Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!

Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!

Mugongo nadhani una matatizo makubwa badala ya Mbowe ambaye unaonekana kumvalia njuga . Mimi naishia hapa wengine wataendelea ila wako watako kupa majibu kutokana na mchango but I bet Mbowe kapiga hadi Ikulu kwa ukali wa maoni yako .
 
Chief - hapa watu wanasema "kukata issue". Mimi nadhani suala sio mimi wala Mbowe, suala ni arguments za Mbowe huwa zina weak intellectual foundations and flawed reasoning. Mara nyingi ni emotions tu na lugha ya mashairi.

Pili, nadhani wana-JF don't appreciate the magnitude ya Mbowe, mgombea Urais jana na kesho, kuwa mwanachama mwenzetu. So, I take advantage of every opportunity kumu-engage ingawa is always a non-show. Akitokea mtu mwingine of significance, I will do the same.
 
Mugongo wa Mugongo,
Tuliwasaidia Wazimbabwe kujikomboa. Damu yetu ilimwagika kule. Kesho na keshokutwa, baada ya Mugabe kuondoka madarakani na demokrasia halisi kusimika mizizi ndani ya Zimbabwe nitakuomba urudi usome tena makala ya kijana Mbowe ndipo tukate issue. Urafiki wa Tanzania na Wazimbabwe si wa government to govenment ni a people to people relationship. Leo Changirai ambaye kapigwa ngeo na mawakala wa Mugabe akiingia mamlakani ninyi Watanzania mliomkumbatia Mugabe na dhuluma zake mtapata kigugumizi.
 
Jasusi,

Inaelekea, kama alivyo Mbowe, na wewe unaamini kwamba basis ya sera ya mambo ya nje ni kuangalia nani anatarajiwa kuwa Rais in any given country duniani, hivyo kuchukua misimamo inayomfurahisha. Kwa maneno mengine, basis ya kujitenga na Mugabe iwe ni kwamba Tsvangirai ndiye anayetegemewa kuwa Rais, kwa maana hiyo tuta-lose out kwa kuwa tulikuwa tunamuunga mkono Mugabe. I'd say that is crap. Ndio maana nasema Mbowe inabidi aingie darasani seriously kuhusu foreign policy. Msingi wa sera ya mambo ya nje ni maslahi ya nchi. Full stop. Na haya yanabaki pale pale, aje Mai Mujuru, aje Gideon Gono, aje Simba Makoni, aje Welshman Ncube, aje Morgan Tsvangirai. And, stability of Zimbabwe is of our national interest. And, if you do things to pursue stability in Zimbabwe, including talking to Mugabe, you will be fine hata Tsvangirai akiingia madarakani.
 
Kwa mtazamo wangu binafsi, sidhani kama Mbowe amekosea kumkosoa Muungwana, WHY ? Because he can ! Thats right, hata kama International Relations hayapandi ( which i doubt ) still nadhani ni busara kwake kumkosoa mtu anapokosea, after all yule mzee has to get off power maana amekaa muda mrefu na hana jipya lolote au sijui anataka wazimbabwe waulize viongozi wake wapo wapi, na jibu la mugambe andhani litakuwa "TUPO TUMEJAA TELE"..... sasa hii wapi na wapi.

One thing is, yule mzee sidhani kama ana mtandao mkubwa wa kuogopwa kiasi kwamba hata wengine waweze kumuogopa hivyo ! Sitoshangaa nikiona wazee walafi wa madaraka wakispend the rest of their lives JELA !!
 
One thing is, yule mzee sidhani kama ana mtandao mkubwa wa kuogopwa kiasi kwamba hata wengine waweze kumuogopa hivyo ! Sitoshangaa nikiona wazee walafi wa madaraka wakispend the rest of their lives JELA !!
Bado wanambebisiti kwanza si unajua kwasababu ni Africa na huenda kunawanaomlinda miongoni mwa hao wazee na Mafuta Hakuna Pale!
 
Mugongo2
Hujanielewa kama ambavyo hukuielewa makala ya Mbowe. Kuna rais mmoja wa Marekani aliwahi kusema Marekani haina permanent friends but permanent interests. Hiyo ndiyo sera ninayofikiria kuwa inafaa. Kumng'ang'ania Mugabe wakati raia wake wamemkataa ni sera mbovu. Ulimsikia Mwanawasa alisema nini karibuni kuhusu Mugabe? Na huyu ni jirani yake pia, tena wa karibu zaidi yetu. Sijasema tujipendekeze kwa Changirai. Ninachosema ni kuwa tuwe na sera ambazo raia wa Zimbabwe, wawe wa ZANU-PF au upinzani watajisikia kuwa katika Tanzania tunao marafiki na ndugu wa kudumu. Lakini kwa sasa sera zetu ni pro-Mugabe, right or wrong.
 
KIKAO cha wakuu wa Jumuiya ya SADC kitafanyika nchini kuanzia leo, kikiwa na malengo ya kuzungumza mambo mbalimbali yanayohusu sehemu hii ya Afrika.


Miongoni mwa mambo hayo ni hali ya kisiasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na pia hali ya kisiasa huko Zimbabwe.


Kuhusu suala la Zimbabwe, nchi za Kiafrika zimeshindwa vibaya kusimamia maslahi ya watu wa Zimbabwe na hivyo kuacha serikali yao kuendelea kutenda kazi kana kwamba imesimikwa na Mungu.


Hali ya kisiasa ya Zimbabwe inasikitisha na haikubaliki!


Ni kwa sababu hiyo basi, kikao hiki cha viongozi wa SADC kina nafasi ya pekee ya kuonyesha msimamo mmoja wa viongozi hao na hatimaye kuwa sauti ya wale "wasio na sauti" wa Zimbabwe.


Kuendelea kufumbia macho kinachoendelea Zimbabwe, ni kuhalalisha serikali ya kidikteta na kufumbia macho uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu.


Tanzania ina nafasi ya pekee katika kuona kuwa suala la Zimbabwe linatafutiwa suluhisho la kisiasa, ambalo litaheshimu Katiba ya Zimbabwe na kulinda haki za raia wote bila kujali vyama vyao au itikadi zao.


Viongozi watakaokutana kwenye mkutano huu, ni lazima wakubali kuwa ile "diplomasia ya ukimya" ambayo imekuwa ikifuatwa hadi hivi sasa katika kulikabili tatizo la Zimbabwe, imefeli, na haina nafasi katika kutafuta suluhisho la kudumu.


Wakati umefika kwa viongozi wetu kuweka mambo kadhaa wazi kabisa kwa Serikali ya Rais Mugabe.


Kwanza, licha ya mchango mkubwa wa Rais Robert Mugabe katika kutafuta uhuru wa Zimbabwe, mchango wake huo si leseni ya utawala wa mabavu au wa kidikteta.


Viongozi wa SADC waseme wazi kuwa, linapokuja suala la haki za raia wote na ulinzi wa utu wa watu wetu, hakuna mtu yeyote ambaye ana haki ya kuvunja, kuondoa, au kuzuia upatikanaji wa tunu hizo.


Kama tulimkatalia Amin, Bokasa, Mengistu na wengine, wakati umefika Waafrika tutambue kuwa Mugabe kwa kuridhia vitendo vya ukiukwaji haki za binadamu, na matumizi ya nguvu katika kuendeleza utawala wake, basi matendo yake mengi yanaanza kupakana na utawala wa kiimla, hivyo lazima abadili mwelekeo au atatengwa.


Pili, wananchi wa Zimbabwe kama walivyo wa sehemu nyingine yoyote ile, wana haki ya kufurahia uhuru wao na haki zao kama raia bila kujali itikadi za vyama vyao au vitu vingine vinavyowatofautisha kama mtu mmoja mmoja.


Katika Zimbabwe ya sasa, kama wewe hauko kwenye chama tawala, basi nafasi yako ya kufanikiwa ni kama sifuri!


Viongozi wa SADC wanapokutana hapa nchini, ni lazima waweke hilo wazi kuwa, tofauti za kisiasa au kimtizamo si sababu hata chembe ya kuwagawa Wazimbabwe na kuwafanya wale walio kwenye chama tawala ndio wazalendo hasa na wale wanaopinga si wazalendo.


Ni wazi kuwa Tanzania ni vigumu kwake kuja na msimamo kama huo, kwani utaakisi mahusiano ya chama tawala hapa nyumbani na wapinzani wao.


Itakuwa sawa na mtu kujaribu kutoa kibanzi kwenye jicho la jirani yake wakati boriti bado liko kwenye jicho lake.


Zimbabwe lazima ionyeshwe upotovu wake huo na itakiwe ijirudi, si kwa ajili ya kuyaridhisha mataifa makubwa bali kwa ajili ya watu wake na hatma ya nchi hiyo.


Tatu, wapinzani wa Serikali ya Zimbabwe ni lazima nao wapewe nafasi ya kusikilizwa na hoja zao kufanyiwa kazi.


Kitendo cha mkuu wa kambi ya upinzani kupigwa na kunyanyaswa pamoja na watu wengine, ni mwanzo mbaya na ni hatua mbaya ambayo viongozi wetu wanapokutana hawana budi kuilaani kwa maneno makali.


Inapofikia kuwa tofauti za kisiasa zinaanza kusababisha watu wapigwe na kufungwa, basi tujue ya kuwa, Zimbabwe imeanza kuunusa mstari utenganishao utawala wa sheria na haki kutoka maisha ya vurugu na uchokozi.


Ukweli ni kuwa, inavyoendelea kuungua Zimbabwe, ndivyo nchi jirani na hususan eneo hili la Afrika zinavyozidi kupoteza sifa zake na kubebeshwa mzigo wa matatizo yanayotokana na Zimbabwe.


Endapo itatokea kuwa serikali ya Mugabe iendeshe operesheni ya kukamata wapinzani wake na kuwafunga, basi jumuiya hii itakuwa imepoteza umuhimu wake na kubakia kuwa klabu ya kupigiana soga, na baraza la kuchukuana picha.


Nne, wapinzani wa Mugabe nao waambiwe wazi kuwa, lolote watakalofanya kama ni kinyume cha sheria za nchi, watasababisha kugongana na serikali.


Hivyo ni lazima watiwe moyo, watumie njia zinazokubalika kisiasa ili kufikia malengo ya kisiasa.


Ingawa jambo hili kwa sasa ni kama haliwezekani, lakini jumuiya ya SADC ni lazima ichukue nafasi ya makusudi na ya wazi ya kutafuta suluhisho la kudumu, ambalo litaheshimu uhuru wa Zimbabwe kujiamulia mambo yao, litatambua haki za raia wa Zimbabwe kuishi kwa uhuru bila hofu ya serikali yao, na kusimamia utaratibu wa ujenzi wa hatua za kisiasa ambazo zitarudisha umoja na heshima kati ya makundi mbalimbali ya kisiasa nchini humo. Katika hili Tanzania ina nafasi ya pekee.


Katika kutafuta suluhisho la swali la Zimbabwe, Tanzania inaweza kuonyesha njia kwani sisi ni marafiki, ambao wakati mwingine inabidi tuwaambie rafiki zetu ukweli.


Maneno makali yanapotoka kwa wakubwa kuzungumzia suala la Zimbabwe, inaonekana wana ajenda ya siri na hilo sisi sote tunajua.


Waingereza wanapozungumzia suala la Zimbabwe, si kwa sababu wana uchungu na maisha ya watu weusi wa Zimbabwe, bali wana uchungu na ndugu zao Wazimbabwe weupe ambao wamenyang'anywa ardhi na wengi kulazimika kutimka.


Lakini sisi Watanzania na watu wa bara hili la Afrika, hatuwezi kukaa kimya wakati ndugu zetu wa Zimbabwe wanazidi kujichimbia shimo ambalo jinsi ya kutoka haionekani.


Hapa, Tanzania inaweza kufanya jambo ambalo litasaidia kuondoa mgogoro wa ndani wa Zimbabwe na ule dhidi ya mataifa ya Magharibi.


Tanzania baada ya mkutano huu wa viongozi wa SADC, ikubali jukumu la kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa hali ya kisiasa ya Zimbabwe kwa kuitisha mkutano usio na masharti wa wadau wa hali ya kisiasa wa nchi hiyo.


Wakati umefika wa Tanzania kutoa mwaliko kwa Serikali ya Zimbabwe, vyama vya upinzani vya nchi hiyo na taasisi za kiraia kukaa pamoja na kutafuta chanzo cha mgogoro na kutatufa utatuzi wa mgogoro wa Zimbabwe.


Hatuwezi kuendelea kukaa kimya hadi tuone ndugu zetu, wanaharakati za ukombozi wenzetu wakiendelea kudidimia katika hali mbaya ya kiuchumi huku maisha yao ya kisiasa yakiwa matatani.


Ingawa Tanzania inaweza kufanya hili, lakini kwa Serikali ya Kikwete kuamua kujaribu kutafuta suluhisho la Zimbabwe, inawezekana ikawa ni "kinyume nyume" kwani wakati tunahangaika kutafuta suluhisho la matatizo ya Zimbabwe, ya kwetu bado yanatuzungusha kichwa.


Hata hivyo, hilo lisiwe kizuizi cha kujaribu kutatua mgogoro wa Zimbabwe, kwani kutatupa na sisi ari zaidi ya kushughulikia matatizo yetu kabla hayajafikia mahali pa yale ya Zimbabwe.


Kwa kuanzia hata hivyo, tuwasaidie Zimbabwe waondokane na hali ya wasiwasi ya sasa, mgongano wao wa ndani, uhasama na nchi za Magharibi na uundaji wa mazingira mapya ya kisiasa ambapo kila Mzimbabwe atafurahia matunda ya uhuru wa nchi yake bila kujali rangi zao, itikadi zao, au mfungamano wowote wa kisiasa.


Tukifanikiwa kufanya hivyo, basi wito wetu kama Watanzania tunaojigamba nao wakati wa kukimbiza mwenge kila mwaka utatimia, nao ni "kuleta matumaini mahali ambapo hakuna matumaini, upendo mahali ambapo pana chuki, na heshima ambapo pamejaa dharau."


Hakuna mfano mzuri wa mahali kama hapo kuliko Zimbabwe ya sasa.
 
Mugabe aambiwe ukweli





MKUTANO wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), umeanza jana chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.


Miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kuchukua nafasi kubwa kujadiliwa katika mkutano huo, ni migogoro ya kisiasa nchini Zimbabwe na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Macho na masikio ya Waafrika wengi yako jijini Dar es Salaam ambako mkutano huo unafanyika, na kikubwa wanachofuatilia ni nini viongozi wa jumuiya hiyo watamuambia au kumshauri Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ambaye pia anahudhuria mkutano huo.


Wengi wanataka kusikia viongozi hawa watasema nini kuhusu Zimbabwe na Mugabe, kutokana na matukio ya hivi karibuni ambayo yamevuka mipaka ya kawaida ya ushindani wa kisiasa na hata ubinadamu, yaliyofanywa na vyombo vya dola vya serikali ya Mugabe dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani, wanaharakati na viongozi kadhaa wa dini.


Ni jambo lililo dhahiri kuwa viongozi wa jumuiya hii wanamkumbatia Mugabe, wanayafumbia macho maovu anayofanya dhidi ya wananchi wake kwa kisingizio cha kupambana na maadui wake wa kisiasa, ambao pia ni Wazimbabwe kama yeye.


Sababu kubwa ya kumkumbatia Mugabe ni ile ile, ya huyu ni mwenzetu, tumetoka naye mbali.


Lakini cha ajabu katika hilo ni kwamba, viongozi hawa wanasahau kuwa hata hao Wazimbabwe walio katika mateso makali kutoka utawala wa Mugabe, nao ni wenzao, walipigania uhuru pamoja, na kwamba Mugabe peke yake, bila kuwapo hao anaowatesa, asingefanikiwa kutimiza ndoto aliyokuwa nayo ya kuung'oa utawala wa kikoloni na kuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo.


Lakini la kusikitisha zaidi kwa viongozi wa jumuiya hii, Tanzania ikiwa kinara wao, ni pale wanaposhindwa kumwambia ukweli Mugabe, kuwa damu ya wananchi wake wakakti wa kudai uhuru, haikumwangika kwa ajili ya kutafuta mateso anayowapa sasa.


Viongozi wengi wanaounda jumuiya hii nchi zao zimetawaliwa na watu weupe na zimepata uhuru kwa njia ya mtutu wa bunduki, tunajiuliza, hivi hawa wamesahau mateso waliyokuwa wakiyapata msituni wakati wa kudai uhuru?


Tunashangazwa na ukimya wa viongozi hawa dhidi ya vitendo vya Mugabe, ambao unaweza kutafsiriwa kuwa anayofanya Mugabe dhidi ya wana wa Afrika wazaliwa wa Zimbabwe, kwao viongozi hawa, kwa sababu Mugabe ni Mwafrika, ni sahihi.

Hii ina maana kuwa, ni Wazungu tu wanaopaswa kulaaniwa wanapofanya vitendo vinavyokiuka haki za binadamu, lakini kwa Waafrika ni sahihi?


Sisi tunadhani muda wa kumwambia ukweli Rais Mugabe umefika, ili kuepusha aibu inayoweza kuwakuta viongozi wa jumuiya yetu hii wanaoendelea kumkumbatia. Hatutaki Mugabe ang'olewa kwa aibu madarakani na wananchi wake ambao tunaamini wamechoshwa na mateso anayowapa.


Tunatambua kuwa Mugabe na Chama chake cha ZANU - PF ni maswahiba wakubwa wa viongozi walioko madarakani pamoja na vyama wanavyo viongoza.


Lakini pamoja na uswahiba huo, litakuwa jambo la busara walau, wakiyakataa matendo yake, lakini wakaendelea kumpenda, vinginevyo watambue kuwa tafsiri iliyopo sasa ni kwamba, wapigania uhuru wa Afrika waliomwaga damu yao nchini Zimbabwe, waliimwanga ili Mugabe aingie madarakani na kumwaga damu ya Wazimbabwe wenzake.


Chonde chonde, tunawasihi viongozi hawa, wawe wawazi kwa Mugabe kwa ajili ya masilahi ya Wazimbabwe walio wengi ambao sisi sote ni ndugu zetu.
 
Muungwana umeaga kwamba utakuwa na udhuru sasa mbona unarudi tena kwa chuki zako dhidi ya Mbowe na Chadema kama kawaida yako ? yaani umetuhadaa na sasa unarudi kwa jina na mlango mpya ? Kwa kuwa una nongwa na Mbowe binafsi na Chadema hutaacha kujulikana kwa msimamo mna uandishi wako . Wacha kutupotezea muda kwa mambo yako binafsi na Mbowe ila tuache tuendelee kuangalia tafakuri ya Mbowe na tuseme , lakini kumbuka ana haki ya kutoa maoni na yeye hutoa bila ya matusi kama unavyo jaribu kutufanay tukufuate hapa kwa maneno ya dharau kwa ndugu huyu . Manano yako yamejaa chuki na hutaki kuelewa Mbowe anasema nini .Hata hutaki basi heshimu mawaoz yake na wacha kumkandia kijinga .
 
Mugongo: I think you did not understand what Mbowe is saying in his article or as usual, you are wittingly trying to politicise the issue.

The message from Mr. Mbowe's article is simple and straightforward: Mugabe is hiding his tyranny and brutality under the cover of land redistribution programme. This is synonomous to CCM, which has for years disguised his political and economic woes under the cover of peace and tranqulity.

Haya majambo inabidi uyaone katika picha kubwa. Nenda kule kwenye thread ya 'Let's talk about Zimbabwe'. Kuna vitu vizito huko. Achana na hizi cheap politics za kuficha maovu katika gunia la uzalendo.
 
The message from Mr. Mbowe's article is simple and straightforward: Mugabe is hiding his tyranny and brutality under the cover of land redistribution programme.

Mwanasiasa, I wish Mbowe had said that. Kwasababu kwa hilo tungekubaliana mia kwa mia. Lakini nionyeshe pahala kwenye article amesema hivyo. Yeye amelalamikia mikutano ya Othman na spies wenzake Zimbabwe. In any case, hata kama angeandika Mugabe is hiding his tyranny and brutality under the cover of land redistribution programme, that is really not a new insight, is it? If you are going to state the obvious, why write an op-ed?
 
Murangira,

You can go hang if you think mie ni Mzee ES nimerudi "kwa mlango wa nyuma". Watu wa CHADEMA bwana, akisemwa Mbowe watatafuta mchawi nani badala ya kujibu hoja. What do you care hata kama ni kweli niliaga na nimerudi na njia nyingine. Hoja kwamba Mbowe kilaza inaondoka?
 
Watu wa Chadema?
Mimi na wewe tutakula sahani moja hadi uache unafikia hapa . Issue ni personal attack zako kwa Mbowe . Nadhani kama mmekuwa wote ni sawa lakini si size yako kwa sasa . Tunalinda heshima ya forum na si personal problems zako na Mbowe unazipeleka kila mahala. Hapa mimi na wewe nani anaonekana Kilaza ?

yaani ukilaza wako unataka kuuvalia njuga . The issue ni kwamba ulitaka Mbowe aandike exactly kama alivyosema Mwanasiasa ama wewe unavyotaka .Lakini Mbowe has spread his message na hata mawazo kwa njia ambahyo yeye anaielewa na mtu wa kawaida kawaida anaweza badala ya kutumia maneno magumu.
watu wanaona umeanza kuja na maneno yako ya kila siku ya kebehi kwa Mbowe lakini wengi wameona lugha ya Mbowe juu ya Mugabe na Zimbabwe sasa wewe na yeye nani kilaza? Unashangaza forum sana ila hawakuelezi mimi nitakueleza kila mara .

Wewe na mambo yako na NY ni mengi mbona watu hawasemi ? Ama kwa kuwa Mbowe kagusa issues ambazo Malecela anahusika moja moja kwa kama kiongozi wa CCM amabayo haina mwelekeo ? Wacha ushamba kata issue achana na Mbowe klesha kupita .Unamwita kilaza lakini wewe hujioni hivi wewe na pia kukaa NY kwa msaada wa mkeo na wewe kuendesha Ma lori na Mkeo kufanya Ubalozini ndiyo unaona ume win ama ndiyo wale wale kwamba Mbwa wa Mfalme naye ni mfalme ?

You have me now na nitakula nawe hadi uache maandishi ya kijinga . Moderatpr nilinde nilete heshima ya forum hapa .
 
Nasikitika kuona ukiandika ulichokiandika and yet unamkosoa Mbowe kuwa hajui foreign diplomacy, while wewe huijui hata local diplomacy.

Why i said those is due to the following,
1.diplomacy is all about to agree what we disagree, kukubaliana kutokubaliana kwenye masuala kwa kujenga hoja na sio kwa kuporomosha mitusi . ona unasema kuwa Mbowe akasome diplomacy ila ningekutaka wewe walau uanze kwa kusoma theory of diplomacy.

2. In diplomacy we argue and we never shout.
Unaonekana kuwa unapiga kelele pasipo kujenga hoja wewe tueleze kuwa Mbowe alipaswa kufanya nini na sio kuporomosha mitusi kwa Mbowe kisa ili uweze kuwafurahisha watawala.,

3. In diplomacy we are shot and clear and we never argue the same issue over and over again. Ungekuwa unaijua diplomasia basi wewe usingekuwa mtu wa malumbano bali ungewasubiri wana JF wachangie then ndio wewe uje na argument na sio kuwashambulia wale wote unaoona kuwa wanatofautiana na wewe kimsimamo kama unavyofanya.

4. In diplomacy we do always show the basis of our argument. kitu ambacho mugongo mugongo huonekani kukijua wala kukielewa ni vyema ukayajua haya ili uweze kumtaka Mbowe aende akasome ila wewe ni bora ukaenda kusoma kwanza walau principles za diplomacy kwa kuanzia ili usiwe unafanya uliyoyafanya wakati mwingine.

5. Mugabe ni lazima aambiwe ukweli kwani anachowafanyia wananchi wa zimbabwe sio kile ambacho watanzania walimuunga mkono na kumtaka aende kukifany hicho kwani amekuwa mbaya kuliko hata Ian Smith ambavyo alikuwa akiwatenda wana wa zimbabwe.

6.Naamini unaujua ukweli kuhusu rate ya inflation kule zimbabwe je?kwa level hiyo Mugabe aendelee kukumbatiwa?

7.Ni kweli kuwa mugabe na JK wao lao moja inapokuja hoja ya wapinzani angalia ilichofanyika kule tunduru je?umejiuliza ni kwa nini voters turn out imekuwa ndogo kiasi hicho? ni kuwa CCM haiko tayari kuwaona wapinzani wakiweza kuwashinda hata kwa kutumia mbinu chafu kama walivyofanya .

8.sOCRATES alitembea na taa mchana sokoni kule Athens ila utawala wa kule ukamwona kama ni mchawi wa utawala wao ,Mbowe ameamua kutembea na taa mchana ili kuwaonyesha watanzania walivyo kizani unategemea nini kutoka kwa watawala ambao hawataki watu wajue kuwa wapo kizani?

9.Wana JF HUYU MTU NI KWELI KUWA AMEPEWA ASSIGNMENT NA TUMJIBU KWA HOJA NA WALA TUSIMTUKANE KWANI YUPO KWENYE KAZI AMBAYO YEYE BINAFSI HAAMINI KILE ANACHOKITETEA JAPO ANAFANYA HIVYO.
 
In any case, hata kama angeandika Mugabe is hiding his tyranny and brutality under the cover of land redistribution programme, that is really not a new insight, is it? If you are going to state the obvious, why write an op-ed?


Yes, indeed it is an obvious and a naked fact, yet no body dares to tell Mugabe just that including our honourable President Kikwete. This is what Mbowe, and by the way Mzee Mwanakijiji, were trying to accomplish in their articles. In essence, Mbowe was not trying to write a scientific paper for you to say that there was nothing new. You must understand the tone of a feature article. Feature articles by and large discuss contemporary issues in dfferent perspectives; they never claim to present new discoveries!

So can you tell us your opinion as to why do you think African leaders are not telling Mugabe the obvious? Do you think they admire his style of leadership?
 
Kama kina Bush walijitahidi kumuondoa mtu mweupe mwenzao kule Serbia na jinsi watu weupe walivyoamka kule Ukraine, Georgia na kwingineko na kuwapinga watawala wao, wakati umefika kwa sisi nasi kuwakataa watawala ambao licha ya nafasi zao zi kihistoria wamegeuka kuwa watawala wa kiimla!! Nyerere kwa watu wengine alikuwa ni kiongozi mbaya, lakini hakufikia kutenda yale yanayotendwa na Mugabe... Kwa watu wengine Kaunda alikuwa ni kiongozi mbaya, lakini ukimlinganisha na Mugabe hata nusu hamfikii!! Kama wananchi wa DRC waliwaza hatimaye kumchoka Mobutu na wakaamka dhidi yake, hata wale wa Zimbabwe siku moja watafikia hapo!!!

Nimesema mahali fulani kuwa unaweza kumlazimisha punda kubeba mizigo na akatii kwa muda mrefu, lakini siku moja ukizidisha punda hugoma!! Utachapa weeee mpaka mikono ikuote kutu lakini punda hendi!! Nafikiri Zimbabwe inakaribia kufikia hapo. Endapo Mugabe hatasaidiwa kutatuta suluhisho la kisiasa la nchi yake, na wananchi wake wakalipuka dhidi yake na hatimaye kujikuta akiikimbia nchi yake kama walivyofanya kina Mengistu Haile Mariam au Aristide... itakuwa amejitakia.

Mugabe anazo nyezo na uwezo wote wa kutatua matatizo ya Zimbabwe lakini kutokana na hisia ya kujiona yeye "ndiye mtawala anayestahili" huko Zimbabwe na ambaye anataka watu waamini kuwa pasipo yeye Zimbabwe haitawaliki basi amegoma kutatua matatizo hayo!! Saa iko na tena imefika, viongozi wa Afrika wasisubiri wapigiwe simu na kina Blair na Bush ndio waamue kuingilia kati!! Mwenzetu siyo mwenzetu kama anachinja watu wetu!! Hata urafiki una kikomo!!!

Tatizo ni nani atakuwa tayari kumfunga paka kengele. JK hana ubavu wa kusema kweli kwani atajihisi msaliti lakini tukumbuke tulipotoka jamani!! Tulisema huko nyuma kuwa "Tanzania siyo huru mpaka Afrika yote iwe huru", wakati umefika wa kusema kuwa "Tanzania haina amani, mpaka Afrika yote iwe na Amani".

Sera yetu ya nje ni lazima tuigawe pande mbili. Moja ni hiyo diplomasia ya uchumi hususan tunapohusiana na mataifa makubwa ya kimagharibi na yale yaliyopiga hatua za maendeleo. Upande mwingine ni lazima tuanzishe Diplomasia ya Amani (Peace Diplomacy) ambapo tunajitahidi kutumia nafasi yetu kuhakikisha kuwa bara la Afrika linakuwa na amani ndani yake hata kufikia kuwa na amani ya kiafrika pax africana

Watanzania tunaweza kuongoza katika kufikia lengo hilo. Sababu tunayo, uwezo tunao, na nia tunayo, kwanini basi tusiiongoze Afrika katika kutafuta amani? Kama tuliongoza na kuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa kusini mwa Afrika, kwanini tusiongoze katika kutafuta Amani! Kama tuliwasaidia Zimbabwe (Rhodesia) kuung'oa utawala wa Ian Smith, kwa sababu ya kuwa utawala huo ulikuwa siyo halali na ni wa kimabavu, kwanini leo tukumbatie utawala mwingine wa kimabavu kwa vile tu aliyekalia kiti hicho cha utawala safari hii ni mweusi mwenzetu? Je udikteta wa mtu mweusi unavumilika zaidi kuliko udikteta wa mtu mweupe? Sote tunajua kuwa watu weusi wakiwa madikteta rekodi yao haifurahishi.. Amin, Mengistu, Mobutu, Bokasa n.k ni mifano dhahiri!!

Mugabe ni lazima aambiwe kweli na ikibidi atengwe!!!!
 
Kwa kweli mimi binafsi sioni tatizo la JK kumtuma othman kwenda Zimbabwe!
Historia inaonyesha kwamba, Kwenye kwenye issues za Conflicts Spy Bosses wametumika sana!
Israel wanamtuma sana Mossad's boss kufanya mazungumzo na Egypt na Palestines, na Mubarack naye hufanya hivyo hivyo pindi akitaka kufanya mzungumzo na israel!
Russia na USA wametumia style hii kwa muda mrefu kipindi cha cold war!
Clinton alimtumia sana George Tenet kufanikisha mazungumzo ya amani kati ya Rabin na Arafat.
Conflicts nyingi zimekuwa solved kwa kutumia intelligence!

Tusisahau influence ya Tanzania kwenye nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Bila shaka wakati makao makuu ya Kamati ya Ukombozi ya OAU ilipokuwa DSM hapakuwa na maswali kuhusu matumizi ya "intelligence" Zimbabwe, msumbiji, Angola, Namibia na South Africa.

Kuna ajabu leo president akimtumia Spy chief kuendeleza kile kilichofanya na watangulizi wake ili kutatua mgogoro wa Zimbabwe?

Nd. Mwanakijiji, Peace/Security diplomacy ndio Intelligence yenyewe. ndio maana JK ameamua kuweka msisitizo kwenye Economic Diplomacy maana haikuwekewa msisitizo huko nyuma!
 
Brutus, kama hiyo intelligence ndiyo peace diplomacy basi tumefeli kupita kiasi!! Tunahitaji kupanua wigo wake ili kuweza kutafuta amani huko Darfur, Somalia, DRC, Zimbabwe n.k...
 
Back
Top Bottom