Wazee Heshima mbele,
Maraisi 15 walikutana hapa bongo kuzungumzia ishu za nchi zao na hasa umoja wao wa kusini, Zimbabwe ilikuwa ni moja ya ishu zilizozungumziwa,
Zimbabwe ni nchi huru kama zilivyo nchi zingine zote za dunia, inao uhuru wa kufanya itakavyo kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, hakuna nchi yoyote nyingine duniani yenye uwezo wa kuiambia kuwa sheria zake hazifai, Rais Kikwete, hana uwezo wowote kisheria zabongo wala za kimataifa kuingilia shughuli za kisiasa au kisheria kwenye nchi huru ya Zimbabwe,
Mugabe ni rais aliyechaguliwa kuwa rais wa nchi kwa mujibu wa katiba za nchi hiyo, anachohitaji sasa hivi ni ushauri wa nini cha kufanya wakati ardhi ipatayo 95% ya Zimbabwe imo mikononi mwa wazungu, huku wazawa yaani wazimbabwe wenyewe wanamiliki only 3.5% ya ardhi yao wenyewe, yeye kama rais wa nchi anatakiwa kuwaambia nini wananchi wake? Kwamba faida ya wao kupigania uhuru wa kuikomboa nch yao ilikuwa ni nini?
Wazungu kama kawaida yao wamepiga kelele sana kuhusu huu mkutano, na kutushambulia sana na hasa rais wetu, lakini wazungu hawa wanashindwa kufanya lolote kuhusu Iran na utengenezaji wa nyuklia, wazungu hawa wanasema ni sawa Israel kuwa na bomu hilo, lakini sio Iran, halafu wazungu hawa majuzi tu wanajeshi wao 15 wamechukuliwa na Iran, mpaka leo hawajafanya kitu, WHY? kwa sababu wanajua kuwa sheria za kimataifa haziwaruhusu kufanya lolote Iran inapodai kuwa sheria zake zilivunjwa na wanajeshi hao wakizungu,
Je Zimbabwe ingekuwa ndiyo imewashika wanajeshi hao 15 ingekuwaje? Matatizo ya Zimbabwe ni ya wa-Zimbabwe wenyewe na yatatuliwa na wazimbabwe wenyewe, wakihitaji msaaada wataziomba nchi za Afrika kwanza ziwasaidie, tumechoka na wazungu na unafiki wao, kama upinzani Zimbabwe wamevunja sheira za nchi hiyo, Muuugwana hawezi kuwasaidia,
na wazungu wanyamaze watuachie Afrika yetu, maana wao wanaweza kuwakamata watu Afaghanstan na kuwaweka rumande Cuba against sheria zote za kimataifa, vijana tuwe waangalifu na hizi propaganda za wazungu