Zijue mashine na mitambo mbalimbali inayotumika bandarini kupakia na kupakua mizigo na shehena mbalimbali

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,916
Leo nakuletea orodha ya mitambo na mashine mbalimbali zilizotengenezwa mahsus kwa ajili ya kupakia na kupakia mizigo na shehena mbalimbali bandarini.

1. Reach stacker
1707290145947.png

Reach Stracker ni mtambo unaotumika kupanga makontena ndani ya bandari. Mtambo huu una uwezo mkubwa wa kuinua kontena na kulipakia juu ya gari la mizigo, au kulihamisha kontena kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya bandari kwa haraka na wepesi mno.

1707290360560.png


2. RTG Crane (Rubber-Tyred Gantry cranes)
1707290883935.png


RTG ni kifupi cha maneno Rubber Tyred Grant Crane. Mtambo huu ambao huenda kwa kutumia magurumu ni mtambo mkubwa wa kupanga, kupakia na kupakua makontena ndanibya bandari.

Mtambo huu ambao pia hujulikana kwa jina la transtainer, una uwezo mkubwa wa kupanga makontena kwenye intermodal operations (namna tofauti ya usafiri, mfano, reli, semi truck, low bed nk)

3. Mobile Cranes
1707291756486.png


Huu ni mtambo unaotumia nguvu ya hydraulic kunyaanyua na kushusha mzigo.

4. Mobile Hopper
1707299136338.png

Mobile Hopper hutumika wakati wa kupakua bidhaa kama nafaka, mbolea, chumvi, sukari, nk. Winch zinafungwa kifaa kinaitwa Port Clamshell Grab Bucket au kwa kifupi grabber, ambapo huchota nafaka, ngano au mbolea kutoka melini na kumimina kwenye Hopper, kisha ngano hiyo hupita kwenye Hopper na kwenda ndani ya gari tayari kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa.

1707299555880.png

Lori likibeba ngano inayotoka kwenye Hopper.

4. Port Grab Bucket
1707310690369.png

Port Grab Basket, hutumika kuchota vitu mhalimbali kama nafaka, mbolea, chumvi nk kutoka melini na kuingiza kwenye Hopper ili mzigo upakowe kwenye gari au kwenye treni.

5. Port Gooseneck Tractor
1707311190533.png

Hutumika kuvuta ma trailer mbalimbaali ndani ya bandari.

6. Gooseneck Lowbed Trailer
1707310974681.png

Hutumika kwa ajili ya kubeba magari, matrekta, vifaru nk kutoka sehemu moja ya bandari kwenda sehemu nyingine.
 

Attachments

  • 1707291494468.png
    1707291494468.png
    100.4 KB · Views: 9
Back
Top Bottom