Je ni muda gani sahihi wa kubadilisha shokapu (shock absober,) ya gari yako?

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Umiliki wa gari ni jambo zuri sana ambalo ni ndoto ya watu wengi lakini ujuzi wa magari ni jambo linalofahamika na watu wachache sana. Kama unamiliki au umekabidhiwa chombo chochote cha usafiri kuna mengi sana unatakiwa uyajue japo madogo madogo ili uweze kukifurahia chombo na kikakutunza nawewe.

Leo naomba nizungumzie maswala ya suspension System kwenye kipengele cha shock absorber yani shokapu. Shokapu ni nini? Nitajitahidi kuelezea katika namna ambayo uweze kuelewa.

Shokapu ni mfumo uliopo kweny upande wa tairi ya gari yako ambao husaidia gari inapokua kwenye mjongeo au kwenye mwendo kupunguza mtetemeko au kujigonga kwa body ya gari pindi unapopita kwenye sehemu zenye mashimo au barabara ambayo si nzuri yani unaweza kuwa unaendesha kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa alaf ukakutana na shimo au barabara mbovu na gari ikapita bila tatizo zaid ya wewe kusikia sauti na mtetemeko kidogo tu. Au kuna wale wanaotumia barabara za vumbi gari ikaenda spid kubwa pamoja na mashimo au vijimawe vidogo lakini wewe ndani ya gari hali inakua kawaida tu husikii sauti ya kujigonga kwa tairi wala gari kuyumba yani kiufupi inafanya tairi za gari zako kupanda na kushuka kwa wakati sahihi pindi unapopita kwenye sehemu kama hizo.

Kuna aina mbalimbali za shock up kulingana na aina ya gari na mwaka wa gari iliyotengenezwa kwa maana gari ya mwaka 2010 ina mfumo mzuri zaid wa shock up kuliko ya mwaka 97 kulingana na mabadiliko ya teknolojia.

Tukirudi kwenye swali la mada husika kutokana na wataalamu muda sahihi wa shock up original za gari kuisha huwa ni miaka 4 mpaka 5 kulingana na matumizi kitu ambacho watu wengi hawajui na ndiyo maana mtu ana gari miaka mingi hajawahi badilisha yani gari ukiingia ndani ni kama watu wanacheza ngoma Lakini pia kuna mtu anabadili shock up ndani ya miezi miwili zimeisha hili nitakuja kulielezea mwishoni lakin kwa sasa hebu tuangalie ni nini kitakachokufanya utambue kwamba unahitaji kubadili shock up za gari yako.

1.Makelele pindi unapoendesha kwenye barabara hasa za vumbu (rough road) yani naamini wengi tumeshawahi kupanda gari ambalo likipita tu barabara ya vumbi basi ndani hamsikilizani ni kelele mtindo mmoja.

2.Unapokata kona gari unaona kabisa tofauti sehem ya tairi za mbele body ni kama haikai vema kama inavotakiwa na kule kuinama kunakuwa hakuna uhiano.

3. Pindi unapopita kwenye shimo lolote unasikia kitu kinagonga kama jiwe hasa sehemu ya mbele ambapo shock up hairudi inavotakiwa hapo lazima body lijigonge.

4. Gari kutokutulia barabarani na hasa kwenye rough road au kwenye yale matuta madogo tunayoyaita rasta ukipita na spidi "raaa raaa" gari inahama hata kama umenyoosha steering.

5. Alama za majimaji kutoka kwa juu ya shock up pindi unapochungulia ambapo kunakuwa na seal ndani zinakua zimeisha lakini pia gesi ndani yake inakua imevuja hii unaiona kwa macho kabisa

Hizo ni sababu kubwa ambazo ukiziona jua shock up zako ni kipengele unatakiwa kubadilisha japo gari ni kama mwili wa binadamu kwamba si kila homa ni malaria kwa maana hizo dalili zinaweza kuwa pia ni sababu ya tatizo jingine kwani suspension system ni pana hivo kama unaona dalili hizo ni vema ukamchek fundi wako akupe uhakika asilimia mia kama ni kweli basi unaweza nichek nikakusaidia kupata shock up nzuri tu kwa gari yako.

MAONI BINAFSI NA USHAURI
Kwa hali halisi ya nchi zetu zinazoendelea kupata shock up original za gari ni mtihani labda uagize hali inayofanya wengi kununua shock up ambazo hazina ubora. Unaambiwa hizi shock up ni mpya kabisa na kweli unazikuta kwenye maganda yake unazifunga baada ya mwezi unakumbana na dhahma ile ile shock up zimekufa so kwa ushauri wangu ni bora ufunge shock up used ambazo ni used nje ya nchi si Tanzania ambazo zimekatwa kwenye magari japo unaweza bahatisha shock up nzuri tu mtu labda kanunua gari haina wiki kapata ajali kaamua kuichinja ukanunua wewe hapo utakua umelamba dume lakini ni nadra sana kukumbana na hiyo bahati ila jambo la msingi ni kwamba tunatakiwa tuwe makini sana na kubadili vifaa vya magari yetu kwani ubahili wa laki mbili unaweza kukuletea kilema au ukapoteza maisha nakuacha na swali moja tu. Kama unaona ubahili kubadili kifaa kwani gari ulinunua shilingi ngapi?


MZIGO USED DUBAI

IMG-20230610-WA0016.jpg
 
Nikishaanza kusikia tu ngoo ngoo, najua tayar. Na sijui kwann hiz makitu huwa zina loga sana vipindi vya mvua?
 
Nikishaanza kusikia tu ngoo ngoo, najua tayar. Na sijui kwann hiz makitu huwa zina loga sana vipindi vya mvua?
Bosi kwenye kipindi cha mvua mara nyingi inakua sio shock up ni cv joints na ma ball joints unakuta rubber zimeisha sasa ukipita kwenye maji unayeyusha grisi yote ile hapa sasa ni chuma kwa chuma kwenye joints

Ntakuja na somo lake hiyo
 
Gari hua nabadilisha muda wowote nikisikia shockup inagonga.
Lakini BMW hua nabadilisha kila ninapo pata ushauri kutoka kwa Nduvini Garage.
 
Back
Top Bottom