Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 80,839
- 93,626
Watu wanapiga pesa ndefu kujifanya wanapelelezaKuna baadhi ya kesi huwa zina ngazi ya kimahakama kusikilizwa.
Mfano kesi ya mauaji na uhujumu uchumi haiwezi kusikilizwa mahakama ya mwanzo,lakini wahalifu wamekuwa wakipelekwa katika mahakama hizo ,kesi inapotajwa mtuhumiwa anaambiwa haruhusiwi kuzungumza kwa vile mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi ya namna hiyo
Ushauri wangu
Kwa nini wasiwepo mahakama wenye hadhi ya kusikiliza kesi kama hizo ili aipandishe hadhi mahakama ile kwa muda au wahalifu wawe wanapelekwa moja kwa moja kwenye mahakama ambazo zina mamlaka ya kusilikiza kesi hizo kuliko kupoteza muda na fedha katika mahakama ambayo haina mamlala kisheria kusikiliza kesi hizo.?