antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 44,643
- 120,172
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ametoa taarifa kuhusu mashambulizi dhidi ya Israel yanayofanywa na wanamgambo wa Kipalestina.Hawawezi kumsaidia Ukraine na Israel kwa wakati mmoja.
"Ninafuatilia kwa karibu matukio nchini Israel. Ahadi yetu kwa haki ya Israel ya kujilinda bado haijayumba, na ninatuma rambirambi zangu kwa familia za waliopoteza maisha katika shambulio hili la kuchukiza dhidi ya raia," anasema.
"Katika siku zijazo Idara ya Ulinzi itafanya kazi kuhakikisha kuwa Israel inapata kile inachohitaji ili kujilinda na kuwalinda raia dhidi ya ghasia na ugaidi usiobagua."