Zifahamu hatua halisi za kutoa gari kwenye Meli na bandarini

Naongezea, kabla ya Meli ya magari kufika.

Mnunuzi akinunua gari Kwa kupitia ma agent hupewa taarifa za Meli gari iliyopakiwa na Estimated Time of Arrival (ETA) katika Bandari ya Dar es Salaam. Hivyo unaweza ukaanza kuitrack Meli Kwa kupitia Vessel Finder au Marine Traffic.

Shipping Agent wa Meli ya magari hupeleka taarifa TPA kuwa anataraji kuleta Meli, hivyo hutoa taarifa za Meli na mzigo utaoshuka au kupakiwa. Hapo hiyo Meli itaanza kuonekana katika website ya bandari kwenye kipengele Cha TPA Daily Shipping List na hii hutolewa Kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa baada ya kikao Cha ship planning kuhusu Meli za kuingia na kutoka.

Meli ikiishafika Tanzania eneo la nje la bahari (Outer Anchorage Area) Captain wa Meli hutuma email Kwa agent kutoa taarifa ya kufika, ambapo watatoa muda wa kufika (End of sea passage), Kisha kama Meli ipo tayari taarifa ya kuwa tayari kwenda kushusha bandari hutolewa (Notice of Readiness).

Hapo Kwenye Notice of Readiness(NOR) Meli inaweza isitoe muda huo huo endapo Kuna marekebisho au kuweka vitu sawa Ili wakifika bandari waanze kazi Direct.

Baada ya NOR kama agent wa Meli (Shipping Agent) alikamlisha kulipa malipo ya kuingiza Meli (Mfano; Tugging, Pilotage, Wharfage) Captain hupewa taarifa ya kuomba nafasi ya Pilot kuja kuifata Meli(Pilot Booking) Ili waingie bandari.

Pia Meli inaweza ikawa imekamilisha malipo na nafasi ya gari(Berth) hakuna hivyo Meli itashusha nanga (Anchor down) kusubiri nafasi Bandari, vivyo hivyo kama malipo hayajakamilika watashusha nanga.

Meli kuingia bandari huwa baada ya Pilot kuwa Booked muda ukifika pilot hupelekwa nje au eneo Meli ilipo na boti ndogo(Pilot Boat) hii huambatana na taarifa ya kuingia Meli ambayo hutolewa Control Tower na Mooring Gangs (wafunga meli). Kisha hupanda melini Kwa kutumia ngazi maalum iliyopo pembeni ya Meli (Pilot Ladder) Kisha hupokelewa na kukaribishwa kwenda sehemu ya kuongozea Meli (Ship Bridge) ambapo hatakuwa anakuwa na Captain wa meli kuelekeza meli iingie vipi na namna Gani itafunga katika gati la Bandari.

Meli inapoingia Bandari baada ya kuvuka eneo la ferry Tug Boat husogea Kwa ajili ya kuipa Meli msaada wa kufunga kwenye gati. Baada ya Meli kusukumwa mpaka kwenye gati zoezi la kuifunga kamba (Ship Mooring) huanza ambapo Kamba ya kwanza (First line) hufungwa mbele na nyuma, Kisha kamba nyingine na kumalizika kamba ya mwisho(Last line) zoezi hili wastani huchukua Kuanzia robo saa mpaka nusu saa.

Baada ya kumaliza kufunga kamba ngazi ya kupandia melini hushuka (Gang way) ili Pilot ashuke na Maafisa wa Afya waweze kuingia Kwa ajili ya ukaguzi.

Pilot hushuka Kisha Maafisa Afya wa Bandari (Port Health Officers) nao hupanda melini Kwa ajili ya ukaguzi. Kipindi Maafisa Afya wanapanda melini Meli hupeperusha Bendera ya njano kuonyesha kuwa Meli Bado haijakidhi Watu kuingia (No permit granted for anyone to board). Muda ambao Watu wa Afya wapo Melini mlango wa kushusha magari (Lamp) huanza kufunguliwa na mabaharia na kuweka vitu sawa Kwa zoezi za upakuzi.

Baada ya Watu wa Afya kumaliza ukaguzi wa Meli na kukagua magonjwa ya mlipuko, usafi wa Meli na vipimo vya COVID-19 hutoa taarifa kuwa Meli ipo salama Kisha Bendera ya Njano hushuka kitendo hiki Cha Meli kuwa sawa na ruhusa ya wengine kuingia Kwa ajili ya kazi huitwa Free Pratique Granted.

Maafisa Afya wakishuka ndipo Maafisa Uhamiaji, Forodha(TRA), Shipping Agent na TPA officer na madereva hurusiwa kuingia melini Kwa ajili ya taratibu za kushusha magari.

Maafisa uhamiaji huomba list ya mabaharia na passport zao, Mtu wa TRA hukagua store na kuweka seal Ili kuzuia mizigo na vitu vyao vikaingia nchini bila kulipa Kodi, Mtu wa Port Security huomba documents za meli, mabaharia na utaratibu wa meli kuhusu wageni wanapoingia kuhakikisha hakuna wazamiaji wakati wa kutoka au wizi (International Ship and Port Security {ISPS} level 1) ambapo wataweka visitors log book, vitambulisho vya meli na ukaguzi Kwa aingiaye na kutoka. Mtu wa Port Operation huomba documents za kuonyesha mzigo wa kushuka Dar na kupanga utaratibu wa namna Gani madereva watafanya kazi.

Baada ya Hapo magari huanza kutolewa Kwa kushuka Kwa njia ya kuendeshwa, muda wa Kuanza Operation ni pale gari la kwanza linaposhuka na muda wa kumaliza ni pale gari la mwisho linapomalizika.

Utaratibu unaofata kama ndugu mtoa mada alioanza mpaka kumfikia mteja wa gari husika.
Je mafuta ya kutolea gari hiyo yanapatikanaje au huwa gari zinakuja na mafuta kidogo ndani yake??
 
Je mafuta ya kutolea gari hiyo yanapatikanaje au huwa gari zinakuja na mafuta kidogo ndani yake??
Zinakuja na mafuta ila hayatakiwi kuwa full tank. Maana mafuta yanachangia uzito wa gari. Mfano gari ina full tank 65 ina maana ni kilo za gari plus kilo 65. Chukua hizo kilo 65 zidisha mara idadi ya magari uone unapata kilo ngapi hapo.
 
Asante mkuu kwa elimu nzuri sana... Mimi nilikuwa naswali, kuna gari ndogo nimenunua kutoka Rwanda... Sasa sijafaham kipi kitahitajika hadi gari kufika hapa Tz hadi kusajiliwa kwagari. Document zipi zitahitajika pinditu nafika border? Msaada wenu wakuu.
 
Kama kichwa kinavojieleza ni vitu gani unahitaji kujua wakati unaagiza gari na mlolongo wake wa utoaji wake bandarini kuanzia
- Ushuru wa gari
-Malipo ya bandarini


Mawasiliano
WhatsApp & Call 0652802379
 
Asante kwa somo nzuri mkuu . Na kuhusu flatbed trailer springs leaf double tyre , 3 Axle , 40 feet , ushuru wake kwa TRA ni milioni ngapi please , Kichanja ni mpya .
Screenshot_2023-02-28-12-11-56-640_com.whatsapp.jpg
 
Hey members naombeni kujua kazi ya kutoa gari kwenye meli ina vigezo vipi
Kutoa kupeleka wapi.

Kuendesha kutoka melini mpaka nje sehemu ya parking za Bandari ni kazi ya vibarua wa Bandari, kulitoa nje ya Bandari mpaka Bandari kavu au kwa mteja agent ndio anamcheki dereva wa kumpa kazi
 
Back
Top Bottom