Sikukuu ya Krismas, yaani tarehe 25 December, husherehekewa duniani kote kama kumbukumbu ya siku aliyozaliwa Yesu Kristo. Watu wengi hudhani kuwa Yesu alizaliwa siku hiyo, lakini ukweli ni kuwa hakuna anayejua siku kamili ya kuzaliwa kwa Yesu. Jambo la muhimu lijulikanalo kuhusu December 25 ni kuwa ni siku ambayo iko katikati ya kipindi cha winter kwa nchi za kaskazini. Siku hii ya katikati ya winter ilikuwa inasherehekewa kwa njia mbalimbali na watu wa zamani wa ulaya ambao walikuwa wakiabudu miungu "wadogo wadogo" mbalimbali. Watu hao baadaye walikuja julikana kama "wapagani" baada ukristu kuanza kuingia. Walikuwa na sababu mbali mbali za kusherehekea siku hiyo. Kwa mfano, wajerumani walikuwa wakiamini kuwa Mungu wao aliyejulikana kama Oden alikuwa akipaa angani siku hiyo na kuamua nani wa kusaidia aendelee na nani wa kuteketezwa. Sasa kwa vile hakuna aliyejua uamuzi wa mungu huyu, waliogopa wasijechaguliwa kuangamizwa. Kwa hiyo walijificha kwa kukaa ndani siku yote wakinywa pombe bila kutoka nje wasije wakaonekana na huyu "mungu" Oden na kuamuliwa kuangamizwa.
Roma nako walikuwa na sababu zao tofauti za kusherehekea siku hiyo, mojawapo ikiwa ni kuwaenzi watoto, kama ambavyo leo siku hii inaonekana kama siku ya watoto. Kulikuwa na sababu nyingine mbalimbali za kinajimu kama vile kuangalia nafasi ilipo sayari kubwa ya Saturn ambayo ndiyo iliyokuwa Mungu wao wa Kilimo.
Baada ya ukiristu kuingia sehemu za ulaya, Krismas ilionekana kama ni siku ya kishetani tu. Sikukuu ya kidini ilikuwa ni moja tu: pasaka, yaani siku ya kifo cha yesu kwa vile hiki kilikuwa kinajulikana kuwa kilitokea siku ya Ijumaa na akafufuka siku ya Jumapili. Hata hivyo kunako karne ya nne, viongozi wa kanisa waliamua kuienzi siku ya kuzaliwa Yesu, lakini wakawa hawajui alizaliwa lini kwa vile haikuandikwa kabisa kwenye biblia. Papa Julius wa Kwanza ndiye aliyechagua siku hii ya December 25 ili kusudi imeze na kumaliza zile sherehe za kipagani zilizokuwepo Ulaya. Ilianza ikiwa inajulikana kama "the Feast of the Nativity." Siku hii haina uhusinao kabisa na siku halisi ya kuzaliwa kwa yesu kwa vile yesu hakuzaliwa katikati ya winter. Ushahidi uliopo unaonyesha kuwa yesu alizaliwa wakati wa Spring, ndiyo maana wachungaji walikuwa wakichunga kondoo. Katikati ya winter kusingekuwa na wanachunga kodooo wale.
NAWATAKIENI WANAKIJIWE WOTE FURAHA YA SIKU YA KRISMAS NA HERI YA MWAKA MPYA WA 2008. TUTUMIE MUDA HUU WA SHEREHE KUTAFAKARI MABAYA NA MAZURI TULIYOFANYA MWAKA 2007 KUSUDI TUENDELEZE MAZURI NA KUREKEBISHA MABAYA YETU KATIKA MWAKA MPYA WA 2008.