Unaweza kusema CCM inalazimisha mapenzi kwa wananchi. Wananchi wameichoka. Wananchi hawaipendi CCM. Leo nimefika katika kituo changu nilichojiandikishia kupiga kura hapa jijini Mbeya, nikiwa na hamu kabisa ya kutumia haki ya msingi kumchagua kiongozi nimtakaye. Mbali na mimi niliwakuta pia wananchi wengine waliokuwa kituoni kwa lengo hilo hilo. Cha ajabu na cha kusikitisha tunaambiwa hakuna kupiga kura, kisa mgombea wa CCM amepita bila kupingwa. Kwamba mgombea wa UKAWA alienguliwa katika hatua za mwishoni kwa kutokutimiza taratibu za wagombea. Wananchi tukasema basi tumpigie kura huyo huyo wa CCM kuonesha kama tunamtaka yeye au la, wasimamizi wakasema kanuni haziruhusu kufanya hivyo! Tunajua hizo ni hila za CCM kuengua wagombea wa vyama vinavyounda ukawa kiujanja ujanja lakini naomba niwaambie kuwa kufanya hivyo ni sawa na kulazimisha mapenzi kwa wananchi! Kufanya hivyo ni sawa na mwanaume kulazimisha mapenzi kwa mwanamke ilihali hakutaki au kinyume chake! Naomba CCM wajue kuwa wakati wa kuongoza watapata shida kwani watakuwa wanaongoza wananchi wasiowapenda!