Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Unazungumzia Arusha ipi?

Hebu eleza Arusha unayoifaham wewe ambayo CCM walikuwapo jana ukiacha wale wafiwa wachache waliokuwa wamejazana kwenye fusso na hiece pale fillips karibu na wauza fenicha huku wamevaa mavazi ya kijani wakijiandaa kwenda msibani!?
 
Siasa za upinzani zinanishangaza sana kiukweli. Ukiwa unashinda hapa Jf nakusoma yanayoendelea juu ya kuchukiwa CCM utadhani uchaguzi ukiitishwa kesho hakuna tena CCM. Lakini ukipita huko mtaani watanzania hawana wanachojua zaidi ya CCM. Nimepita sehemu majuzi nikiwa tanga mjini watu/wanawake ndio wanajadiliana wanasema nasikia kuna chama kipya chaitwa UKAWA kimeunganisha CUF na CDM. Sasa huyu akienda kwenye sanduku la kura asipoikuta UKAWA ataichagua nini kama si CCM?

Mkuu CHAMVIGA hapa Jf kila uchaguzi huwa hizi harakati za chadema na wafuasi wake zipo hivi hivi kila uchaguzi, subiri ikifika usiku wa leo watakuja na hadithi mpya, utasikia daftari la wapiga kura halijaboreshwa, utasikia kura zimeibiwa, yaani zitakuja sababu hapa kama elfu 10,
Ajabu kuwa hii CCM ndio hiyo hiyo miaka yote na mbinu zao za ushindi ni zile zile, kifupi upinzani hauna mikakati ya maana kushinda, nategemea leo usiku upinzani utarudia Yale Yale ya miaka yote kulalamika bila kupata suluhu
 
Last edited by a moderator:
Nipo hapa Mbeya, kada wa chama tawala. Hata hivyo pita pita ya ngu mitaani hadi kule Rungwe nimejionea mwenyewe hali ilivyo tete kwa CCM.

Ni kama CHADEMA wao wamejitayarisha vizuri, na wapo kila mahala. Huu si oungo ,maana wameteka vijana wengi na bendera hasa Ile pana ziko kila mahala.

Jana niliona magari kadhaa ya matangazo na uhamasishaji ya CHADEMA, lakini sikubahatika kuona hata moja la CCM.

Nimefika Kiwira ndo balaa! Mchana vijana walifunga barabara kwa mdundiko uliokuwa ukiongozwa na gari ya matangazo ya CDM!

CCM najionea huruma lakini tusubiri tu.
 
Kata ya ifakara kuna vitongoji 33, hali c nzuri kwa ccm...chadema inashinda vyote
 
Habari za asubuhi wandugu. Mbunge wa CCM Mtwara mjini Murji jana kagawa elfu ishirini ishirini kwa vijana wa mtaa wa kizota hapa Mtwara na kina mama na wazee kuambulia kofia, tisheti na elfu tano tano. Hayo yamefanyika wakati mbunge huyo alipokuwa akifunga kampeni za CCM mkoani hapa. Kazi kweli kweli
 
Mwakyembe alikimbia jana!
Ccm Mbeya ulishajifia kitambo tu.
 
Mnakesha kama manesi wa zamu,nye kweli buku 7,hamwezi kuishi bila lumumba

Wewe unafanya nini kama sio kukesha wao wamecomment saa 12 alfajiri kama wewe ulivocomment saa 12. Huo ndio ujinga wa mwisho dunian vijana mumeletewa munaongea hata hamujielewi.
 
aMini usiamini, mpaka sasa ni sa 2:33 hakuna kituo hata kimoja kimeshafunguliwa. Tumefika kituoni zaidi ya mara 3 hakuna majina, wasimamizi bali mawakala ndo wamefika. tumejaribu kupiga simu vituo kadhaa bado hari iko hivyo tu. Miaka 53 ua uhuru oyeee!
 
kuna gamba mmoja kanipigia simu asubuhi hii akiniambia tusiiangushe ccm,lakini nikamkumbusha suala la Esrow kwa nini mwenye kiti wao hataki kulitolea maamuzi,akajifanya na yeye analaumu ukimya wa mwenyekiti wao, hivyo nikamuambia kama mwenye kiti wa ccm hana uchungu na mali ya umma nani mwanachama wa ccm atakuwa na uchungu?nikamshauri la msingi ni kuwanyima kura wote wanaogombea kwa tiketi ya ccm
 
Nakunywa viroba nikichelea matokeo, hali si nzuri chama changu.
Na tetesi ninazozipata hata viongozi chmani hawako vizuri.

Ndugu mwache huyo ni mtu asiyejitambua kabisa. Anaendeshwa na tumbo hivyo tumbo linaufunika ufahamu wake.
 
sisi huku Tabora mpaka sasa ni zaidi ya saa 2 unusu hakuna majina, wasimamizi wala chochote. hii ndo Tanzania
 
Nipo safarini muda huu kutoka Hometown Lushoto naelekea pande za Tanga mjini nimepita soni,mombo,korogwe asubuhi hii watu wamejaa stendi wanapiga dili za kusongesha maisha yao wala hawana habari na kitu inayoitwa uchaguzi na hawahawa ndio huwa wanakuwaga kipembelembele kwenye kuiponda CCM lakini hawanaga tabia ya kupiga kura je CCM mtaitingisha lini nyie wapinzani?

Watanzania wamekoseshwa elimu na hilo ndio mtaji mkubwa wa chama tawala.

Itabidi mfikirie upya uendeshaji wa siasa zenu otherwise mtapiga sana kelele.
 
Back
Top Bottom