Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
zitto ameongea vizuri sana... tatizo humu jamvini tunataka mambo ya upinzani yaende kama mechi ya kinondoni muslim na tambaza

na hayo ya kupingana yangetokea ccm kesho ungesikia mtu katolewa chamani

Samahani wakuu kwa kudigress, bab ACID umenikumbusha mbali sana kuhusu mechi za Kinondoni na Tambaza.

 
Me nadhani chadema ni chama cha demokrasia so demekrasia inatakiwa ipewe kipaumbele in everything including kukiendesha na sio tu kuipigania hiyo democracy kwa ajili ya wananchi. ME nadhani zitto alikua na haki ya kidemocrasia kufanya vile but cha msingi ni kwanini! So if posible angeombwa azitaje hizo sababu na zikipimwa zikaonekana ni za msingi hamna shida ataendelea kuwa kiongozi wetu but if nat ndo tuzijadili na iangaliwe azabu ya kumpa thats it..!

4me im taking zito kama changamoto kwenye chama so inazidi kuimarisha chama, hatutaki chama kama sisiem cha ndio mzee ndio mzee hapana lazima kuwe na watu wanaotuchalenge sisi kwa sisi ili tuzidi kuimarika kwani me ni muumini mkubwa sana wa ile usemi usemao wagombanao ndo wapatanao...! Kama mtu na mkewe wanagombana bwana sembuse viongozi wa chadema..! tuendeleze mapambano mambo madogomadogo kama haya yasiturudishe nyuma...!
 
Me nadhani chadema ni chama cha demokrasia so demekrasia inatakiwa ipewe kipaumbele in everything including kukiendesha na sio tu kuipigania hiyo democracy kwa ajili ya wananchi. ME nadhani zitto alikua na haki ya kidemocrasia kufanya vile but cha msingi ni kwanini! So if posible angeombwa azitaje hizo sababu na zikipimwa zikaonekana ni za msingi hamna shida ataendelea kuwa kiongozi wetu but if nat ndo tuzijadili na iangaliwe azabu ya kumpa thats it..!

4me im taking zito kama changamoto kwenye chama so inazidi kuimarisha chama, hatutaki chama kama sisiem cha ndio mzee ndio mzee hapana lazima kuwe na watu wanaotuchalenge sisi kwa sisi ili tuzidi kuimarika kwani me ni muumini mkubwa sana wa ile usemi usemao wagombanao ndo wapatanao...! Kama mtu na mkewe wanagombana bwana sembuse viongozi wa chadema..! tuendeleze mapambano mambo madogomadogo kama haya yasiturudishe nyuma...!

Zitto anaweza kusema tu kwamba hakuweza ku walk out kabla ya kuwasiliana na wapiga kura wake kujua wanavyofikiri kuhusu hilo, hii sababu tosha kwangu. Wawakilishi wanatakiwa wafanye matakwa ya wananchi, sio kuwaamulia wananchi.
 
Hivi CHADEMA haina msemaji? Manake hizi kauli za mtu mmoja mmoja ndizo zinazoleta mgawanyiko. Pamoja na kwamba CHADEMA walipiga kura, suala hilo ni suala la ndani ya chama ambalo halikupaswa kuzungumzwa na mtu mmoja mmoja bali na msemaji wa chama tena kwa protokali...! Haikupaswa Zitto kuja na kusimama kwenye TV na kuanza kujielezea yale ambayo walishaamua kwa pamoja, na haswa kwa nia ya kujisafisha au kufanya wengine waonekane walikosea...!

With this background, bado nahoji sana credibility ya Zitto na aina ya Siasa anazofanya...! Amekua anajisahau sana na kuleta siasa za ki-ulaya kwa kufikiri kujitangaza ovyo ovyo misimamo yake (kwenye facebook, twitter etc) itamfanya aonekane ni bora zaidi.

Kauli kama hizi ambazo zinaonyesha wazi wazi mgawanyiko wa CHADEMA (kwa nia ya kujitangaza ili aonekane yeye alikua na msimabo bora zaidi ya wengine) zinapunguza credibility badala ya kuongeza credibility ya CHADEMA...! Hapo tu ndio Zitto pamoja na umahiri wake anapojisahau...! It will cost him in a long run...!

Hivi CCM inapotumia suala la AMANI kulinda nafasi yake katika utawala inapokuwa haramu iweje Chadema kutumia kuepuka migogoro/tafauti ambazo zipo iwe halali? Chadema na haswa uongozi wake wametumia sana huu wimbo wa kuepeka kuonekana kuwa wana migogoro katika kufunika maovu na mapungufu mwengi sana ambayo yanakichimbia chama chao kaburi huku wakisheherekea.......

Dr Slaa anapomsema vibaya Zitto katika mitandao na Facebook hakuna makosa na wala haleti mgawanyiko lakini Zitto anaposema kuna tofauti, analeta mgawanyiko na kuchochea mgogoro ambayo ukweli ipo mingi mno......

Dr Slaa anapokimbilia kutoa kile anachokiita msimamo wa chama kuhusu wabunge kususia hotuba ya Rais huku wabunge wakiwa na kiongozi wa kambi na mnadhimu wa kambi hadi kupelekea Mwenyekiti wa chama kusema msimamo unaopingana na Dr Slaa kuhusu uhalali wa Rais Kikwete ni sawa, lakini Naibu Katibu Mkuu anapotoa ufafanuzi wa msimamo wake na wenzake zaidi ya 15, ni dhambi....

Acheni kumdanganya Dr Slaa. Mtambue kuwa Jamiiforum na Facebook ndio imekuwa authority yake katika kufikia na kuetetea maamuzi ambayo apart from headlines zinazowafaidisha wanahabari, in a long run ni CHADEMA na Watanzania ndio watakaoumia. Mkitaka kujua nani mbinafsi ni bora kwanza mkajua the whole story na labda mumuulize Dr Slaa ni nani mwanzilishi na aliyeshinikiza ama kuwashawishi wabunge kususia hotuba ya Rais na kwanini msimamo wake na Mbowe kuhusu kumtambua ama kutomtambua Rais Kikwete unatofautiana.....

Kumbukeni hata Hitler alikuwa hero wa wengi na waliothubutu kutofautiana naye walikuwa ni wasaliti wachache.....Well haya ni maoni ya ndugu wa karibu wa Dr Slaa hivi karibuni...
 
Sipendezwi na jinsi Zitto anavyoropoka hovyo, lakini ili asikichafue Chadema bora aachwe atajikuta mwenyewe yupo nje. Tukichukua mifano michache tangu wakati ule wa kugombea Uenyekiti wa Chama vyombo vya habari na hata CCM walionekana kumbeba Zitto kama vile wanaitakia mema Chadema. Wakati anagombea ubunge mwaka huu akasema 2015 anataka urais. juzi juzi tena akawa anataka kuwa Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Sasa amekuja na suala la kilichaamuliwa na kikao cha wabunge wa Chadema na kukiongea nje ya vikao wakati akijua yeye siyo msemaji wao. Kama walipiga kura hata kama alikuwa na mawazo tofauti anaendeleaje kupingana na mawazo ya Chama?
 
:whoo:Guys huyu jamaa karibu kila wakati anaingia geti la Rostam: Kwale street so naamini kuna jambo tu hapa...soon ataleta mgogoro ndani ya chama

Na yule anayeingia na miwani na kuvaa kapelo/Cap(Kofia) wakati CCTV zinamrekodi naye tusemaje??? Wengine wana ushahidi mwingi tu wa huyo anayevaa miwani sasa kama mko tayari kuendelea na majungu haya....mnakaribishwa
 
to me Zitto is a coward, a traitor and an impostor.
So he must go out of cdm.
 
Zitto unasema wewe ni democrat na unapenda kuongea unaloliamini na unapenda uwazi na ukweli. Lakini yanayojiri kwenye vikao vya chama ni siri ila matokeo ya hivyo vikao sio siri. Hivi ulivyokwenda TBC 1 na kubwabwaja yaliyojiri ndani ya vikao vya chama ulikua unataka wananchi wakueleweje? Kuwa utoto unakusumbua mpaka uropoke kila unachokijua bila ya kupima unaongee na nani na nini unakiongelea? Kuwa wewe umekua kimwili tu na sio kimawazo? Naomba nikupe mfano. Hivi wewe Zitto ukiingia chumbani kwa mama yako na bahati mbaya ukamkuta anavaa nguo, utatoka na kuwaambia watu kuwa umemwona mama yako akiwa mtupu?
 
Kumfukuza Zitto itakuwa ni kukubali kwamba CHADEMA haina utamaduni wa kukubali tofauti ya mawazo chamani.

Kwa chama kinachotaka kuleta demokrasia zaidi Tanzania, ambacho jina lake linabeba neno demokrasia, jambo hili litakuwa baya sana.
Kiranga - tatizo sio CDM haina utamaduni wa kukubali kutofautiana mawazo. utamaduni upo sana na ndio maana wakafikia hata kupiga kura kwa ishu hii. Tatizo ninaloliona ni kule kwa Zitto kutangaza TBC kuwa hukukubaliana sasa unamtangazia nani? hii ina maana yeye Zitto ndiye hana utamaduni wa kukubali wenziwe wakiwa tofauti na yeye, anajifanya yeye ndo kila kitu. Mimi naona ni bora tukapoteza jimbo lake hilo kuliko kuipoteza CHADEMA. Life without CHADEMA in TZ I can't imagine! Viongozi wakuu wamchukulie hatua haraka (au kama muungwana aombe msamaha) la sivyo fukuza tu hiki ni kirusi hatari....:angry:
 
zitoo ni nani katika chama mpaka apingane na wakuu wake hakuna demokrasia katika hili huyu ni msaliti na chama kichukue hatua dhidi yake faster au wananchi tuchukue hatua???????msaliti na auawe uchi na aibu imrudie mamaake.;;;

Tumeingiliwa na Mungithi wajameni !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
wao wanataka katiba mpya/tume huru ya uchaguzi, nyinyi mnataka nini hasa?

Wengi tunataka katiba mpya ingawa wengi hatuijui hata hii iliyopo wakiwemo zaidi ya asilimia hamsini ya wabunge wetu...

Lakini je, hatua ya wabunge wa chama chenye wabunge 47 kutomtambua RAIS aliyepata kura zaidi ya asilimia sitini ama tuseme hata hamsini tu na kiongozi wa chama chenye wabunge zaidi 260, ni hatua itakayoweza kutupatia hiyo katiba mpya??? Hivi kutoa ishara za kutothamini ama kuheshimu UTAWALA mbele ya jamii ambayo asilimia 45 ya waliopiga kura wanasema wameshawishiwa na kuthamini AMANI na haswa katika taifa lenye kutishiwa na mgawanyiko wa kijamii huku tukijua wazi matokeo ya migawanyiko ya aina hiyo, ndio njia muafaka wa kufanikisha kupatikana kwa katiba mpya?
 
Hizo siri za chama ndo zinatufikisha kubaya siri siri mpaka lini? Mbona mkiambiwa mikataba ni siri ya serikali mnalalamika weeeeee.
Siri siri siri ndo mdudu gani huyo jamani??

Mkama - Kwa ustaarabu tu wa kimaisha ya kawaida sio lazima kila kitu kiwe open kila wakati. Kuwacha kila kitu open kila wakati ni rahisi kuruhusu mashambulizi unnecessarily.Mfano wako wa mikataba ya siri na hapa wala hauendani - umejichanganya. Siri ni lazima hata nyumbani kwako na mke wako, au kwenye mambo ya kifamilia otherwise utalia huku umesimama hapo hapo badala ya kulia huku unakimbia.....
 
Zitto anaweza kusema tu kwamba hakuweza ku walk out kabla ya kuwasiliana na wapiga kura wake kujua wanavyofikiri kuhusu hilo, hii sababu tosha kwangu. Wawakilishi wanatakiwa wafanye matakwa ya wananchi, sio kuwaamulia wananchi.

Wabunge ukaa kama kamati na kukubaliana...... kichama. wewe vipi? nyie ndo wachafuzi wa hali ya hewa?
 
Kumuondoa Zitto kwenye chama sio ufumbuzi! Inabidi CHADEMA wakae naye na kumkumbusha wajibu wake kama kiongozi na utaratibu wa utoaji habari hususani zile za siri! Huu ni wakati ambao CHADEMA inahitaji mshikamano wa hali ya juu kuliko wakati mwingine wowote na kwavile madai yao ni ya msingi, umma wa watanzania uko nyuma yao! Tunahitaji Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na udhibiti imara wa rasilimali za taifa ambazo kwa sasa ni kikundi kidogo cha CCM (mafisadi) ndicho kinachofaidi!! Majority of CCM pia hawafaidi wanabakia kusubiri kila baada ya miaka mitano wahongwe kanga,t-shirts, kofia na chumvi kwa kina mama! Jamani mabadiliko ya katiba ni kwa manufaa ya watanzania wote, tuwaunge mkono CHADEMA!!
 
Kwani waliopiga kura za hapana ni Zito tu?Mbona ni yeye tu ndo aseme kuwa anasubiri hatima yake ndani ya chama? Kama anajua kilichofayika ni demokrasia ndani ya chama kwanini ahofie mustkabali wake ndani ya chama?Au anajua kuropoka kwenye vyombo vya habali ni kosa.Hajui ni wakati gani aseme nini.Watu kama yeye hawafai kuwa na madaraka makubwa kwenye jamii,ndiyo maana hata hawamuachii kushika uenyekiti wa chama.Mambo mengi sana kuhusu huyu jamaa ni ya uwalakini,anajiona yeye ndiyo mjuaji sana na amekomaa kisiasa.
Anapenda mashindano yasiyo na tija ndani ya chama.
 
zitto anaweza kusema tu kwamba hakuweza ku walk out kabla ya kuwasiliana na wapiga kura wake kujua wanavyofikiri kuhusu hilo, hii sababu tosha kwangu. Wawakilishi wanatakiwa wafanye matakwa ya wananchi, sio kuwaamulia wananchi.
mkuu leo asubuhi kwenye jambo tz tbc1 ndi alichosema kwamba mimi sikuchaguliwa na slaa/mbowe bali na wanakigoma kwa hiyo ridhaa yao ilikuwa yamhimu sana ili kuwalk out.
Halafu wanasema nini? Kumfukuza, thubutu, walifanya hivyo kwa kafulila na mwenzake siunaona yaliyowafika, siwamepoteza majimbo yote mawili? Au hawajifunzi?
Kwa taarifa yako chadema haina nguvu wala mvuto kwa majimbo ambayo yana waislamu wengi, zaidi ya umaarufu wa mgombea husika ndo maana hata akina kafulila walipoondoka chadema na mwenzake bado walipata hayo majimbo kupitia nccr mageuzi
leo hii natamani imfukuze zitto ili kifo chao kiwadie kwani watachaguliwa mbeya na kilimanjaro na sehemu zinazofanana na hizo tu.
Trust me.
Solution, (binafsi siipendi ccm lakini siipendi chadema zaidi ndo maana hata kura yangu nilikuwa tayari kuwapa ccm kuliko chama hicho cha kikabila/kidini/kifamilia.
Dr. Slaa you are the hores, i trust you, kupitia uongozi mwanana wa kikwete umeweza kupata nafasi ya kuananika mengi ambayo tulikuwa hatuyafahamu na vyombo vya habari vikapewa nafasi ya kuyaandika, thats big thanks kwa slaa,
lakini ndugu yandu slaa hao watu waliokuzunguka wengi si watu wazuri we know them and we can not trust them anytime hata leo kuwapa nchi, ndo maana hata wabunge wakuteuliwa wamewekana ndugu tu ni tofauti kabisi na cuf ambapo hatuoni ndugu yake seif au lipumba akipendelewa kupewa viti maalum.
Watch it out au fanya hima uungani na watu wa cuf hao wamekomaa kisiasa na hawanatamaa na madaraka then itakuwa easy kuwapeni nchi, other no and go to hell.
See you next time.
 
The only problem i see here ni fact kwamba hajakubali democracy wakati anaihubiri. Huwezi kupiga kura ya wengi wape alafu wakipewa unalalamika. Kitu kingine ambacho naona amekosea ni fact kwamba kwenda kwenye vyombo vya habari na kuropoka wakati sio makubaliano ya hiyo democracy. Lastly kila kikundi, taasis au chama huwa na msemaji mkuu na utaratibu wa kuongea na vyombo vya habari. kama zitto alikiuka huu utaratibu then chama kwa kupitia taratibu zilizopo kinatakiwa kimuonye na kumkumbusha hizo taratibu.
mi nitawapa mfano mdogo tu, niliwahi kutoa takwimu kwenye vyombo vya habari zinazohusu organization niliyokuwa nafanyia kazi, ilikuwa ni right data na very good peace of information ambayo ilikuwa inatoa good picture ya organization. Staffs wenzangu kibao walinisifia na kunipongeza in a good will. Lakini sikufuata utaratibu na wala sikumuambia head of communication dept, na mabo hayakuwa mazuri kwangu ilibidi niandike barua ya apology na warning kali ilifuata.
Sasa kama we si msemaji mkuu na wala hujaombwa kuwakilisha kherehere cha nini?!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom