Ze Utamu blogger under arrest?

Ze Utamu blogger under arrest?

Status
Not open for further replies.
Pole sana ndugu yangu. Hayo yalikuwa maoni yangu mimi Chokambaya..heri wewe vumbi sio kali huku ulikokania uraia wako ukapokelewa au tuseme ukolewa....mmmh Sikonge vumbi lilikuwa kali sana hasa vumbi la tumbaku ukaamua kupakacha ukaenda hukoooo walipopatengeneza pakawa pazuri...hata hivyo mtu kukana uraia wake ili apate wa nchi nyingine kwa bado ni tatizo na si wivu maana siwezi kumuonea mtu wivu kwa kufanya kitu nisichopenda mimi......mmmh hii ya Mkapa kusema wtz tuna wivu wa kijinga...nakubaliana nawe kabisa....kujiuzia mgodi kwa millioni 700 tu halafu unalipa milioni 70 nakuanza kuvuna...lazima hao watu uwaite wajinga....Mkapa the national traitor......haya bwana Sikonge.

Sasa hapa unaandika nini? Si hadi mwenyewe unaona kuwa Mkapa na Genge lake wamefanya MABAYA zaidi kuliko zeutamu? Mwisho wa siku kila mtu anarudi kwake na hakupoteza hata senti moja, ila hao akina Mkapa na UTANZANIA wao wamekula hela yetu na sasa TUNAPIGWA RUMBA. Unajua, kila mtu anapigwa rumba ila wengine tuna jinsi ya kuhandle. Nikipigwa si sababu nianze ROHO MBAYA. Kama kuna wengine watafaidika na baadaye na sisi tufaidike, why not? Mchukulie Hasheem. Kama angelipata uraia wa USA, mambo yake yangelinyooka haraka sana. Angelikuwa Mtanzania na Mnyamwezi vilevile. Hiyo mihela si angelikuja kuiwezeka Tz kwa ndugu zake? Ila utakuta hawezi kwa ajili ya hii sheria inayoumiza WALALAHOI.

Mie sijapata uraia bado wa nje. Sasa hivi nataka nikausake Seychelles na nikipata huko, Sikonge watakuwa wananiona kwa nadra sana. Sasa mie na tumbaku wapi na wapi? Na Asthma hii kwenye familia yetu jamani? Mie nalima tu nyanya, miwa, kabeji, vitunguu nk na huwa zinanipa hela ya kutosha kutanua hapa Sikonge. Karibu Sikonge siku yoyote uone ninavyokula Vumbi kijana. Ukifika tu Sikonge Mission, uliza Mwana Itimba ndiyo nani na utanipata.... Siku nikikimbia nchi, utakuwa wa kwanza kujua. Ila punguza ROHO KOROSHO kwa wenzio. Kama nikija weza pata uraia wa nje, basi siku nikichoka kuishi huko, narudi tu Sikonge na ninakaa kimya. Nani atakuja nifuata? Mbona sasa mnampa Ubunge Mganda na mambo poa tu? Rostam Aziz yupo tu anadunda, ila Mnyamwezi mie ninakuja ambiwa UKIMPA SIKONGE URAIA WA NCHI MBILI BASI ATAGEUKA ZEUTAMU. Hii ni sawa na Theory ya Mbuzi kula nyazi na kutoa nyuma KARANGA 🙂
Jamani twaishi maisha mafupi sana, mnapata wapi hadi muda wa kufikiria kuwazibia wenzenu? MTAKUFA NAVYO VIJIBA VYA ROHO.
 
Mtanzania,
Mie nafikiri nchi nzuri kwenda ni zile zisizo na mikataba na Tanzania au nchi kama Banana Republic. Huko wataimba wee, hadi wachoke, wewee wadunda tu bila matatizo. Siyo siri, kama una magamba mengi, wee mipaka mingi ukiingia wasikia "welcome home..." Heee heee, ukifika Sweden unawapa na HEJ HEJ!!! Warusi unawapa Dobridin na HARASHOO nyingiiiii Italy wewe ingia na jezi yao ya mpira wa miguu, hata passport hawakuulizi....
 
Kaswaiba Zeutamu is gone,kalikuwa kanafunza adabu mafuska,kosa pekee tu ni la kugusa Mkuu wa Nchi.Wanaolalamika waulizwe walikuwa wapi hadi wapigwe picha za utupu?

na ambao picha zao hazikuwa za utupu?ama hata na ambao zilikuwa za utupu umejua vipi ni za kweli?sababu hata ya mkuu ilikuwa ya utupu....acha pumba
 
I wish I could be on system
ulishajitoa lini kwenye system mkuu???

nasikia ukishaingia hutoki. Raha yake uwe rafiki yao wala usiingie mule maana utabeba dhambi si zako. Unakumbuka ule wimbo uitwao ZOMBI wa Fela Anikulapo Kuti?
 
Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol),wamefanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu.

Ndugu Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza, kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania akishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.

Idara ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.

Malecela ni Mtoto wa Mzee Job Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa unadhalilisha watu, kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo, Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania.

Licha ya Ndg. Malecela Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani,ambao pia wanahusishwa na Mtandao huo wa Ze Utamu.


Source: Swahili Time: Ze Utamu Blogger Adakwa
 
na ambao picha zao hazikuwa za utupu?ama hata na ambao zilikuwa za utupu umejua vipi ni za kweli?sababu hata ya mkuu ilikuwa ya utupu....acha pumba

ninacholia na sirikali ni kwamba walisubiri hadi 'mchawi wa IT' amshike pabaya prezidaa ndio wakaamua kuwa sirias na hii blog,WHICH IZ NOT FAIR

lakini........POA TU!YENDE TU HIVYOHIVYO
 
Hivi jamani mboni hivyo?huwa mnasoma kweli hii post leo imekwisha tumwa zaidi ya mara mbili na wewe unaendelea tu ku post.Acheni hizo mnatumalizia bandwith zetu LOL
 
Mkuu sitaki kuamini kwamba wewe ni mvivu wa kusoma.
Hii thread tayari imeanzishwa jana na Nyani Ngabu.... halafu ipo active inaonekana kirahisi kwenye forums.

Mods pls iunganishwe na thread ile ya awali ama ifutwe...
 
We should be more serious on serious issues maana thread ambayo iko more than active jana na leo ni ile by Nyani Ngabu on this very same issue.
Naweza kuelewa kuwa ndugu yetu huyu anaweza kuwa ameshindwa kuvumilia kutuvunjia hii habari..lakini nadhani kama angekuwa na subira kidogo wakati anaanzisha thread angeona chini pale inamwambie threads nyingine zenye mfanano na nachotaka kukianzisha.
Anyway imeshatokea tumvumilie mwenzetu.
 
....lakini nadhani kama angekuwa na subira kidogo wakati anaanzisha thread angeona chini pale inamwambie threads nyingine zenye mfanano na nachotaka kukianzisha.
Anyway imeshatokea tumvumilie mwenzetu.
Sio tatizo kumwambia, na maelezo yako yamekamilika.. next time ataukuwa na subira wakati wa kuanzisha mada..!

Leo mitaa ya kwangu ni midsummer na hapa ninajitreat na Irish Coffee ...What a day!
 
ninacholia na sirikali ni kwamba walisubiri hadi 'mchawi wa IT' amshike pabaya prezidaa ndio wakaamua kuwa sirias na hii blog,WHICH IZ NOT FAIR

lakini........POA TU!YENDE TU HIVYOHIVYO

nakusoma ndugu,but nashangaa jamaa alivyowatia hatiani wote waliotolewa kwenye zeutamu except mkuu..eti mafuska!miafrika kweli ndivyo tulivyo..
 
We should be more serious on serious issues maana thread ambayo iko more than active jana na leo ni ile by Nyani Ngabu on this very same issue.
Naweza kuelewa kuwa ndugu yetu huyu anaweza kuwa ameshindwa kuvumilia kutuvunjia hii habari..lakini nadhani kama angekuwa na subira kidogo wakati anaanzisha thread angeona chini pale inamwambie threads nyingine zenye mfanano na nachotaka kukianzisha.
Anyway imeshatokea tumvumilie mwenzetu.
Yeah
mimi kabla sijaanzisha thread huwa nafanya search kujua kama ipo au la ndipo nachukua hatua
 
Hebu ngojeni kwanza wajameni. Mmemtaja bw. Male kuwa ndio mhusika mkuu wa zeutamu. Hapo hapo mkadodosa kuwa alikuwa na washirika wake wawili huku Wichita na San Diego. Lakini sasa mbona hamuwataji majina ya hao washirika wawili wa huko Marekani? Kama bw. Male ameshatajwa, kwa nini hao wangine wawili hawatajwi?
 
Lakini sasa mbona hamuwataji majina ya hao washirika wawili wa huko Marekani? Kama bw. Male ameshatajwa, kwa nini hao wangine wawili hawatajwi?

Labda ni watoto wa vigogo ...maana jana hapa watu walipata kigugumizi kumtaja mtoto huyo wa JOB Lusinde Malecela....with time all will be revealed
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom