Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Nasikitika saana na siasa za Zitto na simwelewi kuwa yeye ni msemaji wa chama au anaamua kuharibu tu. Zitto hakubali maamuzi ya wengi kwa nini? Sitta mbona hakutoka na kusema hakukubaliana na maamuzi ya kutemwa ? baada ya kuwa wameshakubaliana kwenye kikao ikawa imekubalika na wote. Lakini sasa wewe ukitoka nje na kuanza kuongea ovyo unadhani unajipa ujiko? aisee bora utoke chamani maana watu wana uchungu na maendeleo hatutaki kuona ukilikwamisha taifa hili. Harafu hujui maana ya upinzani, angalia siasa za nje, mpinzani ni lazima amkosoe yule aliyepo madarakani kwa point zinazgusa jamii vinginevyo kakungekuwa na upinzani. Unajikomba nini Zitto??? na vimali ulishapewa ukasema hutaki siasa umerudi kufanya nini huku tena, ulisema unataka kufundisha huko kungekufaa sana.
 
sikuona sababu ya Zito kwenda kuongea kwenye vyombo vya habari, ulishawaona lini sisiem wakitofautiana na kwenda kukimbilia vyombo vya habari, tunajua kuwa kuna watu ndani ya chama wanatumiwa vibaya nasema mtapita , mimi hapa simuelewi zito hata kidogo kwani angekaa kimya kungemuumiza nini kwanini akimbilie vyombo vya habari? anashindwa hata na shibuda ameongea ki mafumbo, inauma sana watu wanapoleta mzaha wakati wanatuwakilisha
 
Ajifunze nini?kuna la kujifunza ndani ya CCM kweli? mpe ushauri mzuri sio umtume mtu mwenye akili timamu akajifunze MIREMBE.
 
I am sick 'n' tired of zitto. shida ndo zinampelekea kuwa hivyo mdomo wote ule aliokuwa nao ilikuwa ni ziki tu. Sasa anaharibu kweli kweli. Nakubaliana kuwa mambo ya ndani ya chama yabaki kuwa ndani ya chama sasa wewe ukitoka na kwenda kuongea kuwa furani na furani ndio waliosema unawasemea na wewe kujiosha? nashindwa hata kujieleza nilivyo panic . . .
 
Hata ccm wana nafuu,hawatoki nje ya vikao vya chama na kuanza kuropoka hovyo kwenye vyombo vya habari.
Jamaa ni destructive kwenye chama.Kuna haja gani ya kuzungumzia kile kilichotokea nyuma ya pazia.Kwa sasa hivi chadema wamuache tu, atajimaliza mwenyewe tu kama CUF walivyojimaliza.
 
Zitto inataka aelewe kuwa CHADEMA hakuna utamaduni wa kumbembeleza mtu abaki ndani ya chama wakati yeye ndiyo chanzo cha kutaka kukigawa chama.

Kama vipi anaweza kuondoka asituletee kinyaa! Namwelewa anataka kuhamia NCCR ili waufanye mkoa wa kigoma tawala yao! Naomba CHADEMA wampe discipline.
 
Nasikia alikula mlungula kuhusu suala la madini baada ya hapo akawa kimya.
Naungana na anaesema kuwa njaa ni tatizo apa kichwani anaona kama atafukuzwa ubunge so ngawila zitatoweka
 
sidhani kama anaweza kuacha chama cha kitaifa na kwenda cha mkoa,ina maana kelele zote kuwa yeye ni nationalist ataziacha na kuwa regionalist?
 
Kutokana na kichefuchefu (haswa baada ya kusema anamtambua JK ni amiri jeshi mkuu na alama ya bunge na hivyo si vizuri kutoka bungeni na kwa kiburi kabisa kusema anasubiria hatma yake chamani kutokana na uamuzi wake huo) ambacho mh. Zitto Kabwe ameendelea kuleta ndani ya CHADEMA wana JF wenzangu nilikuwa ninatoa mapendekezo kuwa huyu jamaa ni wa kuogopwa kama ukoma, na ni kidudu hatari kuliko KIRUSI CHA UKIMWI kwa wana upinzani, wapigania haki na kwa wananchi wa Tanzania waliodhulumiwa haki zao kwa muda mrefu na chama tawala cha CCM. Kwangu mimi namwona ni msaliti mkubwa wa Watanzania na upinzani. Hivyo ni nilikuwa napendekeza aondolewe CHADEMA haraka kwani amepandikizwa na CCM. Nakishauri CHADEMA kimvue uanachama ili kunusuru upinzani wa ukweli ambao umebaki peke yake CHADEMA. Je wana JF wenzangu mnaonaje? Je aendelee kubaki CHADEMA au aondolewe. Ushauri utakaopatikana hapa ukiambatana na sababu za msingi, naomba CHADEMA waufanyie kazi.
 
Amefanya nini Zitto wa Kabwe? Amesema nini na lini?
 
zito unatuabisha please, ikiwa sisi wananchi wa kawaida tunawaunga mkono wewe mbona upo kinyume unajua hatupendi hayo mambo yako , tulikuamini sana ila sasa unapoenda sio, ivi unajua kuwa sisi tuna uchungu na nchi hii na tumekupa tu dhamana ya kutuwakilishi, ona akina Warioba, Jaji Mkuu maneno yao yantutia moyo .

Dear Zito , still you have an ample to change tunakupenda na tuna kuamini kindly usituangushe wala usituhudhunishe, when you fight you need to be risk taker, all the best,

MZEE GOMEZI

Inaelekea watanzania tumeathiriwa sana na style ya siasa za CCM.

Kwanza: Alokisema Zitto sio kigeni kwani tayari kilishatoka katika umma kabla hata ya yeye kusema....kama aliulizwa hilo swali mlitaka adanganye? Waswahili wanasema, mficha uchi/magonjwa......Sasa kama mnataka CHADEMA hali iwe mbaya hadi kufikia stage ilipofika CCM ndio muanze kuambiwa hali halisi then no wonder watanzania/wapiga kura walio wengi bado wanaamini kuwa hakuna MBADALA BORA WA CCM..........

Tuache kukumbatia siasa za ujanjaujanja zinazolenga kutulaghai kwa kuficha ukweli wa hali halisi......Mabadiliko ni pamoja na jinsi ya kufanya siasa lakini sio cut and pest ya CCM halafu tutegemee ukombozi wa kweli kutakana na aina ya wanasiasa hao ama siasa za aina hiyo....
 
Zitto aangalie wachawi wasijeingilia mwenendo wake wakamfanya kama marehemu Chacha Wangwe, nasikia CCM kuna wachawi wengi.
 
ZITTO anahitaji uenyekiti wa kamati hasa ile ya hesabu za mashirika ya uma. Sasa atafanyaje ili asipewe mtu wa NCCR au CUF ni kujifanya kuwa yeye haungi mkono mamabo yanafanywa na CHADEMA. Anapenda vyeo sana huyu jamaa kwa hiyo huwa anafanya lolote kwa maslahi yake binafsi ya kupata vyeo. Ni bora angenyamaza kimya ingawaje kutokwenda pia ni credits kwa CHADEMA kuliko angeenda halafu angebaki bungeni wakati wenzake wameendoka ingekua more worse.

Shapecha yaani uko right kabisa!
Hakuna kingine zaidi ya hiki, huyu bwana inaonekana kuna faida aliipata huko na kwenye swala la DOWANS sasa anataka kutowaudhi wafadhili wake ili akumbukwe kwenye hizo kamati, hakuna kingine ni tamaa na ubinafsi kwa mjinga huyu, ameniudhi sana kwa kweli!! Kabisa i recall his DARUSO days!!

Hivi hizi kamati zinachaguliwaje bungeni? manake naona dogo sasa amekuwa prostitute wa kisiasa!
 
Analeta tabia kama za CCM kila mtu anaongea madhara yake anatoa mpaka siri za chama ooh tulipiga kura wengi ikawa wape.
Zitto nowdays amekuwa muoga kiasi icho ata akasita kuingia bungeni?
 
sikuona sababu ya Zito kwenda kuongea kwenye vyombo vya habari, ulishawaona lini sisiem wakitofautiana na kwenda kukimbilia vyombo vya habari, tunajua kuwa kuna watu ndani ya chama wanatumiwa vibaya nasema mtapita , mimi hapa simuelewi zito hata kidogo kwani angekaa kimya kungemuumiza nini kwanini akimbilie vyombo vya habari? anashindwa hata na shibuda ameongea ki mafumbo, inauma sana watu wanapoleta mzaha wakati wanatuwakilisha

Sasa kama CCM ndio reference ya aina ya siasa za kutuletea Taifa bora then kuna umuhimu gani wa kujenga CHADEMA Makini na yenye nguvu na sio huu ujanjaujanja tunaoanza kuumona waziwazi sasa......
 
Shapecha yaani uko right kabisa!
Hakuna kingine zaidi ya hiki, huyu bwana inaonekana kuna faida aliipata huko na kwenye swala la DOWANS sasa anataka kutowaudhi wafadhili wake ili akumbukwe kwenye hizo kamati, hakuna kingine ni tamaa na ubinafsi kwa mjinga huyu, ameniudhi sana kwa kweli!! Kabisa i recall his DARUSO days!!

Hivi hizi kamati zinachaguliwaje bungeni? manake naona dogo sasa amekuwa prostitute wa kisiasa!

Simple minds = Sustainable mediocre nation
 
Zito ulianza taratiibu.
Mara ukatetea mitambo ya dowans inunuliwe.
Hadi Mwakyembe wa ccm akakushangaa.
Leo unajifanya wewe ndio wewe chadema hawana sauti kwako.
Yuko wapi Lawrence Masha?
Na wewe utapotea kama yeye.
 
mie nadhani atupe sababu kwanini alikuwa hakubaliani na pendekezo hilo,lazima alikuwa na sababu,sasa asiseme tu tulipiga kura wengi wape,vilevile atuambie kwanini hakukubaliana na maamuzi yale then uamuzi utolewe na wana JF.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom