Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Mgombea wa kitongoji cha Isandula juu kupitia CHADEMA ndugu Kasema amevamiwa usiku wa kuamkia leo tarehe 14/12/2014 na kukatwa katwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili wake hali iliyompelekea kupoteza fahamu.

Ndugu Kasema anatarajiwa kushinda kitongoji hicho kutokana na nguvu kubwa aliyonayo, siku kadhaa zilizopita alifuatwa na viongozi wa ccm na kumtishia maisha iwapo ataendelea na msimamo wake wa kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.

Hivi sasa amelazwa katika hospital ya Magu akiendelea kupatiwa matibabu. Tunamwombea kwa Mungu apone ili aendelee na harakati za ukombozi wa kitongoji chake
 
hadi saa tatu hii asubuhi utaratibu wa kupiga kura hauleweki.. kuna chaos tu hapa..
*HAKUJABANDIKWA MAJINA YA WAPIGA KURA
*MPIGA KURA HAJUI ATAPIGA KURA KATIKA KITUO KIPI (MAJINA SI HAMNA)
*WANASOMA MAJINA KWA MDOMO RAIA MSIKILIZE MAJINA.YENU ..VITUO VITATU WASOMAJI WANATUMIA MDOMO ..NI MKANGANYO TUU.. HUJUI UMSIKILIZE MTANGAZA WA KITUO GANI..
*WAKO SEHEMU YA WAZI TU AMBAYO HATA KUBANDIKA MAELEKEZO NI NGUMU MNO... hili eneo lina mashule mengi tu walishindwa hata kuweka kituo cha uchaguzi katika shule moja wapo
*MISTARI INAPANGWA WASIMAMIZI WANAIVURUGUA NA WATU NI MAMIA..
......NI UGOMVI NA MAKELELE TUPU...kuna dalili zote za kupigwa ngumi hapa
............huu utaratibu sijawahi kuuona sehemu yoyote....mwenye namba ya watu wa tume ya taifa ya uchaguzi tafadhali aweke hapa tupeleke madai yetu kwao
 
Mgombea wa kitongoji cha Isandula juu
kupitia CHADEMA ndugu Kasema amevamiwa
usiku wa kuamkia leo tarehe 14/12/2014 na
kukatwa katwa mapanga sehemu mbali mbali
za mwili wake hali iliyompelekea kupoteza
fahamu
Ndugu kasema anatalajiwa kushinda
kitongoji hicho kutokana na nguvu kubwa
aliyonayo, siku kadhaa zilizopita alifuatwa
na viongozi wa ccm na kumtishia maisha
iwapo ataendelea na msimamo wake wa
kujitoa katika kinyang'anyilo hicho
Hivi sasa amelazwa katika hospital ya Magu
akiendelea kupatiwa matibabu,tunamwombea
wa Mungu apone ili aendelee na harakatib za
ukombozi wa kitongoji chake
Mungu amjaalie apone na aendeleze harakati.
 
Majengo, Msua, Katuma, Katandala, Tunesco, Kisiwani, nk ni kata za Sumbawanga mjini hadi sasa ni saa 10:00 am hakuna kinachoendelea
 
Huku kwetu Kinyerezi kituo cha Midway secondary school vifaa vya kupiga kura mpaka naondoka kituoni mida ya saa tatu asubuhi vifaa vya kupigia kura vilikuwa havijafika kabisa. Tatizo ni kwamba vifaa vilivyopokelewa ni vya Gerezani badala ya Kinyerezi!
 
Habari zenu wakuu. Nipo mbezi mwisho kama kijana nilijiandikisha sasa naitumia vyema haki yangu. Vijana ni wengi nina hakika cdm kuibuka kidedea.
 
wadau naomba kujua kwa mwenye data anipe idadi ya vijiji, mitaa na vitongoji vyote tanzania
 
Nipo kituocha kimandolu shuleni. Turn up ni kubwa sijapata ona. Kama usipofanyika utaratibu mwingine, kuna hatari ya watu kutopiga kura leo. Sina uhakika kama hawa watu wote wanawezapoga kura ndani ya muda uliopangwa.
 
Uchaguzi huu umekua na baadhi ya Changamoto. Kinondoni wino umekosekana. Mtu anapiga kura na kuondoka hivo kuna uwezekano watu kupiga kura mara mbili. Msimamizi wa Uchaguzi amewapa kazi mawakala kuhakikisha mtu harudii. Je wakala kazi yake ni kuhakikisha mtu harudii kupiga kura au kuhakikisha kura haziibiwi?

Changamoto namba mbili ni majina. Majina yamefifia, huwezi kuliona jina kirahisi. Hii imekua changamoto kwani watu wakikosa majina wanaondoka.
attachment.php

Watu wakijitahidi kutafuta majina yao
attachment.php

Hapa ni kituo cha kijitonyama. Mia
 

Attachments

  • mtaa.jpg
    mtaa.jpg
    51.8 KB · Views: 1,233
  • mtaa2.jpg
    mtaa2.jpg
    63.6 KB · Views: 41,882
Hivi huyu mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala hapa Shinyanga anasubiri nini ofisini!?.Mpaka sasa saa nne na dkk kibao zoezi halijaanza la upigaji kura wilayani hapa,kisa upinzani umetawala.
 
Mabendela na mdundiko havipigi kura! Labda wamejipanga kivingine. Binafsi ningefikiria kampeni nzuri kwenye serikali za mitaa ingekuwa nyumba kwa nyumba kwa mgombea kujitambulisha kuliko hizi za makelele na helkopta!
Sikuona chopa, na mkuu kama hao vijana walio hamasika watapiga kura basi twafwa!
 
Wakuu karibuni hapa tujulishane kinachoendelea katika eneo lako. Nitarudi tena...
 
Uchaguzi wa kijiji cha Kagunga, Kigoma Kaskazini umefutwa hadi siku nyingine baada ya mtendaji wa kata kusema ACT imefutwa katika uchaguzi huo. Hata hivyo msimamizi mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza.

Wagombea wa vijiji 2 wa chama cha ACT walitumia anuani ya Shule kama anuani yao. Mtendaji kawaeungua. Wananchi wamemgoma. Uchaguzi umeahirishwa
.

Kijiji cha Kagunga na Zashe kata ya Kagunga Jimbo la Kigoma Kaskazini
 
Back
Top Bottom