Hardlife

JF-Expert Member
Apr 11, 2021
2,750
6,247
64243AF0-0893-4C1E-8E21-AE4E61A439F2.jpeg
Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Hans Pope amefariki usiku huu katika Hospitali ya Aga Khan alipokuwa akipatiwa matibabu.

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya UVIKO-19 na alinukuliwa na kituo cha E-FM akisema alikuwa ICU akipambana na maradhi hayo.


Marehemu Hanspope alishawahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba kwa muda mrefu.

Simba imethibitisha taarifa za kifo cha Zacharia Hanspope aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi:

“Uongozi wa Klabu ya Simba umepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Zacharia HansPope ambaye amefariki dunia usiku huu”

Poleni wana Simba.
===

KESI YA HANSPOPE ILIAHIRISHWA AGOSTI 31, 2021 KWA DHARURA YA KUUGUA

Taarifa zinaeleza kuwa inaelezwa kuwa mnamo Agosti 31, 2021 Hans Pope alishindwa kuhudhuria kesi yake katika mahakama ya Mkazi Kisutu kutokana na kuugua. Hivyo, wakili wake aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kusikiliza shauri hilo.

Hans Pope na wenzie wanakabiliwa na mashtaka nane yakiweno ya kughushi, matumizi mabaya ya madaraka kwa kuhamisha fedha bila kamati ya utendaji ya Simba, kukaa kikao.

Hata hivyo, Hans Pope na wenzake wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili, ambapo kila mdhamini alisaini dhamana ya Sh30 milioni.

Soma pia: Zacharia Hanspope ni nani?
 
Back
Top Bottom