Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3. Shahidi wa 13, Tumaini Swila kuendelea kutoa ushahidi Februari 15, 2022

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
790
2,881
Habari Wakuu,

Leo 14/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3. Mawakili wa Serikali waliomba ahirisho la kesi hadi leo Februari 14, 2022 kutokana na Shahidi Tumaini Swila kushindwa kufika Mahakamani siku ya Februari 10, 2022 kutokana na ugonjwa. Awali Februari 9,2022 aliomba ahirisho kwakuwa alikuwa hajisikii vizuri.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3: Shahidi wa 13, Tumaini Swila ashindwa kufika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2022

Baki nami.

Updates:

Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 Kamili Asubuhi

Kesi Namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili

 • Pius Hilla
 • Abdallah Chavula
 • Jenitreza Kitali
 • Nassoro Katuga
 • Esther Martin
 • Ignasi Mwinuka Mawakili Wa Serikali Waandamizi na
 • Wakili Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili

 • John Malya
 • Faraji Mangula
 • Nashon Nkungu
 • Fredrick Kihwelo
 • Livino Haule
 • Edward Heche
 • Sisty Aloyce
 • Seleman Matauka
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo shahidi namba 13 ameweza Kufika Kwa ajili ya Kuendelea Kutoa Ushahidi Wake ambapo Upande Wa Utetezi Walikuwa wanahoji Maswali ya Dodoso. Tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari Kuendelea

Inspector Tumaini Sosthenes Swila anapanda Kizimbani na Kaunda Suti ya Kijivu kisha anasimama..

Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa kabla Shauri halijahairishwa ulikuwa Chini ya Kiapo na leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nakumbuka Nilipo Ishia naomba Nipewe Kielelezo Namba P4, P5 (Risasi na Maganda Yaliyo tumika)

Kibatala: Shahidi Unakumbuka Mara ya Mwisho Zoezi lilisimama Kwa sababu Ulisema unataka Kupata huduma za Afya

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Na kweli ulitoa Kauli hiyo Ukiwa kwenye Kiapo

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Una Daktari Wako au Una Daktari Wako Mahususi

Shahidi: Kimya

Shahidi: Nahudumiwa na Madaktari tofauti

Kibatala: Unahudumiwa kwa Muda gani

Shahidi: Zaidi ya Miaka Miwili

Kibatala: Wanaitwa nani

Shahidi: Namkumbuka Mmoja anaitwa Mohammed

Kibatala: Mohammed nani

Shahidi: Simkumbuki

Kibatala: na Amekuhudumia kwa Muda gani huyo usiyemkumbuka

Shahidi: Miaka 2

Kibatala: Je unafahamu Niliandika Barua katika Hospitali ambayo Ulisema Kwamba wanakuhudumia

Shahidi: Sijapewa

Kibatala: Kwa hiyo ujui Kwamba Hospitali imesema ipo tayari Kusema wapo tayari Kuja Kutoa Ushahidi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni hali ya Kawaida kutomfahamu Mtu anayekuhudumia Miaka 2

Shahidi: kawaida

Kibatala: ulilazwa au ulipumzika nyumbani

Shahidi: Nilikuwa nimepumzika Nyumbani

Kibatala: Nyumbani kulikuwa na Daktari anayekuhudumia

Shahidi: Hapana

Kibatala: Tukoke hapo Nitarudi baadae

Kibatala: Unakumbuka Nilikuuliza Kwenye Viashiria Vya Ufadhili wa Ugaidi

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Ni sahihi Tulikomea eneo la Fedha

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Shahidi Tulikubaliana Kwamba Mshtakiwa wa kwanza, Wapili na watatu Walitumia pesa zao Kuja Morogoro

Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Nauli ya Mohammed Ling'wenya kuja Morogoro ilitolewa na Baba Yake

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Hukupeleleza hilo eneo

Shahidi: Sikupeleleza

Kibatala: Uliona Siyo Muhimu

Shahidi: Ndiyo Siyo Muhimu

Kibatala: Je Kwa Ufahamu Wako Baba yake Mohammed Ling'wenya alishawahi Kuhojiwa Ofisi ya RCO Mtwara

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Jeshi la Polisi Kila Mtu anajifanyia kazi yake au Mnafanya Kwa Pamoja

Shahidi: Tunafanya Kazi kwa Pamoja

Kibatala: Je Uliwa Kufahamu Kwamba DCI akimuelekeza Kingai Kumuhoji Baba Yake Mohammed Ling'wenya kupitia RCO Mtwara

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Source Zako ni Maelezo Ya Denis Urio, Inspector Ndowo Kutoka Cyber Forensic na Washtakiwa Wenyewe, Je ni sahihi

Shahidi: Ni Maeneo Mawili siyo Matatu

Kibatala: yataje

Shahidi: Kutoka Kwa Denis Urio na Taarifa Iliyo andaliwa kutoka Maabara

Kibatala: Kwa hiyo Taarifa Ya Maelezo ya Watuhumiwa Kuhusu Pesa walizotumiwa siyo Sehemu ya Eneo Muhimu

Shahidi: Ni Eneo Muhimu

Kibatala: Kwa hiyo NI Eneo la Tatu

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Tukianza na Denis Urio, Fedha ambazo anasema aliwapatia Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya aliwapatia kwa Matumizi yapi

Shahidi: Kwa Lengo la Kukutana na Freeman Mbowe

Kibatala: Ni sawa sawa na Kusema Aliwapatia Fedha hizo kwa Matumizi ya Nauli

Shahidi: Ni sawasawa

Kibatala: Kwa hiyo Wakili wa Serikali Pius Hilla alipo pinga Kwamba neno nauli Je alipatia au alikosea

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Tunapinga hilo swali, Sisi tunapinga alipokuwa ana refer Kuna zile pesa zilikuwa za Nauli

Kibatala: Mheshimiwa Jaji wacha Niendelee eneo lingine, ila Mtu akisimama awe na Kitu cha Msingi

Kibatala: Shahidi Kwahiyo pesa hiyo Walipewa sababu ya nauli

Shahidi: Sahihi ya nauli na Matumizi Mengine

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Washitakiwa Wame Elezea pesa hiyo Katika Maelezo Yao

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Fedha hizo pia zime zungumzwa katika Maelezo ya Luten Denis Urio ambayo Uliandika Wewe

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unakumbuka Luteni Denis Urio alisema aliwapatia TSh ngapi

Shahidi: Ni TSh 195,000 na Kisha TSh 199,000

Kibatala: TSh 195,000 zinaonekana katika Maelezo Ya Washitakiwa Wote Ya Onyo?

Shahidi: Ndiyo zinaonekana

Kibatala: Katika Figure hiyo?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu hayo Kwa sababu Wewe Kama Mpelelezi Makini na Mzoefu Kwa sababu Ulitake Trouble ya Kusoma na kuelewa

Kibatala Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P4 na P 13

Kibatala: unafahamu Kwamba Adam Kasekwa alisema Kuwa Sehemu ya Fedha alizopewa alitumia Kununua Shati la Mauamaua ambalo alikuwa amelivaa Siku anahojiwa.

Shahidi: Nakumbuka Maneno Kwamba alinunua Shati lenye Maua Maua

Kibatala: Kwa Upelelezi Wako Wewe hilo Shati lenye Maua Maua linahusika Vipi na Ugaidi (Maana alitumia Fedha Kununua Shati lenye Maua Maua)

Shahidi: Ni Fedha ambazo zilitolewa na Freeman Mbowe Kwenda Kufanya Vitendo Vya Kigaidi

Kibatala: Kwa hiyo Shati ambalo alikuwa amelivaa lilikuwa ni sehemu ya Ugaidi

Shahidi: Kimyaa

Kibatala: Na Je Kipengele cha Yeye Kununua Shati Mli' rekodi Chenyewe au Hapana

Shahidi: Kilirekodiwa

Kibatala: Kwanini Sasa Unanikataza Kuuliza Kitu Kimoja kimoja

Shahidi: Ukiulizwa Kimoja Kimoja uwezi Kupata Ugaidi

Kibatala: Shika Maelezo ya Adam Kasekwa Kwanza, Katika Eneo hilo Kuna Matukio Kadhaa yalitokea, Tafuta Eneo la Luten Urio alitupa Nauli ya TSh 87,000 /=

Shahidi: Nimeona

Kibatala: Soma Kuanzia hapo tujue nauli ya Kwenda Moshi ni TSh ngapi

Shahidi: Tarehe 24 July 2020 Nilikutana na Mohammed Ling'wenya kasisitiza tuende Morogoro tukakutane Luteni Urio tuliondoka Siku hiyo hiyo na Kukutana na Luteni Denis Urio alituambia kuwa kuna Kazi ya Kulinda VIP kwa Freeman Mbowe na Kwamba Maelezo Zaidi tutayakuta huko huko, kila Mtu alipewa TSh 87,000

Kibatala: kwa hiyo Kila Mtu alipewa TSh 87,000 Ka Nauli

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na wewe Kama Mpelelezi uliona Kuna Kosa lolote

Shahidi: Hapana

Kibatala: Na wewe Ukaona hapo Kuna Mantiki Kama Mpelelezi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Jumla Walipewa TSh ngapi wote Wawili Kama Walipewa Kila Mmoja TSh 87,000

Shahidi: Walipewa TSh 174,000/=

Kibatala: Tafuta katika Maelezo hayo pesa Iliyo Bakia katika TSh 199,000 ambayo ni TSh 25,000 kama Utaona katika Maelezo Ya Adam Kasekwa

Shahidi: haijaelezwa humu

Kibatala: na wewe Kama Mpelelezi Ulifanyia Vipi Kuhusu hiyo Tsh 25,000,je Uliandikia Maelezo ya Nyongeza

Shahidi: Ya nani

Kibatala: Kwani hapa tunamuongelea nani

Shahidi: Adam Kasekwa

Kibatala: Je wewe Kama Mpelelezi Uliandika Maelezo ya Nyongeza au Kumtaka Mtu amuhoji

Shahidi: Hapakuwa na Umuhimu huo

Kibatala: Mwambie Sasa Mheshimiwa Jaji Tunaipata Wapi hiyo Tsh 25,000

Shahidi: Hutoiona

Kibatala: Uliwahi kufundishwa Kuwa Maelezo Ya Onyo ya Mshtakiwa Yanatakiwa yabebe kila Kipengele ya Fact inayounda shtaka

Shahidi: Sijafundishwa, Siyo lazima ibebe kila kitu

Kibatala: Na wewe hiyo Tsh 25,000 siyo Muhimu kwako

Shahidi: Siyo Muhimu

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Denis Urio anasema Kwamba aliwapa TSh 199,000 kama Nauli Kwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya, Je 199,000 ya Denis Urio Inafanana na TSh 174,000

Shahidi: Zinafanana, Ni sawa na kusema 45 na Mtu Mwingine akasema ni 90 gawa kwa 2

Kibatala: Swali ni kwamba 174,000 na 199,000 zinafanama Vipi

Shahidi: Nishasema zinafanama

Kibatala: Kwa Figure zinafanama

Shahidi: Nishasema zinafanama

Kibatala: Shika na Maelezo ya Mohammed Ling'wenya, Soma Pale Baada ya Mazungumzo Luteni Denis Urio alinipa..

Kibatala: Au anzia Baada ya Kufika tulikutana na Luteni Denis Urio Bar Moja eneo la Msamvu

Shahidi: Nimeona

Kibatala: Soma Mpaka Ufike TSh ngapi walipatiwa

Shahidi: Baada ya Kufika tulikutana na Luteni Denis Urio Bar Moja eneo la Msamvu Bar hiyo Sikumbuki, Baada ya Kufika Luteni Denis Urio alitueleza Kuna Kazi ya VIP kwa Freeman Mbowe, na Siku hiyo hiyo alitutaka tusafiri Siku hiyo hiyo

Baada ya Mazungumzo Luteni Denis Urio Alini uliza huko Mtwara kwenye Kibarua chako ulikuwa unalipwa TSh ngapi, nikasema Posho ya TSh 15,000 basi akasema Nikifika huko niombe Mshahara Wa TSh 800,000 alitupatia TSh 190,000 Fedha ambazo tulinunua Nguo ilituonekane nadhifu

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Fedha hizo walinunulia Nguo

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Luteni Denis Urio aliwapa TSh 190,000

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Yeye Denis Urio alisema Kwamba Alitumiwa TSh 199,000 na hiyo Tsh 199,000 aliwapa Mohammed Ling'wenya na Mwenzake Adam Kasekwa na Tsh 190,000 anayosema Mohammed Ling'wenya na walipatiwa na Denis Urio. Je hizo figure zote zinafanana au zinatofautiana

Shahidi: Zina fanana

Kibatala: Sawa Shahidi

Kibatala: Na Maelezo ya Kasekwa na Maelezo Ya Mohammed Ling'wenya kwenye Figure ambayo Mmoja anasema Jumla Walipewa TSh 174,000 na Mmoja anasema TSh 190,000 Je zinafanana au zinatofautiana

Shahidi: Zinafanana

Kibatala: 199,000 ukito TSh 190,000 zinabakia TSh ngapi,

Kibatala: Je Katika Maelezo ya Mohammed Ling'wenya tafuta TSh 9000 inafafanuliwa ilitumikaje

Shahidi: Haijafafanuliwa

Kibatala: Na wewe Kama Mpelelezi uliye bobea Wa Zaidi ya Miaka 20 na Ukateuliwa na DCI, Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa hiyo Tsh 9000 ulifanyiaje Kazi

Shahidi: Wote Wanakiri Kupokea Fedha kutoka kwa Denis Urio

Jaji: Sikiliza Swali vizuri Unaulizwa hiyo Tsh 9000 ulifanyiaje Kazi

Shahidi: Ndiyo nilikuwa naeleza, Wote Wanakiri Kupokea Pesa kutoka Kwa Luten Denis Urio

Kibatala: Kwahiyo hapo Ndiyo umefanyia kazi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nikiuliza kwa namna gani utarudia Maelezo ya awali

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Basi Mahakama Imesikia

Kibatala: Soma pale Baada ya Kupokea Pesa hizo kutoka Kwenye Maelezo ya Denis Urio

Shahidi: Niliwapatia TSh 195,000

Kibatala: Sasa soma Maelezo Ya Washitakiwa Wote Wawili Wanaizungumzia Wapi.. Katika Maelezo Ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya

Shahidi: Kimyaa

Kibatala: Nikisema kuwa hawajazungumzia Kuokoa Muda nitakuwa nimekosea

Shahidi: Hawajazungumzia

Kibatala: Je unakubali Kwamba Hakuna Sehemu waliyokiri Kupokea

Shahidi: Amezungumzia Denis Urio

Kibatala: Achana na Luteni Denis Urio, Nataka hiyo Refund kutoka Walipotoka Kuja Morogoro, Swali Je Washtakiwa Wali acknowledge? Simple and Clear

Shahidi: Hawajazungumzia

Kibatala: na hiyo hali wewe Kama Mpelelezi Uliona ni Hali ya Kawaida tuh

Shahidi: Siyo Mimi niliyeandika Maelezo

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi

Shahidi: Ni hali ya Kawaida

Kibatala: Kwa hiyo hukuhangaika Kutafuta fact Ziada

Shahidi: Nilichukua Jitihada za Kutafuta Fact Ziada

Kibatala: Kwakuwa ni Hali ya Kawaida hukufanyia kazi

Shahidi: Nilifanyia kazi

Kibatala: Haya Ndiyo Utuambie Kuwa Ulifanyia Kazi vipi

Shahidi: Maelezo ya Denis Urio yalikuwa ya Uhakika

Kibatala: Na Maelezo ya Washitakiwa

Shahidi: Na yenyewe yalikuwa ya Uhakika

Kibatala: lini Ulianza Kuona au Kukufikia kati ya Maelezo ya Denis Urio au Watuhumiwa

Shahidi: Maelezo ya Washitakiwa

Kibatala: Wakati una Muhoji Denis Urio Ukiwa na Faida ya Maelezo ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Siku Nne Kabla

Shahidi: Nilikuwa sijayasoma bado

Kibatala: Na Uliyosoma lini sasa Maelezo ya Onyo ya washitakiwa

Kibatala: Baada ya Kuandika Maelezo ya Luten Denis Urio, Ulifanya zoezi la Kulinganisha

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ukaona Kila Kitu Kipo Sawa

Shahidi: Kimya

Kibatala: Sawasawa, Haya Denis Urio anasema Kwamba alitumiwa TSh 500,000 akatoa 300,000 akawapa Bwire na Lijenje na Baadae Waka patikana Vijana wawili akawapa akatoa Tsh 195,000 akawapa Jumla ni TSh ngapi

Shahidi: Jumla ni TSh 495,000

Kibatala: na Je 500,000 Ukitoa TSh 495,0000 inabakia TSh ngapi

Shahidi: Elfu 5

Kibatala: Ilienda Wapi

Shahidi: Ni Gharama za Mtandao

Kibatala: Hiyo Gharama za Mtandao ulitoa Katika Maelezo Ya Denis Urio

Shahidi: Kimya

Kibatala: Kuna Mahala Popote Katika Maelezo Ya Denis Urio ambayo umeandika wewe, Kuna Mahala Popote ameielezea

Shahidi: Hajaielezea

Kibatala: Uliambiwa Kuwa Denis Urio alifafanua hiyo Tsh 5000 hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je hata Wakili Mwenzetu Gladys Fimbari aliwahi Kuzungumzia hapa Mahakamani hii TSh 5000

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je Upo Makini na hii kesi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kama Kuna Gharama Za TSh 5000 kama zimekatwa na Mtandao zilitakiwa tuzione katika Taarifa ya Mtandao

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ndiyo Maana Nikamuuliza Je wewe ni Mpelelezi Makini

Shahidi: Ndiyo Mpelelezi Makini

Kibatala: Wa hadhi ya Kesi ya Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa Ushahidi Wako na Mashahidi Wengine Wanaojenga Kesi, Baada ya Kufika Moshi Mshitakiwa Wa Pili na Watatu walikuwa Wanapita Maeneo ambayo Sabaya anapenda Frequently Kuyatembelea, Ndiyo Ulivyo sema

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: katika ile 699 000 ambayo Mnasema Mbowe alitumia Kufadhili Ugaidi, Ni TSh Ngapi Adam Kasekwa alitumia Kumtafuta Sabaya

Shahidi: Kwa Mujibu Wa Upelelezi Wangu Mbali ya TSh 699 000 Kuna Pesa zingine alikuwa anawapatia

Kibatala: Fedha hizo Zipo Katika Hati ya Mashitaka

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Kwa hiyo Fedha ambazo hazipo Katika Hati ya Mashtaka unaona zinatusaidia sisi

Shahidi: aaaahhh Zinasaidia

Kibatala: Weeeee Kweli Enheeeee

Shahidi: Anainama Chini

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kuna Mahala unazungumzwa TSh 80,000 Mbayo Khalfani Bwire wakibafilishana Mikono na Freeman Mbowe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: TSh ngapi

Shahidi: Ni TSh 80,000

Kibatala: Hiyo Tsh 80,000 Kuiona Katika Shughuli zako za Upelelezi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Uliona Wapi

Shahidi: Katika Taarifa Uchunguzi Wa Kisayansi

Kibatala: Kwani wao wanahusika na Kutunza Mihamala ya Fedha ya simu

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe Kielelezo namba P 15,16,17,18,19 Mpaka 20

Shahidi: Ni sahihi Kwamba Taarifa iliombwa Chini ya Ofisi Yako hata Kama ni DCI

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Nakuonyesha Kielelezo Cha Barua namba P16 ya + 01 July 2020 Kutoka Forensic Beaural, Je unaitambua

Shahidi: Ndiyo Naitambua

Kibatala: Uliomba Taarifa za Lini hadi lini

Shahidi: 01 June 2020 - 31 July 2020

Kibatala: Barua Ilisainiwa kwa niaba ya nani

Shahidi: Kamishina Wa Polisi Wa Uchunguzi wa Kisayansi

Kibatala: anaitwa nani

Shahidi NAFTALI J MANTAMBA

Kibatala: Unamfahamu

Shahidi: Hapana Simfahamu

Kibatala: Wewe Kuto Mfahamu huyo ni Jambo la kawaida

Shahidi: Ni Jambo la Kawaida

Kibatala: Kwani Taarifa ya Uchunguzi Iliombwa kwa nani

Shahidi: Na DCI

Kibatala: ambaye DCI alimpa nani Mamlaka ya Upelelezi

Shahidi: Mimi

Kibatala: Kwa hiyo ni sahihi Kutomjua huyo

Shahidi: Ndiyo, Kuwajibika na hilo

Kibatala: umeona hizo Tarehe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Hizo Tarehe Mliwapa au Walijibunia wao

Shahidi: Tuliwapa

Kibatala: Kwa kupitia Barua ya Tarehe 13 August 2020 Kumbukumbu CID/HQ/KUM/C. 8/VOL VIII/171

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Barua Ilikuwa ya Muhimu au Siyo Muhimu

Shahidi: Ilikuwa Muhimu

Kibatala Katika Ushahidi Wako Umeitoa Barua hii kama Ushahidi Wako Muhimu

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: Ulitoa Mahakamani Sababu Ya Kwanini Hukutoa Mahakamani

Shahidi: Sikutoa Sababu

Kibatala: Uliongozwa Kuitambua hapa Mahakamani

Shahidi: Sikuongozwa hapa Mahakamani

Kibatala: Kwahiyo Barua hii Ndiyo ilipelekea Simu 8

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Ulimwambia pia Mheshimiwa Jaji kuwa Hakuna Simu hata Moja ya Mbowe Katika Simu Mlizokamata

Shahidi: Sikueleza

Kibatala: Bado tupo eneo la Fedha bado sijahama, lakini ilituzungumzie Fedha lazima Twende Maeneo Mengi

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Simu ambayo ilichukuliwa Kwa Mohammed Ling'wenya, Nilisikia Ukisema Kwa Mujibu Wa Seizure Certificate ya Mohammed Ling'wenya haikuwa na IMEI namba

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Na Ukatoa Ushahidi Namna ambavyo Ulipata IMEI namba

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulifanya Nini Tena Ikumbushe Mahakama

Shahidi: #*06# OK

Kibatala: Ukapata IMEI namba

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Hiyo IMEI namba Uliyopata Ulimwambia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Mhe Jaji ni Manufacturer Directives IMEI namba Ikifutika ndiyo Ufanye hivyo

Shahidi: sikumueleza

Kibatala: Je Ulimwambia Mhe Jaji Kwamba Manufacturer au Agent Wa TECNO ndiyo Uliye Kwenda Kwake na akakupa Ushauri Wa Kitaalamu

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba TECHNO Wana Mawakala Wake Tanzania Wanaofanya Kazi hizo

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba ukijifunza wapi namna ya Kutafuta IMEI

Shahidi: Sikueleza

Kibatala: Hiyo IMEI namba ndiyi Uliweka Katika Barua ya Kwenda Ofisi Ya Uchunguzi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa garbage in and Garbage Out

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo Wao wamenukuu IMEI namba ambayo wewe Ndiyo Ulipata

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Report ya Inspector Ndowo Wewe Uliona?

Shahidi: Niliona

Kibatala: Umemwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa hiyo IMEI namba, Kwamba Riport Uliyopata Ulilinganisha NA IMEI namba ya Mchunguzi Ukaona zinafanana

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Maana ya authentication

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Simu zinaweza Kuingiliwa

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba IMEI namba ni DNA ya Simu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Mwenye Simu Mwenyewe amezungumzia Lolote Kuhusu IMEI namba ya Simu yake

Shahidi: Naomba Maelezo nijikumbushe

Shahidi: hakueleza

Kibatala: Tafuta kwanza Katika Maelezo Ya Mohammed Ling'wenya Kuna Mahala Popote ametaja Kuwa SIMU zake zote Mbili ametaja ICCID

Shahidi: Hakutaja

Kibatala: Na Kurudisha Kwenye Barua Ya Kutoka Polisi kwenda Airtel, Soma namba zote Tatu zilizoombewa Taarifa Airtel

Shahidi: 0784779944, 0782 237913 na 0787 555200

Kibatala: Nenda Katika Taarifa Ya Gladys Fimbari, Je alitoa Namba zinazo one kana Katika Mihamala alitoa Taarifa za Mihamala Ya Simu Ngapi

Shahidi: Namba Mbili za 0784779944 na 0787 555200

Kibatala: na Hapo unasoma Katika Kielelezo namba P 15

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unakubaliana na Mimi Gladys Fimbari aliombwa Miamala ya Namba 3 ila Yeye Katika Barua yake Miamala Ya Simu 0782 237913 imeachwa

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu Record ya Miamala ya Gladys Fimbari Kutoka Airtel Imetokana na Barua ya Polisi Kwenda Airtel

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nenda Katika Taarifa Ya Mihamala Kielelezo namba P 20, Mhamala Wa Mwisho kabisa wa Tarehe 31 July 2020

Shahidi: Nimeona

Kibatala: Angalia namba Iliyotuma fedha

Shahidi: 0784779944

Kibatala: Namba iliyotumiwa 0782 237913

Kibatala: Unakubaliana na Mimi namba" 0" inamiss

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Katika Barua yenu ya Kwenda Airtel, Je namba sifuri ilikwepo au Haikuwepo

Shahidi: ilikuwepo

Kibatala: Wewe Ndiyo ulimuandika Maelezo Gladys Fimbari

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Uliandika Sababu ya Kutofautiana hiyo Prefix ya "0"

Shahidi: Sikumuuliza, Kwa sababu...

Kibatala: SITAKI SABABU HAPA MIMI

Kibatala: Nenda Kwenye Barua, Ni sahihi Kwamba namba iliyotumiwa hapo Ndiyo namba ambayo ipo Kwenye Barua

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwanza imetumiwa TSh ngapi

Shahidi: 200,000

Kibatala: UNASOMA WAPI WEWE, KUWA MAKINI

Shahidi: Ni TSh 80,000

Kibatala: Je ni sahihi Kwamba namba iliyotumiwa TSh 80,000 ndiyo namba iliyokuwa Kwenye Barua Ya Polisi Kwenda Airtel

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Lakini hiyo namba katika Covering Latter ya Airtel hiyo namba Haipo

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je unafahamu Legal Implication ya suala hilo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Lakini Ulimuhoji Gladys Fimbari Tarehe 05 July 2021

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je Ulifanyia Kazi hiyo tofauti

Shahidi: Sikufanyia kazi

Kibatala: Ndiyo Maana Nilikuuliza Unafahamu Maana ya legal implication

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: angalia Muamala Wa Tarehe 20 July 2020, Ukitumwa kutoka namba 0780 900174 kwenda namba 0787 555200, Je Ulisoma Taarifa za Miamala Vizuri kama Mpelelezi

Shahidi: Nilisoma na kuzielewa

Kibatala: Na ni sahihi Kwamba Moja ya Source zako za Information Mpaka Kusema Mbowe alifadhili Ugaidi Ilikuwa ni baada ya Kusoma na Kuelewa Taarifa za Miamala

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ulifahamu, Kwamba hii namba ni ya Wallet

Shahidi: Hapana Nilizingatia Covering letter ya Kutoka Uchunguzi

Kibatala: Wewe Unapeleleza Faili, Kupitia Forensic Beaural, na Yeye Kwakuwa hakuwa na Utaalamu akaomba Kutoka Airtel, Na Ndiyo Mwanzo Nilikuuliza Kwamba Unafahamu Hizo Taarifa

Shahidi: Ndiyo Nilifanyia kazi

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi amesha Jibu hilo swali Akasema hafahamu Kuhusiana na hii namba, Kwa hiyo tunaona Swali linajirudia hapa

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Hakuna Swala la Kanuni hapo, Kwa sasa Kwa sababu ni Mapema, Wacha Niendelee, ila baadae nitawahoji Kwa Sheria ipi kwa Kanuni ipi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ilikiwa ni Maamuzi yako, Wala Siyo Sheria Wala Kanuni

Kibatala: Nishasema kuwa Kwa sasa naendelea ila wakiendelea hivyo Tutaomba Ruling sababu hili ni zoezi la Truth Findings

Kibatala: Wewe Binafsi kama Inspector Swila Ulisoma na Kuelewa au Ulisoma hukuelewa

Shahidi: Nilipitia lakini Sikuelewa

Kibatala: Kwa hiyo tuachane na hiyo Taarifa, Sababu hujaielewa

Shahidi: Anayeweza Kufafanua hiyo ni Mtu wa Airtel

Kibatala: Sawasawa Nimekuelewa

Kibatala: Haya Kuhusu KYC unazijua

Shahidi: Kwa kiasi Chake

Kibatala: lakini ulizo fanyia kazi KYC za Denis Urio na Mbowe, Mohammed Ling'wenya

Kibatala: Kwa hiyo ulizielewa au hukuzielewa

Shahidi: Nafahamu Vitu baadhi

Kibatala: Unafahamu Kwamba KYC inayo Purport namba ya Mbowe, Denis Urio na Mohamed Ling'wenya zote Zina namba ya NIDA

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba NIDA ndiyo Primary Source

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Wewe Kama Mpelelezi Ulipokea Taarifa ili Uchunguze na Kuthibitisha Kwamba kweli I alikuwa na Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Sikuwahi

Kibatala: Kwani nani alikuwa Mpelelezi Kati yako wewe na Airtel

Shahidi: Mimi pamoja na Wapelelezi Wengine

Kibatala: Kwa hiyo wewe hukufanya lolote la Kwenda NIDA Kuona Kama Kweli zilikuwa Taarifa zao

Shahidi: Si Kufanya

Kibatala: Je unafahamu Kwamba hiyo pesa iloyotumwa kwenda namba ya Tigo ilitumwa kutoka namba 0719933386

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Mliomba TIGO Taarifa Ya Namba hiyo

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu namba ya Faili ya Mbowe, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Khalfani Hassan Bwire ni CD /IR /2097 /2020

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Ndiyo Ulisema Wewe Ulifungua Faili hilo Tarehe 18 July 2020

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na wewe Ndiyo Uliandika Maelezo Ya Frank Kapala

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Pia Ulisema katika Ushahidi Wako Kuwa Ulifanyia Kazi Taarifa za Tigo

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na wewe Ulisema ni Mpelelezi Makini

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Haya Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Jalada Walilojibu Tigo ni lipi..?

Shahidi: ni CD/IR/ 2097/ 2021

Kibatala: tukumbushe Kuwa Jalada lako ulilofungua ni la Mwaka Gani?

Shahidi: Ni Mwaka 2020

Kibatala: Je Tigo Walijibu Jalada lako kwa Kunukuu Mwaka gani

Shahidi: Mwaka 2021

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulifanya Juhudi gani za Kiupelelezi Ku Reconcile Utofauti Wa Mwaka 2020 na Mwaka 2021

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: na Mhamala unaobebwa na Barua hiyo ni wa TSh 500,000 ambao unasemekana Kwamba Mbowe alimtumia Denis Urio

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unajua Author Wa hiyo Barua

Shahidi: Hapana

Kibatala: Angalia aliyeandika hiyo Barua pale Chini ni nani

Shahidi: Imeandikwa Mwanasheria ila Jina halija andikwa

Kibatala: na wewe Tarehe 08 July 2021 ulimuhoji Mtu anaitwa Kapala

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sasa Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulijuaje Kwamba Aliyeandika Barua ile ni Frank Kapala

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Nikisema Kwamba Ushahidi Ulikuwa wa Kupangwa kwa fact hizo Nakosea

Shahidi: Siyo Sahihi

Kibatala: Je unafahamu Kuhusu Mihamala ya Tigo ambayo Mnasema Kwamba ilikuwa Mihamala ya Freeman Mbowe

Shahidi: anafahamu Mtu Mwingine

Kibatala: Kwa hiyo Ukiacha Miamala Ya Tigo hii Hakuna Kitu Kingine Unachokifahamu

Shahidi: Kuhusu Miamala anafahamu Denis Urio

Kibatala: Bado tupo Kwenye pesa, Umetaja Mara Kadhaa Kuhusu Taarifa Ya Cyber Kama Moja ya Kitendea kazi chako

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Tutaona nini na nini

Shahidi: Taarifa za Mawasiliano na Usajili Wa Namba za Simu

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P 23 na P 26 Na P22 ya Covering letter

Kibatala: Sasa Shahidi Nakuonyesha Barua Kutoka Uchunguzi Wa Kisayansi Kielelezo namba P22

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Barua Imeelekezwa Kwa nani

Shahidi: Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai

Kibatala: Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai ambaye ndiyo Mlalamikaji

Shahidi: Inaenda Kwenye Ofisi

Kibatala: Kwani Imesema "Kurugenzi " au "Mkurugenzi "

Shahidi: Mkurugenzi

Kibatala: Soma namba ya Jalada iliyobeba Barua

Shahidi: Ni CD/IR/ 2097/2020

Kibatala: Na Barua Iliyo rejewa ni Kumbukumbu namba Ngapi

Shahidi: CID/HQ/C8/9/Vol viii/171/ ya 13 August 2020

Kibatala: Barua ambayo ujaitoa Mahakamani Kama Kielelezo

Shahidi: Sijaitoa Mahakamani

Shahidi: Mheshimiwa Jaji naomba niende chooni

Mahakama ipo Kimya kusubiri Shahidi arudi

Na Sasa Shahidi amerejea Kizimbani


Kibatala: Tunaweza Kuendelea Shahidi

Shahidi: Tuendelee

Kibatala: Je Barua ambayo Haipo Mahakamani Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Kwenda Ofisi ya Cyber Imeandikwa lini

Shahidi: Tarehe 13 July 2020

Kibatala: Na Majibu yamekuja lini

Shahidi: Tarehe 09 July 2021

Kibatala: Kama Kipindi Cha Mwaka sasa

Shahidi: Miezi 11

Kibatala: Walikwambia kwanini Kufanya Extraction tuh Kesi Kubwa kama hii Vielelezo Vinakaa Miezi 11

Shahidi: Walisema Kuna Vielelezo Vingi

Kibatala: Unafahamu Kwamba Tarehe hizo ndiyo zilikuwa za Vuguvugu za Maswala ya Katiba

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwenu Kesi hii ya Ugaidi Ilikuwa ni Priority au Mlianza hata Kuchunguza Maswala ya Mapenzi Kwanza

Shahidi: Nisha Jibu

Kibatala: Wakati Nyie Mnasubiri Kwa Speed Ya Kawaida Mlikuwa mnatambua Kuna Watu wapo Ndani

Shahidi: Tulikuwa tunatambua

Kibatala: Wakati kwa Ushahidi Wako Mwenyewe, Ulisema Kwamba Wakina Gabriel Mhina na Khalid Walikaa Mwaka Mzima, Je Mnafahamu Madhara Ya Kukaa Mwaka Mzima

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Madhara Waliyo Pata Washitakiwa Wa Kwanza, Wapili na Watatu Kama Vijana Kwa Kukaa Ndani Muda Mrefu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Maana ya Polisi Impunity

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ulifanyia Kazi Extraction Reports

Shahidi: Nilifanyia kazi Kwa Ufahamu Wangu

Kibatala: Unafahamu zilikuwa ngapi

Shahidi: Nne

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kuna Extraction Report Siku ambayo Covering Latter Imeandikwa

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Walifanya Extraction Tarehe 09 July 2021 Saa 11 na Dakika 29 Jioni

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Walikuwa Wanakimbizana na nini, hizo Siku Mbili za Mwisho

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Baada ya Kukimbiza Extraction Report kwa Siku Mbili ndiyo Baada ya Siku 12 Mbowe akakamatwa

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Na Unafahamu a baada ya Extraction Report kukamilika na Mbowe Kukamatwa ndiyo Elia Kaaya akaachiwa na Baadae akaja kuwa Shahidi Kwenye kesi hii

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Haya nipeleke hayo Maeneo ambayo yalokuingiza Kufikiria Kwamba Freeman Mbowe alifadhili Ugaidi

Shahidi: Ukurasa wa Nne, Bullet ya Pili

Kibatala: Unasema nini

Shahidi: Kwa Mujibu wa Report ya Tigo ya Tarehe 20 July 2020, Namba Ya Simu 0719933386 ilituma namba Kwemda 0787 555200

Kibatala: Ni sahihi Kwamba hapo amekopi Kutoka Tigo

Shahidi: Siyo Sahihi

Kibatala: Tuambie Sasa Inspector Ndowo alifanya nini

Shahidi: Hapo bullet ya Chini inaposema Kwamba Kwa Mujibu Wa Report kutoka Tigo...

Kibatala: Nitafutie Mahala ambapo Inspector Ndowo Ali Originate Uchunguzi kutoka kwake, Zaidi ya Taarifa Ya Tigo (Mbali na Primary Source kutoka Tigo)

Shahidi: Alifanyia Kazi Taarifa Kutoka Tigo akaanda Taarifa hii

Kibatala: Hiyo kazi ambayo alifanya yeye Inspector Ndowo nauona katika Bullet ipi

Shahidi: Ndiyo ungemuuliza yeye Inspector Ndowo

Kibatala: Kwa Mdomo tena

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Report inatakiwa Kuiongelea Yenyewe

Shahidi: Ndiyo Ungemuuliza Yeye Sasa

Kibatala: Nisionekane na Kuharass, Je Unakubaliana na Mimi Taarifa inayo Tajwa hapo ni ileile ya Tigo ambayo Kwenye Barua ya Tigo ni CD/IR 2097 /2021

Shahidi: Hapana ni CD /IR/ 2097 /2020

Kibatala: Kwani Barua Kutoka Tigo imeandika jalada gani

Shahidi: CD /IR 2097 /2021

Kibatala: Siyo Kuuliza tena hapo.

Kibatala: Haya bullet gani Nyingine inayo zungumzia Kuwa Mbowe akiwatumia pesa

Shahidi: Ya Pili Kutoka Mwisho, 0784779944 imesajiliwa kwa Majina Freeman Mbowe ilituma Pesa Kwemda namba 0782 237913 ilituma Kiasi cha TSh 80,000

Kibatala: Je unafahamu Unachosema hapo Hakipo katika Hati ya Mashitaka

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Sasa Lengo la Kuleta Mahakamani Kitu Hakipo katika Hati ya Mashtaka ni nini

Shahidi: Hizo ni fedha ambazo hazikuweza Kutolewa Maelezo na Denis Urio

Kibatala: Lengo la Kuleta pesa hizo hapa Mahakamani na nini, Zilikuwa ni Mahaba au Ufadhili wa Ugaidi

Kibatala: Ni sahihi Katika Maelezo Yako uliyo andika wewe Unaandika hivi, Vilevile Uchunguzi Wa Cyber Ulikuwa Unaonyesha Mshitakiwa Mbowe akiwatumia Pesa wenzake na Kutoa Maelekezo nini cha Kufanya

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Hiyo Taarifa Wewe Ulipata Wapi Kwamba Mbowe alikuwa anatuma pesa na Kutoa Maelekezo nini cha Kufanya

Shahidi: Kwenye report

Kibatala: Haya nitafutie Kwenye Riport Mahala inaposema Kwamba Mshtakiwa Freeman Mbowe alikuwa anatuma Pesa na Kuelekeza Wenzake nini cha Kufanya (Vitendo Vya Ugaidi)

Shahidi: anapekua Report

Shahidi: Kwenye Report Hakuna

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa katika Report Hakuna Mahala ambapo Mbowe anatoa Maelekezo nini cha Kufanyia Fedha hiyo

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Katika Report Hakuna Maelezo hayo

Kibatala: Infact Ukisoma hiyo Riport anaye Omba Pesa ni Denis Urio

Kibatala: pale Kwenye Wamekwambia Wanataka nini.? Na wa Umri gani (Katika Kielelezo G) page 3 Mpaka page ya 4

Shahidi: Nimeona,

Kibatala: Ni nani anayesema naomba Nitumie nauli kwa ajili ya Kuwa Mobilise nikutane nao Morogoro Kwa Mujibu wa Riport ya Inspector Ndowo

Shahidi: Imetumwa na Denis Leo Urio

Kibatala: Ni sahihi Meseji hiyo inaonyesha na Matumizi ya hiyo pesa

Shahidi: Ukisoma Moja Moja huwezi Kupata Maana halisi

Kibatala: Sijakubishia, Ila tunazumgumzia Kuhusu Report ambayo wewe ndiyo Umesema Kwamba Ni Source ya Conclusion Yako

Kibatala: Sasa Kwa Mujibu Wa Inspector Ndowo, Ni sahihi Kwamba Lengo lipo katika Meseji ni Kuwa Mobilise

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na Kwa Mujibu wa Riport hiyo nani Kasema "No Problem kaka ni Kwa namba Ipi na Kwa kiasi Kipi"

Shahidi: Ni Freeman Mbowe

Kibatala: Na Kwa Mujibu wa Report hiyo nani Kasema Usiwe unatumia namba yako Kaka

Shahidi: Denis Leo Urio

Kibatala: Katika Maelezo Uliyokuwa Unamuandika, Ulimuhoji Denis Urio kwanini Yeye Kama Mtu wa Kumtoa gaidi pangoni aje aonekane Ushahidi Wake badala yake ndiyo anamfucha gaidi pangoni

Shahidi: Ndiyo alieleza

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Maelezo Ya Luten Denis Urio

Kibatala: Haya Tafuta Mahala ambapo Luteni Denis Urio alifafanua katika Maelezo Yake kwanini anamwambia Mbowe atumie namba ya Wakala au Wasaidizi Wake

Shahidi: Wakati Wa Maongezi Yetu Afande DCI alifanya Mawasiliano, na Baada ya Muda Mfupi aliingia Afande Mwingine

DCI aliniambia ili tuweze Kukusanya Ushahidi Niendelee Kuwatafuta Watu hao, Ili kumweka Karibu

Kibatala: Nitafutie Mahala ambapo Denis Urio anasema alimwambia asitumie namba yake atumie namba ya Wakala au Wasaidizi Wake ilikumweka Karibu

Shahidi: Ili asiweze Kumtilia Mashaka

Kibatala: Hayo Maneno Yapo au hayapo, wewe Umesoma Kielelezo namba P23 Meseji inasema Usiwe unatumia Namba yako, Tumia namba ya Wakala au Wasaidizi Wako, Sasa nataka Sehemu Katika Maelezo ya Denis Urio sehemu ambayo amesema nilifanya hivi ili Ku gain Confidence

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Tunapinga hilo swali, Sababu limeshajibiwa

Kibatala: Naomba Mwenzangu unisomee Nione Kama limejibiwa

JAJI: ulikuwa Umeulizaje Mr. KIBATALA

Kibatala: Nataka Kwa Maelezo Ya Denis Urio Kwamba anitajie sehemu ambayo amesema Kwamba Ile Meseji ya Kumshauri Mbowe Kuwa Usitumie Namba yako, Tumia ya Wasaidizi Wako au Wakala, Je Katika Maelezo hayo Kuna sehemu ambayo amesema?

Shahidi: Maneno hayo kwenye Maelezo Hayapo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kutoa Hoja, Naomba uridhie tupate Break Kidogo Kama Ilivyo Utamaduni Wetu, Kisha turejee Saa 8 Kasorobo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji na airisha Kwa Muda Wa Dakika 45, tutarudi tena Saa 7 na Dakika 45

Jaji anatoka, saa 7:00


***************************

Jaji amerejea Mahakamani Muda huu 02:18

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani tena

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wa Jamhuri Quorum ipo Kama Awali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia kwa Upande wet Quorum ipo Kama Ilivyo kuwa awali na tupo tayari Kuendelea

Shahidi Karejea Kizimbani

Mwenyekiti Freeman Aikael Mbowe amenyoosha mkono wake wa kulia hapa

Freeman Mbowe: Mheshimiwa Jaji naomba kuleta Kwenye Mahakama yako kuwa tumekosa haki ya kula chakula mchana kwa Miezi 5, Wakati nyie Mna' break kwenda kula sisi hatupati chakula wala maji kwa miezi Yote 5

Pale mwanzo tuliambiwa kuwa kama chakula tuchukue Kutoka Jela, tutoke nacho Jela tuje nacho Mahakamani, tkitoka hapa tunakutana Magereza Wameshakula tunakwenda kulala na njaa siku zote.. Hawa vijana wanakonda kila Siku hata kusikiliza kesi ni geresha.. Ni hayo tu.

Jaji: sasa nyie Kibatala mnatoa uwakilishi gani hapa Mahakamani kama wateja wenu hawali miezi mitano?

Kibatala: sisi tulifkisha kwa Officer wa Magereza, Suluhu aliyotoa ndiyo hiyo Asubuhi Watoke na Chakula Kutoka Jela Kitu ambacho tulibishana na hatukufikia Muafaka kwa sababu haiwezekani.. Nafikiri hata Msajili Wa Mahakama analijua hilo, sutaki kumsemea.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Mujibu Wa Jambo lililo letwa naomba Tubreak Kidogo tuweze Kuishauri Vyema Mahakama.. Imekuwa ghafla sana..

Jaji: basi nawaita Mawakili Kuwakilisha Watu wote Ofisini Kwangu, Tuweze Kujadili

Jaji anatoka 02:27

Askari magereza wamemfuata Freeman Mbowe, anahitajika ofisini kwa Jaji katika kikao cha pamoja na mawakili wa pande zote (serikali na utetezi), Washtakiwa wengine watatu bado wamebakia kizimbani.

************
Jaji amerejea 03:56

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji upande wa Jamhuri Quorum yetu ipo Kama awali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi upande wetu Quorum ipo Kama awali

Jaji: Mshtakiwa Namba Nne aliibua Hoja ambayo tumekutana Mahakamani na Kuwatafuta Wa husika, Na tumemshirikisha yeye Mwenyewe Katika Mchakato Wa Kufikia Maamuzi, Kama una jambo la Kusema Mshtakiwa Wa Nne Karibu kabla ya Kusema Uamuzi.

Freeman Mbowe: Mheshimiwa Jaji Kwanza nashukuru Kwa kunisikiliza pamoja ni Nje ya Utaratibu, Siku washirikisha Mawakili Kutokana na Kutaka lishughulikiwe kwa Haraka Nashukuru sana..

Na Kilichoendelea kwa Mahakama Kuu nimeshirikishwa Kwa Hatua zote. Pamoja na Kwamba tuna Njaa ila Nguvu za Kuendelea Kusikiliza Kesi bado tunayo, Kwa kuwa bado Jambo litahusisha na Idara zingine linaweza lisiishe Leo, Kwa hiyo napenda tuendelee Na shauri Wakati tunasubiria Maamuzi

Jaji:Umeomba Radhi Mawakili Wako Mawakili wa Serikali Umewasahau

Freeman Mbowe: aaahh! Na wenyewe tunawaomba Radhi sana, Sasa tuendelee tu Mheshimiwa Jaji..

Freeman Mbowe anaketi kizimbani.

Kibatala: Shahidi Sasa tuendelee, Shahidi Utakumbuka tulipo Ishia, Nakuonyesha Kielelezo namba P 13 Maelezo Ya Inspector Ndowo na Wakati huo Ulikuwa na Maelezo Ya Luten Denis Urio

Kibatala: Ni sahihi Shahidi katika Matokeo Ya Uchunguzi, Ni sahihi Kwamba Kwamba Meseji Unazosema Ulieleza ni Kielelezo namba G

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na Katika Upelelezi Wako Uligundua hilo Kielelezo namba G ni simu ya Luten Denis Urio

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Utakubaliana na Mimi Kwamba Ukisoma Riport ya Uchunguzi, achosema Luteni Denis Urio, Kwamba Namba ya Simu ya Kielelezo namba G ni 0719933386 imehifadhiwa katika Kielelezo hiki kwa Jina Free

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na ni sahihi Kwamba hii namba ya 0754612518 ndiyi Simu Card ambayo Tarehe 11 August 2020 ndiyo Simu ambayo ulimpatia Denis Urio Kwa Maelezo kuwa ataiwasilisha baadae

Shahidi: Ndiyo Simu Card hii

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Sim Card hii Hujawahi Kuitambua hapa Mahakamani

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Kwa Vyovyote Vile hata Kama tuki assume wewe ndiye Uliyemrudishia Sim Card hiyo, lakini Hakuna Handover ya Simu Tatu (Hati za Makabidhiano ya Simu 3) ikiwemo hiyo Samsung Duo yenye Sim Card hiyo

Shahidi: Si Kutoa Hati Ya Makabidhiano

Kibatala: Na shahidi Kwakuwa Una Kielelezo namba D4 Maelezo Ya Luten Denis Urio, Je Kuna Mahala Popote anazungumzia Namba ya Simu Zifuatazo 1130138344.?

Shahidi: Haja zungumzia

Kibatala: Ni sahihi pia Katika Kielelezo Namba D4 Hakuna Mahala Popote Ambapo Luten Denis Urio anazungumzia chochote Kuhusu 729414989

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Katika Kielelezo namba P 23 Riport ya Uchunguzi Ya Inspector Ndowo Hakuna Mahala anapo zungumzia Kuhusu hizo namba

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Zile Meseji uliokuwa unasoma Mawasiliano Kuhusu Fedha, Je unafahamu Kuhusu Extraction Report Kielelezo P26, Kuhusu Fedha, Je namba hizo 1130138344 na 729414989 zilipo Sababisha Kutafuta Extraction Report Kuhusu Mih+amala ya fedha

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Kuna chochote ambacho ulifafanua Kwa Mheshimiwa Jaji Ulichogundua Kutoka Kwenye hizo namba

Shahidi: Siku fafanua

Kibatala: Naomba turudishe Kielelezo Namba P 23 hiyo Report, Kwa Ruhusa Ya Mahakama Nakuonyesha Kielelezo namba P26 ambayo NI Extraction Report

Kibatala: Zile namba ambazo Unasema Uligundua Kuwa Zina Meseji Ambayo zilikuwa za Freeman Mbowe zikiwa zinajadili Matendo ya Kigaidi.

Shahidi: Ndiyo nimeziona

Kibatala: Na hiyo Riport Ukisoma na Kuielewa

Shahidi: Nilisoma na Kuilewa Kwa Kadri ya Uwezo Wangu

Kibatala: Meseji zote hizo zimebebwa na namba ambazo umesema hukufafanua

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je unafahamu Implication za Kisheria

Shahidi: Kimya

Kibatala: Wewe Binafsi hjawahi Kuzichunguza Mahususi zinazoonekana Katika Extraction Report

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Hii Namba ya 0754612518 Ulishawahi Kuwaandikia Vodacom Kuweza Kupata KYC kuweza Kujua ilikuwa imesajiliwa kwa Jina la nani

Shahidi: Sikuwahi Kuandikia ila nilikuwa najua ni ya Luten Denis Urio

Kibatala: Na Ulijulia Wapi Shahidi, Je Denis Urio ametaja Katika Maelezo Yake Popote

Shahidi: Ndiyo ametaja

Kibatala: Wapi na Sehemu gani ametaja

Shahidi: Kwenye Particulars

Kibatala: Je ni sahihi Katika Maelezo Kuna sehemu Imeandikwa Kwa Herufi Kubwa "MAELEZO" halafu inafuatiwa na Maneno Jeshi la Wananchi

Shahidi: sahihi

Kibatala: Kwa hiyo Baada ya Neno MAELEZO huku ndani Hakuna Mahala Popote Luteni Denis Urio aja zungumzia lolote Kuhusu hii namba

Shahidi Upande Wa Maelezo haijatajwa

Kibatala: Ulipata nafasi ya Kufafanua Kwanini Ipo Juu lakini Haipo Kwenye Maelezo huku Ndani

Shahidi: Siku fafanua

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Kuna Mahala Popote Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Wewe una Utaalamu wa Mawasiliano ya Mtandao Wa Telegram

Shahidi: sikumueleza

Kibatala: Ulimfafanulia Mheshimiwa Jaji ya Kwamba Ulipata Wapi hiyo Knowledge au Information Kwamba Meseji ya Telegram zinabakia kwenye Simu

Shahidi: Sikumueleza

Kibatala: Nikiwa bado Kwenye simu, Twende Simu za Mshitakiwa Wa kwanza Khalfani Bwire, Ulishawahi Wahi Kufika Kituo cha Polisi Chang'ombe

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na Bila Shaka Ulishawahi Kufika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Kutoka Chang'ombe hata Kama Una Priveledge za Kipolisi inaweza Kuchukua Dakika ngapi

Shahidi: Dakika 10 Mpaka 15

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Simu za Bwire Zichukuliwa na Kingai Pamoja na Goodluck

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ilikuwa Muda wa Saa ngapi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ulipigiwa Simu Muda gani

Shahidi: Saa 2 Kamili za Usiku

Kibatala: Kwa hiyo tuseme Kuwa Ulipigiwa Simu Kujua Simu za Bwire Wanazo, Ilikuwa Saa ngapi

Shahidi: Saa 2 kwenda Saa 3

Kibatala: Toka ulipopigiwa Simu Kuwa Simu zipo, Je Ilikuwa Saa ngapi Mpaka Wanakuja Kukukabidhi

Shahidi: Ni Nusu Saa baadae

Kibatala: na tunakubaliana kuwa hizi Simu, Hapa Mahakamani hujaleta Makaratasi ya Makabidhiano

Shahidi: Ni sahihi Nilieleza Mahakama, Ila Sikutoa

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P1 na P 13

Kibatala: Shahidi Nakuonyesha Maelezo Ya Onyo ya Adam Kasekwa Kama Moja ya Chanzo chako Cha Uchunguzi, Soma Hapo Kwenye IMEI namba

Shahidi: 3547289120275

Kibatala: Naomba namba P 23

Kibatala: Nakuonyesha Report Iliyoandaliwa na Inspector Ndowo Simu aina ya ITEL kwenye IMEI Namba ya Pili ni Namba ipi

Shahidi: 353736289120273

Kibatala: Je Inafanana na Kwenye Maelezo?

Shahidi: Zinafanana

Kibatala: Kwa hiyo Katika Maelezo ya Onyo ya Adam Kasekwa inasomeka 353736289120273

Shahidi: Haipo Kwenye Maelezo Ya Kukiri

Kibatala: Kwenye Maelezo Ya Adam Kasekwa Hakuna 36? na 298 Je tofauti hiyo ulitoa ufafanuzi

Shahidi: Sikutoa Ufafanuzi

Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Namna katika IMEI namba Ukikosa namba Mbili Unaleta Utofauti

Shahidi: Kimyaaaaaaaa

Kibatala: Tafuta Katika Kielelezo namba P23 Je Kuna Mahala Popote Kuna Maneno yameandikwa PUK

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Ni simu card ipi ambayo Adam Kasekwa anai' verify kama PUK

Shahidi: Maneno PUK ambayo ametatumia Katika Maelezo ya Onyo hayapo Katika Report ya Inspector Ndowo

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa katika Upelelezi Wako Uligundua Kuwa Maneno PUK ndiyo Sawa na IC +CID namba

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Soma Maelezo ya Adam Kasekwa Namba zake za PUK

Shahidi: ni 892550509065499312

Kibatala: Soma Sasa Katika Report Ya Inspector Ndowo Simu D Yanaonekana Wapi

Shahidi: 892550509065499322

Kibatala: Ni sahihi huku Kuna 22 wakati Kule Kuna 12

Shahidi: Ndiyo ila ni hiyo hiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Kama ulitoa Ufafanuzi

Shahidi: Sikutoa Ufafanuzi

Kibatala: Na Kutoa Eneo la Simu nakupeleka katika Eneo Lingine, Katika Riport ya Silaha aina ya Luger A5340 ya Tarehe 15 November 2021. Je ni sahihi Kwamba Taarifa hiyo ina rejea Jalada la CID/IR /2097 /2020

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Lakini Ulifanya Upelelezi Kwa Makini kisha Ndipo Kesi hii ikafunguliwa

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je hii Report Iliyoandaliwa kuwa ni Moja wapo ambayo Ulifanyia kazi

Shahidi: Sahihi Kabisa

Kibatala: Soma Hapa ni Jalada namba ngapi

Shahidi: CD/IR/2097/2021

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Utofauti huo

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Hilo Jalada la CD /IR /2097 /2021 Uliwahi kulifungua

Shahidi: Mimi nilifungua la CD/ IR /2097 /2020

Kibatala: Ukiwa Mpelelezi Makini, Je Ulipo wasiliana na Wakamataji, Walikwambia Adam Kasekwa alikamatwa Saa ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Sasa Nikisema Walikamatwa Saa 7 Mchana utabisha

Shahidi: Nisha sema Kuwa Sikumbuki

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Kwa Maelezo Ya Adam Kasekwa alikamatwa Majira Ya Saa ngapi

Shahidi: Tarehe 05 August 2020 Muda wa Saa 5 Asubuhi Nikiwa Eneo la Rau Madukani, Glocery Nikiwa napata Kinywaji

Kibatala: Kwa hiyo alikamatwa Saa 5 Asubuhi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kati yako wewe na Adam Kasekwa nani anafahamu Muda Wa Kukamatwa

Shahidi: Mkamatwaji na Mkamataji

Kibatala: Wakamataji Washasema Saa 7 Mchana, Je Maelezo ya Mohammed Ling'wenya Ulifanyia kazi?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na Unafahamu Kwamba Adam Kasekwa Na Mohamed Ling'wenya Walikamatwa pamoja

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Kuwa Mohammed Ling'wenya anasema alikamatwa Rau Madukani Saa ngapi

Shahidi: Majira ya Saa 7 Mchana

Kibatala: Ni tofauti ya Masaa Mangapi Kwa Watu Unaosema Walikamatwa Pamoja

Shahidi: Masaa Mawili

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Ulifanyia Vipi kazi Kuhusu Utofauti Wa Muda

Shahidi: Nilifanyia Kazi, Ila Kila Mtu anaweza Kusema anachoona ni sawa

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Nakupeleka Eneo Lingine Kuhusu Sampuli za Maandishi Ambazo Unasema Ulichukua

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Unasema Ulichukua Sampuli za Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Ulichukua Sampuli ngapi Kwa Kila Mtu

Shahidi: Kwa Adam Kasekwa 8, Mohammed Ling'wenya 8 na Khalfani Bwire 8

Kibatala: Baada ya Kuzichukia Ukazipeleka Wapi

Shahidi: Maabara Ya Uchunguzi

Kibatala: Na Yakafanyiwa Uchunguzi na Mtu anaitwa Khamis Nankaa

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Wakati Unaongozwa na Mr Kidando, Ile Taarifa Ulifanyia kazi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Pamoja na Hukutoa ile Taarifa, Je Unafahamu Kwamba Nankaa anasema Kwamba Ulimpeleka Karatasi 9 ikiambatana na Barua Moja, Kwa hiyo anasema Kuwa Karatasi 9 na Barua Moja Jumla Barua 1 inakuwa 10 Wakati wewe Ulisema 8

Shahidi: Nilisema 8 ndiyo

Kibatala: Kwanza hiyo application Latter Ulitaja hapa Mahakamani

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Je Uliongozwa Kufafanua Mfanano wa Karatasi 9 na 8 ulizotaja

Shahidi: Siku fafanua

Kibatala: Unakumbuka Wakati nakuuliza Maswali Nilikuuliza Kuhusu Maswali ya Sayansi ya Uchukuaji Wa uandishi wa Habari

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Samahani hili Neno la Uandishi Wa Habari Sijui limetoka Wapi

Kibatala: Samahani Mr Chavula ni Uimi Uliteleleza

Kibatala: Unakumbuka Kwamba nilikwambia Ina shauriwa Kuwa Katika Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi, Unatakiwa Kuwa na Sampuli 15

Shahidi: Nilisema Siyo lazima

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Shahidi alizumgumzia Kuhusu Report Kwa Mambo aliyofanya, Shahidi Siyo Maker aulizwe yake aliyofanya, Wakili asiende Katika Details Sana Kwa Sababu Shahidi Siyo Maker wa hiyo Nyaraka

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote, Kwa Maneno ya Wakili Pius Hilla, Nakumbuka nilisimama hapa Mahakamani Kuwa Omba Pamoja na Kwamba hatuwezi Kuwapangia Ushahidi Wao nilishauri Kuwa Haipo Mahakamani, Waachane nao

Lakini Wao Wakasema Kuwa ni Ushahidi Wao, Walikuwa wana zungumzia Kuhusu Notebook ambayo miye Nikiwa naita Diary, Na haikuwa Mahakamani

Jaji: Notebook haikuwa tendered, Hoja yangu ni kwamba Wewe unafanya Rejea Katika Nyaraka ambayo Haipo Mahakamani

Kibatala: Kwa Heshima Mheshimiwa Jaji Wao wakati wanaongelea Kuhusu Kidaftari na Michoro Mpaka wake na Kituo cha Mafuta cha Morocco, Wao walileta Kwenye Ushahidi Kuonyesha Kwamba Mwandiko Wa Bwire upo katika Kidaftari. Mimi siwezi Kujua kitatokea nini, Namimi siwezi Kuliacha hilo

Jaji: Hoja hapa ni Kwamba Wewe Unapo +uliza Maswali una Rejea Katika Report hiyo ambayo haijawa tendered

Yaani Unatakiwa Kurejea Maswali yote lbila Kurejea hiyo Rrport

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Univumilie, hii Report Wao wameshaitumia hapa Majina kama Khamis Nimepata Wao Baada ya Wao Kulitaja Kutoka Katika hii Report

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji bora Kuweka Sawa, akichukuwa anarejea Kabisa Kwamba Khamis Nankaa anasema Kitu.... Wakili ajikite tu Kwa Kile ambacho Shahidi ajafanyia kazi

Jaji: Shida yangu Kubwa Mazungumzo Kuhusu hiyo Report ambayo Siku ya Mwisho Mimi Ndiyo naandika Hukumu Kulinganisha Ushahidi Wa Serikali Na Utetezi wakati hiyo Report Mimi sina

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba niishie hapa, Kesho tukija naomba uturejeshe alichosema Kuhusu report

Jaji: tusilale na Kiporo, Wewe Unakumbuka Nini?

Kibatala: Alisema Kuhusu Sampuli, Kwa Kumbukumbu zangu Sioni tatizo, Mimi sina Shida na Maamuzi Yako, Ila soon kama Ni sahihi Kufanya Supress Kama Wao Kitu Walileta wenyewe Nina right ya Kufanya Cross Examination..

Jaji: Mimi Dhumuni langu siyo Kukuzuia Wala Siyo nia yangu, nimekuacha Uulize Maswali Mengi na Siyo Leo tu hata Siku ya Kwanza Uliuliza Maswali Mengi, Mimi Hoja yangu Mna refer katika Report ambayo Sina Uhakika Kama nitaipata au Mna mpango wa Kuleta Mahakamani.

Jaji: Musifanye Reference Kwa Report ambayo bado Haipo Mahakamani, Mimi nita' refer nini?

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kwa sasa turidhie Ku airisha Mahakama yetu Kwa Muda ambao Utakuwa Umependekeza, Kutokana na Muda kwenda Sana

Wakili w Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi hatuna Pingamizi

Jaji: Basi shauri lina airishwa mpaka kesho Tarehe 15 February 2022

Shahidi: unaonywa Kesho Utaendelea Kuwa Kizimbani Kuendelea Kutoa Ushahidi Wako

Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya Magereza mpaka kesho Asubuhi saa 3
 

Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
65,317
69,368
Habari Wakuu,

Leo 14/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3. Shahidi Tumaini Swila jana Februari 9, 2022 aliomba ahirisho kwakuwa alikuwa hajisikii vizuri.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3: Shahidi wa 13, Tumaini Swila ashindwa kufika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2022

Baki nami.

Updates:
MUNGU akatende miujiza yake katika jina la Yesu, mwana na baba ameni
 

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
1,700
5,614
Habari Wakuu,

Leo 14/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3. Shahidi Tumaini Swila jana Februari 9, 2022 aliomba ahirisho kwakuwa alikuwa hajisikii vizuri.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3: Shahidi wa 13, Tumaini Swila ashindwa kufika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2022

Baki nami.

Updates:
Sawa sie tuna washukuru kwa kazi njema mnaofanya kutuhabarisha yanaojiri hapo mahakamani, tuko tayari kuendelea kuona comedy ya mawakili wa serikali, sijui leo wanakuja na lipi jamba la ku-bayi mda lina mwisho wake pia, wajua katika sheria "right delayed is right denied" sijui walisomea wapi sharia
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
45,175
137,696
Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Huyu Freeman Mbowe aliwahi kufungwa lakini akatoka baada ya kulipa faini baadae Mahakama ya Rufaa ikaona alifungwa bila kuwa na hatia ( alionewa)

Maisha ya hii dunia ni ubatili mtupu!
Ndio maana wengine hatukusikitika Jiwe lilipoondoka katika uso wa hii dunia ingawa wote njia yetu ni hiyo hiyo.
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
17,887
31,412
Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Huyu Freeman Mbowe aliwahi kufungwa lakini akatoka baada ya kulipa faini baadae Mahakama ya Rufaa ikaona alifungwa bila kuwa na hatia ( alionewa)

Maisha ya hii dunia ni ubatili mtupu!
Lakini Jana ulituambia tuendelee na Ugaidi wetu
 

liwaya

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
1,578
894
Habari Wakuu,

Leo 14/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3. Mawakili wa Serikali waliomba ahirisho la kesi hadi leo Februari 14, 2022 kutokana na Shahidi Tumaini Swila kushindwa kufika Mahakamani siku ya Februari 10, 2022 kutokana na ugonjwa. Awali Februari 9,2022 aliomba ahirisho kwakuwa alikuwa hajisikii vizuri.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3: Shahidi wa 13, Tumaini Swila ashindwa kufika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2022

Baki nami.

Updates:
Tuko nawe kk
Mvua hakuna leo maana asije na issue ya nimonia bure leo
 
45 Reactions
Reply
Top Bottom