Yaliyojiri Bungeni leo: Februari 2010

Hii nchi kwa senema tumetia fora..Tunawazidi hata waigizaji maarufu duniani Wahindi..lakini bora wao wanaliingizia \taifa pato kupitia uigaizaji wao.Sisi ni magizo mpaka kwenye vyombo vya maamuzi.
 
Usikatishe tamaa wapambanaji/ wafuatiliaji wa mambo...kama umeona habari hiyo haifai kwako ipotezee kuliko kutoa comments za kukata tamaa!

Kuandika kwa rangi nyekundu kunamaanisha nini? au hatari? Wanaofahamu maana yake watufafanulie zaidi.

Turudi kwenye mada. Hata mimi nashangaa bunge kuahirishwa ghafla nilifikiri kuna msiba kumbe sio. Ok tusubiri lifuatalo.
 
hayo ndo matokeo ya serikali inayoendeshwa kama mchezo wa kuigiza ikiongozwa na stering......
 
Wabunge walipokubali hoja za uongo za Chegeni kuhusu madaraka yao wamebakia kuwa ni consultants wa serikali! Probably they are proud too kuwa hivyo. Shameful.
 
Ni kama wanaahirisha matatizo wanakufukia moto kwa majivu siku ukilipuka midomo itabaki wazi hata kikao cha CC na NEC kimeahirishwa iliyokuwa ifanyike kesho kupata majibu ya tume ya Mwinyi mimi nasema watabana lakini itafika mwisho mambo yatakuwa wazi
 
na jamaa mwenyewe kashaziba mdomo na kapunguzwa speed(Mhe Six), sasa unategemea nini hapo?
 
teh teh ..aaaah mtoto wa mkulima naona vitu vyako..unatisha lakini kwa ma strategy yako makeniko...kuna siku utalia tena tu we ngoja tufanyie mazingaombwe tunakuangalia tu..Na wewe spika sita huna lolote toka utishiwe kuporwa kadi ya uanachama umefyata mkia
 
Wanabodi,

Kama kawaida wananchi kama mimi, tupatapo nafasi huwa tunajituma mpaka mjengoni ili kuisikia live kwa naked eyes baadhi ya mijadala muhimu. Ndivyo ilivyokuwa kwa jioni ya leo, nimejihimu ili nisikie mjadala wa taarifa mbili za serikali ikirindima.

Saa 11:00 akaingia Naibu Spika, Mheshimiwa Sana, Mama Anna Makinda.

Aliposimama na kunza kuongea, kwanza nilinote, anaongea akiwa na pressure, huku anajitahidi sana kubana pumzi, kama vile anataka kutangaza taarifa muhimu, ningekuwa siko mjengoni, ningeweza kudhani labda kuna taarifa ya msiba!.

Kumbe, alikuwa anatangaza Kikao cha Bunge Cha Jioni Hii, kilichokuwa kijadili utendaji usioridhisha wa TICTS na RITES, kimeahirishwa ghafla kufuatia taarifa hizo zote mbili kutokuwa tayari!.

Hivi jamani, hii ni serikali inalichezea bunge na kulifanyia mzaha, au ni Bunge lenyewe haliko serious enough hivyo serikali kulifanya bunge ni shamba la bibi!?.

Nilishasema hapa ukumbini hili Bunge letu si Bunge tukufu. Asilimia kubwa ya Wabunge wameweka mbele zaidi maslahi yao kuliko yale ya nchi.
 
Nilikwisha sema Watz tunachezewa tu. Wengi wanaingia bungeni kushiba tu sasa mjadala ndo umeahirishwa au umefutwa kabisa? Kazi ipo!
 
Na mwezi wa kumi mnawarudisha hao hao bungeni si mmewasikia wakijinadi na kulazimisha wananchi lazima wawachague wao? haya wengine waliyazungumza wakati wa sherehe za kuzaliwa chama kinachopindua?
Kazi kweli kweli!
 
wakulu hili bunge lina vituko

Hivi punde Mh Spika amewatahadharisha wabunge wasiwe na homa sana ya uchaguzi,

na kwa kutoa mfano akasema kuwa kuna mbunge mmoja kamwandikia barua akimwita "Madam Speaker'

Amewapa matumaini kama wameandikiwa , wamendikiwa tu.

Sasa je ni kweli kuwa homa ya uchaguzi imepanda kiasi hiki wa wabunge? Si inaathiri hata uchangiaji wao wa hoja na hata maswali wanayouliza serikali kwa kweli mengi unakuta yameelekezwa kwenye majimbo yao na machache sana yenye kugusa masuala ya kitaifa...

Sijui lakini ni mtizamo wangu tu.
 
ana vituko huyu mbaba,kamtambulisha mgeni wa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,Mr Tanzania wa 2001, eti kwa vile ni bodybuilder, Sitta akasema (kwa utani lakini) eti haishirii mazuri kwenye uchaguzi ujao!! ilipofika zamu ya miss Intercontinental, eti kadai jua linamzuia kumuona vizuri.....teh! teh!
 
Who let this beggar in? Sitta anataka kulifanya bunge letu liwe unruly kama the commons.
 
ana vituko huyu mbaba,kamtambulisha mgeni wa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,Mr Tanzania wa 2001, eti kwa vile ni bodybuilder, Sitta akasema (kwa utani lakini) eti haishirii mazuri kwenye uchaguzi ujao!! ilipofika zamu ya miss Intercontinental, eti kadai jua linamzuia kumuona vizuri.....teh! teh!

Yaani nimecheka kweli!

hapa anadai eti hana presha yoyote ya uchaguzi (Speaker)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom