Ze Utamu blogger under arrest?

Status
Not open for further replies.
I don't get this. If this guy is not a Tanzanian citizen (according to some posts he is not) and the offence was not commited in Tanzania. What exactly is he being charged with?

And how can a non citizen who breaks a Tanzanian law while not in Tanzania be charged in Tanzania for violating the law?
 
Siku kadhaa zilizopita FMES alisema hivi, watu wakamuijia juu sana kuwa anaangalia movie,

https://www.jamiiforums.com/488002-post37.html

Nyani Ngabu thanks for breaking it. Lakini nina maswali lukuki, are we sure that it is him who manipulated the photo or he just posted a photo which was manipulated by another chap? will he be charged for manipulating the photo or will he be charged for hosting a blog which published the manipulated photo? If he is Tanzanian by birth not by law, and if he is a "foreigner" who happens to have a father who is a big shot, is he going to face our "justice"? Or we are just chasing a ghost.
 
Mh! ni yeye kweli? Kama yeye kweli basi pepo mchafu alimkumba hadi kukubali kuweka uchafu kama ule kwenye blog yake.
 
Nyepesi nilizopenyezewa sekunde chache zilizopita zinadokeza kuwa mmiliki wa ZeUtamu yuko karibu kuwekwa chini ya ulinzi bongo.....stay tuned...more to come

Malecela+Peter+Lusinde.jpg


Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol),wamefanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu. Ndugu Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idara ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee Job Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.

Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania. Licha ya Ndg. Malecela Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani, ambao pia wanahusishwa na Mtandao huo wa Ze Utamu.


Chanzo cha habari: Swahili Time: Ze Utamu Blogger Adakwa
 
Kama unajua sheria then utakubaliana na mimi asilimia 100% kwamba hakuna kesi ya kumfunga hapo. Kama angekuwa raia wa Tanzania mngeweza kumsweka ndani. Lakini huyu jamaa kama ni raia wa UK, kwanza lazima mjiulize ni jurisdiction gani itatumika, Tanzania au UK. Na tangu lini UK wakatuma raia wao Tanzania ili aje ashitakiwe?

Kingine, sidhani kama Tanzania kuna cyber act yoyote. Kama wazee wao wameongea na kukubaliana kwamba mlete Tanzania kijana kisha tutaongea nae, then hii ni kesi nyingine.

Mwisho sidhani kama zeutamu alikuwa guru. Alichokifanya ni kuwatumia washikaji zake wa US ili kulipia host hapa, na host alikuwa Houston na namba walizo register zilikuwa ni za san Diego. Na address ya Host ilikuwa ni Gessner, each means ni small host. Waliogopa kutumia watu kama Yahoo au Goo Daddy sababu ya policy..... Other than that i wish afungwe maisha maana alichokuwa anafanya ni sawa na SHINGONGO nae ana diserv LIFE JAIL TIME.
 
Mimi huwa na pita pita humu kupata habari nyeti lakini si mchangia mada. Lakini sijapendezewa na huu mtindo wa kuto taja majina especially kwa watu kama Zeutamu walio umiza watu wengi kwa kutumia mtandao vibaya. SASA MIMI NINAWEKA JINA LAKE HAPA KUMALIZA MZIZI WA FITINA. JAMAA ALIYEKAMATWA NI:

MALE LUSINDE YES I SAID IT!!!!!!!!!!!!!

next time lets just do what we do yaani "where we dare to talk Openly"

mbona hamumtaji jina lake??tumjuee??

Mkuu nadhani hapo umepata jibu lako.
 
Ukoo huu umeutaka URAIS wa Nchi hii kwa UDI na UVUMBA tangu mwaka 1995. Nadhani kijana wao huyu hajaridhika na kuukosa Urais kwenye ukoo wao. Njia hii anayotumia sasa ndio inaelekea kumliwaza kidogo ingawa itakuwa imemuumiza sana Mzee wetu JSM.
 
hehehe Komredi NN naona leo umewashiiiiiiiiiiiiika
Tarehe 7th October 2008, Saa 04:24 PM kaka/dada Invisible aliandika hivi:

Yep, aliyeisajili hiyo blog si wa awali. Ninachomshauri aloanzisha blog hii ajaribu ku-filter matusi kwenye comments.

Namtakia mafanikio kwa kazi yake mpya...! Ni 'mtoto wa mkubwa' huyu mpya na yupo UK ndiye alikuwa anashirikiana na Shigongo!

Leo nimeamini kweli lisemwalo lipo
 
Eeeh bwana daaah kumbe anashirikiana na Shigongo (according to Invisible's post) sasa zile Mil 10 alizotaka kutoa Shigongo kwa yeyote anaemjua mmiliki wa Zeutamu ilikua longolongo aisee!!
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom