Kwanini tunawachukulia poa watoto waliorithi utajiri toka kwa wazazi wao

Jadda

JF-Expert Member
May 20, 2019
29,327
83,772
Habari

Kumekuwa na kasumba ya kuwachukulia poa wale watoto ambao wamezaliwa kwenye familia za kitajiri, na kukuta kila kitu kisha kurithi utajiri au mali toka kwa wazazi wao, hasa sisi masikini ngozi nyeusi

Huwa nashindwa kuelewa kwanini inakuwa hivyo, wakati kila siku watu wanasisitiza kutafuta pesa kwa ajili ya kuwarithisha watoto, wajukuu pamoja na vizazi vingine vitakavyofuata ili wasije kuteseka

Lakini cha ajabu hao watoto wanaorithi hizo pesa au mali za wazazi wao hasa wale matajiri, kuna namna jamii hasa masikini inawachukulia, yani inawaona kama some spoiled and inexperienced brats tu

Kwamba we utatuambia nini hujui hustle za kitaa, mtu mwenyewe mtoto wa mama tu mara sijui geti kali mara wa kishua mboga saba, huna cha kutushauri hivyo huwezi kutuinspire kwa utajiri wa kurithi tu

Huwa sielewi ni kwamba tunawaonea wivu plus chuki na husda, sababu labda wazazi wetu walishindwa kutuachia mali au huwa ni njia ya kujifariji na umasikini wetu tu, kwanini huwa tunaona kama kuanzia kwenye umasikini na kuhustle ndio sifa

Je ni lazima kila mtu mafanikio yake yawe yametokea kwenye umasikini na kuhustle ndio awe na story to tell, kama ni hivyo sasa tunawasisitiza watu watafute utajiri kwa ajili ya vizazi vyao ili iweje, kama bado tuna hiyo mentality ya kwamba mtu aliyehustle from the scratch ndio legend

Na wengi tuna ile imani ya kwamba watoto wa kishua wakirithi utajiri toka kwa wazazi wao, huwa haudumu wanaishia kutapanya mali na kuingia kwenye umasikini, sababu walizoea kudekezwa na kupewa kila kitu but in reality that's not always the case

Tuchukulie mfano wa hapa kwetu watu wengi husema matajiri wa kweli ni Said Bakhresa, Reginald Mengi et al, ila Mo Dewji na ndugu zake wamerithi tu utajiri kwa baba yao na siyo self made, mind you hapa siongelei urithi baada ya mzazi kufa, bali utajiri ambao wamepewa waendeleze wakati wazazi wao bado wapo

Kwanza kabisa tunakosea kuwalinganisha hao wazee na Mo Dewji sababu siyo rika moja, pili speaking of kurithi hata Said Bakhresa ana watoto waliorithi utajiri wake, na ndio kwa asilimia kubwa wanasimamia na kuendesha biashara zake sasa hivi wakiongozwa na Yusuf Bakhresa

Na ukiangalia Mo Dewji na Yusuf Bakhresa ndio wako rika moja hivyo wanatakiwa walinganishwe wao, Mzee Said Bakhresa na hao kina Reginald Mengi wanatakiwa walinganishwe na baba yake Mo Dewji Mzee Gulam Dewji, ambaye naye ni self made kama hao wazee wenzie

Lakini bado hatutakiwi kuwachukulia poa kina Mo Dewji na Yusuf Bakhresa eti kisa tu utajiri wao wameurithi, nao wanatakiwa wapongezwe kwa kuuendeleza since the goal is to become rich haijalishi umefanyaje, ukizingatia kurithi utajiri wa mzazi si dhambi wala si kosa kisheria

Well mifano ni mingi ila nimewatolea hao sababu ndio maarufu, lakini wapo watoto wengi ambao wamerithi utajiri toka kwa wazazi wao na wakafanikiwa kuuendeleza vizuri tu bila kufilisika, na si kwamba eti kila mtoto anayeachiwa urithi wa mali basi zitamshinda kisa anaonekana ni mzembe

Na pia haijaandikwa kwamba kila mtoto ambaye hakuachiwa urithi basi akihustle kitaa ndio atakuwa tajiri, wengine huishia kuwa middle class na wengine huishia kuwa masikini kabisa, kuna watu wamehustle from the scratch ila mpaka wanazeeka wameishia kuwa na nyumba, gari, duka Kariakoo au Makumbusho

Na wakati huo huo kuna watu wamezaliwa wamekuta kila kitu kwao, wakarithi utajiri wa wazazi wao na kufanikiwa kuendeleza na mpaka wanazeeka wanamiliki mijumba, magari, makampuni, viwanda et al

So mimi sioni mantiki ya kuwachukulia poa watoto waliozaliwa kwenye utajiri, ikiwa malengo ya watu wengi ni kutafuta utajiri kwa ajili ya watoto wao na vizazi vyao, hakuna na hakutawahi kuwa na tuzo ya kuzaliwa kwenye umasikini na kuhustle from the scratch na wala siyo sifa
 
Watanzania tumezoea umasikini. Tunaupenda na tupo tayari kuulinda na kuupigania kwa hali yoyote, mtu asipopitia msoto tunamchulia kama vile kuna hatua ya maisha kailuka hata home tu unakuta ndugu zako wakubwa wanao uwezo wa kukuinua kiuchumi lakini wanakuacha tu utaabike kwa sababu wao walipitia iyo hali.

Hii kitu wanasiasa na wafanya biashara wanaijua ndio maana hata watu waliokulia kwenye familia za mboga saba kama vunjabei akielezea mapito yake lazima aandike yale mapito magumu hata kama ni story ya kutunga sababu anajua iyo angle ndio atavutia zaidi akili za watu
 
Habari..

Kumekuwa na kasumba ya kuwachukulia poa wale watoto ambao wamezaliwa kwenye familia za kitajiri, na kukuta kila kitu kisha kurithi utajiri au mali toka kwa wazazi wao, hasa sisi masikini ngozi nyeusi..

Huwa nashindwa kuelewa kwanini inakuwa hivyo, wakati kila siku watu wanasisitiza kutafuta pesa kwa ajili ya kuwarithisha watoto, wajukuu pamoja na vizazi vingine vitakavyofuata ili wasije kuteseka..

Lakini cha ajabu hao watoto wanaorithi hizo pesa au mali za wazazi wao hasa wale matajiri, kuna namna jamii hasa masikini inawachukulia, yani inawaona kama some spoiled and inexperienced brats tu..

Kwamba we utatuambia nini hujui hustle za kitaa, mtu mwenyewe mtoto wa mama tu mara sijui geti kali mara wa kishua mboga saba, huna cha kutushauri hivyo huwezi kutuinspire kwa utajiri wa kurithi tu..

Huwa sielewi ni kwamba tunawaonea wivu plus chuki na husda, sababu labda wazazi wetu walishindwa kutuachia mali au huwa ni njia ya kujifariji na umasikini wetu tu, kwanini huwa tunaona kama kuanzia kwenye umasikini na kuhustle ndio sifa..

Je ni lazima kila mtu mafanikio yake yawe yametokea kwenye umasikini na kuhustle ndio awe na story to tell, kama ni hivyo sasa tunawasisitiza watu watafute utajiri kwa ajili ya vizazi vyao ili iweje, kama bado tuna hiyo mentality ya kwamba mtu aliyehustle from the scratch ndio legend..

Na wengi tuna ile imani ya kwamba watoto wa kishua wakirithi utajiri toka kwa wazazi wao, huwa haudumu wanaishia kutapanya mali na kuingia kwenye umasikini, sababu walizoea kudekezwa na kupewa kila kitu but in reality that's not always the case..

Tuchukulie mfano wa hapa kwetu watu wengi husema matajiri wa kweli ni Said Bakhresa, Reginald Mengi et al, ila Mo Dewji na ndugu zake wamerithi tu utajiri kwa baba yao na siyo self made, mind you hapa siongelei urithi baada ya mzazi kufa, bali utajiri ambao wamepewa waendeleze wakati wazazi wao bado wapo..

Kwanza kabisa tunakosea kuwalinganisha hao wazee na Mo Dewji sababu siyo rika moja, pili speaking of kurithi hata Said Bakhresa ana watoto waliorithi utajiri wake, na ndio kwa asilimia kubwa wanasimamia na kuendesha biashara zake sasa hivi wakiongozwa na Yusuf Bakhresa..

Na ukiangalia Mo Dewji na Yusuf Bakhresa ndio wako rika moja hivyo wanatakiwa walinganishwe wao, Mzee Said Bakhresa na hao kina Reginald Mengi wanatakiwa walinganishwe na baba yake Mo Dewji Mzee Gulam Dewji, ambaye naye ni self made kama hao wazee wenzie..

Lakini bado hatutakiwi kuwachukulia poa kina Mo Dewji na Yusuf Bakhresa eti kisa tu utajiri wao wameurithi, nao wanatakiwa wapongezwe kwa kuuendeleza since the goal is to become rich haijalishi umefanyaje, ukizingatia kurithi utajiri wa mzazi si dhambi wala si kosa kisheria..

Well mifano ni mingi ila nimewatolea hao sababu ndio maarufu, lakini wapo watoto wengi ambao wamerithi utajiri toka kwa wazazi wao na wakafanikiwa kuuendeleza vizuri tu bila kufilisika, na si kwamba eti kila mtoto anayeachiwa urithi wa mali basi zitamshinda kisa anaonekana ni mzembe..

Na pia haijaandikwa kwamba kila mtoto ambaye hakuachiwa urithi basi akihustle kitaa ndio atakuwa tajiri, wengine huishia kuwa middle class na wengine huishia kuwa masikini kabisa, kuna watu wamehustle from the scratch ila mpaka wanazeeka wameishia kuwa na nyumba, gari, duka Kariakoo au Makumbusho..

Na wakati huo huo kuna watu wamezaliwa wamekuta kila kitu kwao, wakarithi utajiri wa wazazi wao na kufanikiwa kuendeleza na mpaka wanazeeka wanamiliki mijumba, magari, makampuni, viwanda et al..

So mimi sioni mantiki ya kuwachukulia poa watoto waliozaliwa kwenye utajiri, ikiwa malengo ya watu wengi ni kutafuta utajiri kwa ajili ya watoto wao na vizazi vyao, hakuna na hakutawahi kuwa na tuzo ya kuzaliwa kwenye umasikini na kuhustle from the scratch na wala siyo sifa..
Kutunza na kulinda urithi sio kazi rahisi pia. Hakuna mtu anayewachukulia poa lakini mara kibao hapa bongo wanashindwa kuendeleza na kusimamia mali au utajiri wanaoachiwa. Hapo ndio maskini sasa huleta dharau.
 
Umenigusa sana, mimi sio tajili na hata baba yangu hakuwa tajili ,ila nabaguliwa mno , nikiwa kazini walimu wenzangu huwa hawaniruhusu niongee kitu utasikia huyajui maisha wewe mtaani usiseme, jana nimeuliza hivi mshahara umeisha toka nikajibiwa na madam hata wewe unaulizia salary wengi wasicho jua ni kuendelez mari za urithi ni ngumu sana
 
Mtoa mada uko sahihi hamna tuzo ya kuteseka wala kutafuta utajiri kwa shida, waafrika wengi tuna wivu na roho za kimasikini tu, na kuwachukulia poa watu kama hao ndio njia yetu ya kujifariji..
 
Back
Top Bottom