Mkuu Invisible,
Mkuu Invisible mie nina mawazo tofauti sana kuhusu hili.
Ni vema kutofautiana mkuu... Ndo discussion yenyewe!
Ndiyo ilikuwa inawachafua ila kwa kiasi flani iliweza kueleza bayana yaliyo muhimu,hasa wale wenye tabia ya uzinzi ,ilisaidia watu kuwafahamu watu hao jinsi walivyo.Ye s ilisaidia kupunguza maambukizo ya ukimwi sababu watu walipata tahadhari kuhsu hili.
Kuna mengine nakubaliana naye jamaa, tatizo ni kuwa kuna vitu vingine alishindwa kuvi-manage. Yani kuna ukweli katika baadhi ya kashfa alizokuwa akiibua, kweli kabisaa, tena imesaidia watu kuwajua watu flani... Binafsi tatizo langu ni kwenye uwekaji picha huku zikiambatana na matusi, angekuwa detective mzuri kama angesajili tovuti, aweke fomu ya watu kujisajili kabla ya kuanza ku-comment ili wanachama wake wanapochangia wachangie kwa heshima kidogo. Matusi yalizidi mkuu!
Yani kazi yake ingekuwa na heshima kubwa na wengi wangenyooshwa kwa kuwa na tovuti au blog ambayo mtu anapojisajili anatambua anafanya hivyo kwa hiari yake, hapo analindwa na COPA laws!
Suala la kurekodi e-mail za watu nina mashaka nalo sana kwa kuwa nafahamu structure ya blog ilivyo.inachukua path tu na mwenye uwezo wa kujua ni nani huwa ana post picha inafahamika na administrator wa google na tena anajua kwa kutumia IP address.si rahisi kumfahamu owner wa blog kama akidanganya.what google stores is the Path only..Hivi nchi hii ambayo haina hata Data Protection Act kwanini tunapenda kuwatisha sana watanzania???this shit happen hata kipindi kile Jf inafungwa kwa sababu ya kijinga sana 'uhalifu wa kimtandao'?sheria ya wapi?
Emails labda hujaelewa ni kivipi... Ni kuwa mhusika anafahamika tu, clearly kabisaa! Na barua pepe yake nahisi akibanwa anaweza ku-reveal waliokuwa wakimtumia barua pepe (labda watumie fake mail accounts kutuma picha husika) na hilo ndilo nililolenga kuwahadharisha ambao walikuwa wanaendelea kusukuma picha huko, watambue barua pepe hiyo imekuwa chini ya uangalizi tangu Julai mwaka huu.
tusiwatishe watanzani kuwa kuwa uwezo wa kuwakamata wachangiaji labda kama mwenye blog awataje mwenyewe.
Niwahakikishie watanzania kuwa wasitishike na masuala ya online, ila unapoona kuna kitu si fair basi unaposhiriki ujue kuwa unafanya vile kwa ridhaa yako mwenyewe! Huyu labda awe nunda asimtaje mtu na ahakikishe anafanya kufuta kila kitu kwenye barua pepe yake!
I know why imefungwa na nina uhakika kaifunga mwenyewe kwa kupewa kitu kidogo sababu ilimgusa flani mwenye maslahi huko.
Hapana, si kwa hiari yake mwenyewe... Sina maelezo zaidi juu ya hili
🙂
Sikuwahi kuchangia huko ila kila weekeend nilikuwa nikipita katika blog hiyo kujua ni upuuzi gani unaendelea katika nchi yangu.Yes kuna mengine aliharibu ila alisaidai madada zetu kuwajua mabazazi.
Binafsi sikuwahi kwenda kule hadi ilipoanzishwa hii topic nikajua watanzania wameguswa pabaya! Kumbuka, huyu aliwahi kuwa kwenye server yangu pia, alipozidisha mambo zake nikaona hapana, nikamwacha aende penye uhuru zaidi! Kazi ilikuwa nzuri, tena sana mkuu... Naamini dada zetu waliweza kuwajua mabazazi kama unavyosema hapo juu, si dada zetu tu, hata kaka zetu naamini... Tatizo lake ni moja "Uhuru wa commenting..." Ulizidi. Too much of anything is harmful bro!
Hakuna tofauti kati ya Jf na The utamu,The utamu wanajadili mafisadi wa ngono,siye tunajdili mafisadi wa wizi wa mali zetu.tofauti ni kwamba kule watu wako huru zaidi
Hata JF watu wako huru, watu wamewajadili wengi humu kutokana na tabia zao chafu, kuna watu wa BoT wamejadiliwa humu, commenting ya hapa inakuwa na heshima kwakuwa mtu anapoandika anatambua wazi kuwa amejisajili kwa hiari yake na anabeba jukumu la kulinda nickname aliyojisajili nayo! Inawezekana matusi yaliyokuwa yanaonekana kule yakawamo yangu, yako, ya GT na ya hata Mwanakijiji etc... Ni kwakuwa tulikuwa hatuna ID maalumu ya kuandikia!
Admin wa Utamu,kama wakifungulia Kesi naomba unitafute nikusaidie sababu wewe hauna kosa
Naamini anakusoma, kesi hana, akiwa nayo hata mimi naweza kumsaidia...!