Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Hii ni mara nyingine Zitto anajikuta katika hali tata! Ni vyema awe anapima vizuri matendo yake before execution. Kama mumepiga kura na kukubaliana bac huna haja ya kukumbia, wengine watadhani hii kwake ilikuwa plan B! kwamba kama watanzania hawatafurahishwa na kitendo hicho iwe rahisi kwake kusema mie nilikuwa nimekipinga ndio maana sikwenda. Tafakari!
 
HATARI: Nyoka kaingia ndani ya CHADEMA

Tumepata taarifa kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA, Zitto Kabwe, akiongea na TBC1 amesema kuwa yeye ni miongoni mwa Wabunge wa CHADEMA waliokuwa wanapinga ile walkout isifanyike Bungeni Alhamisi iliyopita wakati Kikwete anahutubia.

Watu wametoa mawazo mbalimbali kuhusu suala hili. Kuna waliosema ameonesha ukomavu wa kisiasa na demokrasia ndani ya CHADEMA.

Mimi nina mawazo tofauti sana. Kitendo alichofanya Zitto Kabwe ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kwa uongozi wa CHADEMA.

Yeye kama mwanachama wa CHADEMA, Mbunge, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni anapaswa kuelewa kuwa maamuzi yote yanayofanywa na chama yanakuwa ndiyo msimamo wa mwisho wa chama. Hapa kuna suala la collective responsibility.

Alichokifanya Zitto kwa kuongea na TBC1 ni sawa na waziri ambaye anatoa siri ya vikao vya Cabinet kwa vyombo vya habari.

Mfano, kwenye cabinet kunatokea mvutano kuhusu suala fulani, let's say uuzwaji wa nyumba za serikali. Mawaziri wanajenga hoja zao halafu serikali inafikia uamuzi wa mwisho kuwa itauza nyumba za serikali kwa vigogo wa serikali.

Then atokee waziri mmoja aseme hadharani kwenye media kuwa yeye alipinga mpango wa kuuza nyumba za serikali kwenye Cabinet lakini akazidiwa kura na mawaziri wengine. Huyo mtu angefukuzwa kazi mara moja.

Ni jambo la kustusha sana kuona kuwa Zitto amekiri hadharani kuwa yeye alipinga jambo hili na kulikuwa na mvutano ndani ya CHADEMA. Kwa matamshi haya, ametoa siri za vikao vya ndani vya chama.

Uamuzi unapofikiwa na chama hata kama wewe binafsi haupendi unakuwa ni wa mwisho na lazima wewe uukubali, uunge mkono na uutekeleze.

Nadhani kama kiongozi wa CHADEMA, Zitto ameonesha utovu wa nidhamu kwa chama, amevunja kiapo cha kutunza siri za chama na ameonesha kukosa maadili.


Tena Zitto alienda mbali zaidi na kusema kuwa yeye aliamua kutokwenda kabisa Bungeni kwa kuwa hajakubaliana na walkout. Hili ni kosa kubwa sana la kupingana na maamuzi halali ya chama.

MASWALI YA KUJIULIZA:

1. What is Zitto Kabwe trying to achieve?

Je, anataka kuonesha umma wa Watanzania kuwa kulikuwa na mgawanyiko kwenye CHADEMA juu ya hili jambo na yeye hakuunga mkono uamuzi huu? Au pengine huenda anataka kuwaonesha vigogo wa CCM kuwa kazi waliyomtuma kuzuia walkout aliifanya kwa bidii na jitihada zote lakini akashindwa.

Kwa ufupi, kitendo cha Zitto si jambo childish tu, bali kinazidi kujenga zile hisia zilizopo mura mrefu kuwa yuko karibu mno na vigogo wa CCM na ni mtu ambaye huwa anatumiwa tumiwa hovyo kulinda maslahi fulani ya watu wachache.

CHADEMA ijihadhari na nyoka huyu hatari.
acha kufananisha mawili; kuhusu kuuza nyumba ni wizi, na sihafiki ukimya, naweza kumuunga mkono Waziri anayetoka nje ya kikao cha cabinet na kupinga hata kama amezidiwa kura na msimamo wa serikali maana that's is good citizenry cum patriotism! ila suala la Zitto+wenzie siliafiki maana sidhani kama amefurahishwa na matokeo na sidhani kama hatua iliyochukuliwa na chama chake ilikuwa mbaya kwa maana ya kuvunja sheria kiasi cha kuwa na utovu wa nidhamu na kuamua kutohudhuria akiwa na wakina Ndesamburo na mwanae Owenya na wakina Prof. Kahigi (niko disappointed kwakweli)! huo ndo tunaouita ukosefu wa togetherness na nina uhakika CHADEMA had a strong cause to present by what they did! Zitto ni wazi anakuwa in dilema situation maana kwa hali inavyoendelea ni wazi urafiki wake na wabunge wa NCCR-Mageuzi unamweka katika a compromise situation akidhani anaweza kuwaunganisha na CHADEMA for his own gain na hapo ndo atakapojimaliza maana hiyo heroism he wants to show itawapa chance CCM kumvuruga na CHADEMA na natabiri ataingia NCCR-Mageuzi na huo ndo utakuwa mwisho wake! Mwana siasa makini ajaribu kuangalia what happened to the likes of Dr Kabour! na ajifananishe na anachotaka kufanya! nathani atakuwa smart politician kama ataona nguvu ya CCM behind the scene katika kubomoa Upinzani na kuacha chokochoko zisizo na mpango na nathani CHADEMA wanapaswa wawe waangalifu saana na hawa watu wasio na nidhamu na kuleta chochoko kila siku! sasa si muda wa mavurugu ila kujipanga na ku-set goals of what they wanna achieve before the next election!
 
Uhalisia wa mambo na fikra za mtu siku zote una mtazano hasi na chanya. Ingekuwa vyema sana kama Zitto angekuwa practical kusupport hisia zake ambazo amezieleza kwenye media. Msimamo wake ni tete vipi afanye jambo kwa kufuata mkumbo? angeganda kwenye kiti chake wakati wa walk-out, historia ingejiandika. Huo msimamo uko wapi?
 
Wanachama wa Chadema Tunashauri Uongozi Ukae na Zitto Kujadili "Statements" Zake. Inaonekana Zitto Aweza Kuleta Matatizo Hapo Baadae na Isionekane Kuna Agendas za Zitto Ndani ya Chama. Huyu Bwana ni Hatari.
 
Sasa nimeelewa ni kwa nini CDM hawakumuacha agombee uenyekiti kwa chama,Maana walisha muona kijana hana hekima.
 
It is soo sad kwa kaka yangu mpenzi Zitto. Anapaswa kukaa kimya... Yuko juu ktk media, alikua juu kwa mema na sasa anakoelekea atakua juu kwa mabaya. Asidhani hii hali ni nzuri kwake hata kidogo maana anakua kamna amerogwa, atakwisha kabisa kisiasa na hatakuwa tena Zitto anayekubalika na jamii. Nadhani Zitto the only way ya kutoka tena ni kutafuta BUZWAGI nyengine bungeni Anne Makinda amfukuze apate ujiko na iwe issue atakayowalipua mafisadi akiwamo RA, Lowassa na Chenge, na hata JK ili kurudisha imani ya wananchi kwake, vinginevyo anakoelekea wananchi wataendelea kuaminishwa na kuamini kwamba amenunuliwa na akienda CCM ama NCCR atakua kama Mbatia, Tambwe Hiza ama Salum Msabaha.
 
Kama kweli walipiga kura basi utaona kuwa tunaposema ni chama cha democrasia basi ni democrasia kweli wala si kama wengine walivyosema kuwa walilazimishwa. Bado simkubali Zitto!
 
Mheshimiwa ZITTO unajua kuwa Rasilimali za nchi zinaporwa na wageni kwa msaada wa Mafisadi.

Kura za uraisi zimeibwa na wewe unajua, wewe ZITTO unategemea tutapataje Tume Huru na Katiba Mpya bila kuchukua maamuzi magumu??

Mikataba feki ya madini na vitalu vya uwindani Tanzania -Viongozi wa Si CM wanajineemesha na familia zao. Inakuaje kwenye madini tupate 3% na wageni wachukue 97%???? Je sisi watanzania ni vipofuuu??

Kura zimeibwa mchana kweupe, ushahidi wa kutosha upo. Tume ya uchaguzi imechakachua kura kwa maelekezo ya UDikteta wa CCm. Mh ZITTO yote haya huyajui? Kura za wananchi umezipata kwa sababu wananchi wanataka ukombozi, uhuru wa kiuchumi.

Zitto tunakuheshimu sana usiwe mnafiki, usitafute umaarufu wa Si CM.

Huyu dogo amesha wekewa virus ya ufisadi na RA na ndio itakayo muua kisiasa hajulikani anasimamia upande gani aondoke akamfuate Nakaaya huko s****t.
 
It is soo sad kwa kaka yangu mpenzi Zitto. Anapaswa kukaa kimya... Yuko juu ktk media, alikua juu kwa mema na sasa anakoelekea atakua juu kwa mabaya. Asidhani hii hali ni nzuri kwake hata kidogo maana anakua kamna amerogwa, atakwisha kabisa kisiasa na hatakuwa tena Zitto anayekubalika na jamii. Nadhani Zitto the only way ya kutoka tena ni kutafuta BUZWAGI nyengine bungeni Anne Makinda amfukuze apate ujiko na iwe issue atakayowalipua mafisadi akiwamo RA, Lowassa na Chenge, na hata JK ili kurudisha imani ya wananchi kwake, vinginevyo anakoelekea wananchi wataendelea kuaminishwa na kuamini kwamba amenunuliwa na akienda CCM ama NCCR atakua kama Mbatia, Tambwe Hiza ama Salum Msabaha.

Na mengi zaidi tutayaona, tena makubwa zaidi. Chamsingi ni mtu kujua haki zako na kuzisimamia bila ULAFI; yaani kwa manufaa ya wanyonge.

Hivi kwa nini ndg wa Nyerere wako CHADEMA? Lakini, mbona mke wa Nyerere yuko CCM? Hii ni kuonyesha kuwa, sisi sote ni waTanzania, na mtu yeyote asitugawe kwa visingizio vya CCM au CHADEMA. Tunataka TUME HURU na KATIBA MPYA, FULLSTOP.
 
Nyinyi munapenda Zitto aseme yes sir! kila wakati? Anayo haki ya kukataa kuunga mkono kitu kama hawafikiani nacho na huo sio usaliti.<br />
<br />
Usaliti ni ile kujidai umekubali kumbe rohoni mwako hupendi kile kinachofanyika.<br />
<br />
Jaribuni kufikiri nje ya boksi jamani!
<br />
<br />
hatukatai yeye kuwa na mawazo tofauti, tunachopinga ni kwamba kulikuwa na ulazima gani kwa yeye kwenda kwenye media kusema alikuwa hakubaliani na uamuzi wa wengi? Binafsi naona ni kujipendekeza kwa JK na CCM. Niliwahi kusema hapa kwamba binafsi namuona Zitto kama mtu mwenye tamaa sana na madaraka. Si mtu unayeweza kumuamini kujenga na kuimarisha chama. Hata mchango wake kwenye kampeni ya Dr. Slaa ulikuwa kama hakuna kabisa na alionekana akimtetea sana JK kama kafanya kazi nzuri sana!
 
Bintimkongwe, unaweza kuwa ni shabiki wa Zitto na tunaelewa ana mashabiki wengi. Lakini usiwe shabiki kipofu. Kwa vyovyote vile, lazima ukiri kuwa Zitto amekosa maadili kwa kutoa siri za chama hadharani. Alikuwa na kila haki ya kupinga uamuzi huu akiwa ndani ya vikao vya chama. Lakini uamuzi wa mwisho ulipochukuliwa, alitakiwa kukaa kimya. Hata kamati kuu ya CCM wenyewe ilipoamua kumfukuza Spika Samuel Sitta kulikuwa na mvutano mkubwa. Je, umemsikia Bernard Membe kwa mfano kujitokeza hadharani na kusema yeye alipinga uamuzi wa kumfukuza Sitta?

Kwa kweli Zitto lazima alaaniwe kwa kujaribu kuleta mtafaruku ndani ya CHADEMA, ambacho ndiyo chama sisi Watanzania tunakitegemea kituokoe kwenye janga la utawala wa CCM.

Kwa maslahi ya taifa, tuweke ushabiki wa majina ya wanasiasa fulani pembeni na tuangalie masuala kwa upana wake.

Mie naona mnampa unnecessary attention ambayo hadeserve kabisa. Nadhani kumnyamazia kimya ni busara sana kuliko hivi tunavyomuongelea. Kwanza yawezekana ni strategy yake ya kututoa kwenye agenda ya katiba, so we need to act very carefully with him.

Sisi tuungane na CHADEMA na wananchi wote kudai mabadiliko ya katiba, tuachane na Zitto. Hizo ni tantrums tu, si unajua siku hizi attention ipo kwa wengine akina Mnyika na vijana wengine wengi wa CHADEMA so he also wants to be recognized, anaona kama mmeanza kumsahau.(Attention seeking).

My advise ni kutompa attention, basi! Tufocus kwenye mabadiliko ya nchi hii, ni muhimu kuliko mtu mmoja.
 
Wabunge wa Kigoma hasa kutoka CDM wanakawaida ya kuwa wasaliti, haya anayofanya Zitto wala si mageni sana si mnamkumbuka Warid Kaborou!
 
Jamani huyu zito ametia mno kichefuchefu, kama unataka kula usisome thread yoyote inayomhusu zito kwani appetite yako itashuka. Je ana matatizo ya kisaikolojia? kuna mtu anayeweza kutupa historia yake alivyokuzwa alipokuwa mdogo? mimi siamini mtu mwenye akili timamu angerudia tena tabia kama hizi baada ya kukosolewa sana hapa janvini mara baada tu ya uchaguzi mkuu wa Octoba
 
Tukubali tukatae Zitto ni kijana kiumuri HIVYO HATA KIFIKIRI. MIENENDO YAKE INAZIDI KUTIA SHAKA. NADHANI ALISAHAU MSINGI WA CHADEMA KUTOKA NJE YA BUNGE KWANI CHAMA KIKISHASEMA HAKIMTAMBUI RAIS KINGEWEZESHA KUKAA ILI AKIHUTUBIE? HAONI KUBAKI KUBAKI BUNGENI ILIKUWA NI KUINYIMA NGUVU HOJA WALIYO IANZISHA?

NI VYEMA ZITTO KUELEZEA MSIMAMO WAKE HADHARANI KAMA ANAONA ANA HAKI/UHURU KUFANYA HIVYO. LAKINI KAMA ALIKUWA HAKUBALIANI NA MAAMUZI HAYO SI ANGEBAKI NDANI YA BUNGE? MAANA BADO ALIKUWA NA HAKI/UHURU KUFANYA HIVYO!

NADHANI ZITTO ATAMBUE KUWA NI MTU MUHIMU SANA NDANI YA CHADEMA NA AELEWE ATABEBA FAIDA AU LAANA YA KUPARAGANYIKA KWA UPINZANI NCHI HII. KUHESHIMU MAAMUZI YA PAMOJA NI MUHIMU LAMSINGI MAAMUZI HAYO YAWE NA MANUFAA KWA WANANCHI WANAO WAKILISHWA. KATIKA HILI NAAMINI UAMUZI WA CHADEMA ULIKUWA NA MANUFAA KWETU TUPENDAO MABADILIKO.

KAMA ZITTO ANADHANI KUJIOSHA KWAKE KUTAMUONGEZEA UMAARAFU, KAKOSEA, MAANA MIMI KAMA MOJAWAPO YA WAFUASI WAKE WA KARIBU AMENIHUDHUNISHA

AELEWE SERIKALI, CCM NA VYAMA PINZANI KWA SASA VINATAFUTA KILA NAFASI KUIANGAMIZA CHADEMA, MOJAWAPO YA NJAMA HIZO NI KUFANYA UPOTOSHAJI NA KUMOBILIZE PUBLIC BIAS AGAINST CHADEMA.

ZITTO JARIBU KUFIKIRI BEYOND PERSONAL INTEREST
 
All well said, I can see national interest first, whoever contravenes this, is too shallow and narrow to see new TZ
 
Huyu dogo mie nilishamshtukia siku nyingi sana, tangu wakati ule alipokuwa anainadi Dowans. Kulikuwa na taarifa kwamba yupo karibu sana na kiranja mkuu wa mafisadi Rostam.
 
Huyu Zitto mie nilishasema nae ana element za u-CCM, ameshanunuliwa na CCM. Ndio maana anavijisenti visivyoeleweka vimetoka wapi. Yaelekea alinunuliwa wakati ule alipokuwa ile kamati ya madini. Atakuwa alihongwa huyu, ndio maana anauma ,kung'ata na kupulizia! Jamani huyu tusimwesabie kama mwana mapambano! Simwamini kabisa huyu! Njaa kitu kibaya sana. Huyu amekuwa kama CUF, TLP, NCCR, n.k.
 
Huyo bwana mdogo zitto kabwe anajisikia sana na chadema isipoangalia itapotea njia. Chadema iache style za ccm kwamba mtaji wa chama eti ni kikwete. Chama kinachosimama kwa nguvu ya mtu hicho siyo chama. Ninachokiona mimi kwa zitto ni kwamba anadhani yeye ni muhimu sana kwa chama. Hata ongea yake ni ya 'nyodo' sana. Ushauri wangu kwa chadema ni lazima ikomeshe tabia hiyo ya kipuuzipuuzi na kama mwenendo wake ukiendelea basi ni bora aondolewe ili akajiunge na hao mafisadi walioanza kumlainisha. Sidhani kama zitto hafahamu kwamba maamuzi yanayofikiwa kwenye vikao halali vya chama ndiyo yanakuwa maamuzi na msimamo wa chama. Kinachobaki ni kutetea maamuzi hayo na kama hawezi kutetea basi ilikuwa bora akae kimya badala ya kubwabwaja bwabwaja kama kasuku mbele ya waandishi wa habari. Huyo bwana mdogo ameniudhi sana na kitendo cha kueleza kilichotokea ndani ya kikao cha chama.
 
It is soo sad kwa kaka yangu mpenzi Zitto. Anapaswa kukaa kimya... Yuko juu ktk media, alikua juu kwa mema na sasa anakoelekea atakua juu kwa mabaya. Asidhani hii hali ni nzuri kwake hata kidogo maana anakua kamna amerogwa, atakwisha kabisa kisiasa na hatakuwa tena Zitto anayekubalika na jamii. Nadhani Zitto the only way ya kutoka tena ni kutafuta BUZWAGI nyengine bungeni Anne Makinda amfukuze apate ujiko na iwe issue atakayowalipua mafisadi akiwamo RA, Lowassa na Chenge, na hata JK ili kurudisha imani ya wananchi kwake, vinginevyo anakoelekea wananchi wataendelea kuaminishwa na kuamini kwamba amenunuliwa na akienda CCM ama NCCR atakua kama Mbatia, Tambwe Hiza ama Salum Msabaha.
Tina,
Ni faraja kubwa kukuona tena hapa JF.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom