Siasa za upinzani zinanishangaza sana kiukweli. Ukiwa unashinda hapa Jf nakusoma yanayoendelea juu ya kuchukiwa CCM utadhani uchaguzi ukiitishwa kesho hakuna tena CCM. Lakini ukipita huko mtaani watanzania hawana wanachojua zaidi ya CCM. Nimepita sehemu majuzi nikiwa tanga mjini watu/wanawake ndio wanajadiliana wanasema nasikia kuna chama kipya chaitwa UKAWA kimeunganisha CUF na CDM. Sasa huyu akienda kwenye sanduku la kura asipoikuta UKAWA ataichagua nini kama si CCM?
Una roho mbaya sana mkuu! Naomba mungu alaani vizazi vyako vyote! Machungu ya watanzania yabadilike kuwa laana na mateso kwa vizazi vyako vyote! Ulaaniwe sana mkuu!
Mabendela na mdundiko havipigi kura! Labda wamejipanga kivingine. Binafsi ningefikiria kampeni nzuri kwenye serikali za mitaa ingekuwa nyumba kwa nyumba kwa mgombea kujitambulisha kuliko hizi za makelele na helkopta!Nipo hapa Mbeya, kada wa chama tawala. Hata hivyo pita pita ya ngu mitaani hadi kule Rungwe nimejionea mwenyewe hali ilivyo tete kwa CCM.
Ni kama CHADEMA wao wamejitayarisha vizuri, na wapo kila mahala. Huu si oungo ,maana wameteka vijana wengi na bendera hasa Ile pana ziko kila mahala.
Jana niliona magari kadhaa ya matangazo na uhamasishaji ya CHADEMA, lakini sikubahatika kuona hata moja la CCM.
Nimefika Kiwira ndo balaa! Mchana vijana walifunga barabara kwa mdundiko uliokuwa ukiongozwa na gari ya matangazo ya CDM!
CCM najionea huruma lakini tusubiri tu.
Twendeni Tukapge Kura Tukijua Wazi Kwamba Mwenyekiti Wa Kijiji Au Mtaa Ana Uwezo Wa Kutatua Kero Ndogondogo Tu Mf. Ulinzi,kuptsha Barua,kusuluhsha Mizozo etc, Miradi Kama Maji, Umeme, Zahanati, Ni Jadi Ya Siasa Za Uwongo Za Tanzania.
Mkuu CHAMVIGA hapa Jf kila uchaguzi huwa hizi harakati za chadema na wafuasi wake zipo hivi hivi kila uchaguzi, subiri ikifika usiku wa leo watakuja na hadithi mpya, utasikia daftari la wapiga kura halijaboreshwa, utasikia kura zimeibiwa, yaani zitakuja sababu hapa kama elfu 10,
Ajabu kuwa hii CCM ndio hiyo hiyo miaka yote na mbinu zao za ushindi ni zile zile, kifupi upinzani hauna mikakati ya maana kushinda, nategemea leo usiku upinzani utarudia Yale Yale ya miaka yote kulalamika bila kupata suluhu
Nipo safarini muda huu kutoka Hometown Lushoto naelekea pande za Tanga mjini nimepita soni,mombo,korogwe asubuhi hii watu wamejaa stendi wanapiga dili za kusongesha maisha yao wala hawana habari na kitu inayoitwa uchaguzi na hawahawa ndio huwa wanakuwaga kipembelembele kwenye kuiponda CCM lakini hawanaga tabia ya kupiga kura je CCM mtaitingisha lini nyie wapinzani?
Watanzania wamekoseshwa elimu na hilo ndio mtaji mkubwa wa chama tawala.
Itabidi mfikirie upya uendeshaji wa siasa zenu otherwise mtapiga sana kelele.