Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 17,923
- 42,365
Kwema Wakuu!
Sikuwepo zamani sana. Lakini miaka ya tisini mpaka elfu mbili hivi ilikuwa kawaida Baba kumtelekeza mtoto au watoto huku akiacha maneno ya shombo, jeuri na kiburi. Kuwa akikua atanitafuta mwenyewe.
Na kweli zamani hizo niliona watoto wengi wakifanya hivyo, wakitafuta wazazi wao hasa kina baba waliowatelekeza.
Sababu zilikuwa nyingi lakini kubwa zaidi ni Mambo ya mali (urithi) na michango ya maisha pamoja na Baraka(Radhi) kwani iliaminika zamani hizo kuwa huwezi kufanikiwa bila baraka za wazazi (jambo ambalo ni uongo wa wazi).
Sasa kuanzia miaka ya 2010 mpaka hapa ninapoandika mambo yamegeuka sio kidogo.
Siku hizi Wazazi hasa Baba ndio wanaotafuta Watoto wao(waliowatelekeza) na watoto hawana habari kabisa na kuwatafuta wazazi wao.
Ile kasumba ya Wababa waliyokuwa nayo kuwa Mtoto akikua atamtafuta kwa sasa ni useless, yaani ukijichanganya umekwisha.
Watoto hawategemei tena urithi, watoto hawategemei tena michongo kutoka kwa wazazi wao. Watoto siku hizi hawategemei ule uongo wa kizamani kuwa ili ufanikiwe itakupasa upewe sijui baraka sijui radhi za wazazi.
Wapo watoto maelfu kwa maelfu duniani kote ambao hawana mahusiano mazuri na Baba na wazazi wao na wanamaisha mazuri kuliko wale wenye mahusiano mazuri. Hii inatoa picha kuwa kauli zile zilikuwa uongo.
Nami kama Mtibeli nasema, ukitelekeza utatekelezwa tuu. Ukifanya wajibu wako na watoto watafanya wajibu wao. Watoto wa kizazi hiki wamevurugwa sio Pouwa.
Tufanye wajibu wetu.