Nimeagiza gari Japan na imepakiwa kwenye meli lakini sijatumiwa tracking number

Joyce wohwoh

Member
Sep 17, 2021
78
180
Naombeni msaada kwa wazoefu kwenye hili, nimeagiza gari japan, imefikia hatua gari imepakiwa kwenye meli, nimejulishwa tarehe ya kuondoka na kufika japo pia hua zinabadilika.

Uhitaji wangu uko hapa sijatumiwa tracking number ya kufatilia meli ya mzigo. Naombeni kujua huwa inatumwa lini?
 
Kwenye documents panakuwa na jina la Meli pamoja na voyage no.. ukiweka details za meli kwa maana Meli au voyage no kwenye search engine kama google utapata details ya location ya meli.

Kama una wasiwasi unaweza kwenda kwa agent wa hiyo meli Shipping line wakakupa details.

Incase bado hujapata wakala yaani Clearing and Forwading agent nakukaribisha kufanya kazi na mimi kwa bei ya punguzo
 
Naombeni msaada kwa wazoefu kwenye hili, nimeagiza gari japan, imefikia hatua gari imepakiwa kwenye meli, nimejulishwa tarehe ya kuondoka na kufika japo pia hua zinabadilika.

Uhitaji wangu uko hapa sijatumiwa tracking number ya kufatilia meli ya mzigo. Naombeni kujua huwa inatumwa lini?

Angalia kene documents jina la meli then nenda google fatilia kupitia websites mbalimbali
 
Meli haina track no. Unachotakiwa kujua meli gani imepakia Gari yako utapakuwa app inaitwa Marine traffic au myshiptracking utaingiza jina la meli utakuwa unaona kila inapopita ports zote hiyo meli ,pia docs huwa zinatumwa kupitia DHL hizo ndizo mala nyingi unapewa track no na utafatilia mpaka pale zitakapofika ulipoandika address yako na utaenda zipokea na hizo ndiyo gari lenyewe sasa bila hizo hutoi hiyo gari na huwa zinachukuaga katika siku 4 mpaka 5 za kazi kutoka Japan to Dar airport.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom