Wazazi wazembe wanatoa Elimu kama Urithi, Sheria ya Mirathi inakataa Elimu sio Urithi, Biblia inataka baba kuacha Urithi

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,870
6,273
WhatsApp Image 2024-02-08 at 12.40.41.jpeg

tunaanza na mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi​

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na
Bwan
a”

NIMEGUNDUA WAZAZI WA ZAMANI WASIOENDA SHULE WANA AKILI KULIKO WAZAZI WA KISASA.

Elimu ya Mzungu imezalisha wazazi wajinga kuliko wazee ambao hawajapata hiyo elimu.

Wazee wa zamani hawakuwa na elimu ila walikuwa na akili sana. Walikuwa wanaandaa ajira za watoto wao.

Walijua mahitaji ya msingi ya binadamu ni nini chakula, Mavazi na malazi.

Baba ilikuwa wajibu wake kuhakikisha kizazi chake kinapata uhakika wa chakula, mavazi na maradhi kwa wakati.

Kijana akifikisha miaka 18 baba yake alikuwa anampa shamba, mifugo na malazi. Kisha anamuozesha.

Hapo maana yake ajira ameshampatia mwanae kwenye hilo shamba na mifugo

Wazazi wa siku hizi mtoto wa miaka 25 hapewi chochote kwa kisingizio amepewa elimu. Na elimu ndio urithi.

Ukweli elimu sio urithi. Hakuna sheria ya mirathi inayotambua elimu kama urithi.

Wazazi wa zama hizi Wanajifanya wanapenda dini ila mafundisho ya dini kuhusu urithi wanayakataa. Biblia inasema Nyumba na mali mtu atapewa na baba yake. Hakuna walipo sema elimu ndio urithi

Wazazi wengi siku hizi wanatumia asilimia kubwa ya vipato vyao kusomesha watoto wao, ila wanasahau wajibu wao wa kidini hasa Wakristo kuwarithisha mali hao watoto wao.

Watoto wengi wamesoma, wamemaliza vyuo vikuu ila hawajapata ajira. Wanashinda wanazurura tu na kulala nyumbani kutwa nzima. Sababu baba hana rasilimali za kumpa mtaji. Ama baba amefariki hajamuachia urithi wa mali, sababu kuu ameshapewa urithi wa elimu.

Elimu ni basic need kama kumpa mtoto chakula, Hivi unaweza wapa watoto chakula ati ndio useme Urithi,
Elimu ni basic need Kwa mtu inayomsaidia kutumia Rasilimali. Mzazi unapaswa uache Urithi WA rasilimali ambazo mtoto atazitumia kuendesha maisha yake baada ya kupewa elimu. Elimu bila Rasilimali ni Sawa na mdomo pasipo Meno.

Baba yake Mo dewji kamsomesha Mo dewji IST na chuo kikuu kikubwa duniani.. ila baada ya kumaliza tu chuo bado baba akaja kumpa urithi wa mali kijana wake yaani kampuni ya Mohammed Enterprises

Tatizo la Ajira linaletwa na Wazazi wahuni.

Hujamrithisha mtoto Mali ataachaje kukosa Ajira?

Maisha ni yaleyale Ila binadamu ndio wanajifanya yaonekane yamebadilika

Kwa maoni yako je elimu ni urithi wa kuwekewa nguvu kuliko urithi wa mali ?
 
Haya sasa! Hayp mashamba makubwa ya kuwakatia watoto wakalime bado yapo? Hata kama yapo bado yanarutuba ya kuotesha na kuzalisha chakula cha kushiba? Bado elimu ndo urithi mbadala wa mashamba! Ukimpa elimu atasoma na kuelewa ulimwengu wa sasa na kama anajitambua atajitafuta nakujipata!
 
naomba nikupe mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi;​

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”
 
Wazazi wa zamani wasioenda shule wana akili kuliko wazazi wa kisasa.

Elimu ya Mzungu imezalisha wazazi wajinga kuliko wazee ambao hawajapata hiyo elimu.

Wazee wa zamani hawakuwa na elimu ila walikuwa na akili sana. Walikuwa wanaandaa ajira za watoto wao.

Walijua mahitaji ya msingi ya binadamu ni nini chakula, Mavazi na malazi.

Baba ilikuwa wajibu wake kuhakikisha kizazi chake kinapata uhakika wa chakula, mavazi na maradhi kwa wakati.

Kijana akifikisha miaka 18 baba yake alikuwa anampa shamba, mifugo na malazi. Kisha anamuozesha.

Hapo maana yake ajira ameshampatia mwanae kwenye hilo shamba na mifugo

Wazazi wa siku hizi mtoto wa miaka 25 hapewi chochote kwa kisingizio amepewa elimu. Na elimu ndio urithi.

Ukweli elimu sio urithi. Hakuna sheria ya mirathi inayotambua elimu kama urithi.

Wazazi wa zama hizi Wanajifanya wanapenda dini ila mafundisho ya dini kuhusu urithi wanayakataa. Biblia inasema Nyumba na mali mtu atapewa na baba yake. Hakuna walipo sema elimu ndio urithi

Wazazi wengi siku hizi wanatumia asilimia kubwa ya vipato vyao kusomesha watoto wao, ila wanasahau wajibu wao wa kidini hasa Wakristo kuwarithisha mali hao watoto wao.

Watoto wengi wamesoma, wamemaliza vyuo vikuu ila hawajapata ajira. Wanashinda wanazurura tu na kulala nyumbani kutwa nzima. Sababu baba hana rasilimali za kumpa mtaji. Ama baba amefariki hajamuachia urithi wa mali, sababu kuu ameshapewa urithi wa elimu.

Kwa maoni yako je elimu ni urithi wa kuwekewa nguvu kuliko urithi wa
 
naomba nikupe mistari ya biblia

Mithali 13:2 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi;​

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”
Acha maneno ya kukariri! Namimi ukitaka naweza kukupa mistari kibao "kwa vile umeyakataa maĥarifa mimi nami nimekukataa"; "mkamate sana elimu na wala usimwache aende zake"; "mpende sana Mungu kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote na kwa AKILI zako zote; akili=elimu".
 
Yaelekea hujui hata huu uzi unaongelea nini.

elimu ni maarifa. hoja ya huu uzi ni kwamba maarifa sio urithi

sheria gani ya mirathi imetambua elimu kama ni urithi ?

hukumu gani ya mirathi umeona mtu karithishwa elimu ?
 
ndo wale wazazi unakuta kwenye harusi wanaitwa waseme zawadi waliomuandalia kijana/binti yao....unakuta kanaletwa kajifuko unaweza sema labda ni burungutu la ela...unaona mtu anatoa biblia alafu anachukua MIC ''Mimi kama baba napenda kumpa mwanangu zawadi ya biblia'' KAMALIZA 😁
Inasikitisha! Hiyo Biblia na mistari ungetakiwa huwe umempa kitambo alipokuwa mtoto mpaka ukamkuza! Sasa hivi mpe maokoto! Mxiuuuuh
 
Acha maneno ya kukariri! Namimi ukitaka naweza kukupa mistari kibao "kwa vile umeyakataa maĥarifa mimi nami nimekukataa"; "mkamate sana elimu na wala usimwache aende zake"; "mpende sana Mungu kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote na kwa AKILI zako zote; akili=elimu".
Elimu sio urithi lakini ni mfumo wa kukufanya uwe na maarifa katika mambo mbalimbali Na sio lazima uipate darasani.
 
Yaelekea hujui hata huu uzi unaongelea nini.

elimu ni maarifa. hoja ya huu uzi ni kwamba maarifa sio urithi

sheria gani ya mirathi imetambua elimu kama ni urithi ?

hukumu gani ya mirathi umeona mtu karithishwa elimu ?
Una kajumba kako ka vyumba viwili na kaeneo ka kuotesha mazao kadhaa au mboga mboga! Umezaa watoto 7! Haya! Nipe mchanganuo wa jinsi ya kugawanya urithi!
 
Haya sasa! Hayp mashamba makubwa ya kuwakatia watoto wakalime bado yapo? Hata kama yapo bado yanarutuba ya kuotesha na kuzalisha chakula cha kushiba? Bado elimu ndo urithi mbadala wa mashamba! Ukimpa elimu atasoma na kuelewa ulimwengu wa sasa na kama anajitambua atajitafuta nakujipata!
Shamba ni kama alama tu....yaweza kuwa genge,kuku na mikokoteni.
Na hata hivyo kwa Tz ardhi bado ipo kubwa na nzuri sana.
 
Haya mambo ya urithi sijui blahbkah yako Africa! Ulaya mtoto akifikisha miaka 18 anatakiwa atoke kwa wazazi akapambane! Labda wazazi wakifariki ndo hayo mambo ya next of kin na urithi yanakuja! Mtoto anatakiwa umpe elimu ya kujitambua na kupambana!
 
sio kweli TRUMP mwenyewe karithi mali za baba yake

ulaya wana richest family nyingi sana ambazo zimerithi mali za wazazi wao, mfano glazers family wamiliki wa manchester united.
 
Back
Top Bottom