Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Hii nchi kwa senema tumetia fora..Tunawazidi hata waigizaji maarufu duniani Wahindi..lakini bora wao wanaliingizia \taifa pato kupitia uigaizaji wao.Sisi ni magizo mpaka kwenye vyombo vya maamuzi.
Usikatishe tamaa wapambanaji/ wafuatiliaji wa mambo...kama umeona habari hiyo haifai kwako ipotezee kuliko kutoa comments za kukata tamaa!
Mhimili wako wa tatu umeniacha hoi, lol.
Wanabodi,
Kama kawaida wananchi kama mimi, tupatapo nafasi huwa tunajituma mpaka mjengoni ili kuisikia live kwa naked eyes baadhi ya mijadala muhimu. Ndivyo ilivyokuwa kwa jioni ya leo, nimejihimu ili nisikie mjadala wa taarifa mbili za serikali ikirindima.
Saa 11:00 akaingia Naibu Spika, Mheshimiwa Sana, Mama Anna Makinda.
Aliposimama na kunza kuongea, kwanza nilinote, anaongea akiwa na pressure, huku anajitahidi sana kubana pumzi, kama vile anataka kutangaza taarifa muhimu, ningekuwa siko mjengoni, ningeweza kudhani labda kuna taarifa ya msiba!.
Kumbe, alikuwa anatangaza Kikao cha Bunge Cha Jioni Hii, kilichokuwa kijadili utendaji usioridhisha wa TICTS na RITES, kimeahirishwa ghafla kufuatia taarifa hizo zote mbili kutokuwa tayari!.
Hivi jamani, hii ni serikali inalichezea bunge na kulifanyia mzaha, au ni Bunge lenyewe haliko serious enough hivyo serikali kulifanya bunge ni shamba la bibi!?.
ana vituko huyu mbaba,kamtambulisha mgeni wa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,Mr Tanzania wa 2001, eti kwa vile ni bodybuilder, Sitta akasema (kwa utani lakini) eti haishirii mazuri kwenye uchaguzi ujao!! ilipofika zamu ya miss Intercontinental, eti kadai jua linamzuia kumuona vizuri.....teh! teh!