Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi Februari 01, 2022

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,243
4,333
Habari Wakuu,

Leo 31/ 01/ 2022 shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki:Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022


Fuatana nami kupata yatakayojiri

UPDATES:

Jaji ameingia Mahakamani, Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na

 • Wakili Pius Hilla,
 • Abdallah Chavula
 • Jenitreza Kitali
 • Nassoro Katuga
 • Esther Martin
 • Ignasi Mwinuka
 • Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

 • Wakili Michael Mwangasa
 • Sisty Aloyce
 • Gaston Garubindi
 • Idd Msawanga
 • Maria Mushi
 • Nashon Nkungu
 • John Mallya
 • Dickson Matata
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tutaendelea na Shahidi, Tupo tayari Kuendelea

Shahidi anaingia kutoka Nje

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Jaji: nakukumbusha Kwamba Tarehe 28 ulikuwa upo chini ya kiapo na leo utaendelea kutoa ushahidi wako chini ya kiapo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba sababu ya kelele za Jenereta tufunge madirisha tafadhali.

Kibatala: Mr Urio how are you?

Shahidi: Am fine

Kibatala: Did you have a nice Weekend?

Shahidi: like speak again

Kibatala: Did you have a nice Weekend?

Shahidi: like That!

Kibatala: Shahidi Umesha wahi Kukutana na Mazingira ya Kuambi Maneno Mazito Unayosema ya Ugaidi

Shahidi: Sijawahi Kukutana nayo

Kibatala: Umesema hauna tatizo la Kumbukumbu

Shahidi: Sina tatizo la Kumbukumbu

Kibatala: Iweje usikumbuke Tarehe 2 Muhimu Wewe Kukutana na Mbowe na Kwenda Ofisini Kwa DCI Ukizingatia wewe ni Mwanajeshi, na Luteni wa Jeshi

Shahidi: Mhe Jaji Mheshimiwa Mbowe alikuwa ni Ndugu yangu, Nilikuwa sijui kuwa ni kweli au si Kweli, Mpaka nikaona kuwa Kumbe ni Serious

Kibatala: Wewe Luteni unaona Umejibu swali Langu la inawezekana Vipi usikumbuke Tarehe

Shahidi: Sijawahi Kusikia Maneno Mazito, Ndiyo Maana Nikaenda kutoa Riport Polisi Wafanye Uchunguzi

Kibatala: Swali langu inawezekana Vipi Ushindwe Kukumbuka Tarehe ya Matukio Kama hayo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mimi naona Kama Nimejibiwa

Jaji: Swali lilikuwa linawezekanaje Kuwa asahau Tarehe za Mambo Muhimu

Shahidi: Ilikuwa ni Mara ya Kwanza, Kusikia Kutoka Kwa Mheshimiwa Mbowe, Sikuwa nategemea

Kibatala: Vipi Kuhusu Tarehe ya kwenda Kwa DCI na yenyewe Ulikuwa shocked

Shahidi: Siyo Duty yangu Mimi Kukumbuka, Kazi yangu Ilikuwa Kutoa Riport tu

Kibatala: Kwakuwa Unaomekana Kujivua Duty ya Record Ya Tarehe, Unaweza za Ku tuisaidia Kwanini na Yeye DCI hakumbuki Tarehe Uliyo Kwemda Ofisini Kwake

Shahidi: Sifahamu, Siwezi Kumjibia

Kibatala: Siku Unakwenda Kwa DCI Kingai alikuwa Summoned akaja, Unaweza Kutuisaidia Kwanini huyu Kingai Mtu wa Tatu na Yeye hakumbuki ni Tarehe ipo Mlimkutana

Shahidi: Siwezi Kujua ni Kwa nini

Kibatala: Ni kwanini hata Inspector Swila ambaye ndiyo Afisa wa Upelelezi Aliyefungua Faili Tarehe 18 July 2020, Hakumbuki Tarehe hiyo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Kwa wewe Kama Luten Wa Jeshi unaona ni sahihi Kwa Nyinyi Watu wote hakumbuki Tarehe

Shahidi: Siwezi Kujibia

Kibatala: Umewahi Kusikia Msemo "The Lights are on but nobody at home"

Shahidi: Hapana Sijawahi Kusikia

Kibatala: Kwanini Tarehe 11 August 2020 ndiyo Maelezo Yako yaandikwe Mtoa Taarifa Ambaye ndiyo Ulisababisha Faili Kufunguliwa Tarehe 18 July 2020?

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Wewe ni Luteni wa TPDF uoni Kwamba Inategemewa Maelezo Ya Mtoa Taarifa Kuandikwa Mapema Kadriri inavyowezekana

Shahidi: Siwezi Kujibia Polisi, Sababu Wao Wana Utaratibu Wao wa Kazi na Mimi Nina Utaratibu Wangu Wa kazi

Kibatala: DCI alikifafanulia Kwamba Kwanini Maelezo Yako hayawezi Kuchukuliwa Siku ambayo wewe Umeenda ku report

Shahidi: Hawakufafamua chochote

Kibatala: Tarehe 11 August 2020 kwa Ushahidi Wako Ndiyo Ulikwenda Kutoa Maelezo Ushahidi Wako Kwa Inspector Swila.. Inspector Swila alikufafanulia Kwanini alisubiri Mpaka Mwezi Mmoja Baadae?

Shahidi: Hakufafanulia

Kibatala: Tukisema Kuwa Mlitunga Kesi Mapema Kisha Baadae Ndiyo Makaanza Kutafuta Watuhumiwa, Nitakuwa Nakosea Kwa Fact hizo

Shahidi: Utakuwa unakosea

Kibatala: Unafahamu Dhana ya Infiltration,.?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Maana yake

Shahidi: Kutoka sehemu Moja Kwenda sehemu Nyingine Kwa siri

Kibatala: Ni sahihi pia Maana yake Pana ni Kutuma Mtu Kwenda Kwenye Kambi ya Upinzani, Ili Kupata Taarifa Kamili

Shahidi: Hapana, Tactics inasema Kwamba ni Kitendo Cha Kutuma Mtu Kwa Siri

Kibatala: Nikumbushe tena Elimu yako

Shahidi: Form Four

Kibatala: Unafahamu Decoy

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Luteni wa Jeshi hufahamu Decoy

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Mlijadili Kwa Pamoja Kumpeleka Mtu kwa Mbowe akiwa na Vifaa aweze Kupeleleza na Kurekodi Ushahidi

Shahidi: Hatujawahi Kujadili

Kibatala: Ni Kweli Katika Ushahidi Wako Kwamba Mheshimiwa Mbowe alikwambia atachukua Dola Kwa namna yoyote, Je Uchaguzi ulitajwa

Shahidi: Nafahamu Uchaguzi Ulitajwa

Kibatala: Bado Jeshi lilikuwa halina Role to Play Kwamba wewe ni Mwanajeshi uliye kazini na Mbowe anataka Ex Commandos, Bado Jeshi lilikuwa halina sababu ya Kupewa Taarifa?

Shahidi: Ni Taarifa ambazo hazina Ushahidi, Bado Jeshi litapeleka Kule Kule Kwa Polisi

Kibatala: Unamfahamu Aliyekuwa Chief of Staff Luteni Generali A. Shimbo

Shahidi: Namfahamu

Kibatala: akiwa katika Majukumu Yake ulikuwa Jeshini

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Namnukuu Tarehe 13 10 2010 "Katika Uchunguzi huu, Jeshi limejipanga Kuhakikisha Uchaguzi Unakuwa wa Amani na utulivu".. Uliwahi Kusikia?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Bado Unasisitiza Kwamba Mambo Ya Kiuchaguzi Jeshi halihusiki

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: huoni Kwamba Kwa Kutoa Kwako Taarifa Jeshi lingefanikisha Kuweka Decoy, (Mamluki) wa Kwenda Kukusanya taarifa ambazo ni sahihi?

Shahidi: The issue ni kwamba Mtu anaitwa Freeman Mbowe hapokei Simu za Kawaida, anasema Nitumie picha na Profile yake ili ajiridhishe Kwamba bado Wapo Katika Service, Kwa hiyo Endapo tungetuma Mtu ambaye bado yupo katika Service angegundua

Kibatala: Kwa hiyo Tactical appreciation Yako ilikwambia Kwamba Mheshimiwa Mbowe ana uwezo wa Kujua profile zao?

Shahidi: Ndiyo, Unafikiri Kwanini alitaka Picture na Profile zao?

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Wote Kuna Mahala Popote Ulisema Kwamba Mbowe alikwambia Kwamba ana Access ya Mtu Mwingine Jeshini

Shahidi: Hapana

Kibatala: Tujadili Kuhusu Tactical Appreciation, Ni sahihi Kwamba Kamanda anakutana na Mazingira Fulani ambayo Kamanda anapanga Vikosi Vyake Kukabiliana na Mazingira hayo kwa Muda kwa Kupanga Mkakati

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Sasa Wewe Palikuwa na Several Unknown, Nimekuuliza Kama Mbowe alikuwa na Access Jeshini Ukasema hujui, Sasa huoni Kwamba Tactical appreciation Yako Ilikuwa si sahihi

Shahidi: Huyu Bwana ningemwambia kuwa Sitaki angemtumia nani, Ndiyo Maana nilifanya Tactical Appreciation na Kwenda Kuripoti Kwa DCI

Kibatala: Unakubaliana na Mimi kwamba Katika hali hiyo Kuna mambo Kadhaa wa Kadhaa ulikuwa huyafahamu, Ndiyo Maana Ukasema Kwamba Ulikuwa hujui Kama alikuwa ameshaongea na Watu Wengine

Shahidi: Ndiyo nilikuwa sina Uhakika Kama Mbowe ana Option A, B na C

Kibatala: Sasa Jambo hilo Linaendana na Tactical Appreciation

Shahidi: Ndiyo linaendana

Kibatala: Kazi yangu ni Kuuliza Maswali

Kibatala: Umesema Ulikuwa huna Uhakika Mbowe alikuwa na Option A, B na C, Je ulijihakikishia Kwa Kumuhoji

Shahidi: Sikumuhoji

Kibatala: Unathibitisha alikuwa na Trust Yako yote

Shahidi: Sijui Kwa Yeye Sasa

Kibatala: Nakuuliza Wewe

Shahidi: Je ni Mimi peke yangu anaye niamini

Kibatala: Hakuna Mahala Uliposema Kwamba Mbowe alikutishia Wewe au Familia yako

Shahidi: Sijasema

Kibatala: Kwamba Mbowe alikuahidi Cheo Kama Incentive yako

Shahidi: Mbowe Hawezi Kunipa Cheo Jeshini

Kibatala: Kwa hiyo Mbowe alikuwa hawezi Kukuhaidi Cheo Sababu alikuwa Mbunge

Shahidi: Sahihi hawezi

Kibatala: Nashukuru Kwa jibu lako Zuri

Kibatala: Wakati Mbowe anakupa Maombi , Ulimkubalia au Moyoni Ulimkatalia

Shahidi: Ilikuwa Tactical Appreciation, Ile Kwamba nitachoma Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Masoko,

Kibatala: Na Kumdhuru Sabaya pia Ulikuwa Unachakata

Shahidi: Sijawahi Kumtaja Sabaya Mimi, Nilitaja Viongozi

Kibatala: Akili ya Kawaida ya Luteni haikuwa na zaidi ya Kumchimba Kwamba anataka Kulipua Vituo gani, Kukata Miti sehemu gani?

Shahidi: Hata Ingekuwa ni Mimi, Ukishaanza Kunidodosa nakosa trust na wewe.

Kibatala: Wakati Mnakutana Kupanga Matendo ya Ugaidi, Mahakama Itakapopima, Maneno yako Dhidi ya Maneno ya Mbowe sababu Hakuna Sauti Nyingine wala Decoy?

Shahidi: Ndiyo Maana nikatuma Vijana

Kibatala: Kwani Vijana hawa si Washtakiwa? Au Wapelelezi Wako?

Shahidi: Washtakiwa

Kibatala: Unakubaliana na Mimi sasa Mahakama itabidi ipime neno lako dhidi ya Mbowe kwa sababu Hapakuwa na Mtu Mwingine pale

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unakumbuka Wakati wa Utejelezaji Wa Majukumu Yako, namna ulipompata Ling'wenya

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Unakumbuka Uliongea na Baba Yake Ling'wenya

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Unakumbuka Kwamba uliongea naye Tarehe ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Unakumbuka uliongea naye Majira gani

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Unafahamu a kwamba Mzee Ling'wenya alikukatalia Kumtoa Mwanaye sababu ya Mambo yaliyomtokea Mwanaye Jeshini

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kwamba Yeye alishamtafutia Mwanaye Kazi ya kokoto

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba huyu Mzee (Baba yake Ling'wenya) ni Mwenyekiti wa Kijiji fulani huko Kusini

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Baba Yake alipokutafuta baada ya Kusikia Mwanae kakamatwa Unakumbuka Ulimjibu nini

Shahidi: Sikumbuki, Ila Niliwambia kuwa amuulize Boss wao

Kibatala: Kwani Boss wao ndiye aliye Mpigia Kumuombea Ruhusa Kwamba Kuna kazi

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Ulimwambia Mzee Ling'wenya Kwamba Kuna kazi Kwa Mbowe lakini nataka akafanye Mipango ya Ugaidi

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Maana ya Intrapment

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Maana ya Kumtoa Mtu kafara

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unakumbuka Kwamba Nilikuuliza Unasali Wapi kwa sababu gani

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: umeapa kwa Biblia Je Unafahamu Kuhusu Daniel

Shahidi: Nafahamu Kuwa walitupwa Kwenye Tundu la Simba

Kibatala: Wewe Kuna tofauti na Walichomfanyia Daniel na Ling'wenya Mkristo Mwenzangu.?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwamba Ling'wenya alikuwa na kazi yake ya Kubonda Kokoto wewe Kwa Kikao Chenu na DCI ukamtafuta Kumwimgiza kwenye Matatizo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wakati Baba Yake Ling'wenya anakutafuta Kukuuliza Kwamba Mwanaye yupo wapi Ukajibu Ongea na Boss wake, Ni kweli

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu kwamba Mzee Ling'wenya alistaafu Bila Doa Lolote Serikalini

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kama Mzazi, anaumia Ka Ilivyokatwa kwa Mama Maria Kumuona Mwanaye anateseka Msalabani wakati hajafanya Kitu chochote

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Je inawezekana kwa Mafunzo yako wewe yanaruhusu Kiongozi wa Askari Wa Chini, awaache Askari Wake Wa Chini wakati wa hatari.?

Shahidi: Inategemea kwa Mazingira

Kibatala: Je ni Mazingira Gani kwa Mafunzo yako wewe yanaruhusu Kiongozi wa Askari Wa Chini, awaache Askari Wake Wa Chini wakati wa hatari?

Shahidi: Kiongozi anaweza asiwe Sehemu Moja

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwanini Kwenye Platoon Kiongozi anakuwa Mbele, Hata katika Biblia

Shahidi: Sifahamu, Sijawahi Kuona

Kibatala: Unafahamu Kwamba Adam Kasekwa alipatwa na Battle Traumatic Fatigue

Shahidi: Mimi sifahamu Sijawahi Kusikia ana historia hiyo

Shahidi: Je Shahidi alitoa cheti cha Daktari

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Ulisema Kwamba ulienda Kwenye Ofisi ya Admin officer ukasoma Mafaili yao

Shahidi: Siyo Mafaili ya Taarifa individual, Bali Taarifa za Matukio tangu Siku Natoka

Kibatala: Je ni sahihi Kwamba Ujui sababu ipi ambayo ilipelekea Adam Kasekwa Kufukuzwa Jeshini

Shahidi: Sijui zaidi ya Utovu wa Nidhamu

Kibatala: Unafahamu ni Maeneo gani Mahususi ambayo Walitembelea kwa ajili ya Kumdhuru Sabaya

Kibatala: Wewe Ukiwa katika kazi Maalum, Hukuona sababu kuuliza Kwa Bwire ni wapi Walipanga Kufanya Uhalifu

Shahidi: Mimi siyo Kazi Maalum

Kibatala: Kwani aliyetafuta Vijana ni Polisi au wewe?

Shahidi: Mimi

Kibatala: Mbowe aliomba Polisi wamtafutie Vijana?

Shahidi: Hapana

Shahidi: Bwire Hakuniambia

Kibatala: Katika Ushahidi Wako hujui wala hujazungumzia Kuhusu Milestone, Kokoriko na Triple B

Shahidi: Sijazungumzia

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Walikamatwa kwa tuhuma za Kupanga Kufanya Uhalifu wa Kumdhuru Sabaya

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Ni kweli Uliwatafuta Vijana Kwa ajili ya Kufanya Ukamataji kabla ya Uhalifu haujatokea

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Bado Hukuona Sababu ya Kumuuliza Bwire

Shahidi: Polisi Walitakiwa Wafanye Uchunguzi Wao

Kibatala: Kwani nani aliyemtafuta Adamoo

Shahidi: Ni mimi

Kibatala: Kwani nani alikuwa anaaminiwa na Adamoo kati yako na Polisi

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: akuna Taarifa a kwamba siku za Adamoo na Ling'wenya Wanakamatwa walikuwa wanapokea Taarifa Kutoka kwa Msiri wao, Je huyo Msiri ni wewe

Shahidi: Siyo Mimi

Kibatala: Je Kwa Ufahamu Wako palikuwa na amtu Mwingine aliyekuwa anatoa Taarifa kwa DCI na Kingai

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Kwa Ufahamu Wako wewe Kuna mtu Mwingine ambaye alikuwa anawajua Adamoo na Ling'wenya

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu Kwamba Adamoo na Ling'wenya Siku Wanakamatwa pale Rau Madukani walikuwa wanafanya nini.

Shahidi: Wala sijui Kama Walikamatwa Rau Madukani

Kibatala: Unafahamu a kwamba pale Rau Madukani Mohammed Ling'wenya alikuwa na Dada yake anaitwa Athima

Shahidi: Sifahamu, Hakuwahi kuniambia

Kibatala: Wewe Hukumu uliza Bwire

Shahidi: Sikumuuliza

Kibatala: Ulikuwa unafahamu Kwamba Moses Lijenje ana Dada yake anaishi Arusha

Shahidi: Hapana Sijui

Kibatala: Na wala Msiri wao unasema Siyo wewe

Shahidi; Siyo Mimi

Kibatala: Kuna sehemu katika maelezo yako Uliandika "Nilimpatia ACP kingai Namba za Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya aweze Kuwa fuatilia" ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Swala la Kwamba ACP kingai alikuwa namba za watu Watatu Mpaka Siku wanakamatwa, Je uliliongelea.?

Shahidi: Sikuongelea

Kibatala: Ni Suala la Kuwapa namba za Simu ni Swala la Muhimu au siyo la Muhimu

Shahidi: Ni suala la Muhimu

Kibatala: Unafahamu kwanini Kingai Wala Mtu Mwingine yoyote Hakuna anaye zungumzia Swala la Wewe Kuwapa namba za Simu kabla

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Swala la Kingai Kuwa na namba za Simu za Watu hawa Zina Implication gani Katika Uchunguzi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Mashahidi ambao Wamekutangulia, Walikuwa Wanamtafuta Lijenje Manually wakati Wana namba zao za simu

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba hata baada ya Watu hawa kukamatwa Kingai hakufanya chochote Katika Kuwafahamisha Wapendwa Wao

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Wakati Wa Tarehe 12 August 2020 Ulisema Ulimkabidhi Inspector Swila na kuandikishwa ID02

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Mwanzo Ukasema Kwamba Wakati Unamkabidhi Simu yako Ulitoa Line ya Vodacom ambayo ilikuwa na Mawasiliano yako na Watu Wengine

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwahiyo wewe Ulimkabidhi Inspector Swila Simu bila Sim card

Shahidi: Nilitoa ya vodacom ni kabakisha Moja

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Sim Card ya Vodacom,ulirudisha lini.?

Kibatala: Katika Nyaraka ipi Tukiangalia Tutaona Mlikabidhiana Sim Card ya Vodacom na Inspector Swila

Shahidi: Ipo

Kibatala: Ipo hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana, Hapa Mahakamani Haipo

Kibatala: Ipo wapi

Shahidi: Sikujua Kama Inahitajika Mahakamani

Kibatala: Ile Simu ya Tecno Uliyowasha hapa, Ina SimCard ndani

Shahidi: Sikukagua kama ina Sim Card ndani

Kibatala: aliye sema Kwamba Ile simu ina Sim Card ndani ni nani

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: nikuombee utuonyeshe sim Card

Shahidi: Vyovyote Vile itakayokuwa

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo P34

Kibatala: haya Fungua utuonyeshe humo ndani Kuna Sim Card ya Mtandao gani

Shahidi anafungua

Shahidi: HAKUNA LINE HATA MOJA (SimCard)

Kibatala: Unafahamu thamani ya Kiapo chako

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba unawajibu wa Kulinda hadhi ya Jeshi la Wananchi Tanzania

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Ukweli na Uongo wako Unapimwa Katika Vitu Vidogo Vidogo Kama hivyo

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Nakuuliza tena, Wakati Unakabidhi Inspector Swila Simu Ilikuwa na Sim Card au Haina Sim Card

Shahidi: Ilikuwa na Sim Card

Kibatala: Unafahamu kwamba SimCard imepelekwa Wapi

Shahidi: Ilikuwa na Line ya Airtel Iliyobakia, Sifahamu Ipo wapi

Kibatala: Ile Sim Card Ya Vodacom na Zile simu zingine 3, katika Maelezo Yako ya Tarehe 12 August 2020 Ulizungumzia Katika Maelezo yako?

Shahidi: Sikuandika katika Maelezo Yangu

Kibatala: sisi tuna thibitisha Wapi Kwamba Ulikabidhi hizo Simu 3 wakati hazipo katika Maelezo yako wala Hakuna Hati ya Makabidhiano

Shahidi: lakini zipo Hapa Mahakamani

Kibatala: Ungekuwa Polisi Nimgekuuliza Unafahamu Chain of Custody wewe, ila wewe Afisa wa Jeshi Nitakuonea

Kibatala: Unafahamu Kwamba Hizo Simu 3 Zina Mahusiano na Kesi Hapa Mahakamani

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Je Ulimwambia Jaji Kwamba Zile simu zingine Mbili Kule Morogoro ulimwachi nani na Zilikuwa Chini ya Uangalizi wa nani

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Wala Hukumwambia Jaji Kama huko Ulipoziacha Zina password au hazina

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je unafahamu Kwa nini yule aliyekwambia ulete Simu 3 Kesho yake, hajazungumzia chochote Kuhusu hizo Simu 3

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu au hufahamu Kwamba Freeman Mbowe alikuwa na Kaka wa Damu, Generali ambaye katika Kifo cha huyo Generali Rais Magufuli alienda kwa Mbowe Kumpa pole

Shahidi: Nilisikia

Kibatala: Na unataka tukubali sisi watu wazima Kuwa aliacha Ndugu yake wa damu aliyenyonya naye ziwe Moja akutafute wewe?

Shahidi: Yule si alishastaafu

Kibatala: alistaafu lini

Shahidi: Sijui

Kibatala: Kati ya Wewe Luteni uliye kazini na Generali ambaye amestaafu nani anawafahamu Watu wengi Jeshini Waliopo na Waliotangulia?

Shahidi: Jenerali

Kibatala: Unasema Siku ya Kwanza Mbowe alikutafuta Siku ya Kwanza, Ukashangaa

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kitendo Cha Mtu wa Kukupigia Simu bila Ridhaa Yako unaweza kutolea Taarifa

Shahidi: Rudia Swali

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kitendo Cha Mtu wa Kukupigia Simu Mtu Muhimu Kama wewe bila Ridhaa Yako unaweza kutolea Taarifa

Shahidi: Kwanza Mimi siyo Mtu Muhimu

Kibatala: Wacha Jaji aandike Kuwa wewe siyo Mtu Muhimu

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kitendo Cha Mtu wa Kukupigia Simu bila Ridhaa Yako unaweza kutolea Taarifa

Shahidi: Siyo Utamaduni Wetu

Kibatala: Je ulitoa Taarifa Jeshini Kwamba Kiongozi Wa Chama Cha Upinzani Chadema Kakutafuta

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: Kwenye Maelezo Yako Ulisema Kuwa Mliendelea Kuwasiliana naye kwa sababu wewe na Yeye Wote ni Kabila Moja

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwa hiyo hili la Ukabila ndiyo Kilikufanya uendelee Kuwasiliana na Mbowe

Shahidi: Hapana ni Mawasiliano

Kibatala: si Ndiyo Mawasiliano na Mwenyekiti wa Chadema wakati wewe Umesema hamfungamani na Chama Chochote

Shahidi: Mbowe ni Mbowe na Chadema ni Chadema

Kibatala: Kwanini sasa Katika Maelezo yako unasema "Freeman Mbowe Mwenyekiti Wa Chadema"

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: hapo ulimtenganisha Mbowe na Chadema?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Shahidi Ushahidi Wako Unasema Kwamba TSh 500,000 ulitoa TSh 300,000 Ikabakia TSh 200,000, Ukawapa Adamoo Ling'wenya TSh 199,000

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: katika Maelezo yako Uliandika Kwamba Mhe Mbowe alikumbushia Kuhusu Vijana, ukamwambia Kuwa wamepatikana 2

Kibatala: kwa hiyo wewe Kwa Maelezo Yako Ulisema Tarehe 20 July 2020 alinitumia Laki TSh 500,000 nikatoa TSh 300,000 Laki 2 Ikabakia Kwenye simu

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Katika Maelezo Hakuna Mahala Ulisema Uki Alisha TSh 200,000 Kwenye simu

Shahidi: Hakuna nilipoandika

Kibatala: Alikwambia Inspector Swila Maana ya haya Maelezo

Shahidi: Hakuniambia

Kibatala: Baada ya Siku Chache wapatikama Vijana Wawili nikawapatia TSh 195,000

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Maelezo yako na unachosema Kwenye Kizimba Vinafanana au Vinatofautiana?

Shahidi: Vinatofautiana

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P 1 na P 13

Kibatala: Nimeshika hapa Maelezo ya Onyo ya Adam Kasekwa ambayo Wenzetu Wanasema alikiri

Kibatala: Katika Ushahidi Wako, Unasema Uliwapa Tsh 195,000 katika TSh 199,000 Uliyotumiwa, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba TSh 4,000 Ilienda wapi

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Kwa hiyo TSh 4,000 ya Ugaidi hujasema Ipo wapi

Shahidi: SIYO YA UGAIDI, BALI YA KUWASAFIRISHA

Kibatala: kwa hiyo Wenzetu Wanasema Yote TSh 199,000 ilitumika Kwenye Ugaidi, Kumbe siyo Ugaidi

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Maelezo haya yanasema kuwa alipokea TSh 87,000 kila Mmoja, Je Ni kweli au si Kweli

Shahidi: Sikumpatia Mtu Mmoja Mmoja, Niliwapa Kwa Pamoja

Kibatala: Kama Adam Kasekwa kasema Walipewa TSh 87,000, Atakuwa Kasema Uongo

Shahidi: atakuwa kasema Uongo

Kibatala: Unakubaliana Kuwa 87,000 Mara Mbili ni TSh 174,000? Unakubali unakataa

Shahidi: amount hiyo Mimi sijui

Kibatala: Nakuuliza kimahesabu 87,000 Mara Mbili ni TSh 174,000

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Adam Kasekwa anasema Jumla Uliwapa Tsh 174,000, Wewe Unasema TSh 195,000, Je Inatofautiana

Shahidi: Inatofautiana

Kibatala: Na Adam Kasekwa anasema Kwamba Fedha hiyo Uliyotumiwa na Mbowe ilikuwa ni Kuwarejeshea (Refund) ni sahihi au Siyo Sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba na sisi tuwe tunaangalia Kama Maelezo yapo Sahihi

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Pia awe anasoma Kile ambacho Kimeandikwa Kwa Mfano Hakuna Sehemu imeandikwa TSh 174,000 lakini Kuna TSh 87,000

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Sasa Kwa Majibu Kuhusu Majibu ya Kielelezo P 1 yaondoke

Kibatala: Ni sawa tufute Mstari Mmoja halafu tuanze Upya

Kibatala: Sasa Nilikuwa nakuuliza awali shahidi Kuhusu Maelezo yako inasema hivi, Baada ya Siku Mbili Waliopatikana Vijana Wawili Adamoo na Ling'wenya Ambao Niliwapatia TSh 195,000, tulipo kutana Eneo la Msavu

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwa hiyo Ni sahihi Kwamba hiyo Tsh 195,000, Kwamba Uliwapatia Kama Gharama ya Nauli zao Kutoka Walipo toka Kuja Morogoro

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Walipo kuja Morogoro Kutoka Walipo toka Uliwapa Tsh 195,000 kwa Ujumla au Lah.

Shahidi: Niliwapa Kwa Ujumla

Kibatala: Adam Kasekwa anasema Walikuja na Ling'wenya, "kwa kutumia Simu ya Mke wangu, Alinipigia Kuna kazi ya VIP PROTECTION, Maelezo sahihi anayo Luteni Urio"

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: anasema "alitupatia Kila Mmoja TSh 87,000 Kwa Maelezo ya Ling'wenya"

Shahidi: sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Fedha zote hizo ilikuwa kwa ajili ya Refund

Shahidi: Ilikuwa kwa ajili ya Kuwafidia

Kibatala: Safi sana

Kibatala: Unakumbuka Ulisema Kwamba Uliwapa Nauli ya kwenda Wapi Adamoo na Ling'wenya Kutoka Morogoro

Shahidi: Niliwapa Cash Tsh 195,000, ila Sikumbuki niliwapatena TSh ngapi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba ile 199,000 Iliyotuma Baadae ndiyo Uliwapa Nauli ili waende Kwa Mbowe

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu Katika Maelezo Yake Adam Kasekwa, Katika Ukurasa wa Nne Mstari ya Mwisho, ni kila Mtu Kufika Moshi.. Wewe Unasema Walikwenda Dar es Salaam Kukutana na Mbowe, Je Statement hii Inafanana au inatofautiana?

Shahidi: Inatofautiana

Kibatala: nimeshila Maelezo ya Mohammed Ling'wenya Kielelezo namba P13, anasema kuwa "Baada ya mazungumzo Luteni Urio Aliniuliza Kuwa Mshahara wa Mtwara TSh ngapi, Nika jibu ni posho ya Elfu 15 kwa Siku, Basi Luteni Urio akanishauri Mshahara uwe Kuanzia TSh 800,000"

Je, ni sahihi Kwamba Ulimshauri Kuhusu Mshahara

Shahidi: Hapana

Kibatala: anaendelea Kusema Kuwa "alitupatia TSh 190,000 nauli ya kwenda Moshi"... Je ni sawa au zinatofautiana na Maelezo yako

Shahidi: tofauti, Pia tofauti hata na Ile ya Adamoo

Kibatala: You're Very Smart

Kibatala: Ling'wenya anazungumzia TSh 190,000, wewe unazungumzia TSh 199,000, Kuna tofauti ya TSh 9000

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kuwa Wapokeajo wa hizi pesa wanasema Kuwa Matumizi Yake yalikuwa siyo Ugaidi bali nauli

Shahidi: Sikubaliani na wewe

Kibatala: Kwani wewe Umesikia Wao wanasema Kwamba ile Fedha ilikuwa kwa ajili ya Nini, Adama Kasekwa Si kwa ajili ya Refund na Mohamed Ling'wenya ilikuwa kwa ajili ya Kwenda Moshi?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Hapa Walikuwa wamekutana na Mbowe?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Walikuwa bado hawajafanya Ugaidi

Shahidi: Walikuwa ndiyo hawajafanya Ugaidi

Kibatala: Unafahamu kwamba wenzio Wanasema Hizo TSh 199,000 Mbowe zilifadhili ugaidi?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: ooh! Kumbe hata wenzako wamekuficha?

Kibatala: Ling'wenya nasema pia alipewa pesa akanunue Mavazi, Ni kweli

Shahidi: Si Kweli

Kibatala: Kwamba wewe unasema Ling'wenya alipewa pesa ya Kwenda Dar es Salaam, Yeye anasema Kwenda Moshi, Mmetofautiana..?

Shahidi: Ni sahihi tumetofautiana

Kibatala: eneo lingine Mlilotofautiana Ling'wenya anasema alipewa pesa ya Kurejeshwe Nauli wewe Unasema Nauli ya kwenda Dar es Salaam

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Nipewe Kielelezo Namba P 26

Kibatala: Ni kweli Kwamba Mbowe alikwambia umtafutie Ex commandos bila Kikomo

Shahidi: Hakuniambia Idadi yeye alisema Wao Waje tu

Kibatala: Kwenye Kielelezo P26, Ni sahihi Kwamba Kwa Mujibu wa Tarehe 20 July 2020 Saa 1 na Dakika 39 yeye Mbowe anasemaje

Shahidi: "Kaka Wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu sana"

Shahidi: Lakini kabla ya hiyo Meseji Kuna Mawasiliano ya Simu

Kibatala: Yapo wapi

Shahidi: Hayapo hapo

Kibatala: Soma Kama Ilivyo, Kwa Mujibu Wa Meseji hiyo Mbowe anauliza Watu wangapi

Shahidi: Kaka Wale Mtu tatu au Nne ni Muhimu

Kibatala: kwa hiyo Namba hapo ni 3 au 4

Shahidi: Ndiyo Waliopatikana

Kibatala: Nenda Kwenye Meseji ya Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 3 na sekumde 30, Nani katuma hiyo Meseji

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Unafahamu hiyo namba hapo

Shahidi: naona Meseji Kwemda Kwa Mbowe tu

Kibatala: kwa ni Meseji hiyo Uliyotuma hiyo Meseji Kwenda Kwa Mbowe, Je ni Namba ipi ya simu

Shahidi: Nilitumia Mtandao Wa Telegram

Kibatala: Mtandao Wa Telegram Unapotumia unahitaji Mtandao

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Namba Uliyotumia Mtandao huo wa Telegram ni namba ipi

Shahidi anaangua kichekoo ghafla hapa.....

Kibatala:
Shahidi Usiche, Ndiyo Maana nilikwambia The Truth Shall set you Free.. Mwambie Mheshimiwa Jaji namba yako ipo au haipo

Shahidi: Haipo

Kibatala: Soma Katika Extraction Report hapo Wanasema Namba gani hiyo

Shahidi: 1130138344 DENIS OWNER

Kibatala: Namba hiyo Unaifahamu au huifahamu

Shahidi Sifahamu

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Shahidi apewe nafasi ya Kutoa Ufafanuzi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wakili anataka Kufanya Submission Muda huu, asubirie Kwenye Re: examination, Swali langu Je Shahidi anaifahamu namba au haifahamu?

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Kama anataka Kuuliza namba, Ni Vizuri Shahidi afafanue tu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji mimi naona Kuna tatizo na Line

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wametoa OBJECTION Nime re-battle, Wao Wafanye rejoinder siyo Mr. Kidando atoe Hoja mpya..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwenye Rekodi za Mahakama Aliyetoa Kielelezo hicho ni Inspector Ndowo, Hatuoni Haki Kwa shahidi Kuulizwa Kielelezo hicho, Si Sawa kuzuiwa Kutoa Maelezo

Jaji: Kama nimesikia Vizuri Mr. Kibatala alikuwa anauliza Kuwa Shahidi anaifahamu au haifahamu hiyo namba, Mimi sijasikia akijibu hilo swali, alipotaka Kufanya Kufafanua Ndiyo Mr Kibatala akakataa, sasa hayo atamueleza Wakili Wake

Jaji: Ni Sahihi Kwa Shahidi Kujibu Maswali anayo Ulizwa na Wakili tu..

Kibatala: Shahidi Hiyo namba Unaifahamu au haifahamu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wakati Wa Ushahidi Wako Kuna Wakili yoyote alikwambia Fafanua

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu Juu ya Application inaitwa Free Sms

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni application ambayo unatuma Meseji halafu pia unaweka namba kwa namba yako na Kuweka ya mtu unaye mtumia

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kuna wakili yoyote aliyekuuliza Kuhusu Free Sms

Shahidi: Hakuna

Kibatala: na Hakuna Wakili yoyote amekuomgoza Kuitambua hiyo Free Sms ilikuondoa hiyo dhana

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Soma, Hapo, Kuna Maelezo Unasema su siyo Salama Sana, Niwezeshe ili tuweze Kukutana

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kuna Sehemu Yoyote Katika Kielelezo namba P 34 ambayo Freeman Mbowe amekueleza wewe Kwamba Mtumie Njia ya Mawasiliano Mbadala Kwa Sababu Simu Siyo Salama

Shahidi: Meseji ya Mwisho

Kibatala: haya tusomee

Shahidi: "Hellow Bro Nilishindwa Kupokea Simu yako Sababu Deshi Deshi"

Kibatala: kwa hiyo kwa Tafsiri yako Ndiyo Kasema kuwa Simu Siyo Salama

Shahidi: Ndiyo Nilivyo Tafsiri

Kibatala: Katika hiyo Meseji ya Mwisho Kuna Neno simu siyo Salama

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Taja namba ya Mbowe Katika hiyo Meseji ya Mwisho

Shahidi: 0713933386

Kibatala: Soma Sasa Katika Kielelezo Kama hizo Meseji zinafanana au Tofauti

Shahidi: Zinafanana

Kibatala: Sasa soma namba ambayo ipo katika Kielelezo namba P 26 Meseji hiyo hiyo

Shahidi: Inatoka namba 729414989

Kibatala: ambayo ni Namba ya nani

Shahidi: FREE

Kibatala: Je namba ULIYOSOMA Mwanzo na Sasa hivi zinafanana.?

Shahidi: Hapana hazifanani

Kibatala: Kuna tofauti eeeeh!?

Shahidi: Ndiyo Kuna tofauti

Kibatala: Kubwa au Ndogo

Shahidi: Kubwa

Kibatala: Uliongozwa Kufafanua hiyo Tofauti

Shahidi: Sikuongozwa

Kibatala: Tafuta Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Saa 2 na Dakika 15 na Sekunde 54

Shahidi: "Naomba nitumie nauli ya Ku' mobilise nikutane nao Moro"

Kibatala: Nani alikuwa anaomba nauli

Shahidi: Mimi ndiye niliye kuwa naomba nauli

Kibatala: Kwa hiyo DENIS URIO ndiye aliye Omba nauli kwa ajili ya Kuwa Mobilise

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Baada ya wewe kuomba nauli ndiyo Mbowe sasa akatuma TSh 500,000

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nitafutie Meseji yoyote ambayo Mbowe anatoa wazo yeye la kutuma yeye TSh 500,000

Shahidi ametumia dakika 1 kutafuta hapa..

Shahidi: HAKUNA

Kibatala: Ni nani kwa mujibu wa Kielelezo namba P 34 (Simu) aliye propose kuwa pesa ya Ku'. obilise iwe TSh 500,000?

Shahidi: Mimi Denis Urio

Kibatala: Kwa Mujibu Wa Meseji ya Tarehe Ngapi na Mwezi wa Ngapi ambayo wewe ndiyo Mtoa wazo

Shahidi: Meseji ya Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 19 na Sekunde 53

Kibatala: ambayo Meseji hiyo wewe Ulituma Kutoka Kwenye namba gani ya Kwako

Shahidi: Haionekani namba

Kibatala: ONGEZA SAUTI

Shahidi: Haionekani namba

Kibatala: Tafuta Meseji ya Tarehe 20 July 2020 Saa 2 na Dakika 24 na Sekunde 02

Shahidi: "Usiwe unatumia namba yako Kutuma Pesa, Tumia Wasaidizi Wako au Wakala Kutuma"

Kibatala: Ni nani aliyetuma Meseji hii

Shahidi: Mimi Denis Urio

Kibatala: Nikumbushe Kule Kwa DCI na Kingai Uliambiwa Jambo gani Vile

Shahidi: Kuwapeleka Watu

Kibatala: Ni sahihi Katika Maelezo Yako uliyo andika, Uliambiwa Uendelee na kazi ya kumtufutia Vijana na Kuku Sanya Ushahidi

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Hao Wasaidizi Wa Mbowe Washa wahi Kukutumia pesa

Shahidi: Hapana

Kibatala: Katika Mawasiliano yako na Mbowe Uliwahi kutajiwa au Kupatiwa Fedha Kufanya Muamala na Mtu anaitwa Willy Kijana wa Mbowe? Na Wily alikutumia TSh ngapi

Shahidi: 199,000

Kibatala: Ndiyo Fedha ambazo Uliwapa Adamoo na Ling'wenya

Shahidi: Ndiyo hiyo

Kibatala: Swali la Mwisho kabla ya Lunch

Kibatala: Hiyo namba ya Willy ambayo ilituma hiyo Fedha ya TSh 199,000, Uliwapa akina DCI na Kingai

Shahidi: Haikuja namba, Alinitumia namba baadae

Kibatala: Hiyo namba hata Ka Ulipewa baadae, Ulimpa DCI au Kingai

Shahidi: Sikumpa

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba Kama Wenzangu wataridhia tupate Health Break baadae tuendelee na Cross Examination, Naomba pia nirudishe Vielelezo

Jaji: nahairisha Kwa Dakika 45 Mpaka Saa 7 na Dakika 45 ambapo Shahidi ataendelea Kutoa Ushahidi

Jaji: anatoka Mahakamani

*******************************

Mahakama imerejea. Muda ni saa 8:07

Jaji amerejea mahakamani.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji Quorum ya Upande Wa Jamhuri ipo Ka Ilipokuwa Mwanzoni

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi Kwa Upande Wetu Quorum yetu ipo Kama Ilivyo kuwa awali, Tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi nakukumbusha tena Kuhusu Kiapo chako, Utaendelea Kutoa Ushahidi Chini ya Kiapo

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kwa Hisani tukumbushwe Jibu la Mwisho

Jaji: kama alimpa DCI na Kingai Namba ya Willy

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kumpa Shahidi Kielelezo namba P34

Shahidi: anapewa Kielelezo ambacho ni simu

Kibatala: Shahidi Ni sahihi Kwamba meseji ya Tarehe 22 July 2020 Saa 3 na Dakika 19 Sekunde 30

Shahidi: "Namba ya Dereva Wangu anaitwa Willy, Wamtafute yeye"

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Kielelezo namba P 26 Saa 9 na Dakika 30 Sekunde 45 ulipokea hiyo namba

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: na Wewe Saa 9 na Dakika 36 na Sekunde 39 ukasema " Nimepata namba, Nitawapa"

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Hao unaosema utawapa ndiyo akina Khalfani..?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Niomyeshe Meseji ambayo Inaonyesha Kwamba Mbowe alituma namba Pele yake Kama Meseji

Shahidi: alituma lakini hapa Haipo

Kibatala: Ipo wapi

Shahidi: alituma Kwa Meseji ya Kawaida, au Sikumbuki Kama alituma wapi

Kibatala: Ipo wapi

Shahidi: Sikumbuki ipo wapi

Kibatala: Kama Nakumbuka Vizuri wewe hujawahi Kukutana na Willy

Shahidi: Sijawahi Kukutana naye

Kibatala: Tu assume Kama Mambo yalivyotokea, Je Freeman Mbowe aliluomba umtafutie Walinzi au Magaidi

Shahidi: Kwa hao nilikuwa namtafuta Watu Wa Kwenda Kufanya kazi ya Ulinzi

Kibatala: Yeye Mbowe alitaja Walinzi au hakutaja

Shahidi: Alitaja Walinzi

Kibatala: Ndiyo Maana wewe Uliwatafuta watu wa kwenda Kufanya Ulinzi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mbowe alikwambia ukionana nao Uwaambie hivi na Vile?

Shahidi: Hapana

Kibatala: aliye, waambia Kuwa Mnaenda Kufanya Kazi ya Ulinzi ni wewe

Shahidi: Ndiyo ni Mimi

Kibatala: Wakina Inspector Swila Walikwambia Kuwa actually Unatakiwa uwe Mshtakiwa namba Moja au namba Mbili

Shahidi: Hawajawahi Kuniambia

Kibatala: DCI au Kingai Walikwambia Kuwa Watakupatia Kinga Dhidi Ya Mashtaka?

Shahidi: Hawajawahi Kuniambia

Kibatala: Tarehe 22 July 2020 Saa 6 Na Dakika 27 na Sekunde 23 Soma

Shahidi: "Kama Ikikupendeza uwe unanitumia Pesa ya Kutosha kwa ajili ya Kuwa Mobilise kwa ajili ya Kuwafanyia Vetting"

Kibatala: Nani Katuma hiyo Meseji

Shahidi: Ni Mimi Denis Urio

Kibatala: Wakati Unatuma Meseji hii, Khalfani Bwire na Moses Lijenje Walikuwa wameshakwenda Kwa Mbowe?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Katika Kukamilisha zoezi la Kutafuta Vijana hao ambao Hakutaja Kikomo, Freeman Mbowe alinitumia TSh 500,000, Ambapo nilizitoa, Je Kwa Maelezo Haya si ni Kwamba Ulitoa Laki 5 kwa Mkupuo Wa Pamoja

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Maelezo Yako Ya Ushahidi Wako na Maelezo Yako ya statement Vinapishana au Kuna vinaendana

Shahidi: vinaendana ila tofauti Kwenye Tafsiri tuh, (anaonyesha Kwa Mikono)

Kibatala: Sasa nakurudisha Kwenye Meseji

Kibatala: Ni sahihi Kwa Meseji hii Ulikuwa Unaomba Pesa za Ziada Kwa Freeman Mbowe?

Shahidi: Ni sahihi Ili Kufanya Mambo kwa Urahisi

Kibatala: Ulikuwa Unaomba Pesa za Ziada Kwa Mtu ambaye bila Shaka Unafahamu Kwamba ana Mipango ya Ugaidi

Shahidi: Ndiyo nafahamu, Kwa Kuwawezesha Watu aliokuwa anawahitaji,

Kibatala: Si Ndiyo Watu ambao alikuwa anataka Kuwatoa Kwa Ugaidi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unafahamu Kuhusu Neno SOLICIT

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa Clarity wakati Unatuma Meseji Kwamba awe anatuma pesa za Kutosha ulikuwa Umeshapokea TSh 500,000

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa hiyo awe anatuma pesa zaidi ya 500,000 sasa

Shahidi: Ni sahihi Kwa Kadiri Itakavyo Mpendeza

Kibatala: Ulisema Kwamba Kila ulikuwa unamfahamisha Kingai

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Katika Simu hiyo Kuna Meseji za Kumtaarifu Kingai Kuhusu Kutumia TSh 500,000

Shahidi: Hakuna, Ni kuwa naongea naye kwa simu

Kibatala: Je Kuna Meseji ya Mhamala Wa TSh 500,000 Ulitumia Kingai Kwenye Njia ya Meseji Kuonyesha Kingai kama Ushahidi

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Tarehe hiyo Hapo Ulimsalimia Mtuhumiwa Wa Ugaidi Shikamoo Mkuu, Ani sahihi

Shahidi: Sikuwa na Ugomvi naye

Kibatala: Mtu akiwa Adui wa Nchi yako si ni Adui Yako

Shahidi: Sikuwa na Ugomvi naye

Kibatala: Unasema Tarehe 04 August 2020 Khalfani Bwire alikupigia kuwa Adamoo na Ling'wenya Wapo Moshi Kumdhuru Sabaya

Shahidi: Tuweke Vizuri, Mimi ndiye niliye Mpigia kisha akanipigia

Kibatala: Kwa Maelezo yako Khalfani Bwire alikuwa Dar es Salaam au Moshi

Shahidi: alisema Kwamba Wale Madogo Wapo Moshi, sikujua yeye Yupo wapi

Kibatala: Kwa Maelezo Yako wewe Ka. Luten Wa Jeshi, Maelezo Yako Ya Wale Madogo Wapo Moshi, Ulitafsiri kuwa Bwire hayupo Moshi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Katika Maelezo Yako Kuna Maelezo Wale madogo wapo Moshi

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Maelezo Mnamo tarehe 04 August 2020 Khalfani Bwire alinijulisha Wapo Moshi Kumdhuru Sabaya, Kwani Tarehe 12 August 2020 Wanatakiwa Kurudi Dar es Salaam, Je Bwire bado yupo Dar es Salaam

Shahidi: Kwa Mtazamo wangu Mimi

Kibatala: Katika Statement hii Kuna Mahala Popote umeandika Kwamba Bwire yupo Dar es Salaam

Shahidi: sikuandika

Kibatala: Kwanini Huku andika Kwamba Bwire alikuwa Yupo Dar es Salaam

Shahidi: hakunitajia Location

Kibatala: Katika Maelezo Yako Mstari Wa Kwanza, Unasema "Nakumbuka Mwaka 2008 Nilikutana na Freeman Mbowe, Kwakuwa wote ni Kabila Moja, Mimi na Freeman Mbowe tumekutana tena CASA Motel kwa Maongezi". Je Neno Kukutana naye tena, Ni Mara ya Kwanza.?

Shahidi: Miye ndiyo Nilikutana naye Kwa Mara ya Kwanza

Kibatala: Lakini haya ni Maelezo yako Uliyosoma Na Kuyathibitisha..

Kibatala: Ni sahihi Kwamba kabla ya Kukutana naye ana kwa ana alikuwa anakutakia Heri za Sikukuu na Event Mbalimbali

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Moja ya Njia ambayo Freeman Mbowe mnawasiliana alikutumia Pongezi za Maonyesho Ya Sherehe ya Muungano

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Mtu ambaye anatuma Ujumbe wa Pongezi Kwa niaba ya JWTZ, Kutokana na Maonyesho ya Muungano.. Ni Mzalendo au Jahiri

Shahidi: Kwa Kipindi Kile niliona Mzalendo

Kibatala: Katika Ushahidi Wako ulitoa Katika Kizimba Ulisema Kwamba Freeman Mbowe ndiye alikuta futa Mara Mliyopelekea Kukutana katika Mambo ya Ugaidi

Shahidi: yeye ndiye alinitafuta

Kibatala: alikutafuta Kwa Njia ipi

Shahidi: Kupitia Kwa namba za Watu wengine

Kibatala: Namba ambazo alikuwa anazitumia Uliwapa DCI na Kingai

Shahidi: Si Kuwapa

Kibatala: Ulizitolea Vipi Maelezo na Namba ambazo huzijui

Shahidi: Sikutoa sababu Nilikuwa sizijui

Kibatala: Mpaka unaenda Kuona Mbowe akakwambia Ishu za Ugaidi, Nani alimtafuta Mwenzie

Shahidi: Mimi Ndiye nilimtafuta, Akakuta Missed Call akanirudia Jioni

Kibatala: Kwa hiyo ambaye Ali prompt Kuonana, Siyo wewe ni simu ya Mbowe

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Nani aliye andika Kwamba Mwezi July Tarehe za katikati nilimtafuta ili tuweze Kuonana, Nani Kasa haya Maelezo

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Narudia tena Kusoma

Kibatala: Kuna Eneo lolote ambalo Palikuwa na Missed Call na Baadae auka Return Call.?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Je Kuna tofauti kati ya Maelezo na Unachosema Kizimbani

Shahidi: Ndiyo Tofauti Zipo

Kibatala: Katika Maelezo Yako, Kuna Maelezo yoyote Kwamba Ulipo Mpigia Simu DCI , Kuna Maelezo Kwamba Ulijitambulisha Kwake in fully

Shahidi: Nilitijambulisha

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kama Wenzangu hawatokuwa na Pingamizi naomba Wanipe nimuonyeshe Shahidi Maelezo yake, Kama ni Foundation nimefanya hivyo Kwa Zaidi ya Masaa Mawili

Kibatala: Shika hayo Maelezo Kwa Dakika 2 au 3 Kwamba Ulipo Mpigia Simu DCI Ulimpigia na Kujitambulisha Kuwa wewe ni Afisa wa Jeshi na Maelezo Yako yote

Jaji: Kanuni zinasemaje Kabla hajatafuta

Kibatala: Sawa Mheshimiwa Jaji Asante,

Shahidi Si Unaifahamu hiyo Statement

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sasa Shika hayo Maelezo Kwa Dakika 2 au 3 Kwamba Ulipo Mpigia Simu DCI Ulimpigia na Kujitambulisha Kuwa wewe ni Afisa wa Jeshi na Maelezo Yako yote

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Ushahidi Wako na Hayo Maelezo hilo Eneo Kuna tofautiana au hapatofautiani

Shahidi: Kwenye hilo Eneo ni tofauti

Kibatala: Kwenye Maelezo Yako Ukisoma hapo, Kuhusu Pongezi ya JWTZ

Shahidi: Ni Meseji ya Pongezi

Kibatala: Maelezo hayo Yanatofautiana au hayatofautiani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kanuni inasema Kwamba isomwe Kwanza

Kibatala: Baada ya Maelekezo ya Mahakama tafadhali Soma hiyo Statement Yote Kwa Sauti

Shahidi ........ ANASOMA

Shahidi: Nimemaliza

Kibatala: Unakumbuka Nilikuuliza Kwamba unaishi Wapi Ukasema Ngerengere

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Ngerengere na Kihonda Kuna Umbali Kiasi gani

Shahidi: Ni Mbali sana

Kibatala: Rejea Katika Maelezo Yako hapo Juu, Adress yako unaishi Wapi

Shahidi: Kihonda

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuhusi tofauti hiyo

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Nani alikuwa ana Propose Kuwa Msitumie Simu kwa Sababu Simu Siyo Salama

Shahidi: Mimi

Kibatala: Katika Statement Yako Unasema Mbowe alikwambia Kuwa Telegram Ndiyo Salama

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwenye Meseji Kuna sehemu tumeona Mbowe Kasema hivyo

Shahidi: Kimyaaa

Kibatala: Shahidi haya si Maelezo yako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Una tatizo tukimpa haya Maelezo Jaji ayatumie katika Kutenda Haki

Shahidi: Hakuna tatizo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Shahidi Kama alivyo Omba, Tunaomba iingie Kama Kielelezo

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: ni Kielelezo namba Ngapi

Kibatala: Kama Kielelezo namba D4

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba tujikumbushe ni Kielelezo namba ngapi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ni sahihi Kuwa ni D4

Jaji: Nayapokea Maelezo Haya Kama Kielelezo namba D4 Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo

Kibatala: Shahidi Nilikuuliza Kuhusu ile Meseji ya Saa 12 na Dakika 27 na Sekunde 23 Mchana kwa ajili ya Kuwa Mobilise na Kuwafanyia Vetting na Kuwaleta Dar es Salaam

Shahidi: Nimeona

Kibatala: Focus yangu Ilikuwa katika Kuwa Fanyia Vetting, Ni Vetting ya Nini hasa

Shahidi: Kuwa Brief Kwamba Mnaenda Katika Kazi ya Ulinzi na Mkikuta Vitu Kinyume Mnitaarifu

Kibatala: Ndiyo Maana ya Vetting?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Hiyo Meseji Kaandika nani hapo

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Kwani Mbowe alikuwa anajua kuwa Vetting Yako Ilikuwa inafanyika Vipi

Shahidi: Vetting kama Kufanyia Orientation

Kibatala: Vetting Siyo Kumuangalia Back ground na Kumuangalia Sifa zake Kama Kweli au za Uongo

Shahidi: Sikuwa na Tafsiri hiyo Mimi

Kibatala: Kwa hiyo Kuna Kitu gani ulitaka Kufanya Mpaka Ukataka pesa zaidi?

Shahidi: Ni hiyo Kuwa Orient tu

Kibatala: Bwire na Lijenje Uliwa' Orient au Hukuwa' Orient?

Shahidi: Niliwa' Orient

Kibatala: Sasa Bwire na Lijenje Kuna Mahala walisema Kwamba Pesa haiwatoshi, Mpaka Upate pesa za Ziada.?

Shahidi: pesa ya awali ilishakuwa Consumed tayari

Kibatala: pesa ya Awali Iliyokuwa Consumed ni TSh ngapi

Shahidi: Ni TSh 500,000

Kibatala: Shahidi nataka Kujua bado Kwanini kwenye Meseji Kuna Nyongeza ya Vetting

Shahidi: Ilikuwa Kuwafanyia Orientation

Kibatala: kwa hiyo ni pesa ya Mbowe ndiyo imefadhili Ugaidi halafu Pia Ukatoa Mafunzo Kuwa Wasifanye Ugaidi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Tarehe 22 July 2020 Saa 8 na Dakika 3 na Sekunde 53 Soma hiyo Meseji

Shahidi: Lakini wewe Usitume kwa namba yako

Kibatala: Nani alituma hiyo meseji

Shahidi: Mimi Denis Urio

Kibatala: Kwanini Ulimtumia Mbowe Taarifa hiyo

Shahidi: Ilikuwa Kuongeza Trust

Kibatala: Lakini Wewe una Maagizo ya DCI ya Kukusanya Ushkabidibkwa Kadri ya Uwezo Wako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Tarehe 22 July 2020 Saa Saba na Dakika 51 na Sekunde 04

Shahidi: Nimeona

Kibatala: Soma

Shahidi: Pamoja na pesa ya Kula Tuma TSh 200,000

Kibatala: Ilikuwa pesa ya nini

Shahidi: Nauli pamoja na Kula

Kibatala: Tafuta Meseji ya Tarehe 22 July 2020 Saa 5 na Dakika 59, na Sekunde 31

Shahidi: Nimeona

Kibatala: S O M A

Shahidi: Kuna pamoja na Mambo Mengine Kuna Swala la Mishahara

Kibatala: Mishahara Uliyokuwa unazungumzia ilikuwa ya kazi gani

Shahidi: Kufanya Uhalifu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kutolipa Mishahara ni Kosa la Jinai

Shahidi: Sifahamu Sheria

Kibatala: Pale Kuna sehemu unasema Kuna Masuala ya Utawala Wanauliza na Mishahara, Je Utawala Una manisha nini?

Shahidi: Utawala ni Masuala ya chakula

Kibatala: Utawala ni Chakula tu?

Shahidi: Pamoja na malazi

Kibatala: Watu wanaokwenda Katika Uhalifu Wanatakiwa Kuwa na Administration Obligation?

Shahidi: Ndiyo Kwani hawali, hawalali, hawavai?

Kibatala: Sawa Shahidi, Twende taratibu tu, tutaelewana

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P20

Kibatala: Kuna Mahala ulikuwa unasa Kwamba Ulikuwa Unawasiliana na Khalfani Bwire kupitia namba 0782 237913 Sasa Nakuonyesha Kielelezo namba P 20 Ni kweli au Siyo Kweli Kwamba Ulituma Kiasi cha TSh 190,000 kutoka 0787 555200 kwenda Kwenye namba 0782 237913

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ulituma TSh ngapi

Shahidi: TSh 200,000

Kibatala: Sasa Ulisema Kwamba Khalfani Bwire Ulimpa TSh 300,000, Je ulitolea Maelezo Kwa Jaji

Shahidi: Transactions hiyo ya Bwire Sikumbuki na Sijatolea Maelezo

Kibatala: Kuna Mahala fulani ambapo inasemekana Mbowe, Kama sehemu ya Kutekeleza Mpango huo Alitakiwa Kupata Mabomu kutoka Ngerengere!?

Wakili wa Serikali, Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Samahani, Sina Hakika Kama Kuna Mahala Popote ambapo imesemwa hilo..

Kibatala: Wacha wanisaidie Kutafuta, Nitarudi baadae

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hilo Swala Halipo hata Akitafuta

Kibatala: Nitaliacha hilo, Nitarudi baadae

Kibatala: Kwani shahidi unaweza kulipua bila ya Kuwa na material ya kulipua (vilipuzi?)

Shahidi: huwezi

Kibatala: Ni kweli Kwamba Mbowe alishawahi kukushirikisha kutafuta material ya Kulipua

Shahidi: hajawahi kunishirikisha

Kibatala: Je Katika Ushahidi Wako Uliwahi Kusema Kwamba Khalfani Bwire, Mohammed Ling'wenya na Adam Kasekwa walikuwa na access ya Kupata Milipuko kutoka 92 KJ?

Shahidi: Sijawahi Kusema

Kibatala: Je umewahi Kuzungumzia Kuhusu Bunduki aina ya Bastola aina ya Luger A5340 kuwa ni Standard Bunduki za Makomandoo

Shahidi: Sijawahi Kusema

Kibatala: Ulisema Kwamba Mohammed Ling'wenya baada ya Kufika Kwa Mbowe Tarehe 24 hujawahi Kuzungumza naye

Shahidi: Hapana, Nilimtafuta bila Mafanikio

Kibatala: Je unasema Kwamba Mbowe aliacha Kuwasiliana na wewe Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 24 July 2020

Kibatala: Kwa hiyo Kwenye Kielelezo namba P 34 Kuna Meseji ambazo Ulimtumia Mbowe Hakujibu?

Shahidi: Zipo

Kibatala: Meseji hizo Ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji ambazo hazikujibiwa na Mbowe Kwa Kuongozwa na Mawakili wa Serikali

Shahidi: Sikuonyesha

Kibatala: Vipi Kuhusu Calls, Ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwenye hii Meseji Mbowe anasema sikuona Simu yako Kwa Sababu Deshi Deshi, l hope Umenielewa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: alisema Simu yako au Simu zako

Shahidi: Simu yako

Kibatala: Kwa kuwa wewe Ulikwepo Kwa DCI na Kingai, Nasikia kuwa Kingai aliteuliwa Kama Mpelelezi

Shahidi: Haja wahi Kuniambia kuwa ni Mpelelezi, alisema Taarifa Utampa Kingai

Kibatala: Katika Maelezo Yako Uliwahi Kufahamu Kwamba Inspector Swila Ndiyo Mpelelezi Wa Kesi yako

Shahidi: Hiyo sifahamu

Kibatala: Wala Ufahamu Kwamba Baada ya Inspector Swila Kufungua Faili, DCI alimteua kuwa Mpelelezi wa Kesi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unaweza Kukumbuka Kwamba Mohammed Ling'wenya alikuwa Sudani katika Peace Keeping

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wakati Unatoa Ushahidi Kambi ya Makomando ipo Ngerengere au Kizuka

Shahidi: Ipo Kizuka

Kibatala: Wakati Wa Maelezo Yako Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kambi ya Komandoo ipo Kizuka

Shahidi: Sikutoa Maelezo

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Wakati upo Sudani Kwenye Peace Keeping Kambi yenu ilikuwa inaitwa KAUBECHE

Shahidi: Inaitwa COLABECHE

Kibatala: Mlipokuwa Sudani, Kiongozi wenu alikuwa Kanali Mbwilo

Shahidi: Hapana ni General Mbwilo

Kibatala: Body Guard Wa huyu Generali Mbwilo yupo hapa Mahakamani

Shahidi: hayupo

Kibatala: Unamfahamu Luteni Omary ambaye alikuwa Sudani

Shahidi: Namfahamu

Kibatala: Je Luteni Msandawe

Shahidi: By Then Namfahamu

Kibatala: Ijumaa Nilikuuliza Maswali Kuhusu namba za Kingai MLIZO badilishana Kwa DCI

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ukasemaje

Shahidi: Niliacha Hotelini

Kibatala: Kwahiyo baada ya Kesi Kuhairishwa Utakuwa Umekuja nayo Leo Diary Yako

Shahidi: Sikuja nayo, Sikuelekezwa na Mahakama

Kibatala: Majibu Kuhusu Pass pale Jeshini Ilikuwaje

Shahidi: Pass ya zaidi ya Wiki Moja napewa Karatasi, Kwenda Katika Ofisi yoyote ninapokwepo.. Pass Chini ya Wiki naandika katika Daftari pale Kambini

Kibatala: Uliulizwa Ukasema Movement Order Ipo wapi

Shahidi: Ipo Hotelini

Kibatala: Wakati Unaitwa Mahakamani Ulipewa Summons au Maboss Zako Walikwambia Unatakiwa kutoa Ushahidi

Shahidi: Nilitoka Kwenye Operesheni Maalum Boss wangu akaniambia kariport kwa DCI

Kibatala: Boss wako anaitwa Nani

Shahidi: Light Kenoth

Kibatala: Ulipo surrender Simu zako zote toka Tarehe 12 August 2020, Ulifafanua Kwa Jaji Kuwa Ulikuwa unatumia Simu gani

Shahidi: Hapana Siku fafanua

Kibatala: Unaweza Kutuambia Kwanini Wewe Kama Mtoa Taarifa Baada ya Kuchukua Simu zako, Hawajawahi Kukupa Simu zako Mpaka

Kibatala: Unakutana nazo tena Hapa Mahakamani

Shahidi: Waliniambia Kuwa Wanafanyia Uchunguzi

Shahidi: Ndiyo Mara ya Mwisho Kama Mwaka Mmoja Umepita nilienda Kuulizia

Shahidi: Kwa Documents walizonipa

Kibatala: ambayo ni Moja

Shahidi: Hapa ninayo Moja lakini Zingine ninazo Nyumbani

Kibatala: Ukiangalia suala hili limeanza Tangu June 2020 Mpaka August 2020

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: kwa hiyo Tukiangalia katika Telegram hatutoona Mawasiliano yako wewe na Mbowe kabla ya Tarehe 25 June

Shahidi: Tulikuwa tunawasiliana Kupitia Whatsup

Kibatala: Mlikuwa Mnawasiliana kabla ya Kipindi cha Hili Tukio au ni Wakati wa Jambo hili tuh

Shahidi: Kimyaaaaaaaaa

Kibatala: Tarehe 07 August 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa Nipo kazini Sanga Sanga

Kibatala: Ni nini ambacho tunaweza Kuku Omba ukatuletea kuwa Ulikuwa kazini

Shahidi: Nilkuwa Commander wa QRF (QUICK RESPONSE FORCE)

Kibatala: zaidi ya Kuandikishana Kielelezo namba P 36 ni Ushahidi I alp Kwamba Inspector Swila Aliingizwa Simu katika Kitabu Kisha Wote Wewe na Yeye Mkasaini Kitabu

Shahidi: Mimi Siku Saini Kitabu

Kibatala: Na Yeye Hukumuona akiandika chochote Katika Kitabu

Kibatala: Zaidi ya Hand over Document, Je Uliwahi Kupewa Risiti yoyote ya Simu zako

Shahidi: Sijawahi Kupewa Risiti

Kibatala: Je Wakati Unamkabidhi Simu Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Inspector Swila alikuwa anabandika Makaratasi Katika Simu (Exhibit)

Shahidi: Sijawahi Kuona

Kibatala: Katika Maelezo ya Ushahidi Ulisema Kwamba haukujisumbua tena Kuhusiana na BWIRE kwa Sababu Lengo lilikuwa Limeshatimia

Shahidi: Nakumbuka nilisema

Kibatala: Lilikuwa Lengo lipi

Shahidi: Baada ya Wahalifu Kukamatwa

Kibatala: Kwa hiyo Lengo lako wewe lilikuwa Kuhakikisha Wahalifu Wanakamatwa

Shahidi: Nazuia uhalifu

Kibatala: Je ilikuwa kazi yako ya Kazi ya Polisi

Shahidi: Ilikuwa kazi ya Polisi

Kibatala: Malya alikuuliza Kwamba Uliwanunulia akina Adamoo Chakula

Shahidi: Nililipa Mimi lakini pesa Nilipewa na Mbowe

Kibatala: Je Ulizungumzia Katika Ushahidi Wako Mkuu Kuwa katika Pesa niliyowapa Adamoo na Ling'wenya Sehemu ya pesa ile Walitumia palepale Kulipa Chakula

Kibatala: Kwa kuwa wewe ulikuwa na Mawasiliano Moja kwa Moja na DCI na Kingai, Uliwahi Kufahamu Kwamba Hakuna Simu ya Mbowe hata Moja iliyokamatwa

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa Maana hiyo Ufahamu Pia Kwamba Polisi Wameshindwa Kuthibitisha Mawasiliano yako wewe na Mbowe

Kibatala: Mhe Jaji Nauliza Swali la Mwisho halafu nitatoa hoja

Kibatala: Ulisema Bwire Alikwambia Wapo katika Utekelezaji Wa Mpango

Shahidi: Siyo Mpango, alisema Samahani Bro tumeshakengeuka, Tumeshawishiwa na Freeman Mbowe, Na Vijana Wapo Kilimanjaro Katika Utejelezaji

Kibatala: Wewe Ulikuwa na Mamlaka Yoyote Ya Kiupelelezi zaidi Ya Kutoa Taarifa

Shahidi: Kila Mtanzania ni Mpelelezi, Sina Mamlaka Nyingine Ya Kiupelelezi

Kibatala: Hoja yangu Ulipata wapi Power Ya Kuagiza Waendelee na Uhalifu

Shahidi: nilishatoa Taarifa

Kibatala Mheshimiwa Jaji Bado Nina Maswali Kadhaa, Naomba tuhairishe Cross Examination, Mpaka Kesho February, Ilituweze Kuendelea.. Ni hayo tu.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi, lakini tunaomba Kesho Tukiendelea Mwenzetu ajieleleze Katika Maeneo ambayo bado hajayahoji

Jaji: Unasemaje

Wakili Peter Kibatala: Hakuna Neno Mheshimiwa Jaji

Jaji: Shauri hili limehairishwa mpaka kesho Tarehe 01.02.2022, Shahidi namba 12 ataendelea Kuwa Mahakamani Kuendelea Kutoa Ushahidi Wake. Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Asubuhi.

Jaji anatoka Saa 10: 38
 
Sasa honey+ngaya aibu imemshika..

Tatizo lake ni mgumu kuchukua hatua.
Alitakiwa kupiga chini akina kamanda sirrrrro walio mpeleka chaka
 
Asante,tunawashukuru sana mnavyojitolea kwa ajili ya kutuhabarisha,Mungu azidi kuwapa nguvu.

Hayo ma- UVCCM waliopanga kumshambulia Martin Maranja eti kisa hayataki kusikia watu wakihabarishwa kutoka mahakamani wampe taarifa Chui Jike kwamba mambo magumu huku atafute cha kuwaambia BBC
 
Draft la Kingai na genge lake lishagoma - Mashahidi wote hadi leo hakuna aliyethibitisha pasi na shaka kosa la Ugaidi la Mbowe na wenzake !! Huyu URIO ndiyo kabisaa kaithibitishia mahakama kwamba Kina Adamoo ni watu wazuri.
AIBU KUBWA
 
Back
Top Bottom