Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,079
- 9,245
1. munapenda sana kuchukulia jambo moja kama ndio tathimini ya mambo yote ya chasema yanavyotakiwa yawe kwa vile kila mtu anaona yeye ndio mtathimini wa kila jambo chadema inafanya watu wanajia mbalimbali za kupeleka ujumbe au kupinga jambo kwenu nyie mungeona la maana kama 2. wangeitisha maandamano nvhi nzima munasemaje pale tume yenyewe inapokiri kutoa takwimu za kura zisizo sahihi watu waa ajabu sana nyakati za ndio mzee zilikwisha chadema wako sa hihi na njia muafaka kabisa wanastahili pongezi kwa ujasiri wao 3. hilo la zitto ni mambo yao ya ndani wewe na mimi hatuwezi kufikia hitimisho kwa hiyo 4. nakushauri usidhani wanatafuta cheap popularity kupishana mawazo hata mume na mke huwa wanapishana baba na mwana pia ndio dynamics za maisha
Hili nalo nenozito wewe ni kiongozi wa chama na kama mlipiga kura na maamuzi yakafikiwa kwa mujibu wa kura hizo, hustahili kutuambia hayo unayotuambia leo bali kusimamia maamuzi ya kikao hicho na kuelezea msimamo wa walioshinda.
Hata kama ni democrasia,kama kiongozi unapaswa kusimamia maamuzi ya chama.
Mnao shabikia upuuzi huu wa zito kwa kisingizio cha demokrasia ndani ya chadema hamjui maana ya uongozi.
Naanza kujiuliza vizuri ni kwanini john mnyika bado anakaimu madaraka ya zito ilhali yeye zito yupo.
I still believe Zitto was sending a message. To whom I do not know. Kwamba yeye hakuunga mkono hoja ya kususia hotuba ya Kikwete.Hivi CHADEMA haina msemaji? Manake hizi kauli za mtu mmoja mmoja ndizo zinazoleta mgawanyiko. Pamoja na kwamba CHADEMA walipiga kura, suala hilo ni suala la ndani ya chama ambalo halikupaswa kuzungumzwa na mtu mmoja mmoja bali na msemaji wa chama tena kwa protokali...! Haikupaswa Zitto kuja na kusimama kwenye TV na kuanza kujielezea yale ambayo walishaamua kwa pamoja, na haswa kwa nia ya kujisafisha au kufanya wengine waonekane walikosea...!
With this background, bado nahoji sana credibility ya Zitto na aina ya Siasa anazofanya...! Amekua anajisahau sana na kuleta siasa za ki-ulaya kwa kufikiri kujitangaza ovyo ovyo misimamo yake (kwenye facebook, twitter etc) itamfanya aonekane ni bora zaidi.
Kauli kama hizi ambazo zinaonyesha wazi wazi mgawanyiko wa CHADEMA (kwa nia ya kujitangaza ili aonekane yeye alikua na msimabo bora zaidi ya wengine) zinapunguza credibility badala ya kuongeza credibility ya CHADEMA...! Hapo tu ndio Zitto pamoja na umahiri wake anapojisahau...! It will cost him in a long run...!
Mjumbe anapokuwa kwenye kikao ni ruhusa kabisa kupinga jambo wakati wa majadiliano lakini jambo hilo likihitimishwa kwa kura na ikionekana wengi ndiyo wanaounga mkono basi huo ndiyo unakuwa msimamo wa chama na kila mwanachama anapaswa kuutetea. Sasa kama Mhe. Zitto bado anaendelea kuupinga nje ya kikao, basi huo utakuwa ni utovu wa nidhamu na lazima akemewe na chama kupitia vikao vyake halali. Alichopaswa kueleza Zitto (kama ilikuwa ni lazima aeleze) ni kusema kwamba wakati wa kikao alikuwa na msimamo tofauti lakini uamuzi wa kikao ndiyo anaouheshimu na kuutetea. Hiyo ndiyo GHARAMA ya demokrasia.
- Mkuu kweli ninakusoma sawa sawa, eti kuwafukuza walio na mawazo tofauti na yako si ndio yamelifikisha hili taifa lilipo sasa, au?
William.
zitto ameongea vizuri sana... tatizo humu jamvini tunataka mambo ya upinzani yaende kama mechi ya kinondoni muslim na tambaza
na hayo ya kupingana yangetokea ccm kesho ungesikia mtu katolewa chamani
Me nadhani katika hili Zitto anakosea wajibu wake wa kuwa naibu Msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani. Ni bora saa zingine akawa anapima maamuzi anayoyachukua. Huwezi kuelezea umma unakutegemea eti ni maamuzi yako wakati wenzako wanafanya analysis ya impact ya wanachokifanya. Huu si mda wa kuirudisha nyuma Tz kwa madai kuwa ni maamuzi ya kukubaliana kutokubaliana
Tufanye utafiti na si kukwepa lawama. Kama upo ndani ya chama by the way, unakubaliana na misingi ya chama sasa huu kutoka nje ya chama na kukimbilia kwenye vyombo vya habari kunatoka wapi. Kwanza, is Zitto Msemaji wa chama? nadhani huyu Mh anapaswa kuangalia vizuri namna ya kuhandle media. Media people brought Lowasa and Kikwete into power and they are now almost killing them except those owned by Rostam