Wakili Msando amvaa Zitto Kabwe kuhusu Mkurugenzi wa Vodacom kulazimishwa kukiri kosa

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722
Wanajamvi salaam

Wakili Albert Msando ambaye kwa sasa anajitambulisha kama Mshauri mkuu wa masuala ya kisheria wa CCM amejitokeza na kupinga tuhuma za Zitto kabwe kuhusu sakata la Mkurugenzi mkuu wa Vodacom na wenzake. Awali Zitto Kabwe alikuwa ametoa tuhuma kuwa Mkurugenzi wa Vodacom na wenzie walilazimishwa kukiri makosa yao.

Wakili Msando amesema kuwa hakuna sheria inayoruhusu mtuhumiwa kukaa na DPP kwa ajili ya ku-bargain kosa lake la jinai ili akiri na kupunguziwa adhabu "Plea bargain"

Msando ameandika yafuatayo kwenye ukurasa wake wa instagram

"Tanzania hatuna sheria ya “Plea Bargain”. Mtuhumiwa yeyote ana HAKI ya kukiri au kutokukiri kosa lake bila kushurutishwa. Ni kinyume cha sheria kumlazimisha mtuhumiwa kukiri kosa. Watuhumiwa wote wanakiri (plead guilty) Mahakamani mbele ya Hakimu. Taarifa ya@zittokabwe kwamba kuna watuhumiwa wanalazimishwa kukiri makosa na DPP SIO ZA KWELI. Kwa mfano, Vodacom ambao walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi kwenye kesi namba 20/2019 iliyokuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi walikiri makosa na kupewa adhabu kulipa fedha zaidi ya shilingi Bilioni Tano walizokwepa, kwa mujibu wa Sheria ya adhabu. Taarifa yao kwa umma inaeleza hivyo na zaidi wenyewe wamechukua hatua za ndani kuchunguza zaidi ili waweze kurekebisha kasoro walizokutwa nazo. Sio sahihi kupotosha suala la kisheria na kuichafua ofisi ya DPP kwa sababu za kisiasa. Albert G. Msando -


Mshauri Mkuu Msaidizi wa Sheria - Chama Cha Mapinduzi."


Hata hivyo kumekuwepo na hisia kama siyo tuhuma kuwa japo sheria ya Tanzania tofauti na nchi zilizoendelea haitambui kuwepo kwa plea bargaining swala hilo limekuwa likifanywa na ofisi ya DPP. Katika tuhuma hizo inasemekana baadhi ya kesi za uhujumu uchumi zimekuwa zikimalizwa na Serikali kwa kukaa na wahusika na kukubaliana kufuta baadhi ya mashitaka au kuwapunguzia adhabu endapo watuhumiwa husika watakiri makosa hayo mapya na mara nyingi adhabu huwa faini tofauti kabisa na adhabu kali za vifungo vya miaka kadhaa zilizomo kwenye sheria ya uhujumu uchumi.

Wanasheria kutoka ofisi ya Victory Attorneys. & consultant Benedict Ishabakaki na mwenzake Wakili Luka katika andiko lao linalokwenda kwa jina

"PLEA BARGAINING ARRANGEMENT: THE INEVITABLE LAW IN TANZANIA"

Wameelezea plea bargaining katika lugha ya kimombo kama ifiatavyo hapa chini

"Plea bargaining refers to the process whereby an accused and public prosecutor reach a mutual agreement without going through long court proceedings. In this process, the accused voluntarily admits charges and the prosecution voluntarily discharges some charges or asks the court to reduce punishment to the accused upon conviction.
This is very common practice in many
developed countries including but not limited to United State of America, Italy, France etc."

Wakili Luka na Ishabakaki wanakiri kuwa plea bargaining haitambuliwi nchini Tanzania hata hivyo wanaeleza wazi kuwa huo umekuwa mfumo mpya sasa unaofanywa na ofisi ya DPP na serikali. Katika mfumo huu ambao wao wameita ni mfumo usio rasmi umeshika kasi baada ya sheria za uhujumu uchumi kuanza kupatiwa uzito miaka ya 2017 na kuendelea

"In Tanzania, the term plea bargaining is not very common because our Criminal Procedure Act is silent on this. Our criminal justice framework does not provide a leeway for an accused person to voluntarily bargain with prosecution to dispose his case without going through the long and complex court proceedings.
Nevertheless, a number of major criminal cases since 2017 to date have been disposed through informal plea bargaining. This is most commonly in economic crimes cases where the accused persons voluntarily admits offences and the prosecution side
either substitutes or withdraw some of offences. A large number of economic crimes cases seem to have ended this way. This is typically a plea-bargaining scheme although it has not clearly been prescribed by the law."

Wakili Ishabakaki na Luka wanashauri ni vyema mfumo huu ukahalalishwa kwani utaweza kuleta faida kwa pande zote mvili kwa serikali kupata mapato, kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani na wafungwa magerezani,

Hata hivyo madhara yake ni kuwafanya hata wasio na hatia kukubali makosa ili kuogopa kusota rumande wakisubiri uchunguzi na usikilizwaji wa kesi zao maana kesi za uhujumu uchumi hazina dhamana. Mfano Rugemalila na Seth wamekuwa gerezani kwa muda mrefu. Katika mazingira kama haya hata Rugemalila akikutwa hana hatia anakuwa ameumizwa kisaikolojia, kiuchumi na kijamii kwa kule kuwekwa tu rumande muda mrefu.

Ishabakaki na Luka wanaandika hata katika ukurasa wao wa Instagram wa Victory Attorney,

"Why plea bargaining is necessary at this particular time?
We should admit that, this is one of the very strict regime ever happened in our land save for Mwalimu Nyerere time where economic sabotage offences were at its apex. This regime is very strict and sensitive when it comes to compliance issues. It is undisputed fact that, the compliance offences are the leading chargeable offences in this era, these includes Money Laundering, Tax Evasion, Economic Organized Crime and Occasioning Loss
t should be made clear that, most of the aforementioned offences do not need ill motives to be charged with. Most of the persons charged, either abstained from fulfilling their obligations or negligence. For example money laundering and occasioning loss offences mostly arise from
negligence."

Therefore, to that end, it is important to have a clear and well recognized legal framework which will allow these people who have been in trouble for negligence and without ill will, to settle with the prosecution without going through tough, complex and long court proceedings."

"By Benedict Alex Ishabakaki & Rayson Elijah Luka
Victory Attorneys & Consultants
IT Plaza, 1 st Floor
Ohio street/ Garden Avenue
P.O.Box 72015
Dar es Salaam
info@victoryattorneys.co.tz"



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasheria wana kitu kinaitwa "lacuna" yaani kama sheria ziko silent basi unachoweza ni kuishawishi mahakama kuchukua mfano yaani "case law" kutoka nchi nyingine na kuitumia.

Mfano hata neno lenyewe "plead bargain" kama kweli halipo katika sheria zetu basi maana yake limeonekana kwenye sheria za nchi zingine. Hivyo, ni kiasi cha kuchukua hukumu ya hiyo case na kuileta huku na inakubalika.

Wanasheria wanaita hii inakuwa ni "persuasive case".

Mfano, hata kwenye affidavit unaweza kuweka maombi fulani na case maarufu ni ile iliyotokea Uganda miaka ya nyuma ingawa nimeisahau.
 
Msando bado hawezi mwamini hata Abdul nondo, kwa tanganyika ya sasa hakuna kinacho shindikana
Wks kumbukumbu zangu..nasumbuka hata Abdul Nondo aliwahi kusema habari ya ya DPP kumlazimisha kukiri kosa na kuandaa mkutano na waandishi wa habari ili azungumze mambo fulani ili awe huru. .i stand to be corrected.

Sent using Jamii Forums mobile app

USOGA WI KUA KATI MWINA NSONGOO
 
Wanasheria wana kitu kinaitwa "lacuna" yaani kama sheria ziko silent basi unachoweza ni kuishawishi mahakama kuchukua mfano yaani "case law" kutoka nchi nyingine na kuitumia.

Mfano hata neno lenyewe "plead bargain" kama kweli halipo katika sheria zetu basi maana yake limeonekana kwenye sheria za nchi zingine. Hivyo, ni kiasi cha kuchukua hukumu ya hiyo case na kuileta huku na inakubalika.

Wanasheria wanaita hii inakuwa ni "persuasive case".

Mfano, hata kwenye affidavit unaweza kuweka maombi fulani na case maarufu ni ile iliyotokea Uganda miaka ya nyuma ingawa nimeisahau.
U said it all.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ni kitu kingine na utekelezaji kitu kingine. Tuna sheria nyingi nzuri tu na hata katiba japo sio nzuri lakini hata hayo yasiokuwa mazuri hayatelekezwi. Kesi zote utasikia uchunguzi bado kuna watu wanaenda mwaka kina Kaburu lakini hawa jamaa 2 days tu hukumu imetoka kwa hiyo mwenye akili anajuwa nini kimetokea. Haya sheria inasema nini sijui hayana nafasi wote tunajuwa kimetokea nini.
 
Tuwe Wazalendo

Huyu Mmisri wa Vodacom angekuwa China angepigwa Risasi ya kichwa sio kulipa Faini

Serikal ipongezwe kwa Intelijensia erevu Na Kabambe iliyowabaini Majambazi haya mpaka yamekubali kosa na kulipa Faini ya zaid ya 6.billion
 
Wanasheria wana kitu kinaitwa "lacuna" yaani kama sheria ziko silent basi unachoweza ni kuishawishi mahakama kuchukua mfano yaani "case law" kutoka nchi nyingine na kuitumia.

Mfano hata neno lenyewe "plead bargain" kama kweli halipo katika sheria zetu basi maana yake limeonekana kwenye sheria za nchi zingine. Hivyo, ni kiasi cha kuchukua hukumu ya hiyo case na kuileta huku na inakubalika.

Wanasheria wanaita hii inakuwa ni "persuasive case".

Mfano, hata kwenye affidavit unaweza kuweka maombi fulani na case maarufu ni ile iliyotokea Uganda miaka ya nyuma ingawa nimeisahau.
Ndugu tulia, wewe si Mwanasheria na wala hujui haya mambo.
 
Back
Top Bottom