Wanabodi inabidi niombe tena msamaha maana ya jana yajirudia leo, Kikao cha usiku huu, kimeahirishwa ghafla leo kama jana, baada ya kuwasilishwa kwa taarifa mbili za uendeshaji usiridhisha wa RITES NA TICKS.
John Cheyo katoa hoja hakuna serikali ilichotekeleza, hivyo tunadajili nini.
Spika akaikubali hoja ya Cheyo, akamuuliza Mwanasheria Mkuu, ambeye aliridhia serikali haitafanya kitu, hivyo taarifa hizo zitaletwa yena bungeni kikao kijacho.
Hivyo Spika Sitta akatangaza kuliahirisha bunge mpaka kesho saa 3 asubuhi kutokana na kutokuwepo kitu cha kujadili.
Du Bunge Hili!.
Nimetoka hapa nje, Marine Hassan Marine, anapiga vox pop za kufa mtu hapa nje kwa kuwahoji watu mbalimbali, yaani natamani kupata nafasi nitoe dukuduku langu.
Amemhoji Hamad Rashid, John Cheyo na Dr. Will Slaa na Ole Sendeka.
Wote wamepiga nyundo baada ya nyundo kwa serikali.
Hivi nikitoa my honest opinion kuwa serikali hii, ni most failure, nitakua ninaionea serikali yetu tukufu?.