Kuachiwa kwa babu seya tena kwa kusamehewa personally bila kuwekwa kwenye group fulani la msamaha lina ukakasi....!! Kwa mtu mwenye itimamu lazima ahoji haijalishi alionewa au laa...ingekuwa mataifa mengine watu wangeandamana. Labda mtoa msamaha atoe uthibitisho kuwa alionewa..!
Pitia tena ile ibara ya 45 aliyotumia raisi. Inampa mamlaka ya kumsamehe mtu yeyote, mwenye kosa lolote, na haimuhitaji raisi kutoa sababu ni kwanini ameamua kumsamehe fulani na kutokumsamehe fulani.
Pia mchakato wa kusamehe ni mrefu, sio Raisi anajiamulia nani wa kusamehe, sababu raisi hawezi jua wafungwa wote nchi nzima. Kuna tume inayohusika kupendekeza majina ya wanaostahili msamaha na sababu zao. Raisi anachofanya ni kukubali ushauri na kuwasamehe waliopendekezwa wote, baadhi au kukataa kusamehe.
Nasikia tume inaundwa na wadau kama mwanasheria mkuu, jaji mkuu, mkuu wa paroli, mkuu wa magereza, waziri wa sheria na katiba, waziri wa ulinzi na usalama, waziri wa mambo ya ndani, etc.
Pia raisi anasamehe kwa kukufutia adhabu ya kifungo iliyobaki au kuipunguza. Hakufutii hatia. Yaani Babu SEYA kafutiwa kifungo lakini kisheria bado alikutwa na hatia.
Pia kila mtu hufungwa peke yake, yaani personally. Hakuna hukumu ya group, na hivyo msamaha pia ni personal. Babu Seya alitajwa kwa jina sababu ni maarufu. Kuna wafungwa wengine waliofutiwa kifo walitajwa majina, hatuyakumbuki kwa vile sio maarufu.