Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
KUHUSU KUTOKA NJE WAKATI RAIS AKIHUTUBIA BUNGE HAIKUWA NA MANTIKI YOYOTE KWANI WALITAKIWA HATA HUKO KUHUDHURIA BUNGE KUSIWEPO KWANI HAKUNA BUNGE BILA SERIKALI NA SERIKALI NI RAIS NA WATEULE WAKE, i MEAN MAWAZIRI,
KWANI HIYO MISWAADA WATAKAYOTUNGA BUNGENI ATASAINI NANI? WATAWAULIZA MASWALI AKINA NANI BUNGENI KAMA SI MAWAZIRI AMBAO NI PRESIDENTIAL APPOINTED?
CUF WALIGOMA KUINGIA BUNGENI KWA MIAKA 3 MPAKA RAIS AKAWAITA WAKAONGEA NA KUKUBALIANA TERMS, SASA KAMA CHADEMA HAWAINGII TU SIKU RAIS AKIWA BUNGENI BINAFSI NAONA KAMA UCHIZI NDO MAANA MIMI MTU KAMA ZITU HUWA NAMKUBALI SANA KWANI MARA NYINGI MAAMZI YAKE YANA MANTIKA NA NDO MAANA HAKUONA UMHIMU WAKUTOKA BUNGENI (IF AND ONLY IF HAKUKUWA NA VIELEMENT VYA UDINI LAKINI)
 
Tatizo la Zitto ni kujitia anajua sana mambo na kujiona yeye anaupeo wa uongozi na ni nyota wa Chadema. Zitto analeta siasa za kimarekani Tanzania, anataka kujifananisha na Obama au Cameron, yaani kuwa ni kiongozi mwenye umri mdogo na ni machachari. Anasahau kwamba hayo machachari ameyapata na kupatia umaarufu kupitia CHADEMA.

Kisiasa, Zitto is declining. Tena , the more anavo kuwa contradictory ndo the more he is loosing his ground. Miaka mitano iliopita Zitto alikua maarufu na mtu wa kusifika, leo hii sio hivyo tena...! Swali ni Je kwa nini iwe hivo?

JIbu analo yeye binafsi, lakini kikubwa ni kwamba, unapokua mbunge wa upinzani na kuonekana kusupport au kukubaliana na mawazo ya chama tawala kiasi cha kufukia kusema kwamba upo tayari kujiuzulu au kudharau chama chako, basi ujue unajiweka katika hali mbaya sana. Assahau kwamba, siasa its a game of words, so kila unachosema huw akiantafsiriwa na kupewa maana na kila mtu kwa upeo wake.

NI ushauri wangu ZItto awe makini lasivo badala ya kupata umaarufu sasa atapata maadui na watu wenye chuki dhidi yake haswa wananchi ambao walitegemea yeye kuwa sehemu ya ukombozi wao. Indeed, Zitto anaonekana kusahau mambo muhumu sana "team playing" kwa maana ya kwamba, he must be a team player with his fellows...!
 
Hawa meku vipi hawa? kwa sababu zito siyo meku basi wanamuona ni tishio kwa slaa. Alichokifanya Zitto siyo kitu kibaya na hakutoa siri yoyote ya chama. Kuelezea kwamba maamuzi ya chama yalifikiwa kidemokrasia kuna kosa gani? Chadema ni chama cha watanzania wote, na kama mnataka kuendeleza u-meku weni, chama cha ki-meku ni nccr-mageuzi.
Heko Zitto kwa kuendeleza sera za u-wazi
 
Zitto hana haja ya kufukuzwa, wakati ukifika atamaliza kazi aluyojipangia
 
Zitto ana haki na uhuru wa kutoa maoni na mtazamo wake. Kitu cha msingi ni kwamba yeye ali vote against uamuzi lakini mwisho wa siku alifuata kile kilichoamuliwa na wengi kwa hiyo demokrasia imetumika na hicho ndicho chadema tunacho kiubiri. Huwezi kutegemea katika kundi la watu 45 wote wakawa na mtazamo unaofanana hakuna kitu kama hicho. Kuhusu suala la kutaka madaraka kwenye chama sioni kama ni tatizo lwa sababu yeye kama mwanachama ana haki hiyo kama hafai watamtosa hukohuko kwenye chama. Suala la kufukuzana uanachama hapa halina tija ila itakapothibitika beyond doubt kwamba anatumiwa na ccm kuivuruga chadema basi anaweza kuchukuliwa hatua kali na chadema itaendelea nikirejea maneno ya rais SLAA aliwahi kusema chadema ni zaidi ya mbowe, ni zaidi ya zitto na ni zaidi ya slaa mwenyewe..
 
huyo kijana hafai kuwa kiongozi kama maamuzi ya chama yaliyopigiwa kura na wanachama wengi wakakubali alafu m2 anakwenda media kuongea pumba hawezi kuwa ni kiongozi bali ni mnafiki nadhani anataka ki2 kutoka ccm tayariameshahongwa na mafisadi bora achape mwendo.na ni kweli cku zake zinahesabika hana tofauti na mrema
 
icon1.gif
Re: Chadema imvue/imfukuze uanachama zitto kabwe!


- Well, Mh. Zitto amesema mawazo yake ambayo ameyaonyesha kwa kura aliyoipiga ndani ya Chadema kwamba hakubaliani na uamuzi wa kumsusia Rais, binafsi ninapata maswali mengi sana hapa kwamba hii agenda ni ya nani hasa maana sio siri kwamba sio ya wabunge wote wa Chadema kama ambavyo nilikuwa nimeaminishwa hapa mwanzoni kwamba wananchi wote waliowachagua wabunge wa Chadema na waliompigia kura Dr. Slaa ndio wanaowakilishwa kwenye hicho kitendo, lakini sasa inaeleweka kwamba sio kweli maana katika ufafanuzi wake leo Mh. Zitto anasema msimamo wake huo ni wa wananchi wa jimbo lake zaidi kuliko yeye!

- Now katika politics hasa hizi tulizonazo bongo, ni muhimu sana kwa chama chochote cha siasa kuonyesha msimamo mmoja mbele ya public na hasa kwenye ishu muhimu kama hii, lakini ukweli ni ukweli kwamba hii hoja haikuwa ya Chadema nzima, ndio maana hata kura ilibidi zipigwe, sasa ni lipi kosa la Mh. Zitto hapa? Unless mkituonyesha hapa katiba ya Chadema inasema nini kuhusu kitendo cha Mh. Zitto!

- Otherwise, tunataka viongozi wawazi kama Mh. Zitto somo kwa Chadema ni muhimu sana mkamaliza mambo yenu huko huko ndani ya chama maana yakifika kwenye public hamuwezi kuwa na control tena kama mnavyojaribu sana hapa JF, kumpaka na kumchafua kiongozi wenu bila sababu za msingi ni kujichafua wenyewe kwamba hamjui maana ya the very Demokrasia mnayoidai toka CCM, acheni Demokrasia ichukue mkondo wake mambo ya kufikirishwa kwa mafungu ndio yamelifikisha hili taifa hapa tulipo!


William.
 
Zitto ni KIRUSI, na Chadema itafanya la maana ikichukua uamuzi mapema wa 'kumuweka mahali pake'.

Hakuna aliye mkuu kuliko chama na wala hamna haja ya kumbembeleza mtu asiyebeba maslahi ya chama.

Hakusimama kugombea ubunge kama mtu binafsi, hivyo anao wajibu wa kuchukua msimamo wa chama chake hususan yanapoamuliwa kwa pamoja. Na hatua ya kutoka na kwenda kuongelea suala lililoamuliwa tayari chamani na kuonesha kwamba yeye hakukubaliana nalo ni dalili kwamba anatafuta umaarufu wa kipekee. Huyo sio team-player!
 
Wengi tunataka katiba mpya ingawa wengi hatuijui hata hii iliyopo wakiwemo zaidi ya asilimia hamsini ya wabunge wetu...

Lakini je, hatua ya wabunge wa chama chenye wabunge 47 kutomtambua RAIS aliyepata kura zaidi ya asilimia sitini ama tuseme hata hamsini tu na kiongozi wa chama chenye wabunge zaidi 260, ni hatua itakayoweza kutupatia hiyo katiba mpya??? Hivi kutoa ishara za kutothamini ama kuheshimu UTAWALA mbele ya jamii ambayo asilimia 45 ya waliopiga kura wanasema wameshawishiwa na kuthamini AMANI na haswa katika taifa lenye kutishiwa na mgawanyiko wa kijamii huku tukijua wazi matokeo ya migawanyiko ya aina hiyo, ndio njia muafaka wa kufanikisha kupatikana kwa katiba mpya?

Hizo kuira zingekuwa ni za UKWELI na za HAKI, ungekuwa na point..lakini wapi kama kawaida yako..hot air.
 
Zito tunakuomba utambue Haya yafuatayo na Gharama zake:

CHADEMA si tu chama cha demokrasia na maendeleo pekee bali ni chama cha Wananchi ambao
kwa namna moja au nyingine wameamua kujitafutia mabadiliko Dhidi ya Udhalimu wa aina yoyote ile
unaofanywa na CCM,.... Hivyo basi Zito asidhani ataivuruga CHADEMA akimbilie CCM nasi tutamsindikiza kwa macho,
La hasha....... Nyakati hizi sio ndio mzee tena..... Pindi chadema itakapovurugika kwa ajili yake...... ajue
CCM ataenda akiwa marehemu ZITO..... Na kama ana nia ya kwenda CCM basi mapema akusanye Virago vyake
kwa amani kabisa anyanyue ****** yake atuachie chama chetu ambacho kwa vijisent vyetu tuliamua kuacha mambo
mengine na kuamua kukichangia ili kifike hapa kilipo.
Na si yeye.... ONYO kali.
 
Mkuu VOR, Zitto ni mmoja wa viongozi wa ngazi za juu katika chama. Amefanya vema kusema neno kwa kuwa maelezo yake yanachukuliwa kwa imani kubwa kama sehemu ya utetezi wa chama. Kukaa kimya wakati mashambulizi hatari ya ccm yenye kulenga kuharibu kila kilichoko mbele yao ni uamuzi wa hatari. Hata bubu huweza kusema akizidiwa na manyanyaso.
 
MIMI WEWE ZITTO UNANITIA WASIWASI MAANA NI JUZI KUNA MTU AMENIAMBIA ETI CCM IMEKUNUNULIA NYUMBA SIJUI NCHI GANI HUKO IKIWA NI KUKUPUNGUZIA MAKALI. LEO UNAPAYUKA HADHARANI MABO YA NDANI YA CHAMA, UNAMUOGOPA NANI HUKO CCM, LABDA KWA SABABU HUJAOA NDIO MAANA HUELEWI MAMBO YA KUTUNZA SIRI ZA NDOA, AAHA NO!NO!:A S-cry:
 
Zitto unasema wewe ni democrat na unapenda kuongea unaloliamini na unapenda uwazi na ukweli. Lakini yanayojiri kwenye vikao vya chama ni siri ila matokeo ya hivyo vikao sio siri. Hivi ulivyokwenda TBC 1 na kubwabwaja yaliyojiri ndani ya vikao vya chama ulikua unataka wananchi wakueleweje? Kuwa utoto unakusumbua mpaka uropoke kila unachokijua bila ya kupima unaongee na nani na nini unakiongelea? Kuwa wewe umekua kimwili tu na sio kimawazo? Naomba nikupe mfano. Hivi wewe Zitto ukiingia chumbani kwa mama yako na bahati mbaya ukamkuta anavaa nguo, utatoka na kuwaambia watu kuwa umemwona mama yako akiwa mtupu?

Duh Zitto ni mtata sana!nashukuru sana hakufanikiwa kuwa mwenyekiti wa chama,angekiuza chama kwa CCM,hii ni hatari sana katika safari yetu ya kuelekea kwenye democrasia ya kweli!!
 
katika kuonesha hali ya masikitiko mh zitto zuberi kabwe amepingana na kitendo cha chadema kutoka nje ya bunge, akiongea na tbc leo zitto amesema yeye kama yeye hakubali kitendo cha chadema kuwalk out

big up zitto :lock1::lock1:hapo umeonesha ukomavu wa siasa
karibu chamani:clap2:

mimi ninavyojua humu kichwani kwangu kwamba zitoo ni ccm si ahame tu asione aibu, mbona wengi tu wamehamia ccm yeye hatakuwa wa kwanza na wala chadema haitakufa zitto akihama
 
Hiyo ndiyo democrasia wengi wape. Unajua hata sisi viongozi wetu wengi ndicho wanachokosea.

Kama kweli unataka democrasia ichukue mkondo wake, ni kupiga kura then walioshinda tunawaheshimu ingawaje huyu bwana hajaheshimu maamuzi ya wengi.

Peoples power
 
<br />
<br />
hatukatai yeye kuwa na mawazo tofauti, tunachopinga ni kwamba kulikuwa na ulazima gani kwa yeye kwenda kwenye media kusema alikuwa hakubaliani na uamuzi wa wengi? Binafsi naona ni kujipendekeza kwa jk na ccm. Niliwahi kusema hapa kwamba binafsi namuona zitto kama mtu mwenye tamaa sana na madaraka. Si mtu unayeweza kumuamini kujenga na kuimarisha chama. Hata mchango wake kwenye kampeni ya dr. Slaa ulikuwa kama hakuna kabisa na alionekana akimtetea sana jk kama kafanya kazi nzuri sana!

hata mimi hilo limenikera sana, hivi jamani katiba ya chadema inasemaje kuhusu kuchagua viongozi wake, yaani huyu tumpige chini fasta kabla 2015 haijafika atatuharibia 'move'
'chadema bila zitto inawezekana'
 
Hivi kama hilo la kutoka tu lilimshida! anaweza kutetea hoja tena za ufisadi?nasikia jina lake latajwa kama naibu waziri wa fedha, au ndio ahadi zakuzuzuza?
 
Kumfukuza Zitto itakuwa ni kukubali kwamba CHADEMA haina utamaduni wa kukubali tofauti ya mawazo chamani.

Kwa chama kinachotaka kuleta demokrasia zaidi Tanzania, ambacho jina lake linabeba neno demokrasia, jambo hili litakuwa baya sana.

Kiranga umenena vema, kufukuzana si suruhisho.. CHADEMA ikitaka kujimaliza kisiasa na kupoteza umaarufu ianze kufukuza fukuza. kikubwa ni kukaa katika vikao halali na kujadili hizo tofauti kwa umakini bila jazba!!! Mimi bado nina imani kwamba viongozi ni watu makini na wanaweza kutatua matatizo kistaarabu!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom