Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Hizo siri za chama ndo zinatufikisha kubaya siri siri mpaka lini? Mbona mkiambiwa mikataba ni siri ya serikali mnalalamika weeeeee.
Siri siri siri ndo mdudu gani huyo jamani??
 
Miye naunga mkono huyo bwana mdogo zitto asimamishwe uanachama. Kilichoniudhi zaidi ni kitendo cha kuongea kilichojili ndani ya chama chake wakati wa kikao. Inavyoonekana huyu bwana mdogo amevimba kichwa. Ninachowashauri chadema wasidiriki hata mara moja kuendesha chama kwa nguvu ya mtu mmoja mmoja. Nguvu ya chama ni wanachama kwa ujumla wao. Kama zitto kabwa ameanza kuwasumbueni na kutoa siri za chama mwekeni pembeni, msonge mbele. Huu siyo wakati wa kupoteza muda. Chadema inahitaji timu imara na yenye msimamo mmoja.
 
Omar.. hivi uamuzi wa kutoka Bungeni ulipigiwa kura na wabunge wa Chadema au uliamuliwa unilaterally na mtu mmoja?
 
Nyinyi munapenda Zitto aseme yes sir! kila wakati? Anayo haki ya kukataa kuunga mkono kitu kama hawafikiani nacho na huo sio usaliti.

Usaliti ni ile kujidai umekubali kumbe rohoni mwako hupendi kile kinachofanyika.

Jaribuni kufikiri nje ya boksi jamani!

Alikuwa na uwezo wa kujibu kuwa hilo swala lilikubaliwa ndani ya vikao vya chama na yeye aliunga mkono! Full Stop. Lakini yeye aliamua kujitofautisha na chama ili awafurahishe mabwana zake, OK ni rafiki wa JK na hakutaka kumuudhi, sasa kwa kuwa ni swala lililopigiwa kura na kukubaliwa ndani ya chama yeye hakwenda si angekaa kimya tu. Kwa wenye akili timamu tunamuelewa huyu Zitto ni ubinafsi, umasikini na uroho tu wa madaraka unamsumbua, anataka abaki kwenye hizo kamati.
Ametusikitisha sana, mijitu misaliti kama hii ni risasi tu ndio za kwao!!
 
I have no comments,so zitto hataki katiba mpya? yeye alipendekeza nini kifanyike badala ya kuingia ndani na kutoka? au kaahidiwa uwaziri na aliona akiingia na kutoka atakuwa kapoteza nafasi yake kwa jk?

Am still watching this movie.


Hivi katiba mpya itapatikana kwa wabunge 47 kumtukana kiongozi wa chama chenye wabunge 260+ na Rais mwenye kukubalika na zaidi ya asilimi 60 ya wapiga kura? Hivi kweli unaamini kuwa CHADEMA wananguvu ya kuwalazimisha CCM kufanya chochote? Hivi yale yaliyofanikiwa katika miaka mitano iliyopita yalitokana na protest and drama politics za CHADEMA ama hoja bora na engagement politics za wabunge wao???

Asilimia kubwa ya watanzania wangependa kuona katiba mpya ingawa iliyokuwepo hata asilimi 50 ya wabunge wao hawaijui....lakini kupata ni kitu kimoja na njia ya kupata ni kitu kingine....kumbuka kuwa asilimia 45 ya wapiga kura wa mwaka hu wamesema kuwa kura zao zimeshawishiwa na umuhimu wa AMANI.....kutomtambua RAIS wa nchi ni kutothamini AMANI....
 
Ningekuona una busara endapo ungejibu hoja nilizozitaja toka mwanzo kuliko kuanza kunivamia mie, wewe umejiunga 2010 mie 2007 na ninajua huu ni mtandao wa Small mind people, wasioweza kujadili maswala, nabadala yake neno lao ni Ufisadi na kumtaja makamba, lowasa kila saa,, grow up. Ukifuatilia kwa makini huu mtandao ni wa MASHABIKI WA CHADEMA na pia watu waliokua very biased kwa hiyo huwezi kua thanked unless uitukane CCM,, hayo ni maono ya kitoto kifikra. Kua

Kama huu ni mtandao wa Small mind people kama ulivyosema. Wewe unafanya nini huku? Au wewe ni wale self described small mind person!
 
Ili kuleta mafanikio ya mikakati inayoendelea, mshikamano kwenye safu ya juu ya CDM ni miongoni mwa silaha muhimu sana!!!!!!!!!! Kwa mwanaJF aliyefuatilia suala la mshikamano ndani ya CDM tangu kipindi cha kampeni, ni rahisi kujenga hisia ya mashaka na mmoja wa wapiganaji Zitto!!!!!!!!!!! Kujitenga kwake na baadhi ya matamshi yake katika nafasi aliyonayo inatia mashaka kama kweli hana agenda ya siri????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!! WanaJF mtuhabarishe zaidi juu yake ili tumshauri Kamanda wa CDM ipasavyo!!!!!!!!!!!!
 
Kumfukuza Zitto itakuwa ni kukubali kwamba CHADEMA haina utamaduni wa kukubali tofauti ya mawazo chamani.

Kwa chama kinachotaka kuleta demokrasia zaidi Tanzania, ambacho jina lake linabeba neno demokrasia, jambo hili litakuwa baya sana.
 
Huyu jamaa ingawa ni kiongozi wetu lakini akiamua kutoka leo nitafurahi sana, ninachoomba Chadema iende naye taratibu wasimpe cheo kikubwa wala wasimfukuze ajiondoe mwenyewe, walikuwapo kina Kabouru enzi chama hakina mvuto atakuwa Zitto wakati chama kina vichwa vya uhakika, kwa busara za uongozi huwezi mlinganisha Zitto na Lissu.

Du ebwana ehh..Tundu Lisu na Busara za uongozi!!!!! Nadhani nahitaji kusoma zaidi nini maana ya busara za uongozi.....no wonder hizi irresponsible stunts.....Zidumu siasa za DRAMA...Ukombozi Daima
 
Huyu Nyerereist amekuwaje akawa JF senior Expert member na utumbo huu? how? inakuwaje awe amepost posts 420 lakini amekuwa thanked mara moja tu? nadhani huyu ni junior member tu kama siye au ni mropokaji tu!

Yawezkana anasema yale ya kusemwa lakini msiyotaka kuyasikia.........
 
:whoo:Guys huyu jamaa karibu kila wakati anaingia geti la Rostam: Kwale street so naamini kuna jambo tu hapa...soon ataleta mgogoro ndani ya chama
 
mie nadhani atupe sababu kwanini alikuwa hakubaliani na pendekezo hilo,lazima alikuwa na sababu,sasa asiseme tu tulipiga kura wengi wape,vilevile atuambie kwanini hakukubaliana na maamuzi yale then uamuzi utolewe na wana JF.

Hao waliosema waliosema hawamtambui Jk , Nasisi hatuwatambui uwepo wao bungeni.
NO NEED OF REASONS IN POLITICS.
 
Hao waliosema waliosema hawamtambui Jk , Nasisi hatuwatambui uwepo wao bungeni.
NO NEED OF REASONS IN POLITICS.

wao wanataka katiba mpya/tume huru ya uchaguzi, nyinyi mnataka nini hasa?
 
mie nadhani atupe sababu kwanini alikuwa hakubaliani na pendekezo hilo,lazima alikuwa na sababu,sasa asiseme tu tulipiga kura wengi wape,vilevile atuambie kwanini hakukubaliana na maamuzi yale then uamuzi utolewe na wana JF.

Sababu kubwa ni uenyekiti wa kamati nyeti.Bado anaitaka ile kamati ya Hesabu za mashirika ya uma. Zitto mpenda vyeo hana subira akajipanga anajiangalia yeye na si chama. mimi nitafurahi akiondoka CHADEMA kwani kiukweli chama kitakua na Amani sana. Chadema ya zamani ilikua haina migogoro hata mtu alikua akiondoka kwenye chama anaondoka kimya kimya tangia zitto aibuke ni makelele tu. Hafai kuwa CHADEMA aende CCM atapata hivyo vyeo anavyovitaka kwa haraka.
 
Sumu. It is not the right time.... tolerance is important in this delicate situation. Play safe! If the changes are for the mass/public nobody can stop them. For he who instigates ill-conflicts will lose credibility before the mass/public. Until that time when public and majority of the members lose trust on such a leader he will disappear in the political arena automatically! The boat has different types of people you cant easily know them unless you give them freedom to speak and show their true colors.



Get lessons from the history.

God Bless Tanzania
 
Sababu kubwa ni uenyekiti wa kamati nyeti.Bado anaitaka ile kamati ya Hesabu za mashirika ya uma. Zitto mpenda vyeo hana subira akajipanga anajiangalia yeye na si chama. mimi nitafurahi akiondoka CHADEMA kwani kiukweli chama kitakua na Amani sana. Chadema ya zamani ilikua haina migogoro hata mtu alikua akiondoka kwenye chama anaondoka kimya kimya tangia zitto aibuke ni makelele tu. Hafai kuwa CHADEMA aende CCM atapata hivyo vyeo anavyovitaka kwa haraka.

CHADEMA ma beef yatakuwepo tu, kulikuwa na ma beef enzi ya Wangwe, kumekuwa na ma beef juzi Tundu Lissu hakutaka uteuzi wa Regia Mtema kugombea ubunge, Regia kamuandika vibaya Kitila hapo kuna shaky grounds kama si beef, na haya ni yale yanayoleak online tu, huko ndani sijui.

Kwa hiyo usijidanganye kwamba Zitto akiondoka beef zitaisha, as long as watu wanapolitiki kutakuwa na intrigues.

Halafu Zitto labda ubovu wake kawa loudmouth tu, lakini fundamentally mi sioni tatizo na uamuzi wake, ukizingatia chama hakina maoni ya wananchi. It is not like wenzake waliamka wakaondoka bungeni yeye akakaidi akabaki bungeni, hakwenda kabisa, kwa hiyo wengine wanaweza kusema ukiondoa the theatrical effect of walking out, which is just fluff, kutofika kabisa is even worse.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom