Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014
Wakuu, leo, Disemba 14, 2014 Watanzania wanapiga kura kuchagua viongozi wao wa Serikali za Mitaa, Tanzania Bara (Tanganyika).

Viongozi wanaochaguliwa leo ni katika nafasi za Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Wenyeviti wa Vitongoji, Wajumbe 6 wa Serikali ya Mtaa (Halmashauri) na wajumbe wa Viti Maalum wa Mtaa/Kijiji.

Kama ilivyo ada JamiiForums itakuwa ikikujuza yanayojiri, katika uzi huu utapata/utaleta updates zinazohusiana na uchaguzi huu.

Karibuni sana

========
UPDATES MUHIMU:

attachment.php

attachment.php

Hapa ni Mtaa wa Kijitonyama
- Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana
Uchaguzi wa kijiji cha Kagunga, Kigoma Kaskazini umefutwa hadi siku nyingine baada ya mtendaji wa kata kusema ACT imefutwa katika uchaguzi huo. Hata hivyo msimamizi mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza.

Wagombea wa vijiji 2 wa chama cha ACT walitumia anuani ya Shule kama anuani yao. Mtendaji kawaeungua. Wananchi wamemgoma. Uchaguzi umeahirishwa.

Kijiji cha Kagunga na Zashe kata ya Kagunga Jimbo la Kigoma Kaskazini
Huku Dodoma, CCM wanadaiwa kumteka na kumsihi mgombea wa CHADEMA atangaze kujitoa... Hadi sasa amepatikana na amekana kujitoa kabisa..

Wananchi wamegoma kupiga kura hadi mgombea huyo awe huru na aje kupiga kura yake..
- Mgombea wa CHADEMA Kijiji cha Darajani huko Liwale, M. Manakwa amepigwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo, amelazwa hospitali

Mgombea wa kitongoji cha Isandula juu kupitia CHADEMA ndugu Kasema amevamiwa usiku wa kuamkia leo tarehe 14/12/2014 na kukatwa katwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili wake hali iliyompelekea kupoteza fahamu.

Hivi sasa amelazwa katika hospital ya Magu akiendelea kupatiwa matibabu.

-Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Suleiman Liwowa ametangaza kuwa katika vitongoji 613 vya Wilaya hiyo vyama vya Upinzani vimeshindwa kusimamisha wagombea.
Kutoka Songea Mjini, anatuambia kuwa kata ya Misufini hadi sasa kura hazijaanza kupigwa kwa sababu fomu za kupiga kura nafasi ya uenyekiti wa mtaa zimechanganywa, kwani kwenye nembo ya CCM jina lililoandikwa ni la mgombea wa CHADEMA kama inavyoonyesha kwenye picha

10801870_315160458677928_8688034558725149839_n.jpg
Hapa Mbagala Saku, Kituo Mfenesini karatasi za kupigia kura zipo 300 tu na watu walio jiandikisha kupiga kura ni 1512 ,kwa hiyo mpaka sasa upigaji kura bado haujaanza

Mkuzo, Songea:

Baada ya watu kuwa wengi; Uamuzi uliotolewa ni kuingia watu wanne wanne kupiga kura.

Atayebainika kurudia atabakizwa ndani au wapiga kura wataamua nini atendewe.

Kutoka Mkuranga; Uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wilaya yote ya Mkuranga umeairishwa mpaka Jumamosi ya tarehe 20/12/2014


Kutoka Moshi, Kilimanjaro;

[15:12, 14/12/2014]: Kutoka Wilaya ya SIHA Kata ya kiruwa kituo cha wanri kati kura haijapigwa wapiga kura wameambiwa waondoke mana kiongozi alishapita kwa kura za maoni.

[15:13, 14/12/2014]: Kutoka Wilaya ya Hai Uchaguzi wa M.kiti wa kijijii Sadala umeahirishwa ila uchaguzi wa vitongoji unaendelea kama kawaida.

[15:15, 14/12/2014]: Kata ya sanya juu vituo vya kilingi kati,kikuyuni,shule ya msingi na sekondari fomu za kujaza matokeo mpaka sasa bado hazijafika.

[15:17, 14/12/2014]: Kutoka Wilaya ya SIHA P20.A.2.7- Vituo vyote kilingi kati na kikuyuni ambapo ndo kuna upinzani kwa maana ya kuwa wananchi wanakuja wamelewa na kutamka hadharani chama wanachokitaka.

Chanzo:LHRC‬
Mpaka muda huu saa nne usiku kata ya Nzowe wananchi wanaendelea kupiga kura! Upigaji wa kura umeanza mnamo saa tatu asubuhi na bado unaendelea mpaka saa nne kasoro usiku huu.
attachment.php

Pichani ni wananchi wakihakiki uwepo wa majina yao masaa kadhaa yaliyopita.
 

Attachments

  • p1.jpg
    p1.jpg
    50 KB · Views: 4,671
wazirii ? Wapi huko ? Nani huyo ? Weka picha video si wote tutaona mkuu

TUFANYE UCHAGUZI WA AMANI
 
mtaa wa Migungani , sokon one, arusha mjini sisi tunasubiria kusherekea ushindi tu kisha wiki inayofuata tuwaburuze mahakamani mwenyekiti wa ccm aliyepita na wajumbe wake kwa kutowai kusoma mapato na matumizi ya mtaa na pia kujivutia bomba la mtaa kwake na kuuza maji pasipo serikali ya mtaa kupata mapato
 
Hivi unawezaje kuupload video? Kuna Waziri alitaitiwa jana usiku akitoa hongo ..

Na nyie RAIA mmekuwa dhaifu sana, mtu anatoa rushwa mnamwangalia tu? Huyo alikuwa Wa kuchoma moto kabisa, hana tofauti na vibaka mnaowatia kiberiti mkidai nyie ni raia wenye hasira kali au kama ni m-mama mngemgegeda hadharani!! Mkuu mmeonesha udhaifu mkubwa kabisa!!
 
Back
Top Bottom