Yaliyojiri Bungeni leo tarehe 16 Mei 2015

Makini

Senior Member
Dec 23, 2014
154
59
Leo bunge la bajeti linaendea, na sasa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndie anaeongea kuiwakisha serikali. Twende pamoja kuona vitokeavyo leo.
=========

Pinda: Kwenye sekta ya afya tunafanya vizuri na tunaongoza kwa kupunguza vifo vya watoto wachanga. Mwisho niseme hili kwa nia njema, nimesikiliza majigambo humu, mimi ntanshinda ntashinda, kwanini tuandikie mate wakati wino upo, chaguzi zote mnajua nani alishinda. Mwisho wa yote watu wanataka kujua barabara mmejenga, maji, barabara, afya. Naomba katika kumalizia niseme pamoja na mikwara yote tuliochimbiana, kazi niliyonayo kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ni kuchuja yale mazuri, niwahahakishie wabunge tumefarijika kwa yote na tutayafanyia kazi. Kubwa tuendelee kuheshimiana na tofauti zetu za kiitikadi zisiwe ishu, mwisho kazi tuliyonayo sasa mpaka kumaliza bunge hili ni ushauri hasa kwa kipindi kilichobaki na yakiwa ya muda mrefu tutayabeba. Nimwambie Mbowe hata akishinda kesho ataanzia tulipoishia. Baada ya kusema haya naomba kutoa hoja.

Spika: CUF leo wana kura za maoni Unguja na Pemba ndio maana mnaona wengi hawapo

Mwongozo(Msigwa):
Tume ya uchaguzi imetoa mwongozo wa vyama vya siasa kuhamasisha wananchi wao, katika jimbo langu wapiga kura wanaandikishwa na vyombo vya kuwatangazia watu ni vichache, tumetoa nguvu yetu kusidia kutoa taarifa lakini tunakatazwa.

Kinachoendelea kwa sasa ni kupitisha makadirio ya matumizi katika ofisi ya waziri mkuu na TAMISEMI.

Jenista Mhagama: Swala la usalama wa Albino linashughulikiwa kwa umakini. Kuwalinda Albino ni muhimu na linaendelea kufanyiwa kazi. Watanzania wote tushirikiane na kuungana mikono katika kumaliza mauaji ya Albino.

Asha- Rose Migiro: Waliohukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kuua albino watashughulikiwa. Kuna taratibu za kufuata, haki itatendeka.

Jenista Mhagama akijibu swali la Suzan Lymo kuhusu utata katika uandikishaji wa wapiga kura: serikali imetoa elimu. Kila mwenye sifa ya kuandikiswhwa kwenye kitabu ni lazima aandikishwe. Wananchi wanaojitokeza wote ni lazima waandikiswhwe. Serikali inajitahidi hata kuongeza ofisi ili kuhakikisha watu wote wanaandikishwa. Tutakaa na tume ya uchaguzi kujua hali ya uandikishaji, lakini zoezi linasimamiwa vizuri.

Kuhusu BVR: Jumla ya mashine zilizopatikana mpka sasa ni 4850, tunaendelea kupokea nyingine mpaka zifikie 8000. Tukisghazipata zote, kwa siku tutaweza kuandikisha watu hadi lakin nane kwa siku.

Machali: Swali kuhusu ujenzi wa barabara. Baadhi ya maeneo yanatengewa fedha kidogo za miundombinu, mfano Kigoma yenye barabara yenye urefu wa kilomita 300 isiyo na lami wakati kuna maeneo ambapo serikali inabandua na kubandika lami. Serikali inajiskiaje kuwa na ubaguzi wa aina hii?

Lwenge: Serikali haina ubaguzi katika kuunda miundombinu. Upendeleo haupo na Kigoma itapata barabara za lami kama ilivyokua imepangwa.

Esther Bulaya: Kwa nini fedha zilizopangwa kwenda katika mfuko wa TEA katika vikao vilivyopita hazijapelekwa huko?

Nchemba: tulipata misukosuko katika bajeti kutokana na madeni, tuliamua kulipa kwanza malimbikizo ya madeni tuliyokua nayo. Lakini bado serikali imejizatiti kuwa fedha zilizotengewa matumizi ya mifuko zitakwenda katika hiyo ,mifuko. Agizo limeshatolewa kwa benki kuu kuwa hizo fedha zitakwenda kwenye mifuko hiyo.

Wenje: Kura ya maoni itafanywa baada ya tume kukamilisha zoezi la uandikishwaji. Lakini ukiangalia muda uliobaki, gharama na shughuli ya uchaguzi mkuu na sheria ya mabadiliko ya katiba iliyoweka muda; muda huo umeshapita. Kwa nini waziri mkuu anaendelea kutoa commitment hewa na kudanganya wananchi?

Asha- Rose Migiro: Baada ya katiba pendekezwa kupatikana, kura ya maoni inaongozwa na sheria ya kura za maoni. Kipindi cha ziada kilipatikana kutokana na sheria. Hakuna sheria iliyokiukwa.

Machali: Naomba ufafanuzi, ununuzi wa magari wanaomba milioni 380, watoe ufafanuzi wa aina ya magari wanayoenda kununua, wasije wakaenda kununua suzuki mbili maana wanatutajia jumla jumla.

Naibu waziri TAMISEMI: Hapa tumekusudia kununua magari kwa ajili ya viongozi na hapa tumekusudia VX

Susan: Education materials, kitengo hiki kina umuhimu sana kwa ofisi ya waziri mkuu lakini kimetengewa milioni 30 tu tofauti na milioni 80 mwaka jana.

Waziri TAMISEMI: Mwaka jana ilikuwa milioni 80 kwa sababu ya uchaguzi serikali za mitaa kwa ajili ya vipeperushi ila mwaka huu hatuna tena uchaguzi serikali za mitaa ndio maana imekuwa hivyo.
 
Wakati anaendelea kufafanua amesikika akisema General Shimbo amesaidie kupitia jeshi la Wananchi katika Ujenzi wa madaraja
 
Akihitimisha hoja ya bajeti ya OWM leo bungeni mh. Waziri Mkuu amesema mfumko wa bei ni njia sahihi ya kukuza na kuelekea kwenye uchumi ulio imara wa nchi.jamani wataalamu wa uchumi híi nadharia ya PM Ni sahihi? Source TBC 1.
 
Akihitimisha hoja ya bajeti ya OWM leo bungeni mh. Waziri Mkuu amesema mfumko wa bei ni njia sahihi ya kukuza na kuelekea kwenye uchumi ulio imara wa nchi.jamani wataalamu wa uchumi híi nadharia ya PM Ni sahihi? Source TBC 1.

Sijamsoma hata mimi
 
Namimi ngoja ni subscribe kwenye hii thread ili nipate majibu ya wanauchumi, maana haya mambo tunatangishana sana, hivi U$ inanunuliwa kwa Tsh nyingi jamaa mmoja CRDB akasema ni faida ila kwa mimi mwananchi wa kawaida sielewi.
 
'Tanzania ni ya 5 kwa afrika, pia ni ya 12 duniani ktk kulima mahindi' - mh. Pinda.


Mbona bei haishuki ? Iwe sh 500/kg
 
idoyo
hoja yako ipo upande ktk fursa ya uwekezaji.

lkn inflation inapunguza mauzo, ivyo mapato/faida hupungua.
 
Last edited by a moderator:
Leo kashindwa kujibu swali la mh.jaffo na kuomba muda atafute majibu.kweli hii serkali imejaza vilaza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom