Whozu afungiwa miezi 6, Mbosso na Billnass wafungiwa miezi 3. Wote wapigwa faini Tsh. Mil. 3. Wimbo wa 'Ameyatimba' umewaponza

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
20231104_233136.jpg

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Msanii Whozu kushusha mara moja video ya wimbo wake wa ‘Ameyatimba’ kwenye digital platform zote, pia limemtoza faini ya Tsh. milioni 3 na limemfungia kujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi 6 kuanzia leo November 04, 2023 kutokana na wimbo huo kuwa na maudhui yanayokiuka kanuni za maadili.

BASATA imesema Whozu alichapisha video ya wimbo huo Nov 02, 2023 akiwashirikisha wasanii wenzake Mbosso na Bill Nass, na kwamba wimbo huo una maudhui yanayokiuka kanuni za maadili kutokana na kuwepo ishara ya vitendo vinavyoashiria matusi kinyume na Kanuni ya 25(6) (j) pamoja na vitendo ya unyanyasaji, ukatili na udhalilisha wa utu wa Mwanamke kinyume na Kanuni ya 25(6)-(f).

“Msanii huyu ameshaonywa mara mbili na kutozwa faini mara moja huko nyuma kwa kukiuka taratibu za kuzingatia maadili katika kazi za sanaa lakini bado ameendelea kupuuza”

“Baraza la Sanaa la Taifa kupitia Sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 na Marekebisho yake ya Mwaka 2019 ambayo inatoa Mamlaka kwa Baraza kusimamia Maadili ya msingi kwenye Sekta ya Sanaa kwa Kanuni ya 25(1)-(8) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018.

Pia soma - BASATA angalieni jinsi wasanii wanavyohamasisha ngono chafu
- Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara
 
Back
Top Bottom