Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Hapa ni kama unatwanga maji kwenye kinu. Matajiri wao wanaangalia watabaki na nini baada ya kutoa gharama za uzalishaji, kodi, usafiri, mishahara. Wanataka wabaki na kikubwa kwahiyo sehemu pekee ya kunyonya (kufidia) ni kupitia vibarua: kwasababu wengi wao hawana options nyingi kwenye maisha za kuwaingizia kipato hawana budi kufanya hizo kazi.

Kwasasa Dunia inahama, viwandani inabidi zibaki mashine tu na Engineers. Tulipofikia ni Akili zaidi inayoweza kukupa pesa ya kukidhi mahitaji yako, na hiyo Akili inaenda sambamba na maarifa (elimu). Sasa turudi kwenye nchi yetu: Je, serikali yetu baada ya miaka 60+ toka uhuru imeweza kuwapatia elimu bora watanzania kwa asilimia ngapi? Wenye elimu tu wanalalamika mishahara midogo, hapa ni kila mtu kupambana na hali yake tu.
Forgotten mbona unaongea maneno kama mungu mjomba Ako?
 
Mkuu hio upo dunia nzima, unaposikia Wazungu wanakimbilia china kwa ajiili ya cheap labor ndio kama hao, saizi wanatoka china wanaenda India kwa ajiili ya watu kana hao,
Unskilled labor dunia nzima mishahara yao ni mbuzi tu, mana wanakuwa hawana mikataba, day worker tu,

Kwa kusema hivyo tuhimizane ndugu zangu kusoma sanaa
Ndugu yangu,hivi msomi ni yupi?
Kuna sehemu niliajiriwa,ilikuwa ukiangalia vibarua wengi ni form four na six ambao hawana
wa kuwaendeleza wanasaka chapaa ili wajisomeshe na wengine hawakupata maksi nzuri
ili kuendelea,Sasa ukiangalia mshahara huo kama huna mtu anayekuhifadhi huwezi fanya lolote
utaendelea kuteseka hadi nguvu ziishe.
Cha kufanya,kama kwenu kuna shamba ni heri urudi ukalime,au basi jitahidi uwe machinga
 
Sad truth, maisha hayaangalii process,
Ni kweli wanatafuta hela ya kujisomesha, ila hapo wapo kama unskilled labor, na issue ya wao kutokwenda shule sio kesi ya mwenye kiwanda ni kesi yao wenyewe, hapo watalipwa pesa ya siku,

Kwenye maisha hulipwi ili kutimiza ndoto zako, unalipwa kwa kiasi cha value unayo add, mwajiri hakulipi ili uende shule, analipa kwa kile unampa kwenye biashara yake,

Huu ni ukweli mbaya, hausound vema ila ndivyo ilivyo
 
Umewahi kufanya kazi kwenye ofis mbalimbali?
 
Kuna kiwanda kiko Pale Keko karibu na ukumbi wa DDC nadhani ni cha cello. Malipo kwa siku ni sh. 3500 kwa siku ilikuwa kwa muda mrefu. Sasa ni sh. 4000, kazi masaa 12 yaani lisaa limoja sh. Mia tatu na centi.

Viwanda vingi malipo ni sh. Elfu 5000 kwa siku, hii maana yake lisaa limoja la kazi ni sh. 400. Viwanda vyenye majina makubwa malipo kwa siku ni sh. 7000 hii maana yake lisaa limoja sh mia 6.

Hata kama ni non skilled labor ni haki Mtanzania alipwe sh. Mia 4 kwa lisaa limoja? Ni utumwa wa wazi uliopata baraka za serikali.

Hawa mabilionea wetu akina Bakhressa na Mo huwabebesha Watanzania viroba vya unga wa ngano kwa sh. 50 au pungufu kwa kiroba kimoja. Ni utumwa.

Nimewahi kufanya kazi siku moja tu kwa wahindi Kariakoo ni zaidi ya utumwa , kula juu yangu, nauli juu yangu malipo 7500 kwa siku na kazi very risk. Kazi ya kupeleka mizigo ghorofa ya 12 kutoka chini. Sikurudi tena.
Ulikuwa unashusha mizigo kwenye makontena?.
 
Kuna siku niliongelea humu swala la civil society (workers civil groups) umuhimu wake. Ila nikagundua Wafanyakazi wengi hawajui hili swala. Na sio kutokujua tu. Hata wale ambao wamejiunga huwa wanatumia vyama hivi kipindi cha shida tu tena kwa uchache. Acha watu waumie. Waendelee kugoma na vyama vya siasa wakati kuna vyama unaweza peleka tatizo elekezi kwao.
 
Kuna kiwanda kiko Pale Keko karibu na ukumbi wa DDC nadhani ni cha cello. Malipo kwa siku ni sh. 3500 kwa siku ilikuwa kwa muda mrefu. Sasa ni sh. 4000, kazi masaa 12 yaani lisaa limoja sh. Mia tatu na centi.

Viwanda vingi malipo ni sh. Elfu 5000 kwa siku, hii maana yake lisaa limoja la kazi ni sh. 400. Viwanda vyenye majina makubwa malipo kwa siku ni sh. 7000 hii maana yake lisaa limoja sh mia 6.

Hata kama ni non skilled labor ni haki Mtanzania alipwe sh. Mia 4 kwa lisaa limoja? Ni utumwa wa wazi uliopata baraka za serikali.

Hawa mabilionea wetu akina Bakhressa na Mo huwabebesha Watanzania viroba vya unga wa ngano kwa sh. 50 au pungufu kwa kiroba kimoja. Ni utumwa.

Nimewahi kufanya kazi siku moja tu kwa wahindi Kariakoo ni zaidi ya utumwa , kula juu yangu, nauli juu yangu malipo 7500 kwa siku na kazi very risk. Kazi ya kupeleka mizigo ghorofa ya 12 kutoka chini. Sikurudi tena.
Hii ni Manamba
 
Halafu mchawi mwingine ni mtanzania mwenzako(supervisor). Muhindi anakupiga kwa kukulipa 5000 per day, halafu msimamizi wako nae anakupiga kwakukulipa 4000 au 4500 per day.Maisha ya viwandani ni magum sana hapa tz
 
Back
Top Bottom