Kheri ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1445

dega

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
3,138
3,042
Tukiwa katika maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu twawatakia kila la kheri ya mwaka mwaka mpya Waislamu wote ulimwengu, tuendeleze mshikamano kuvumiliana na huku tukiendelea kupambana kufata Sheria kandamizi kama Sheria ya ugaidi ambayo ipo maalimu kwa kuwakomoa, kuwaadhibu na kuwauwa watu wasio na hatia yoyote.

Ni juzi tu Mahakama imewaachia huru Waislamu waliokaa zaidi ya miaka tisa gerezani kwa tuhuma za ugaidi, kisha wakaachiliwa huru bila maelezo yoyote. Si hao tu, Wazanzibari zaidi ya 30 pia waliwekwa gerezani huko Tanganyika wakati wanadai Zanzibar yenye mamlaka kamili, wakapachikwa kosa la ugaidi na kukaa zaidi ya miaka tisa kisha kuachiwa bila masharti yoyote.

Waislamu duniani kote wanapitia machungu mbalimbali kisa imani yao kwa Mungu wao. Huko Kenya mshukiwa mmoja wa ugaidi alimwambia hakimu aliemwachilia huru baada kumuona hana hatia kwamba yupo tayari kuendelea kukaa gerezani hata kama kamuona hana kosa kwa sababu wenzake wengi baada kuachiliwa huru waliuwawa na wengine walipotea moja kwa moja.

Wakati tunaadhimisha mwaka mpya kwa njia za amani na za kidemokrasia, tuendelee kupambana kuwatafutia utulivu na haki ya kujueleza wale wanapitia machungu na ukatili duniani kote.

Happy new year 1445, kwetu leo ni mapumziko. Akhsante Serikali yetu sikivu kwa kuliona umuhimu wa hili.
 
ni mwaka mpya wa nini? tujuzane wakuu - je ni kuzaliwa kwa Mtume, kuanzishwa kwa dini ya kiislamu ama ni namna ipi mwaka huo unakuwa counted?
 
Hao waislamu uanolalamika waliwekwa gerezani miaka kumi Tanganyika unajua waliwekwa na nani?

Nyie sherehekeeni huo mwaka wenu, msichimbue mengine mkajiharibia hiyo sherehe yenu wenyewe.
Angetaja pia Wakili aliyewasaidia kuwatoa lupango, nadhani tujifunze ku-appreciate watu. Umeiweka vyema
 
Back
Top Bottom