Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!

Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!

Oh please.. let me edit... intelligence ni kama ubongo wa Security diplomacy!
dah!
huwezi kufanikiwa kwenye peace/security diplomacy bila intelligence!
hatujafeli kwenye hilo!
 
_42742877_mdcoffice_afp_203b.jpg

Zimbabwe police raided opposition headquarters on Wednesday​


Kabla hajaondoka Harare kwenda Dar Robert Karigamombe Mugabe aliamua kuwaweka wapinzani sawa ili wasije wakafanya fyoko fyoko!
 
tusijipe matumaini makubwa katika suala hili. vilevile, habari nyingi zinaandikwa kwa kuangalia upande mmoja--wa mugabe au wa uk,wapinzani.

the way forward ni kumpatia Mugabe an exit plan that would be ACCEPTABLE to him and Zanu-PF. Sasa kwasababu MDC wanadai Mugabe hakushinda uchaguzi kihalali, basi wanataka aondolewe na wao wapewe nchi.

suala ni kuwaridhisha mafahali wanne--Mugabe,Zanu,MDC[Tsivangarai],UK. Hii ni kazi ngumu na tusitegemee sana kwamba kikao hiki kitatoa "muarubaini" wa mgogoro huu.
 
Hivi punde nimemsikia Jeff Koinange (CNN) akizungumza baada ya Mkutano wa SADC na Bro Mugabe kuhusu hali ya Zimbabwe,Jeff ameripoti kuwa Bro Mugabe amesema "Mkutano ulikuwa mzuri na kwamba marafiki wa Africa wanajenga Umoja wenye nguvu ambao unajali matatizo ya ndani ya nchi bila kujali mashinikizo ya nje yakiongozwa na USA na uk".Hivi Punde Mh Jakaya Kikwete atatoa Taarifa rasmi ya Mkutano huo kwa Waandishi wa ndani na nje.Ngoja tuone nini kinaendelea kwa sababu inaweza kuwa Viongozi wa Africa wanazungumza tofauti kwa hawa wakubwa!,na wanamuona Mugabe kwa jicho tofauti pia! Kazi ipo!
 
Hivi punde nimemsikia Jeff Koinange (CNN) akizungumza baada ya Mkutano wa SADC na Bro Mugabe kuhusu hali ya Zimbabwe,Jeff ameripoti kuwa Bro Mugabe amesema "Mkutano ulikuwa mzuri na kwamba marafiki wa Africa wanajenga Umoja wenye nguvu ambao unajali matatizo ya ndani ya nchi bila kujali mashinikizo ya nje yakiongozwa na USA na uk".Hivi Punde Mh Jakaya Kikwete atatoa Taarifa rasmi ya Mkutano huo kwa Waandishi wa ndani na nje.Ngoja tuone nini kinaendelea kwa sababu inaweza kuwa Viongozi wa Africa wanazungumza tofauti kwa hawa wakubwa!,na wanamuona Mugabe kwa jicho tofauti pia! Kazi ipo!

Hapa ndipo ninapomkumbuka JKN(RIP),Mugabe angesomeshwa na uchaguzi ungekuwa ni wake aidha kukubali kuondoka kwa utaratibu au yatakayomkuta Tanzania isingempa Hata nafasi ya Ukimbizi.
 
WELCOMING REMARKS BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC

OF TANZANIA AT THE SADC EXTRAORDINARY SUMMIT, DAR ES SALAAM, 29TH MARCH, 2007

The Right Honourable Pakalitha Mosisili;

Prime Minister of the Kingdom of Lesotho and

Chairperson of SADC;

Your Excellencies Heads of State and Government;

Distinguished Delegates;

Ladies and Gentlemen;

It is my singular honour and pleasure to welcome you all to Dar es Salaam and to this Extraordinary session of the SADC Summit.

I am grateful that despite the short notice you could come to this meeting. Your coming is a clear testimony of your commitment to the maintenance of peace and security in our region. As we say in Kiswahili, KARIBUNI SANA, meaning you are very welcome.

Yours Excellencies;

This Extraordinary Summit has been convened upon the recommendation of the Ministerial meeting of the Double Troika, which met in Maseru on the 21st and 22nd March, 2007. That meeting reviewed the political and security situation obtaining in our region and reached the conclusion that the challenges facing the region at the moment required the attention of the Summit, as a matter of urgency.

Hence the Ministers recommended to me as the Chair of the SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation, the urgent need for the convocation of an Extraordinary Summit. Upon this recommendation, I undertook the necessary consultations with all the Heads of State and Government and upon your concurrence I convened this Extraordinary Summit.

Your Excellencies;

Ladies and Gentlemen;

We are gathered here this morning to consider the situation in the region with a view to addressing the challenges facing us.

Indeed, our region faces some daunting challenges. Fortunately, there are only a few hot spots which demand our attention and action. However complex and difficult some may appear none of them is impossible to fix. The combined wisdom and concerted efforts of all of us in the SADC region should be sufficient to handle any complex situation.

I believe, through open and frank discussions we will be able to diagnose properly the political and security problems facing our region and on the cause of action to deal with them. I am confident that we will be able to recapture the old glory of the SADC region being the most peaceful, the most stable and fastest growing region in the continent.

Excellencies;

Ladies and Gentlemen;

This meeting is being held at the Kilimanjaro Hotel, a historic place as far as the history of liberation of Southern Africa is concerned. Many meetings to strategise on the conduct of the liberation struggle were held in this hotel. President Mugabe, President Mbeki, President Pohamba and many comrades gathered here have vivid memory of that glorious past. We succeeded then against all odds, I am confident that we will succeed in our quest for a peaceful, stable and prosperous post-independence and post-apartheid Southern African region.

Once again I welcome you to Tanzania and wish you fruitful deliberations.

I thank you for your kind attention.
 
Mkutano umeisha huko Darisalama na nasikia wakoloni wetu wamesema together we stand with Mugabe . Ndiyo mambo haya jamani ?
 
Dr WHO: How does the land redistribution programme justify the torture of people perpetrated by Mugabe Government? How do you justify the killing of people undertaken by Mugabe/ZANU PF armed forces? How do you justify the plundering of economy and other miseries Zimbaweans are experiencing? In my view the problems happening in Zimbabwe have been caused by a clique of people in ZANU PF led by Mugabe. Haya ni matatizo aliyoyatengeneza Mugabe na ZANU PF kwa njaa zao za kungang'ania madaraka. Swala la ardhi alilikomalia baada ya upinzani kupata nguvu na yeye akalitumia kama silaha ya kubaki madarakani.

The fact will prevail and I am assure history will attest to this fact that: After, Mobutu, Mugabe and ZANU are the worst evils Africa and the world have witnessed!

What has been astonishing to me is the silence from AU and African governments. The young generation of African leadership should never tolerate what we have seen in Zimbabwe under any circumstances whatsoever! African leaders should not be allowed to hide their tyrany under the cover of a noble course such as land resditribution.

Mugabe would have carried out the land redistribution programme without torturing and killing people and without enchroaching on democracy and human rights. We should never allow Mugabe and ZANU PF to use land redistribution to justify their evil in Zimbabwe.

Just like Nyerere and Nkurumah, Mugabe is the victim of racist demonisation at its worse, and as I said certain things are so transparent it is laughable. 'That does not mean Mugabe is going to get the title of African leader of the century. But he may well do, as 90 percent of what is being pushed here, I know is intuitively rubbish; and nobody is going to tell me how academics, lawyers and journalist can turn on a fact or body of facts, to misrepresent a situation.

It is just a fact of life, political science or governance or just plain common sense, to think you can act like terrorist whether right or wrongly and threaten amongst other things to kill the leader ,and to think for one second when Security Forces get hold of you, they are going to give a damn about Geneva, or the precise letter of the law ,or foreign concerns about Human Rights abuse.

Even to think so is pure folly. Having worked briefly with the CPS i can tell you, if someone was found with plans on them to kill Prince William how do you think the police in this country is going to respond, when they hold you. Section 85 of the Crimal Justice Act, I suggest will be torn up or interpreted so widely you might as well forget talking about legal rights. And no Judge in the land unless he has cancer, and with two days to live; and wants to go out in style is going to challenge the Police action.

It is an intrinisic feature of terror tactics used against a government, that it will respond and in that process traditional standards or norms are suspended, as in instances on national emergencies. It is also a fact regardless of context ,that in that response, often innocent people, or just genuine critics, not terrorist may suffer, or have their liberties suspended. These are necessary evils, as Security and Intelligence work is not a precise science. The enemy does not advertise himself usually, and say here I am come and get me.

Zimbabwe has not set up assassination squads like the British government...yes they killed alot of republicans in Ireland and There is nothing I have heard, even from Western media, which indicates to me that things are out of control, in terms of managing dissent in the country comparing to police states like Uzbekistan or China.The government and State of Zimbabwe has to do what ithas to do to maintain order and stability, and deal with those determine to bring anarchy to the nation. That is very simple to understand, and I wish them well in that endeavour.

That said, i am not saying Mugabe is a saint but i am getting tired of these WAZUNGU telling us what to do and not to do...while they say nothing to regimes like SAUDI ARABIA where even elections do not take place or CHINA where they are basically told off
 
The government and State of Zimbabwe has to do what ithas to do to maintain order and stability, and deal with those determine to bring anarchy to the nation. That is very simple to understand, and I wish them well in that endeavour.
You are words remind me.....................................Lady Zindonga!
 
That said, i am not saying Mugabe is a saint but i am getting tired of these WAZUNGU telling us what to do and not to do...while they say nothing to regimes like SAUDI ARABIA where even elections do not take place or CHINA where they are basically told off

Wazungu wakisema tuuzieni migodi yenu kwa bei ya kutupa hilo si tatizo. Wazungu wakisema genisheni kila kitu hilo nalo si tatizo. Wazungu wakitengeneza kwao kiasi kwamba Waafrika hawataki kutoka huko hilo nalo si tatizo. Tatizo ni pale wanaposema kuna uvunjaji wa haki za binadamu kunakofanywa na watawala!
Tangu lini tumekataa kuambiwa cha kufanya na hao wazungu? Mbona hata Rais wetu mwenyewe ameomba Wazungu waje watueleze cha kufanya na mikataba?
 
Tabasamu umesema maneno mazito sana .Kuna unafiki sana sana na watawala hawa yaani wakoloni weusi JK alipigiwa kelele na makofi where is he taking us Tanzanians? Hivi ni kweli hawakuona sababu ya kumweleza Mugabe Ukweli ? Kumbe ya Zanzibar na Tunduru ni sehemu ya maisha ya Siasa Tanzania chini ya CCM.
 
Yale yale ya mganga huu .Angalieni sasa .
 
Maneno ya Mbowe kabla hajawika jogoo ukweli umebakia kuwa ule ule kwamba hapendi kuelezwa na anawachukia wapinzani kama mshikaji wake Mugabe anavyo ua huko kwao .Darisalama yaamua kutoyajali maisha ya wazimbabwe na waweka sahihi Changarai auawe ?
 
Maneno ya Mbowe kabla hajawika jogoo ukweli umebakia kuwa ule ule kwamba hapendi kuelezwa na anawachukia wapinzani kama mshikaji wake Mugabe anavyo ua huko kwao .Darisalama yaamua kutoyajali maisha ya wazimbabwe na waweka sahihi Changarai auawe ?
Tuelezeni nini kilijiri kwenye Mkutano Acha ushabiki wako wa kwamba wameweka saini Fulani auawe?Wao wana uwezo gani au mamlaka gani ya kuwapa wezo wa kuua raia wa Nchi Nyingine?
 
Lazima tukubali kwamba huu ulikuwa ni mkutano mgumu sana kwa tanzania na members wote wa SADC. Kwa kweli nampongeza JK kwa hili ambalo watu wengi hawawezi kuona picha kamili HIVI SASA.

Huu ni mkutano wa siri kati ya marais na hakuna mtu ambaye atafanya fyoko fyoko yale ambayo wanakubaliana, kwa nini tusiwapongeze kwa kumchagua T. Mbeki kuweza kuongea na chama tawala na cha upinzani. Kweli upinzani hawakuwepo MKUTANONI lakini tumesikia maneno makali yaliyotoka kwa rais wa Zambia na waziri wa South Afrika na JK kwenda Harare, leo hii hatuwezi kuwaambia wazungu ati tumemkemea Mugabe HADHARANI, haitawezekana - hii ni siri yao. SUBIRINI MATOKEO HII NDIO ITAKUWA CHACHU.

Mugabe anafahamu muda wake umekwisha na ameambiwa hivyo na matokeo tutayaona kwani hata wenyewe wenye nchi Zimbabweans wamefika kikomo, mzee mzima anatafuta njia ya kuondoka iliyo nzuri na ya heshima baada ya kuvurunda.
 
JK is just another stunt performer ! Anakaribu kufanya mazingaombwe akiona watu wanamjunia vidole basi anakaa kimya, leo hii tunashuhudia rais kikwete katika kutatua suala la zimbabwe na amekiri kuimudu zimbabwe !!!!

Note: Kikwete amekiri kuimudu zimbabwe !! Ok, thats ok, and good for him !

But will i have made a mistake if a call him "MROPOKAJI" just like "LOWASSA" ??

Siku hadi siku hadhi inazidi kushuka kwa upande wa JK huku shein akiwa nautral. Sasa basi, turudi katika kukiri kwake kwamba anweza kuimudu zimbabwe !

JE ZANZIBAR IMEKUWAJE ? TATIZO LISHAMALIZIKA ? NA KAMA BADO, ( which i know bado na haitakuwa bado mpaka anaondoka ikulu 2010 ) JE WAMEFIKIA WAPI KATIKA SUALA LA ZNZ ? JE AMESAHAU RESPONSIBILITY YAKE AU ANAZI-IGNORE ?

Sasa basi, nilishasikia tokea zamani kwamba kweli JK anapenda sifa, na here he comes confirming this ! Yaani siku hadi siku jk anataka kuonekana katika media oooh jk kafanya hivi jk kafanya vile, sasa basi jk ujumbe kwako :

Kwa kuwa hukujitayarisha kugombea urais, which i know for a fact kutokana na attendance yako ya utendaji wako wa kazi, ningekushauri 2010 uache kugombea urais kwa maslahi ya nchi na urudi tena uchaguzi utakaofuata ! Kwa kweli inasikitisha sana kuona unakimbilia masuala la zimbabwe wakati znz bado kuna matatizo kila siku, ukiachilia mbali matatizo ya kitaifa ( znz+bara) !!

KIKWETE ZANZIBAR KULIKONI MPAKA UKIMBILIE ZIMBABWE ????? AU UMESHINDWA NA NDIO NJIA YA KUTOKEA, YOTE MATOKEO UWE UMESHINDA AU UMESHINDWA WEWE TUAMBIE TU TUTAELEWA !!

ZANZIBAR KULIKONI MH. RAIS ?????????????????????????????????????????????????????
 
Mugabe tatizo Dar
Mkutano wa Wakuu wa SADC
na Tamali Vullu

JINA la Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ndilo lililotawala mkutano maalumu wa wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambao ulikuwa ukijadili masuala ya ulinzi na usalama katika nchi wanachama. Ndani na nje ya kikao hicho, Mugabe ndiye aliyeonekana kuwa kivutio na ajenda kuu ya mkutano huo kiasi kwamba hoja kuhusu uhusiano wake na wapinzani wake ndiyo iliyotawala mazungumzo ya mkutano huo.

Macho na masikio ya waandishi wa habari wa kimataifa na wale wa hapa nchini, tangu juzi jioni alipowasili yalikuwa yakielekezwa kwa Mugabe na hali ya kiusalama ndani ya nchi yake, hasa kwa sababu ya kuendelea kuzorota kwa mahusiano kati yake na yale ya mpinzani wake mkuu, Morgan Tsvangirai. Yeye ndiye aliyekuwa kivutio kikuu cha waandishi wa habari na katika magazeti mbalimbali ya jana picha zilizokuwa zikimuonyesha kiongozi huyo mkongwe ndiyo zilizotawala kurasa mbalimbali.

Mbali ya picha, tahariri na viponzo (katuni) juu ya kiongozi huyo ndivyo vilivyokuwa vikiongoza ndani ya magazeti hayo huku kila gazeti likiwa na ujumbe wake kuhusu mwenendo wa mambo ndani ya Zimbabwe. Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, wanausalama walijikuta wakiwa katika wakati mgumu kuwazuia wanahabari wa kimataifa waliokuwa wamejipanga nje ya jengo la Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski wakimsubiri kiongozi huyo wakati akitoka nje mara baada ya mkutano huo kumalizaka majira ya saa 11:00 jioni.

Akiwa amevaa suti ya kijivu, huku akiwa amezingirwa na wanausalama wake na wale wa hapa nchini, Mugabe aliyekuwa akitembea kwa kujiamini alitoka nje taratibu na pasipo kusita alionekana akijibu maswali mbalimbali ya waandishi waliokuwa wamemuelekezea vipaza sauti virefu karibu yake kabisa.

Mwanausalama mmoja alijikuta akibanwa katikati na wanahabari hao waliofikia hatua ya kutaka kumuadhibu kabla hajaokolewa na wenzake, wakati alipojaribu kutumia nguvu kuwazuia waandishi wa habari kumfikia kiongozi huyo. Kundi la wanahabari hususan wale wa CNN, Reuters, Deutchvelle na BBC wote walionekana wakifanya kila waliloweza kumfikia kiongozi huyo bila mafanikio tangu alipowasili hapa nchini juzi na hata alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa mkutano jana jioni.

Katika mkutano huo ambao Rais Jakaya Kikwete alikuwa mwenyekiti, wamemuagiza Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, kwenda nchini Zimbabwe kuitisha midahalo ya vyama vya upinzani nchini humo, ili kuondoa tofauti zilizokuwapo. Katika midalalo hiyo, vyama hivyo vinatakiwa kueleleza tofauti zao, ili hatimaye upatikane muafaka kati ya Serikali ya Zimbambwe na vyama hivyo.

Akizingumza na waandishi wa habari jana jioni baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC alisema kuwa, jumuiya hiyo inaamini kuwa, hiyo itakuwa njia muafaka ya kumaliza matatizo ya kisiasa nchini humo. "Baada ya Mbeki kuitisha midahalo hiyo ataleta ripoti ya matokeo katika kamati na kama kuna lolote la kufuatilia kamati husika itafanya hivyo.

"Mwisho wa hayo tunategemea kuwa vyama hivyo na serikali vitakaa pamoja na kuendelea kujenga nchi yao," alisema. Kuhusu suala la kutetereka kwa uchumi wa Zimbambwe na kutokuwa na uhusiano mzuri na Jumuiya za Afrika Magharibi, mkutano huo umeazimia kuwa SADC itasaidia nchi hiyo katika masuala hayo ili kurekebisha hali hiyo.

Awali akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa Serikali ya Zimbambwe, George Charamba, alisema kuwa, kukamatwa kwa wapinzani nchini Zimbambwe kunatokana na kuvunja sheria ya nchi. "Mtu yeyote ambaye anavunja sheria ya nchi ni lazima akamatwe na achukuliwe hatua zinazostahili," alisema.

Kuhusu kung'atuka madarakani kwa Rais Mugabe, msemaji huyo alisema kuwa katiba ya nchi hiyo haielezi kikomo cha rais kukakaa madarakani, hivyo Mugabe ataendelea kuwapo hapo hadi katiba itakapofanyiwa marekebisho. Rais Kikwete alisema kuwa katika mkutano huo pia walizungumzia malalamiko ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Lesotho.

Kuhusu nchi ya Lesotho, alisema kuwa SADC itawasaidia kutafuta njia mzuri ya kumaliza tatizo hilo, ila kwa nchi ya DRC, inapaswa kuwa na jeshi moja. "Mkutano umeamua kuwa nchi hiyo iwe na jeshi moja, hivyo vikundi vyote vyenye silaha vipeleke silaha zake kwa jeshi la Serikali ya Uganda, vingivevyo watanyang'anywa kwa nguvu.

"Tunafahamu kuwa malalamiko ya kutofanyika kwa uchaguzi huru na wa haki DRC yamesababisha vifo vya mamia ya raia na wengine kujeruhiwa, hivyo SADC imeona ni busara silaha hizo zipelekwe serikalini na nchi iwe na jeshi moja," alisema Rais Kikwete.
 
Wazee Heshima mbele,

Maraisi 15 walikutana hapa bongo kuzungumzia ishu za nchi zao na hasa umoja wao wa kusini, Zimbabwe ilikuwa ni moja ya ishu zilizozungumziwa,

Zimbabwe ni nchi huru kama zilivyo nchi zingine zote za dunia, inao uhuru wa kufanya itakavyo kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, hakuna nchi yoyote nyingine duniani yenye uwezo wa kuiambia kuwa sheria zake hazifai, Rais Kikwete, hana uwezo wowote kisheria zabongo wala za kimataifa kuingilia shughuli za kisiasa au kisheria kwenye nchi huru ya Zimbabwe,

Mugabe ni rais aliyechaguliwa kuwa rais wa nchi kwa mujibu wa katiba za nchi hiyo, anachohitaji sasa hivi ni ushauri wa nini cha kufanya wakati ardhi ipatayo 95% ya Zimbabwe imo mikononi mwa wazungu, huku wazawa yaani wazimbabwe wenyewe wanamiliki only 3.5% ya ardhi yao wenyewe, yeye kama rais wa nchi anatakiwa kuwaambia nini wananchi wake? Kwamba faida ya wao kupigania uhuru wa kuikomboa nch yao ilikuwa ni nini?

Wazungu kama kawaida yao wamepiga kelele sana kuhusu huu mkutano, na kutushambulia sana na hasa rais wetu, lakini wazungu hawa wanashindwa kufanya lolote kuhusu Iran na utengenezaji wa nyuklia, wazungu hawa wanasema ni sawa Israel kuwa na bomu hilo, lakini sio Iran, halafu wazungu hawa majuzi tu wanajeshi wao 15 wamechukuliwa na Iran, mpaka leo hawajafanya kitu, WHY? kwa sababu wanajua kuwa sheria za kimataifa haziwaruhusu kufanya lolote Iran inapodai kuwa sheria zake zilivunjwa na wanajeshi hao wakizungu,

Je Zimbabwe ingekuwa ndiyo imewashika wanajeshi hao 15 ingekuwaje? Matatizo ya Zimbabwe ni ya wa-Zimbabwe wenyewe na yatatuliwa na wazimbabwe wenyewe, wakihitaji msaaada wataziomba nchi za Afrika kwanza ziwasaidie, tumechoka na wazungu na unafiki wao, kama upinzani Zimbabwe wamevunja sheira za nchi hiyo, Muuugwana hawezi kuwasaidia,

na wazungu wanyamaze watuachie Afrika yetu, maana wao wanaweza kuwakamata watu Afaghanstan na kuwaweka rumande Cuba against sheria zote za kimataifa, vijana tuwe waangalifu na hizi propaganda za wazungu
 
Amani kwenu wana jamboforums. Ni vizuri sana kuwa na hot discussions hapa kwani ndivyo mambo yanavyotakiwa.

Dua nimeona comments zako siyo mbaya kwamba hawa marais 15 wapewe muda tuone. Sidhani kama kuna jipya. Kama kweli kuna jipya kwanini iwe siri? Mimi sioni ni kipi cha kuficha hapa. Na pia Pres. Mbeki kwangu mimi sidhani kama ni msuluishi mzuri kwani tumeona jinsi migogoro ya Rwanda na Congo ilivyompelekesha. my opinion ilikuwa ni kuchagua mtu tofauti aliye na views tofauti.

Viongozi wa africa huwa ni wa siri sana hata kwa vitu ambavyo havitakiwi. HAPA TUNAONGELEA MAISHA YA WATU, WATU WAMEULIWA NA KUJELUHIWA VIBAYA!!!!!! Sasa siri ya nini? Weka mambo hadharani ili watu watoe comments zao kama kuna pa kurekebisha parekebishwe ili kusiwepo na kurudi nyuma.

Pia kuna hii issue ya baadhi ambao walijitokeza na kusema kuwa khali ya Zimbabwe ni mbaya mfano Pres. Mwanawasa!! Tunaitaji watu kama hawa siyo watu wanaotaka kuonekana watakatifu au wastaarabu katika kutatua migogoro wakati watu wanateketea. Msimamo mmoja ulikuwa unatakiwa kuwa jamaa ANG'ATUKE.

LAKINI MIMI MKUTANO WA JANA NAONA POLITIKI ILIJAA SANA KULIKO KUFIKILIA MAISHA YA WAZIMBABWE WANAOTESEKA KUPITA KIASI.

Kila la kheri tukijaliwa...
 
Back
Top Bottom