoni yangu.
  1. Kwanza namvulia kofia na kumnyanyulia mikono juu Mwanaharakati Huru, Cyprian Musiba kwa kuwa ndiye chanzo hadi kuitikisa hivi CCM. Japo namuona kama kichaa fulani mpayukaji, bali ana impact. Whoever feeds him info, amempatia and he does his job well, hongera sana Kichaa Cyprian Musiba, Umetisha!. Mtu wa aina hii kama Musiba, ambaye ni daredevil anahitajika sana katika bunge lijalo la chama kimoja, maana ana guts za kumsema yoyote ndani ya CCM, kama kosa la Makamba na Kinana ni kutaka kutendewa haki baada ya kukashifiwa na mwana CCM kichaa mmoja, badala ya kumuonya huyo kichaa, wao sasa ndio wamekuwa wakosaji, vichaa wa aina hii ndani ya CCM ijayo watahutajika sana.
  2. Baada ya Membe kutimuliwa CCM, namshauri asifanye hasira za mkizi kwa kufanya kosa kama Lowassa kwa kukimbilia upinzani, ili kumkabili Magufuli. Lowassa mwanzo alisema asipoteuliwa na CCM atastaafu kwenda kuchunga ng'ombe, lakini baada ya kukatwa, alibadili msimamo na kuamua kuhama CCM kwa hasira na kujiunga Chadema kusaka fursa, japo aliweza na kufanikiwa kuinyanyua sana Chadema, aliweza kwasababu zile zilikuwa ni enzi za JK, hizi enzi tulizopo sasa ni enzi nyingine!, asithubutu, tuta...
  3. Benard Camilius Membe, kachero mbobezi, umeonewa, ila usiendelee kushupaza shingo na kiburi na jeuri, bali kubali matokeo, pensheni yako iko pale pale, na kama raia mwema, unaruhusiwa kufanya biashara yoyote halali, ukishupaza tuu shingo, kujifanya unataka kupigania haki yako, utaumizwa!, watayafukua yale madudu ya Quadafi na kuyatumia kukusokomeza...
  4. CCM ni chama cha ajabu sana!, kinatoaje adhabu based on datas obtained illegally?. Udukuzi ni kosa la jinai, zile voice notes zote zimepatikana kwa udukuzi ni kinyume cha sheria. Kisheria evidence obtained illegally is not admissible before the court of law, kitendo cha zile Kamati za nidhamu na CC ya CCM kumhukumu mtu based on evidence iliyopatika illegal sio kutapelekea CC ya CCM kuonekana kama a kangaroos courts fulani?. Wanachama wanadhalilishwa kisha wanapeleka malalamiko yao kwa vyombo vya chama ili wapate haki, badala ya kupatiwa haki, ndio kwanza wanadukuliwa illegally, kisha CCM inautumia ushahidi huo uliopatikana illegal kuwageuzia kibao na kuwashitaki, kisha kuwakuta na hatia, kwa chama chenye heshima kubwa kama CCM, kinatumiaje sauti zilidukuliwa kinyume cha katiba na sheria kuwaadhibu wanachama wake walio kitesekea kwa machozi, jasho na damu?.
  5. What next for Membe, atulie tuu kama Sofia Simba, CCM wakijijua makosa yao, watamuomba msamaha Membe, na maisha yataeendelea, wasipojua makosa yao, wataendelea kushupaza shingo na look a like, kangaroos courts zao, huku kutakuwa sio kuwatendea haki wanachama wao, then kutakuwa hakuna lingine ni karma tuu kutimiza wajibu wake.
Ushauri wa bure ni ushauri wa bure tuu, mtu unakuwa uko free kuufuata au kuupuuzia. Wapinzani msimshangilie Membe na kumsubiria upinzani ili aje kuwa mgombea wa Umoja wa Wapinzani against Magufuli, kama ilivyokuwa kwa Lowassa, Membe is no match to Magufuli, uchaguzi wa 2020, the one and only ambaye kwa sasa akisimama na Magufuli, Magufuli at least can feel the heat ni Zitto Zuberi Kabwe pekee. Mwanzo alikuwa Lissu lakini sasa Lissu...

Kwa uamuzi huu dhidi ya Membe, CCM ina send a very strong message kwa wanachama wake, kuwa hii ni CCM mpya, no one is indispensable, hata ukiwa nani, ukiwa tuu na mawazo tofauti, wewe sio mwenzao, hata ukifumwa tuu umesema ukweli wako, ambao hautawapendeza viongozi, unageuka adui ni ama uombe msamaha mapema, ana unakwenda na maji!. Japo hapa CCM kinaonekana ni chama shujaa, ila kiukweli hili sio jambo jema not healthy at all. Huu ni udikiteta. Kama katiba ya nchi inasema uchaguzi ni kila miaka 5, na katiba za vyama vyote lazima vifuate sheria za nchi. Kama katiba ya CCM haijazuia mwanachama kugombea urais, huo utaratibu wa kumwachia rais kipindi cha pili ni utaratibu tuu, CCM inafanya dhambi kubwa kumtimua mwanachama wake kwa kuwa na mawazo tofauti, niliwahi kusisitiza kuwa viongozi wana tatizo la managing Diversity, CCM pia kama chama kina tatizo la kutokubali mawazo tofauti hivyo japo kitatawala milele lakini viongozi wake watahukumiwa na karma za dhambi na dhulma wanazo wafanyia wanachama wao.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika - JamiiForums

Hongera rais Magufuli kuijenga CCM imara yenye uwezo wa kufanya maamuzi mugumu, CCM itaifikisha mbali Tanzania, na Watanzania wote katika mmoja wetu, tunaikubali sana CCM, na hili tutalithibitisha katika Uchanguzi Mkuu ujao, kwa kutumia wembe ule ule wa uchaguzi wa serikali za mitaa, ambao ushindi ulikuwa wa kushindo cha asilimia 99.9%, na ulikuwa huru na wa haki.

Friday night njema.
Paskali
Rejea

Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity

Timua Timua CCM, Hongera M/Kiti Magufuli, Wapinzani Mjifunze Kutoka CCM

Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma

Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika - JamiiForums
 
Paskali nimecheka sana, eti kuna wanaccm walioipigania kwa jasho na damu, kwa taarifa yako hakuna mwanaccm amewahi kuipigania kwa jasho na damu kwani ccm sio chama cha siasa, bali ni taasisi ya kidola iliyojivika koti la chama cha siasa. Hivyo ccm inapiganiwa na vyombo vya dola, hao wanaccm wanachofanya ni kupigania kuingia ndani ya ccm ili wapate mlo.
 
CCM ni Chama Dola, na wana infos zaidi kuhusu Membe kuliko yoyote yule, huo siyo uamuzi rahisi na hawawezi kukurupuka, ...

Hamna cha info wala nini, ni kuwa Magufuli hawezi siasa za ushindani na hatakaa asiweze, hivyo alichofanya ni kutumia madaraka yake kumfuta uanachama huyo Membe, hilo liko wazi wala halihitaji mjadala wowote.
 
Paskali umeongea vema . Ila kumbuka Membe nae ni binadamu ana "nyongo". Yeye kwa sasa ni mchezaji huru ana utashi wa kuamua hatma na mapenzi yake kisiasa. Usimlishe maneno. Pia kuna utofauti baina yake na Lowasa. Lowasa alihamia upinzani. Membe ni mfukuzwa hivyo kuhamia si neno mujarab kwa namnayake.
 
Back
Top Bottom